Miongoni mwa mawakala wenye kufanikiwa sana wa yule mdanganyifu mkuu ni watendaji wa miujiza ya umizimu. Kwa kadiri wanadamu wanavyoukataa ukweli; wanakuwa mawindo ya udanganyifu. TK 322.3
Kosa lingine ni fundisho linalopinga Uungu Wakristo, ikidaiwa kuwa hakuwepo kabla ya kuja hapa duniani. Nadharia hii hukinzana na kauli za Mwokozi wetu kuhusu uhusiano wake na Baba na uwepo wake kabla ya kuja duniani. Huidhoofisha imani katika Biblia kama Ufunuo kutoka kwa Mungu. Kama wanadamu wakiukataa ushuhuda wa Maandiko juu ya Uungu Wakristo, ni bure kuhojiana nao; hakuna hoja, hata iwe nzuri kiasi gani, itakayowashawishi. Hakuna mtu anayelishikilia kosa hili anayeweza kuwa na utambuzi wa kweli Wakristo au juu ya mpango wa Mungu wa ukombozi wa mwanadamu. TK 322.4
Kosa lingine ni imani kuwa Shetani sio kiumbe halisi mwenye nafsi, na kwamba jina hili linapotumika kwenye Maandiko linawakilisha tu mawazo na tamaa mbaya za wanadamu. TK 323.1
Fundisho linalosema kuwa kuja kwa Yesu mara ya pili ni kuja kwa kila mmoja anapokufa ni mbinu ya kuzipotosha akili juu ya kuja kwake na mawingu ya mbinguni. Shetani amekuwa akisema, “Tazama yumo nyumbani” (Angalia 24:23-26) na wengi wamepotea kwa kuukubali udanganyifu huu. TK 323.2
Halafu, wanasayansi wanadai kuwa hakuwezi kuwa na jibu halisi kwa maombi; hili litakuwa ni uvunjaji wa kanuni kwani miujiza ni nadharia tu. Wanasema, ulimwengu unaongozwa na sheria ambazo tayari zipo, na kuwa Mungu mwenyewe hafanyi jambo lolote kinyume na sheria hizo. Na hivyo husema kuwa Mungu anabanwa na sheria zake mwenyewe (kana kwamba sheria za Mungu zingeondoa uhuru wa Mungu). Mafundisho kama hayo yanapingana na ushuhuda wa Maandiko. TK 323.3
Je, miujiza haikutendwa na Kristo na mitume wake?. Mwokozi yule yule yuko tayari kuyasikiliza maombi ya imani kama alivyofanya alipokuwepo kimwili miongoni mwa wanadamu. Wanadamu wanashirikiana na Mungu. Ni sehemu ya mpango wa Mungu kutupatia tunachoomba kwa imani, ambacho hangetupatia kama tusingeomba. TK 323.4