Baada ya miaka mitatu Zwingli aliitwa kwenda kuhubiri kwenye kanisa kuu la jimbo kule Zurich, mji muhimu katika shirikisho la Uswisi. Mvuto ambao ungewekwa hapa ungekuwa na mguso. Maaskofu walitangulia kumwelekeza wajibu wake: TK 114.3
“Utafanya kila jitihada kukusanya mapato ya baraza hili bila kuacha chochote kilicho kidogo...Ukusanye kwa juhudi mapato yanayotokana na wagonjwa, makundi ya watu, na kutoka kwa kila maagizo ya kanisa kwa ujumla. Kwa ajili ya kutoa sakramenti, kuhubiri na kulitunza kundi...unaweza kumtumia mtu mwingine, na hasa kuhubiri.” 100Ibid., bk. 8, ch. 6. Zwingli alisikiliza kwa makini agizo hili na kujibu, “Kwa muda mrefu sana maisha ya Kristo yalikuwa yamefichwa kwa watu. Nitahubiri Injili yote ya Mtakatifu Mathayo...Ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu na sifa kwa Mwanawe, kwa wokovu halisi wa roho za watu, na kuwajenga katika imani ya kweli, ili niiweke wakfu huduma yangu.” TK 114.4
Watu walifurika kwa idadi kubwa kumsikiliza. Alianza huduma yake kwa kuzifungua Injili, huku akifafanua juu ya maisha, mafundisho, na kifo cha Kristo. “Ni shauku yangu kuwaongoza ninyi kwa Kristo,- kwenda kwa Kristo, chimbuko la kweli la wokovu.” Watu maarufu katika nchi, wanazuoni, wasanii, na wakulima, waliyasikiliza maneno yake. Bila hofu yoyote, alikemea uovu na ufisadi wa wakati huo. Wengi walirudi nyumbani kutoka katika kanisa lile kuu wakimtukuza Mungu. “Mtu huyu,” watu walisemezana, “ni mhubiri wa ukweli. Atakuwa Musa wetu kutuongoza kutoka katika giza hili la Misri.” 101Ibid. TK 115.1
Baada ya muda fulani upinzani uliinuka. Watawa walianza kumshambulia vikali Zwingli kwa dhihaka na vicheko vya dharau, na wengine wakamtendea jeuri na vitisho. Lakini Zwingli aliyavumilia yote. TK 115.2
Mungu anapokusudia kuzivunja pingu za ujinga na mapokeo potovu, Shetani hufanya kazi kwa nguvu kubwa kuwafunika wanadamu kwa giza na kuikaza minyororo yao kwa uthabiti zaidi. Kwa nguvu mpya, Kanisa la Roma liliendelea kufungua masoko yake katika himaya yote ya Ukristo, likitoa msamaha wa dhambi kwa pesa. Kila dhambi ilikuwa na bei yake, na watu walipewa leseni za kufanya kila aina ya udhalimu ili mradi tu hazina ya kanisa ilikuwa imejaa vyema. Kwa jinsi hiyo vuguvugu hizi mbili zilisonga mbele- Kanisa la Roma likiruhusu dhambi na kuifanya kitega uchumi chake na Wanamatengenezo wakiishutumu dhambi na kuwaelekeza watu kwa Kristo kama kitulizo na mkombozi wao. TK 115.3