Katika Neno lake, Mungu ameweka ushahidi wa kutosha kuonesha kuwa limetoka kwake. Lakini akili zenye ukomo hazina uwezo wa kufahamu kikamilifu makusudi ya Yule Asiye na ukomo. “Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!” Warumi 11:33. Tunaweza kutambua pendo lisilo na mipaka na rehema vikiwa vimeungana na uwezo usio na kikomo. Baba yetu wa mbinguni atatufunulia mambo mengi kwa ajili ya manufaa yetu; zaidi ya hayo tunapaswa kuamini Mkono wa Mwenyezi, Moyo uliojaa upcndo. TK 324.3
Mungu hataondoa visingizio vyote vinavyosabisha kutoamini. Wote wanaotafuta visingizio juu ya mashaka yao watavipata. Na wale wanaokataa kutii hadi kila kipingamizi kimeondolewa, hawataweza kuja kwenye nuru. Moyo ambao haujaongoka una uadui na Mungu. Lakini imani ni uvuvio wa Roho Mtakatifu na itastawi kwa kadiri inavyotunzwa. Hakuna awezaye kuwa na imani imara bila jitihada za makusudi. Ikiwa wanadamu watajiendekeza kuwa wakosoaji bila sababu; mashaka yatapata nguvu zaidi. TK 324.4
Lakini wale wanaoona shaka na kutoamini uhakika wa neema yake hawamheshimUkristo. Hao ni miti isiyozaa, inayouzuia mwanga wa jua usiifikie mimea mingine, idumae na kufa chini ya kivuli chenye baridi. Kazi za maisha ya watu hawa zitakuwa ushuhuda wa daima dhidi yao. TK 324.5
Ipo njia moja tu kwa wale wanaotafuta kwa uaminifu kuwa huru dhidi ya shaka. Badala ya kukitilia shaka wasichokielewa, hebu waitii ile nuru ambayo tayari wanayo na wataipokea nuru kubwa zaidi. TK 325.1
Shetani anaweza kuleta uongo unaolingana kwa karibu sana na ukweli ili awadanganye wale wanaohiari kudanganyika, wanaotamani kuepuka kujitoa kwa ajili ya ukweli. Lakini hawezi kuidhibiti roho moja inayotamani kwa uaminifu, na kwa gharama yoyote, kufahamu ukweli. Kristo ndiye kweli, “Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.” “Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo.” Yohana 1:9; 7:1 TK 325.2
Bwana anaruhusu watu wake wapate majaribu makali, siyo kwa sababu anaifurahia dhiki yao, lakini kwa sababu ni ya lazima kwa ajili ya ushindi wao wa mwisho. Kwa ajili ya utukufu wake, hawezi kuwakinga na majaribu, kwani lengo la majaribu ni kuwatayarisha kwa ajili ya kuvipinga vivutio vyote vya uovu. Watu waovu na maShetani hawawezi kuuondoa uwepo wa Mungu kutoka kwa watu wake endapo wataungama na kuziweka mbali dhambi zao na kuzidai ahadi zake. Kila jaribu, la wazi ama la siri, linaweza kupingwa kwa mafanikio, “Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.” Zekaria 4:6 TK 325.3
“Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?” lPetro 3:13. Shetani anajua vizuri kuwa roho moja dhaifu inayomtii Kristo ina nguvu kupita majeshi ya giza. Kwa hiyo anatafuta kuwavuta askari wa msalaba mbali na ngome yao yenye nguvu, huku akiwavizia, tayari kwa kuwaangamiza wote wanaojihatarisha kwenye uwanja wake. Ni kwa kumtegemea Mungu pekee na kuzitii amri zake zote ndipo tutakuwa salama. TK 325.4
Hakuna mwanadamu aliye salama kwa siku moja ama kwa saa moja asipofanya maombi. Umwombe Bwana akupe hekima ya kulifahamu Neno Lake. Shetani ni stadi wa kunukuu Maandiko, huweka fasiri yake kwenye mafungu ambayo anataka kutufanya tujikwae. Inatupasakujifunza kwa unyenyekevu wa moyo. Wakati ambapo ni lazima tukeshe daima dhidi ya mbinu za Shetani, ni lazima pia tuombe kwa imani bila kukoma: “Na usitutie majaribuni.” Mathayo 6:1. TK 326.1