Wawakilishi wa Papa kwa mara nyingine walihitaji kuwa ulinzi wa Luther uondolewe. “Mto Rhine ni lazima uyapokee majivu yake, kama ulivyoyapokea yale ya John Huss kame moja iliyopita.” 86Ibid. Lakini wakuu wa Ujerumani, pamoja na kuwa waliapa kuwa maadui wa Luther, walipingana na uvunjwaji wa makubaliano hayo mbele ya umma. Walionesha maafa yaliyofuatia kifo cha John Huss. Hawakuthubutu kuruhusu maovu hayo yajirudie huko Ujerumani. TK 106.1
Akitoa jibu juu ya pendekezo la msingi, Charles alisema: “Ingawa heshima na imani ni lazima vipigwe marufuku kwa ulimwengu wote, ni lazima vipate kimbilio kwenye mioyo ya wafalme.” 87Ibid. Maadui wa Luther, ambao ni wa utawala wa Papa, walimtaka awashughulikie wanamatengenezo kama vile Sigismund alivyomshughulikia John Huss. Akiwa na kumbukumbu za hali ilivyokuwa wakati Huss, mbele ya kusanyiko la hadhara, alipoonesha minyororo yake na kumkumbusha mfalme juu ya imani yake iliyokuwa taabuni, Charles V alitamka kuwa, “Sitapenda kufedheheka kama Sigismund.” 88Lenfant, vol. 1, p. 422. TK 106.2
Lakini bado kwa makusudi Charles aliupuuza ukweli uliokuwa unafundishwa na Luther. Hakuweza kuiacha njia ya desturi ili kutembea kwenye njia za ukweli na haki. Kwa sababu baba zake walikuwa wamefanya hivyo, na yeye alipaswa kuutetea utawala wa Papa. Kwa hiyo alikataa kuikubali nuru mbele ya kile alichokuwa amekipokea kutoka kwa baba zake. TK 106.3
Wengi siku hizi wanazing’ang’ania desturi za baba zao. Bwana anapoileta nuru ya ziada wanakataa kuipokea kwa sababu haikupokelewa na baba zao. Hatutakubaliwa na Mungu kwa kuwaangalia baba zetu ili kuamua juu ya wajibu wetu badala ya kulichunguza Neno la Kweli sisi wenyewe. Tunawajibika kwa nuru ya ziada ambayo sasa inatuangazia kutoka kwenye Neno la Mungu. TK 107.1
Uwezo wa Mungu ulizungumza kwa mfalme na wakuu wa Ujerumani kupitia kwa Luther. Roho wake aliwasihi kwa mara ya mwisho ndani ya kusanyiko lile. Kama ilivyokuwa kwa Pilato, kame nyingi zilizokuwa zimepita, ndivyo ilivyokuwa kwa Charles V, aliikubali fahari ya kiulimwengu, akaamua kuiacha nuru ya ukweli. TK 107.2
Mipango dhidi ya Luther ilikuwa imesambaa kwa upana, na kusababisha msisimko katika mji wote. Marafiki wengi, wakifahamu ukatili na udanganyifu wa Kanisa la Roma, waliazimia kuwa Mwanamatengenezo hakupaswa kutolewa kafara. Mamia ya waheshimiwa waliahidi kumlinda. Katika malango ya nyumba, mabango yalibandikwa, baadhi yakimshutumu na mengine yakimuunga mkono Luther. Juu ya mlango mmoja yalibandikwa maandishi haya, “Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana.” Mhubiri 10:16. Shauku ya wengi kumpendelea Luther ilimshawishi mfalme na baraza kwamba jambo lolote lisilokuwa la haki ambalo angeoneshwa Luther lingehatarisha amani ya ufalme na nguvu za enzi yake. TK 107.3