Mafundisho ya uongo miongoni mwa makanisa yanaondoa mipaka iliyowekwa na Neno la Mungu. Wachache; hukoma kuendelea mbele kwa kukataa kanuni moja ya ukweli. Watu walio wengi huweka kando kanuni moja ya ukweli baada ya nyingine mwisho wanageuka kuwa makafiri. TK 323.5
Makosa yatokanayo na teolojia inayopendwa yamezifanya roho nyingi kuwa na nadharia ya kushuku. Ni vigumu kwake kuyakubali mafundisho yanayopingana na hisia za mtu juu ya haki, rehema, na ukarimu. Kwa sababu haya yanaletwa kama mafundisho ya Biblia, anakataa kuyapokea kama Neno la Mungu. TK 323.6
Neno la Mungu limcangaliwa kwa mashaka kwa sababu linaishutumu na kuihukumu dhambi. Wale ambao hawako tayari kulitii wanajitahidi kuyatupilia mbali mamlaka yake. Wengi wanaamua kutoamini ili kuhalalisha kuacha kutimiza wajibu wao. Wengine, kwa kupenda anasa, hawawezi kukamilisha jambo lolote linalohitaji kujikana nafsi; wanapata sifa ya kuwa na hekima ya hali ya juu kwa kuikosoa Biblia. TK 324.1
Wengi wanahisi ni jambo bora kuwa upande wa kutoamini, mashaka, na ukafiri. Lakini nyuma ya mwonekano wa unyofu kutaonekana kujitumainia nafsi na majivuno. Wengi wanafurahia kutafuta kitu fulani ndani ya Maandiko kitakachoikanganya mioyo ya wengine. Baadhi huanza na kutetea uongo kwa sababu tu ya kupenda mabishano. Lakini baada ya kueleza waziwazi kutoamini kwao, huona kuwa ni vema wakiendeleza misimamo yao. Na hivyo wanajiunga na waovu. TK 324.2