Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini la Vizazi Vyote - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    2 — Watu Ambao Wangalipokea

    Kwa muda wa miaka elfu moja na zaidi, Wayahudi walikuwa wakimtazamia Yesu aje. Walakini alipokuja hawakumfahamu. Hawakumwona kuwa anao uzuri wowote hata wamtamani. Isaya 53:2. “Alikuja kwa watu wake, na watu wake hawakumpokea.” Yohana 1:11.TVV 14.1

    Mungu aliwachagua Waisraeli kati ya mataifa, ili wahifadhi mifano na unabii vinavyoelekeza kuja kwa Mwokozi ulimwenguni. Waebrania walipaswa kumdhihirisha Mungu katika mataifa. Katika kumwita Abrahamu, Bwana alisema, “Katika wewe jamaa zote za dunia zitabarikiwa.” Mwanzo 12:3. Bwana alitangaza kwa njia ya nabii Isaya kwa watu wote.” Isaya 56:7.TVV 14.2

    Lakini Waisraeli walikazana na ufahari wa dunia tu, wakafuata njia za mataifa ambayo ni makafiri. Mungu aliwatumia ujumbe wa maonyo kwa njia ya manabii, lakini ilikuwa kazi bure. kila mara waliposhtushwa na kurudi kwa Mungu muda mfupi, baadaye waliasi vibaya tena.TVV 14.3

    Kama Waisraeli wangalikuwa waaminifu kwa Mungu, angaliwafanya wawe wakuu kuliko mataifa yote. Mataifa ambayo yangesikia amri hizi wangalisema, “Kweli taifa hili kubwa, ni taifa lenye hekima na lenye ufahamu.” Torati 26:19; 4:6.TVV 14.4

    Lakini kwa ajili ya kutokuwa waaminifu kwao, makusudi ya Mungu kwao yaligeuka kuwa taabu na mateso. Walipelekwa Babeli, na kutawanywa katika mataifa yote. Walipoomboleza kwa ajili ya kuteketezwa kwa hekalu, kwa njia yao elimu ya Mungu iliwafikia mataifa makafiri. Ibada za kikafiri ziliachwa na kuigiza zile za Mungu. Waebrania waliwaonyesha njia iliyoagizwa na Mungu. Wenye elimu wengi walijifunza njia za Mungu, na kuona ahadi za kuja kwa Mkombozi.TVV 14.5

    Watu wengi katika mataifa hayo walikotawanywa, walipoinuka kuushambulia ukweli, watu hawa waaminifu walifika mbele ya wafalme na watawala, ili kuifikisha nuru ya kweli. Kwa njia hii wafalme wakuu walimkiri Mungu na uweza wake, ambaye watumwa wa Kiebrania humwabudu.TVV 14.6

    Wakati wa karne zilizofuata kutekwa kwenda Babeli Waisraeli walipona kuabudu sanamu, na imani yao iliimarika, wakawa watiifu kwa Mungu. Lakini wingi wa watu hali ya ubinafsi ilidumu kuwatawala. Walimtumikia Mungu kama njia ya kujipatia ukuu wa taifa. Hawakuwa nuru ya ulimwengu tena, bali walijitenga na kujifungua ili wasipate majaribu. Mungu aliwazuia kuungana na mataifa ili wasipotoshwe. Lakini fundisho hili lilipotoshwa kabisa.TVV 15.1

    Walidhani ni kujenga ukuta imara kati yao na wakafiri. Wayahudi walikuwa na wivu, kwamba Bwana asiwahurumie mataifa kama wao.TVV 15.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents