Giza la kiroho halisababishwi na Mungu kuondoa neema yake, bali linasababishwa na wanadamu kuikataa nuru. Kutokana na kuupenda ulimwengu na kumsahau Mungu, Wayahudi hawakujua cho chote juu ya Ujio wa Masihi. Kwa sababu ya kutokuamini, walimkataa Mkombozi. Mungu hakuliondoa taifa la Wayahudi katika baraka za wokovu. Wale walioukataa ukweli walikuwa “watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza.” Isaya 5:20. TK 239.2
Baada ya kuikataa Injili Wayahudi waliendelea kudumisha taratibu zao za zamani za kidini, huku wakikiri kuwa uwepo wa Mungu haukuwa pamoja nao. Unabii wa Danieli ulitabiri kwa usahihi wakati wa kuja kwa Masihi na ulitabiri kifo chake moja kwa moja. Hivyo walipinga usomaji wa kitabu hicho, na hatimaye maarabi walitoa laanakwa wote ambao wangejaribu kufanya mahesabu ya wakati. Kwa upofu na roho isiyotaka toba watu wa Israeli waliendelea kutokujali fursa za neema ya wokovu kwa kamenyingi, bila kujali baraka za Injili, hali ambayo ni onyo la kutisha juu ya hatari ya kukataa nuru itokayo mbinguni. TK 239.3
Mtu anayetweza ushawishi juu ya wajibu kwa kuwa unaingiliana na matamanio yake atapoteza uwezo wake wa kutofautisha ukweli na uongo. Roho hutengwa na Mungu.Pale ukweli wa Mungu unapokataliwa kwa fedheha, kanisa litakuwa gizani, imani na upendo hupoa, na mivutano hutokea. Washiriki wa kanisa huvutiwa na mambo ya dunia, na wenye dhambi huthibitika katika ukaidi wao. TK 240.1