Katika kipindi hicho, itikadi kali zilianza kuonekana. Baadhi walionesha itikadi kali. Mawazo yao yenye itikadi kali yalilipingwa vikali ya sehemu kubwa ya wale waliokuwa wakiamini juu ya Ujio, lakini yalisababisha fedheha kwa kazi ya kueneza ukweli. TK 249.1
Shetani alikuwa anapoteza watu wake, na ili aifedheheshe kazi ya Mungu, alitaka kuwadanganya baadhi ya wale waliokuwa wanakiri imani na kuwafanya wawe na msimamo uliopitiliza. Wakati huo mawakala wake walikuwa tayari kuchukua kila kosa, kila tendo lisilofaa, na kulitia chumvi ili kuwafanya wale waliokuwa wakiamini juu ya Ujio waonekane kama kero. Kadiri alivyowafanya wengi wakiri imani yao katika Ujio wa pili huku akitawala mioyo yao, ndivyo alivopata nafasi nzuri zaidi ya kufanikiwa. TK 249.2
Shetani ni “mshitaki wa ndugu zetu.” Ufunuo 12:10. Roho yake huwashawishi watu kutafuta kasoro za watu wa Mungu, na kuzifanya zionekane, wakati matendo yao mema yakiachwa bila kutajwa. TK 249.3
Katika historia yote ya Kanisa hakuna matengenezo yaliyofanyika bila kukutana na vikwazo vikali. Kila mahali ambapo Paulo alianzisha kanisa, baadhi ya wale waliokiri kuipokea imani waliingiza mafundisho potovu. Luther pia alikutana na adha kutoka kwa watu wenye itikadi kali waliokuwa wanadai Mungu alikuwa amenena moja kwa moja kupitia kwao, ambao waliyafanya mawazo yao kuwa bora kuliko Maandiko. Wengi walidanganywa na hao walimu wapya wa uongo, na kujiunga na Sheatani katika kubomoa yale ambayo Mungu alikuwa amemvuvia Luther kuyajenga. Wafuasi wa Wesley walikutana na hila za Shetani za kuwasukumia katika itikadi kali wale wasio na ulingano na utakaso. TK 249.4
William Miller hakuendekeza itikadi kali. “Yule mwovu” alisema Miller, “ana uwezo mkubwa juu ya akili za wengine wakati huu.” “Mara nyingi nimekuwa nikipata ushahidi wa utauwa wa kina kutoka katika jicho lenye shauku, shavu lenye machozi na sauti inayokwama, kuliko katika kelele zote za Ukristo.” 224Bliss, pp. 236, 237. TK 249.5
Matengenezo yalilaumiwa na maadui wake kwa uovu wa itikadi kali uliokuwa juu ya wale waliokuwa wanajitahidi sana kuyapinga. Njia hiyo hiyo ilitumiwa na wale waliokuwa wakipinga harakati za Ujio. Kana kwamba kutia chumvi makosa ya wale wenye itikadi kali hakutoshi, walieneza habari ambazo hazikuwa na ukweli hata kidogo. Amani yao ilikerwa na tangazo la kukaribia kwa Yesu. Walikuwa wanahofia kwamba ingeweza kuwa kweli, lakini pia walikuwa wanaombea isiwe kweli. Hii ilikuwa ndiyo siri ya vita yao dhidi ya wale waliokuwa wakiamini juu ya Ujio. TK 250.1
Kuhubiriwa kwa ujumbe wa malaika wa kwanza kulielekea kutokomeza itikadi kali moja kwa moja. Wale waliokuwa wanashiriki katika harakati hizi nyeti walikuwa na umoja; mioyo yao ilikuwa imejazwa upendo kati yao na upendo kwa Yesu, ambaye walikuwa wanatarajia kumwona muda si mrefu. Imani hiyo moja, tumaini hilo moja lenye baraka, lilithibitika kuwa ngao dhidi ya mashambulizi ya Shetani. TK 250.2