Mwenendo wa Luther ulifuatiliwa kwa jicho la uangalifu mkubwa, mtu mkweli na mwenye cheo kikubwa aliazimia kumwokoa. Mungu alimpatia Frederick wa Saksoni mpango wa kumlinda Mwanamatengenezo huyu. Katika safari yake kuelekea nyumbani Luther alitenganishwa na wahudumu wake na kwa haraka alipitishwa katika njia ya msituni na kupelekwa kwenye ngome iliyokuwa kule Wartburg, ngome iliyokuwa mahali pweke mlimani. Kufichwa kwake kulifanyika kwa siri sana kiasi kwamba hata Frederick mwenyewe hakuelewa namna alivyokuwa amepelekwa huko. Kutojua kwake huku kulikuwa kumepangwa ili asitoe siri. Alipojiridhisha ya kuwa Mwanamatengenezo huyo alikuwa salama, alitulia. TK 110.1
Majira ya kuchipua, majira ya joto, na mavuno yalipita na kipindi cha baridi kikaja na Luther alibakia kuwa mfungwa. Aleander na wafuasi wake walishangilia kwa furaha. Nuru ya Injili ilionekana kwamba ingezimwa. Lakini nuru ya Mwanamatengenezo huyu ilipaswa kuendelea kuangaza kwa miali yenye mng’ao mkubwa. TK 110.2