Ujumbe wa malaika wa kwanza wa Ufunuo 14 ulikuwa umekusudiwa kuwatenga watu wanaokiri kuwa wa Mungu na mivuto mibaya. Katika ujumbe huu, Mungu alituma onyo kwa kanisa, ambalo, kama lingepokelewa, lingerekebisha uovu uliokuwa unawatenga na Mungu. Kama wangeupokea ujumbe huo, wakinyenyekeza mioyo yao, na kutaka kujiandaa kusimama mbele zake, Roho wa Mungu angedhihirishwa. Kwa mara nyingine kanisa lingekuwa na umojaimani, na upendo uliokuwepo zama za mitume, wakati waumini “walikuwa na moyo mmoja na roho moja,” na ambapo Bwana alilizidisha “kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.” Matendo 4:32; 2:47. TK 240.2
Kama watu wa Mungu wangeipokea nuru kutoka katika Neno lake, wangekuwa na umoja ambao mtume Paulo anauelezea, yaani “umoja wa Roho katika kifungo cha amani.” Anasema, “mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la mwito wenu; Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.” Waefeso 4:3-5. TK 240.3
Wale walioupokea ujumbe wa kurudi kwa Kristo walitokea kwenye madhehebu mbalimbali, nao tufauti zao za kimadhehebu zilitupiliwa mbali. Itikadi zilizokuwa zinapingana zilivunjwa vunjwa na kuwa kama atomu. Dhana potovu juu ya Ujio wa pili zilisahihishwa. Mabishano ya kiitikadi za kila dini iliyeyushiwa mbali. Mitazamo potovu kuhusu kurudi kwa Kristo ilisahihishwa. Makosa yalirekebishwa na mioyo iliungana katika ushirika mwanana. Upendo ulishika hatamu. Fundisho hili lingefanya hivyo kwa wote kama wote wangelipokea. TK 240.4
Wachungaji, ambao walipasa kuwa wa kwanza kuzitambua dalili za kuja kwa Yesu kama walinzi, walikuwa wameshindwa kujifunza ukweli kutoka kwa manabii au katika ishara za nyakati. Upendo kwa Mungu na imani kwa Neno lake vilikuwa vimepoa, na fundisho la Ujio Wakristo lilichochea tu kutokuamini kwao. Kama ilivyokuwa kwa ushuhuda wa zamani, Nenola Mungu lilikutana na swali: “Ni nani katika wakuu amwaminiye, au katika Mafarisayo?” Yohana 7:48. Wengi walikatisha tamaa usomaji wa unabii, wakifundisha kwamba vitabu vya unabii vilikuwa vimefungwa, tena havikupasa kueleweka. Walio wengi, wakiwaamini wachungaji wao, walikataa kuusikiliza ujumbe huo; na wengine, japo walikuw wameshawishiwa na ukweli, walikataa kuukiri wazi wasije “wakaondolewa kutoka katika sinagogi.” Yohana 9:22. Ujumbe ambao Mungu aliutuma ili kulipima Kanisa ulidhihirisha jinsi idadi ya waliokuwa wameweka mapenzi yao kwa ulimwengu badala ya Mungu, ilivyokuwa kubwa. TK 240.5
Kulikataa onyo la malaika wa kwanza ilikuwa sababu ya hali mbaya ya kupenda dunia, kuasi, na kufa kiroho iliyokuwa katika makanisa mwaka 1844. TK 241.1