Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kufungwa kwa Rehema

    Wakati ujumbe wa malaika wa tatu ulipokuwa ukifungwa, uweza wa Mungu ulikuwa juu ya watu wake. Walikuwa wamekamilisha kazi yao na sasa walikuwa tayari kwa ajili ya saa ya jaribio iliyokuwa mbele yao. Walikuwa wamepokea mvua ya masika, au burudiko kutoka katika kuwapo kwa B wana, na ushuhudaulio hai ulikuwa umehuishwa. Onyo kuu la mwisho lilisikika kila mahali, na lilikuwa limewachochea na kuwakasirisha wakazi wa dunia ambao hawakuwa tayari kuupokea ule ujumbe.PLK 125.2

    Malaika walikuwa wakifanya haraka kwenda na kurudi kutoka mbinguni. Malaika mwenye kidau cha wino wa mwandishi kiunoni alirudi kutoka duniani na kutoa taarifa kwa Yesu kuwa kazi yake ilikuwa imekamilika, na kwamba waliookolewa walikuwa wamehesabiwa na kutiwa muhuri. Ndipo Yesu, ambaye wakati huo alikuwa akihudumu mbele ya sanduku la agano lililo na Amri Kumi, alitupa chini chetezo. Akainua mikono yake juu, na kwa sauti kuu alisema, “Imekwisha.” Na malaika wote wakaweka chini taji zao wakati Yesu alipokuwa akitoa tangazo hili lenye kutisha, “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.” Ufunuo 22:11.PLK 125.3

    Kesi ya kila mtu ilikuwa imekwisha kuhukumiwa kwa uzima au mauti. Wakati Yesu alipokuwa akihudumu katika patakatifu, hukumu ilikuwa ikiendelea kwa watakatifu waliokufa, na kisha kwa watakatifu walio hai. Kristo alikuwa amepokea ufalme wake, akiisha kufanya upatanisho kwa ajili ya watu wake na kufuta dhambi zao. Raia wa ufalme walikuwa wamebainishwa. Arusi ya Mwana-Kondoo ilikamilishwa. Na ufalme, na ukuu wa ufalme chini ya mbingu yote, alipewa Yesu na warithi wa wokovu, na Yesu alikuwa atawale kama Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.PLK 126.1

    Yesu alipokuwa akitoka katika patakatifu mno, kengele za vazi lake zilisikika; na alipokuwa akiondoka, wingu la giza liliwafunika wakazi wa dunia. Ndipo hapakuwapo tena na mpatanishi baina ya wanadamu wenye hatia na Mungu aliyekosewa. Wakati Yesu alipokuwa akisimama kati ya Mungu na wanadamu wenye hatia, kizuizi kilikuwa juu ya watu, lakini alipotoka katikati ya wanadamu na Baba, kizuizi kile kiliondolewa, na Shetani alikuwa na udhibiti wote juu ya wale waliokataa kutubu.PLK 126.2

    Isingewezekana mapigo kumwagwa wakati Yesu alipokuwa akihudumu katika patakatifu, lakini kazi yake pale ilipomalizika na utetezi wake kukoma, hakuna cho chote cha kuzuia ghadhabu ya Mungu, nayo inakuja kwa ukali juu ya kichwa kisichositiriwa cha mdhambi mwenye hatia, ambaye alipuuzia wokovu na kuchukia maonyo. Katika saa ile ya kuogofya, baada ya kufungwa kwa upatanisho wa Yesu, watu wa Mungu, ambao Biblia inawaita watakatifu, walikuwa wakiishi mbele za Mungu bila kuwa na mtetezi. Kila kesi ilikuwa imeamuliwa, na kila kito cha thamani kuhesabiwa.PLK 126.3

    Kuchelewa Mno!-Kisha Yesu alivua mavazi yake ya kikuhani na kuvaa joho la kifalme. Juu ya kichwa chake palikuwa na taji nyingi sana, taji juu ya taji. Akiwa amezungukwa na jeshi la malaika, aliondoka mbinguni. Mapigo yalikuwa yakianguka juu ya wakazi wa dunia. Baadhi walimkana Mungu hadharani na kumlaani. Wengine walikimbia kwa watu wa Mungu na kuomba kufundishwa jinsi ya kuepuka hukumu zake. Lakini watakatifu hawakuweza kuwasaidia kitu cho chote. Chozi la mwisho kwa ajili ya wenye dhambi lilikuwa limemwagwa, ombi la mwisho la kuugua limekwisha kutolewa, mzigo wa mwisho kubebwa, na onyo la mwisho lilikuwa limetolewa. Sauti tamu ya rehema haikuwa inawaalika tena. Wakati watakatifu, pamoja na mbingu yote, walipokuwa wanashughulikia wokovu wao, wao wenyewe hawakuwa wakijali. Uzima na mauti viliwekwa mbele yao. Wengi walitamani uzima lakini hawakufanya juhudi yo yote kuupata. Hawakuchagua uzima, na sasa haloikuwa na damu ya upatanisho ya kumtakasa mwenye hatia, hakuna Mwokozi mwenye huruma wa kuwaombea na kusihi, “Mhurumie, mhurumie mwenye dhambi kwa kitambo kidogo.” Mbingu yote iliungana na Yesu pale waliposikia maneno ya kuogofya, “Imetimia! Imekwisha!” mpango wa wokovu ulikuwa umekamilika, lakini ni wachache tu waliokuwa wamechagua kuukubali. Na ile sauti tamu ya rehema ilipokuwa ikififia na kutoweka, hofu na utisho viliwashika waovu. Kwa uwazi wa kutisha walisikia maneno, “Mmechelewa mno! Mmechelewa mno!” Wengi wa waovu walikasirishwa mno na mateso yaliyotokana na madhara ya mapigo kwa maumivu ya kutisha. Wazazi walikuwa wakiwalaumu watoto wao kwa uchungu, na watoto waliwalaumu wazazi wao, akina kaka waliwalaumu dada zao na akina dada waliwalaumu kaka zao. Sauti kubwa za kuomboleza zilisikika kutoka kila upande: “Ni wewe ndiwe ulinizuia nisipokee ukweli ambao ungeliniokoa kutokana na saa hii ya kutisha.” Watu waliwageukia wachungaji wao kwa chuki kali na kuwashutumu, wakisema, “Hamkutuonya. Mlituambia kuwa dunia yote ingeongoka, na mkasema kwa sauti kuu, Amani, amani, ili kunyamazisha hofu iliyokuwa imeamshwa. Hamkutwambia kuhusu saa hii; na wale waliotuonya juu yake mliwatangaza kuwa ni wazushi na watu waovu, ambao wangetuharibu.” Lakini wachungaji wale hawakuepuka ghadhabu ya Mungu. Maumivu yao yalikuwa mara kumi zaidi kuliko yale ya watu wao.PLK 126.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents