“Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. Lakini usikuwa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.” (Mathayo25:5,6). Katika kiangazi cha mwaka 1844 ujumbe huu ulitangazwa kwa nguvu kama Maandiko yalivyokuwa yanasema. TK 250.3
Kilichosababisha harakati hizo ni ugunduzi kwamba amri ya Artashasta ya kuujenga upya Yerusalemu, ambayo ilikuwa inaonesha mwanzo wa zile siku 2300, ilitolewa katika majira ya kupukutisha ya mwaka 457 K.K., na siyo mwanzo wa mwaka, kama ilivyo kuwa ikiaminika. Ukihesabu kuanzia mwaka 457, miaka 2300 inaishia msimu wa kupukutisha wa mwaka 1844. Vielelezo vya Agano la Kale pia vilikuwa vinaonesha “kutakaswa kwa hekalu” lazima kufanyike katika majira ya kupukutisha. TK 250.4
Kuchinjwa kwa mwana kondoo wa Pasaka ilikuwa ishara ya kifo cha Kristo, jambo ambalo lilitimia si katika tukio tu, bali kwa wakati pia. Siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza wa Kiyahudi, si ku ile ile na mwezi ule ule ambao mwana kondoo wa Pasaka alikuwa anachinjwa kwa kame nyingi, Kristo alianzisha siku kuu ambayo ingeadhimisha kifo chake Yeye mwenyewe kama “Mwana Kondoo wa Mungu.” Usiku huo huo alichukuliwa kwenda kusulibiwa na kuuawa. TK 250.5
Vivyo hivyo vielelezo vinavyo husu Ujio wa pili vinapaswa kutimia katika muda uliotabiriwa katika vielelezo. Kutakaswa kwa hekalu au Siku ya Upatanishao, kulikuwa kunaangukia katika siku ya kumi ya mwezi wa saba wa Kiyahudi ambapo kuhani mkuu, alikuwa anatoka na kuwabariki watu baada ya kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli wote na hivyo kuziondoa dhambi kutoka katika hekalu. Kwa hiyo iliaminiika kuWakristo angekuja kuitakasa dunia kwa kuiangamiza dhambi na waovu, na kuwabariki kwa kuwapa kutokufa watu wake waliokuwa wanamngojea. Siku ya kumi ya mwezi wa saba, Siku kuu ya Upatanisho, siku ya kutakaswa kwa hekalu, ambayo mwaka 1844 ilikuwa inaangukia tarehe 22 oktoba, ilichukuliwa kuwa siku ya kuja kwa Bwana. Siku 2300 zilikuwa zinaishia katika majira ya kupukutisha, hatima hiyo ilikuwa inaonekana kuwa haipingiki. TK 251.1