Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura ya 3—Msiba

  Sura hii imejengwa katika Mwanzo 2:15-17, na Mwanzo 3.

  Katikati ya bustani, karibu na mti wa uzima, ulisimama mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mungu aliumba mti huu mahususi kwa ajili yao ili kutoa ushahidi wa utii, imani, na upendo wao kwake. Bwana aliwaamuru wazazi wetu wa kwanza kutokula matunda ya mti huu, wasije wakafa. Aliwaambia kuwa waweza kula matunda toka miti yote ya bustani isipokuwa mmoja tu, na ikiwa watakula matunda ya mti huo, hakika watakufa.PLK 14.1

  Wakati Mungu alipowaweka Adamu na Hawa katika ile bustani nzuri, walikuwa na kila kitu ambacho wangeweza kukihitaji kwa ajili ya furaha yao. Lakini katika mipango yake ya hekima kamili, Mungu alichagua kuujaribu uaminifu wao kabla hajawafanya kuwa salama milele. Shetani aliruhusiwa kuwajaribu. Iwapo wangelishinda jaribu lile, wangepata kibali cha Mungu na malaika wa mbinguni milele zote.PLK 14.2

  Shetani alishangazwa na hali yake mpya. Furaha yake ilikuwa imeondoka. Aliwaangalia malaika ambao, kama yeye, walikuwa na furaha mno hapo mwanzo, lakini ambao walifukuzwa kutoka mbinguni pamoja naye. Miongoni mwao mlikuwa na migogoro, kutokuelewana, na shutuma kali. Kabla ya uasi wao mambo haya hayakufahamika kabisa kule mbinguni. Shetani sasa aliona matokeo ya kutisha ya uasi wake.PLK 14.3

  Iwapo sasa angepata tena nafasi ya kuweza kuwa kama alivyokuwa wakati alipokuwa msafi, mkweli, na mwaminifu, kwa furaha angeweza kusalimisha madai yake ya mamlaka. Lakini alikuwa amepotea! Uasi wake usio na msingi na wa kijeuri ulimweka mbali mno na ukombozi!PLK 14.4

  Lakini kulikuwa na zaidi. Alikuwa amewaongoza wengine katika uasi na hali hiyo hiyo ya kupotea pamoja na yeye-yaani malaika, ambao kamwe walikuwa hawajafikiria kuhoji mapenzi ya Mbingu au kukataa utii kwa sheria ya Mungu hadi pale alipoiweka fikira hiyo katika akili zao. Sasa walikuwa katika machafuko kutokana na matumaini yaliyovunjika. Badala ya wema kuongezeka, walikuwa wakipitia matokeo ya kuhuzunisha ya kutotii na kudharau sheria ya Mungu.PLK 15.1

  Shetani Atafakari Njia Yake-Shetani alitete-meka alipoiangalia kazi yake. Akiwa peke yake, aliwaza kuhusu siku zilizopita, wakati uliopo, na mipango yake ya siku za usoni. Katika uasi wake, hakuwa na sababu ya kwenda njia aliyoiendea, na kwa namna isiyoweza kuponyeka alikuwa amejiangamiza japo si yeye peke yake bali pia safu kubwa mno ya malaika, ambao bado wangeweza kuwa wanaendelea kupata furaha mbinguni kama wangedumu kuwa wakweli. Sheria ya Mungu inaweza kuhukumu, lakini haina uwezo wa kusamehe.PLK 15.2

  Badiliko hili kuu la cheo halikuongeza upendo wake kwa Mungu au kwa sheria yake ya hekima na haki. Shetani aliposhawishika kikamilifu kuwa hakukuwako na uwezekano wa yeye kurejeshwa katika kukubaliwa na Mungu, basi alidhihirisha kusudi lake ovu kwa chuki iliyozidi na hasira kali mno.PLK 15.3

  Mungu alifahamu kuwa uasi wa kudhamiria jinsi ile usingezimika wenyewe. Shetani angebuni njia za kuwachokoza malaika wa mbinguni na kuonesha dharau kwa mamlaka yake. Maadamu hakuwa anaruhusiwa kuingia katika malango ya mbinguni, angeweza kuvizia pale penye malango, ili kuwadhihaki na kujaribu kuhojiana nao walipokuwa wanaingia ndani na kutoka nje. Angejitahidi kuharibu furaha ya Adamu na Hawa. Angefanya kila juhudi kuwachochea kuasi, huku akifahamu kuwa jambo hili lingesababisha huzuni mbinguni.PLK 15.4

  Njama Dhidi ya Jamii ya Wanadamu - Shetani aliwaambia wafuasi wake kuhusu mipango yake ya kutaka kuwavuta mbali kutoka kwa Mungu Adamu na Hawa waliokuwa waadilifu. Kama kwa njia fulani angeweza kuwadanganya kutomtii, Mungu angeweka njia fulani ya kuwasamehe, ndipo yeye pamoja na malaika wote walioanguka wangetumia fursa hiyo kudai kuwa na sehemu katika rehema ya Mungu pamoja na Adamu na Eva.PLK 16.1

  Iwapo hili lingeshindikana, wangeweza kujiunga pamoja na Adamu na Hawa, kwa sababu kama wangelivunja sheria ya Mungu, wao pia wangekabiliwa na ghadhabu ya Mungu, kama Shetani na malaika zake. Uvunjaji huu wa sheria ungewaweka, wao pia, katika hali ya uasi, kama Shetani na malaika zake, ambao kwa sababu hiyo wangejiunga na Adamu na Hawa, kuimiliki Edeni, na kuichukua kama maskani yao. Na iwapo wangepata nafasi ya kuufikia mti wa uzima uliokuwa katikati ya bustani, nguvu yao, waliwaza, ingeweza kuwa sawa na ile ya malaika watakatifu, na hivyo hata Mungu asingeweza kuwafukuza.PLK 16.2

  Adamu na Hawa Waonywa-Mungu aliwaku- sanya malaika ili wapate kuchukua hatua ya kuzuia uovu uliokuwa unatishia kutokea. Iliamuliwa katika baraza la mbinguni kuwa malaika watembelee Edeni na kumwonya Adamu kuwa alikabiliwa katika hatari kutoka kwa adui yule.PLK 16.3

  Malaika waliwapa Adamu na Hawa kisa cha kuhuzunisha cha uasi na anguko la Shetani. Ndipo kwa uwazi waliwajulisha kuwa mti wa ujuzi uliwekwa bustanini kama njia kwao ya kuahidi utii na upendo wao kwa Mungu. Malaika watakatifu wangeweza tu kudumisha hali yao ya juu na ya furaha kwa sharti la utii, na wao- Adamu na Hawa, pia hali yao ilikuwa ni kama hiyo. Wangeweza kuitii sheria ya Mungu na kuwa na furaha isiyoelezeka, au kutokutii na kupoteza hadhi yao ya juu na kuingia kwenye kukatishwa tamaa kusiko na matumaini.PLK 16.4

  Malaika waliwaambia Adamu na Hawa kwamba malaika aliyetukuka zaidi ya wote, aliyemfuatia Kristo kwa cheo, alikataa kuitii sheria ambayo Mungu aliiweka ili kuwaongoza viumbe wa mbinguni. Uasi huu, walisema, ulisababisha vita mbinguni, ambavyo vilisababisha mwasi huyo kufukuzwa kutoka mbinguni, na kila malaika aliyeungana na kiongozi huyu katika kuhoji mamlaka ya Yehova mkuu alifukuzwa kutoka mbinguni. Malaika huyu aliyeanguka sasa alikuwa ni adui wa kila kitu ambacho Mungu pamoja na Mwana wake walikipenda sana.PLK 17.1

  Waliwaambia kuwa Shetani alikusudia kuwadhuru, na kwamba ilikuwa muhimu kwao kuwa macho, kwa sababu wangeweza kukutana na adui huyu aliyeanguka. Asingeweza kuwadhuru, hata hivyo, wakati ambapo wangedumu kulitii agizo la Mungu, kwa sababu, kama ingelazimu, kila malaika kutoka mbinguni angekuja kuwapa msaada kuliko kuruhusu apate kuwadhuru kwa namna yo yote ile. Lakini iwapo wasingelitii agizo la Mungu, ndipo Shetani angeweza kuwa na uwezo wa kuwaudhi, kuwafadhaisha na kuwataabisha tangu wakati ule na kuendelea. Kama wangedumu kuwa imara dhidi ya madokezo ya awali ya uovu kutoka kwa Shetani, wangekuwa salama kama malaika wa mbinguni walivyo.PLK 17.2

  Lakini iwapo wangeshindwa na mjaribu, Mungu yule yule ambaye hakuwaachilia malaika waliotukuka asingewaachilia wao. Lazima wapate adhabu ya dhambi yao, kwa kuwa sheria ya Mungu ilikuwa ni takatifu kama yeye mwenyewe alivyo, na alihitaji utii wa dhati kutoka kwa wote walio mbinguni na duniani.PLK 17.3

  Malaika walimwonya Hawa asije akajitenga kutoka kwa mume wake katika kazi zake ndani ya bustani, kwa sababu angeweza kukutana na adui huyu aliyeanguka. Kama wangetengana, wangekuwa katika hatari kubwa zaidi kuliko pale walipokuwa pamoja.PLK 17.4

  Adamu na Hawa waliwahakikishia malaika wale kuwa kamwe wasingeacha kuitii amri ya wazi ya Mungu. Hata hivyo, ilikuwa ni furaha yao kubwa mno kutenda mapenzi yake.PLK 18.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents