Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kayafa Katibu Kuamini

    Wazo kwamba watu wote watasimama mbele ya hukumu ya kiti cha Mungu na kupokea kila kinachostahili matendo waliyotenda lilikuwa tishio kwa Kayafa. Mawazoni mwake aliona siku hiyo ya hukumu ya mwisho. Kwa muda mfupi aliona makaburi yakiwatoa wafu pamoja na siri alizodhani kuwa hazitajulikana milele. Akajisikia kana kwamba Jaji Mkuu alikuwa anasoma moyo wake na kutoboa siri zilizodhaniwa zimefichika katika wafu.TVV 397.5

    Kayafa alikuwa amekana ufufuo wa wafu, hukumu, na maisha ya baadaye. Sasa alikuwa kana kwamba amepata wazimu. Akirarua mavazi yake, alitamka kuwa mtu huyu anastahili kuhukumiwa kwa kukufuru; “Tuna haja gani tena ya mashahidi?” “Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake; mwaonaje ninyi?” Na wote wakamhukumu kuuawa, Kayafa alighadhabika kwa kule yeye kuyaamini maneno ya Kristo, na badala ya kurarua moyo wake na kukiri kuwa Yesu alikuwa Masihi, akararua Mavazi yake ya kikuhani katika jitihada ya kupinga. Kitendo hiki kilikuwa na maana kubwa. Katika kuhakikisha kuwa Kristo anahukumiwa kifo, kuhani mkuu alikuwa amejihukumu mwenyewe. Chini ya sheria ya Mungu iliyohusu ukuhani alikuwa hafai kuwa kuhani. Alikuwa amejihukumu mwenyewe stahili ya kifo.TVV 398.1

    Kuhani Mkuu hakupaswa kurarua mavazi yake ya ukuhani. Sheria ya Walawi ilikataza kabisa kuhani kurarua vazi lake. Kristo alikuwa ametoa agizo hilo kwa Musa. (Tazama Walawi 10:6). Mwanadamu aliye na kikomo cha maisha anaweza kurarua moyo wake kwa kujuta kwa kosa lo lote. Lakini vazi la kikuhani haliraruliwi kamwe, maana hili huwakilisha vitu vya mbinguni, na kwa hiyo likiraruliwa huvinajisi. Kuhani mkuu yeyote anayethubutu kuhudumu na hali vazi lake limeraruliwa huwa amejitenga mbali na Mungu. Jambo lililofanywa na Kayafa lilionyesha ufedhuli na upungufu wa kibinadamu.TVV 398.2

    Kwa kuyararua mavazi yake, ya ukuhani Kayafa, alibatilisha sheria za Mungu, kwa kufuata mapokeo ya kibinadamu. Kanuni ya wanadamu ilisema kuwa mtu akikufuru, kuhani angerarua mavazi yake katika kuonyesha chuki kwa dhambi na asiwe na kosa. Hivyo sheria ya Mungu ilibatilishwa na mapokeo ya wanadamu. Lakini katika kitendo hiki, yeye mwenyewe alikuwa anatenda kosa la kufuru.TVV 398.3

    Kayafa aliporarua vazi lake; kitendo hicho kilikuwa na maana ya nafasi itakayochukuliwa baadaye na taifa la Wayahudi mbele za Mungu. Wayahudi walikuwa wamemkataa yule ambaye alikuwa asili ya mifano ya uhakika wa mategemeo yao yote. Waisraeli walikuwa wamejitenga na Mungu. Na huenda Kuhani Mkuu alirarua vazi lake kujihofia binafsi na kwa ajili ya taifa lote.TVV 398.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents