Frederick wa Saxony alizificha kwa uangalifu hisia zake halisi juu ya Mwanamatengenezo. Wakati huo huo alimchunga kwa uangalifu na bila kuchoka, akiziangalia nyendo zake na za maadui zake. Lakini watu wengi hawakujaribu kuzificha hisia zao juu ya huruma yao kwa Luther. Spalatin aliandika kuwa: Chumba kidogo cha Daktari, hakikuwatosha wageni wote waliomtembelea.” 89Martyn, vol. 1, p. 402.Hata wale ambao hawakuyaamini mafundisho yake hawakuweza kujizuia, bali waliustajabia uadilifu uliomwongoza kwenye kifo cha kishujaa kuliko kupingana na dhamiri yake. TK 107.4
Jitihada za dhati zilifanyika ili kupata ridhaa ya Luther kufanya mapatano na Kanisa la Roma. Wakuu na waheshimiwa walimwambia kuwa iwapo alikuwa ameliwekea kanisa na mabaraza hukumu yake mwenyewe, atafukuzwa katika Himaya na hatakuwa na ulinzi wowote. Kwa mara nyingine aliamriwa kujisalimisha kwenye uamuzi wa mfalme. Ndipo hangekuwa na chochote cha kuogopa. Alijibu, “Ninaridhika kwa moyo wangu wote, kwamba mfalme, wakuu, na hata Mkristo wa ngazi ya chini, anapaswa kuichunguza na kuihukumu kazi yangu; lakini kwa sharti moja, kwamba watalitumia Neno la Mungu kuwa kipimo chao. Wanadamu hawana lolote la kufanya ila kulitii.” TK 108.1
Katika mwito mwingine alisema: “Ninaridhika kuondolewa ulinzi wangu. Ninayaweka maisha yangu na nafsi yangu mikononi mwa mfalme, lakini sitalisalimisha Neno la Mungu-kamwe!” 90D’Aubigne, vol. 7, ch. 10. Alitoa tamko juu ya uhiari wake wa kujisalimisha kwenye baraza kuu, lakini kwa sharti kuwa baraza lingetakiwa kufanya uamuzi kwa mujibu wa Maandiko. “Juu ya kile kinacholihusu Neno la Mungu na imani, kila Mkristo ni mwamuzi mzuri kama alivyo Papa, ingawa anaungwa mkono na mamilioni ya mabaraza.” 91Martyn, vol. 1, p. 410 Mwishowe, marafiki na maadui walishawishika kwamba jitihada zaidi za kupatana zingekuwa bure. TK 108.2
Endapo Mwanamatengenezo angekubaliana nao kwa kipengele kimoja, Shetani na majeshi yake wangepata ushindi. Lakini uimara wake usioyumbishwa, ilikuwa ndiyo njia ya kulikomboa kanisa. Mvuto wa mtu huyu mmoja aliyethubutu kufikiri na kutenda yeye mwenyewe, ulileta athari kwa kanisa na kwa ulimwengu, siyo tu wa wakati wake, bali kwa vizazi vyote vijavyo. TK 108.3
Kwa haraka Luther aliamriwa na mfalme kurudi nyumbani. Taarifa hiyo ingefuatana kwa haraka na hukumu yake. Mawingu ya kutisha yalikuwa juu ya njia yake, lakini alipokuwa akiondoka katika mji wa Worms, moyo wake ulijazwa furaha na sifa. TK 108.4
Baada ya kuondoka kwake, akiwa na shauku kuwa uthabiti wake usipotoshwe na kuleta uasi, Luther alimwandikia mfalme kuwa: “Nipo tayari kukutii wewe mtukufu kwa moyo wote, katika heshima na katika kudharauliwa, katika uzima au katika mauti, na bila kuliondoa Neno la Mungu, ambalo kwalo watu wanaishi...yanapohusika mambo ya milele, ni mapenzi ya Mungu kwamba mwanadamu asijisalimishe kwa mwanadamu. Maana kujitoa huko katika mambo ya kiroho ni ibada halisi, na inapaswa kutolewa kwa Mwumbaji peke yake.” 92D’Aubigne, bk. 7, ch. 11. TK 109.1
Akiwa safarini kutoka Worms wakuu wa makanisa walimkaribisha mtawa aliyetengwa, na viongozi wa umma walimheshimu mtu ambaye mfalme alikuwa amemkataa. Alitakiwa kuhubiri, na bila kujali marufuku ya kifalme, alipanda tena kwenye mimbara. Alisema, “Sikuahidi kulifunga minyororo Neno la Mungu na sitafanya hivyo.” 93Martyn, vol. 1, p. 420 TK 109.2
Haikuchukua muda mrefu tangu Luther alipoondoka Worms wakati utawala wa Papa ulipomwamuru mfalme kutoa amri dhidi yake. Luther alikuwa ameshutumiwa kuwa ni, “Shetani mwenyewe katika umbile la mwanadamu akijivalia joho la utawa.” 94D’Aubigne, bk. 7, ch. 11. Mara baada ya hati yake ya ulinzi ikiisha muda wake; watu wote wangekatazwa kumkaribisha, kumpa chakula au kinywaji, kwa maneno au matcndo au kushirikiana naye. Alitakiwa afikishwe mbele ya wenye mamlaka, wafuasi wake pia walipaswa kutupwa gerezani, na mali zao kutaifishwa. Maandiko yake yalipaswa kuangamizwa, na mwisho wale wote ambao wangethubutu kutenda kinyume na amri hii wangejumuishwa kwenye hukumu hiyo. Mjumbe wa baraza la uchaguzi wa Saksoni na wakuu waliokuwa na urafiki na Luther, waliondoka Worms baada ya kuondoka kwake, na amri ya mfalme ilipata idhini ya baraza. Watawala wa Kanisa la Roma walifurahi. Walichukulia kuwa suala la Matengenezo lilikuwa limefungwa. TK 109.3