Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    50 — Katikati ya Mitego

    Katika muda wote wa sikukuu Yesu alikuwa akizungukwa na wapelelezi, kila siku mipango mipya ilipangwa jinsi ya kumwangamiza. Makuhani na wakuu walipanga namna ya kumkomesha kwa nguvu. Siku ya mwisho ya mkutano, walidai kutaka kujua kuwa alikuwa anafundisha kwa uwezo gani?TVV 258.1

    Yesu alijibu: “Mafundisho yangu hayatokani na mimi mwenyewe, ila yatokana na yeye aliyenituma. Mtu akitaka kufanya mapenzi yake, atajua kuwa mafundisho yangu hutoka kwa Mungu, au ni mawazo yangu tu. Yohana 7:16, 17. Alisema kuwa kuona ukweli na kuuelewa hutokana na dhamiri wala si mawazo tu. Ukweli hutaka utambuzi wake utoke katika dhamiri. Ni kazi ya neema ya moyoni. Ukubali wake hutaka mtu aamue kuachana na kila dhambi inayofunuliwa na Roho wa Mungu. Kunatakiwa kuacha vitu vyote na mazoea yote yanayopingana na kanuni za ukweli. Wanaojitoa kwa Mungu namna hiyo, watajua mtu asemaye mambo ya Mungu, na mtu asemaye mambo yake’ mwenyewe. Mafarisayo walikuwa hawatafuti kweli, ila walikuwa wakitafuta sababu za kuukwepa ukweli, na hiyo ndiyo ilikuwa asili ya kutofahamu maneno ya Yesu, na mafundisho yake.TVV 258.2

    Yesu alisema: “Asemaye mambo yake mwenyewe, hutafuta utukufu wake, lakini atafutaye utukufu wake aliyemtuma huwa wa kweli, wala hana uwongo.” Roho ya ubinafsi husaliti ukweli. Lakini Kristo alikuwa akitafuta utukufu wa Mungu. Huu ndio ulikuwa uthibitisho wake alipokuwa akiufundisha ukweli.TVV 258.3

    Yesu aliwathibitishia Marabi uungu wake kwa njia ya kusoma mioyo yao na kuona yaliyomo. Walikuwa wakipanga kumwangamiza, ambayo ni kuvunja sheria, ambayo wanajidai kuitetea. Yesu alisema: “Je, Musa hakuwapa sheria?” Na hivyo hakuna hata mmoja aishikaye. Kwa nini mnatafuta kuniua?” Maneno haya yalifanana kama kimuli kikali kilichomulika mioyoni mwao na kuyaona maovu waliyoficha humo. Maovu hayo walikuwa karibu kuyatenda, yaani kumwua Yesu. Kwa muda waliona kuwa wanapingana na Mungu. Lakini walikaidi tu, huku wakificha kusudi lao la kuua na kufanya uzandiki kuwa hawana kusudi hilo, wakisema: “Una wazimu; nani anataka kukuua?”TVV 258.4

    Kwa kujifanya wazandiki, Kristo hakujali maneno hayo. Ila aliendelea kusema kuwa kazi yake ya kuponya aliyofanya huko Bethsaida siku ya sabato, ilishuhudia kuwa ni ya haki ingawa waliitafsiri vibaya, wala sivyo ilivyo. Ilidhihirika kwamba hawajui sabato inavyotunzwa. Kufuata sheria ni kwamba kila mtoto nwanamume lazima atahiriwe siku ya nane, lakini siku hiyo ikiangukia siku ya sabato, kitendo hicho lazima kitendeke. Je, hakuna uhalali wa kutuponya mtu siku ya sabato? Aliwaonya kwa kusema “Msihukumu hukumu ya macho, bali hukumu ya haki.” Wakuu walinyamaza kimya.TVV 259.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents