William Miller na wenzi wake walikuwa wanataka kuwaonesha wale waliokuwa wanadai kuwa watu wa dini, tumaini la kweli la kanisa na hitaji lao la kuwa na UKristo wa kina zaidi. “Hawakutaka kuwaingiza watu katika kundi lililojitenga na makanisa yao. Walikuwa wanafanya kazi katika makundi na madhehebu yote.” Miller alisema, “Nilikuwa nimekusudia kuwanufaisha wote. Nikidhani kwamba Wakristo wote wangefurahia tumaini la kuja kwa Yesu, na wale ambao hawakuyaona mambo kama nilivyokuwa nayaona wasingepunguza upendo wao kwa wale waliolipokea fundisho hili, sikuwa nafikiria kwamba kungekuwa na haja ya kuwa na mikutano ya pembeni.... Sehemu kubwa ya wale walioamini kutokana na mahubiri yangu walijiunga na makanisa yaliyokuwapo wakati huo.” 215Bliss, p. 328. TK 238.1
Lakini kwa kuwa viongozi wa dini walikuwa wameamua kulipinga fundisho la Ujio, waliwakatalia washiriki wao kuhudhuria mahubiri ya Ujio wa pili au hata kuzungumzia tumaini lao katika kanisa. Wale waumini walikuwa wanayapenda makanisa yao. Lakini walipoona kuwa haki yao ya kuchunguza unabii inazuiliwa, waliona kwamba utii kwa Mungu ulikuwa unawakataza kusalimu amri. Hivyo waliona uhalali wa kujitenga. Katika majira ya joto ya mwaka 1844, takriban watu 1000 walijitenga na na makanisa yao. TK 238.2
Katika makanisa mengi, kwa miaka mingi kulikuwa na ongezeko la kukubaliana taratibu na desturi za ulimwengu na kuzorota kwa maisha ya kiroho. Lakini mwaka huo, kulikuwa na ushahidi wa kuzorota katika makanisa karibu yote nchini. Ukweli huo ulielezwa katika vyombo vya habari na katika madhabahu. TK 238.3
Bw. Barnes, aliyekuwa mwandishi wa kitabu cha ufafanuzi na mchungaji wa moja ya makanisa makubwa ya Filadelphia, “alisema kwamba ... sasa hivi hakuna uamsho, hakuna wanaoongoka, hakuna ukuaji katika neema miongoni mwa wanaodai kuwa waumini, na wengi hawaji kujifunza kwake ili wazungumzie wokovu wa roho zao. ... Kuna ongezeko la kupenda ulimwengu. Hivyo ndivyo ilivyo kwa madhehebu zote. 216Congregational Joumal, May 23, 1844. TK 238.4
Mwezi wa Februari wa mwaka huo, Profesa Finney wa Chuo Kikuu cha Oberlin alisema: “Kwa ujumla, makanisa ya Kiprotestanti nchini mwetu, ama yamekuwa baridi au yamekuwa na chuki dhidi ya kila aina ya matengenezo ya uadilifu katika kizazi hiki. Ubaridi wa kiroho umeenea kote na umezama kwa kina mno; vyombo vya habari vya nchi yetu vinashuhudia.... Kwa sehemu kubwa washiriki wanazidi kuwa wapenzi wa mitindo, wanaungana na watu wasiomcha Mungu katika tafrija za anasa, katika dansi, katika karamu, na kadhalika.... Makanisa kwa ujumla yanazidi kuzorota. Yametanga mbali sana na Bwana naye amejitenga nao. TK 239.1