Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Pambano Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura ya 19—Nuru Gizani

    Kazi ya Mungu duniani inaonesha, kutoka zama moja hadi zama nyingine, kufanana sana katika kila matengenezo makubwa au vuguvugu la kidini. Kanuni za Mungu za kushughulika na watu ni zile zile daima. Matukio muhimu ya sasa yana ufanani na matukio yaliyofanyika wakati uliopita, na uzoefu wa kanisa katika zama zilizopita una masomo yenye thamani kubwa kwa ajili ya wakati wetu.PKSw 263.1

    Hakuna ukweli ambao umefundishwa kwa uwazi mkubwa zaidi katika Biblia kuliko ukweli kuwa Mungu, kwa njia ya Roho Mtakatifu, ana watumishi Wake mahsusi duniani katika vuguvugu kubwa la kupeleka mbele kazi ya wokovu. Watu ni vyombo katika mkono wa Mungu, ambavyo anavitumia kutimiza makusudi Yake ya neema na rehema. Kila mtu ana sehemu ya kufanya; kila mtu anapewa kiasi fulani cha nuru, kinachokidhi mahitaji ya wakati wake, na kinachotosha kumwezesha atekeleze kazi ambayo Mungu amempa aifanye. Lakini hakuna mtu, hata kama amepewa na Mbingu heshima kubwa kiasi gani, ambaye amewahi kuwa na ufahamu kamili wa mpango mkuu wa ukombozi, au hata kuelewa kikamilifu kusudi la Mungu katika kazi kwa ajili ya wakati. Wanadamu hawafahamu kikamilifu kile ambacho Mungu anaweza kukitimiza kupitia kazi ambayo amewapa kuifanya; hawajui, katika vipengele vyake vyote, ujumbe ambao wanautangaza katika jina Lake.PKSw 263.2

    “Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikilia upeo wa huyo Mwenyezi?” “Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.” “Mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi; nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado” (Ayubu 11:7; Isaya 55:8, 9; 46:9, 10).PKSw 263.3

    Hata manabii waliopata upendeleo maalumu wa mwangaza maalumu wa Roho hawakuelewa kikamilifu maana ya ufunuo waliopewa. Maana ya ujumbe wao ilipaswa kufunuliwa kizazi hata kizazi, kwa kadiri watu wa Mungu walivyohitaji mafundisho yaliyomo katika ujumbe huo.PKSw 263.4

    Petro, akiandika kuhusu wokovu ulioelezwa kupitia injili, anasema kuhusu wokovu huu “manabii walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza, ambao walitabiri habari za neema itakayowafikia ninyi. Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo. Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu” (1 Petro 1:10-12).PKSw 263.5

    Hata hivyo, ingawa manabii haewakuelewa kila kitu walichofunuliwa, walifanya bidii kubwa kuhakikisha kuwa wanapata nuru yote ambayo Mungu alipenda kuwafunulia. “Walitafuta-tafuta na kuchunguzachunguza,” “walitafuta, au walichunguza ni aina gani ya wakati Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao aliridhia” Ni somo kubwa kiasi gani watu wa Mungu wa kizazi cha Kikristo wanapaswa kujifunza, ambao kwa ajili ya faida yao unabii ulitolewa kwa watumishi Wake! “Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu” Shuhudia wale watu watakatifu wa Mungu wakitafu-tafuta na “kuchuguza-chunguza kwa bidii” kuhusiana na ufunuo waliopewa kwa ajili ya vizazi ambavyo vilikuwa bado havijazaliwa. Hebu angalia tofauti kati ya bidii yao takatifu na uzembe na kutojali ambako watu waliofadhiliwa wa vizazi vya baadaye wanachukulia karama hii ya Mbinguni. Karipio kubwa kiasi gani kwa kutojali kwa watu wanaopenda starehe, wanaopenda ulimwengu ambao wanaridhika kusema kuwa unabii hauwezi kueleweka!PKSw 264.1

    Ingawa akili finyu za wanadamu haziwezi kupenya mashauri yaYule Asiye na Kikomo, au kuelewa kikamilifu utekelezaji wa makusudi Yake, pamoja na hayo ni kwa sababu ya kosa fulani au kutokujali kwao kunakofanya waelewe kidogo sana ujumbe wa Mbinguni. Siyo mara chache akili za watu, na hata za watu wa Mungu, zinapofushwa na maoni ya wanadamu, mapokeo na mafundisho ya uongo ya wanadamu, kiasi ambacho wanaweza kushika kidogo sana mambo makuu ambayo Mungu ameyafunua katika neno Lake. Hivyo ndivyo wanafunzi wa Kristo walivyokuwa, hata wakati Mwokozi alipokuwa bado yuko pamoja nao kimwili. Akili zao zilikuwa zimegubikwa na dhana iliyokuwa imeenea na kukubaliwa na wengi kuwa Masihi angekuwa mfalme wa kidunia, ambaye angeiinua Israeli juu na kuisimika kwenye kiti cha enzi cha himaya ya ulimwengu wote, na matokeo yake hawakuelewa maana ya maneno Yake yaliyotabiri mateso Yake na kifo Chake.PKSw 264.2

    Kristo Mwenyewe alikuwa amewatuma wakatangaze ujumbe kuwa: “Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili” (Marko 1:15). Ujumbe ule ulikuwa umejengwa juu ya unabii wa Danieli 9. Majuma sitini na mbili yalitangazwa na malaika kuwa yangeishia wakati wa “Masihi Mfalme,” na kwa matumaini makubwa na matarajio yenye furaha wanafunzi walingojea uanzishwaji wa ufalme wa Masihi katika jiji la Yerusalemu kuitawala dunia yote.PKSw 264.3

    Walihubiri ujumbe waliopewa na Kristo, japokuwa hata wao wenyewe hawakuelewa maana ya ujumbe waliouhubiri. Wakati mahubiri yao yalikuwa yamejengwa juu ya Danieli 9:25, hawakuona, katika aya inayofuata katika sura hiyo hiyo, kuwa Masihi angekatiliwa mbali. Tangu kuzaliwa kwao mioyo yao ilikuwa imekitwa juu ya utukufu uliotarajiwa wa ufalme wa dunia, na matarajio haya yalipofusha ufahamu wao kuhusu vipengele mbalimbali vya unabii na maneno ya Kristo.PKSw 264.4

    Walitekeleza majukumu yao ya kuwasilisha kwa taifa la Kiyahudi wito wa rehema, na ndipo, wakati waliotarajia kumwona Bwana wao akitawazwa juu ya kiti cha enzi cha Daudi, walimwona akikamatwa kama mhalifu, akipigwa, akidhihakiwa, na akihukumiwa, na akining'inizwa juu ya msalaba wa Kalvari. Ni kukata tamaa na uchungu mkubwa kiasi gani ulinyonga mioyo ya wanafunzi wale katika kipindi cha siku tatu wakati Bwana wao alipokuwa amelala kaburini!PKSw 265.1

    Kristo alikuja wakati mahsusi na kwa jinsi ilivyotabiriwa katika unabii. Ushuhuda wa Maandiko ulitimizwa katika kila kipengele cha huduma Yake. Alihubiri ujumbe wa wokovu, na “Neno Lake lilikuwa na mamlaka.” Mioyo ya wasikilizaji Wake ilishuhudia kuwa ujumbe Wake ulitoka Mbinguni. Utume wa Kiungu wa Kristo ulithibitishwa na Neno na Roho wa Mungu.PKSw 265.2

    Wanafunzi walidumu kumng'ang'ania Bwana wao mpendwa kwa upendo mkubwa. Lakini bado akili zao zilikuwa zimegubikwa na kutokuwa na uhakika na mashaka. Katika uchungu wao hawakuweza kukumbuka maneno ya Kristo yaliyoeleza mateso na mauti Yake. Ikiwa Yesu wa Nazareti alikuwa Masihi kweli, wanafunzi Wake wangetupwa katika huzuni na kukatishwa tamaa kwa kiwango kile? Hili lilikuwa swali lililotesa roho zao wakati Mwokozi alipokuwa amelala katika kaburi Lake wakati wa saa zisizokuwa na matumaini za Sabato iliyokuwa katikati ya kifo na kufufuka Kwake.PKSw 265.3

    Ingawa usiku wa huzuni ulikusanya giza likawazunguka hawa wafuasi wa Yesu, bado hawakuwa wametelekezwa. Nabii anasema: “Nikaapo gizani, Bwana atakuwa nuru kwangu.... Atanileta nje kwenye nuru, nami nitaiona haki yake.” “Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.” Mungu alisema: “Nuru huwazukia wenye adili gizani.” “Nitawaleta vipofu kwa njia wasiyoijua; katika mapito wasiyoyajua nitawaongoza; nitafanya giza kuwa nuru mbele yao; na mahali palipopotoka kuwa pamenyoka. Haya nitayatenda, wala sitawaacha” (Mika 7:8, 9; Zaburi 139:12; 112:4; Isaya 42:16).PKSw 265.4

    Tangazo lililotolewa na wanafunzi katika jina la Bwana lilikuwa sahihi katika vipengele vyote, na matukio ambayo tangazo lilihusu yalikuwa yakitendeka wakati huo huo. “Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia,” ndiyo ulikuwa ujumbe wao. Mwishoni mwa “wakati”— majuma sitini na tisa ya Danieli 9, ambayo yangeishia wakati wa Masihi, “Mpakwa Mafuta”—Kristo alipokea upako wa Roho baada ya kubatizwa Kwake na Yohana katika mto wa Yordani. Na “ufalme wa Mungu” ambao waliutangaza kuwa umekaribia ulianzishwa kwa kifo cha Kristo. Ufalme huu haukuwa, kama walivyokuwa wameaaminishwa, ufalme wa duniani. Wala haukuwa ule wa baadaye, ufalme wa milele ambao utasimikwa wakati “ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu;” ufalme ule wa milele, ambao ndani yake “wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii” (Danieli 7:27). Kama ulivyotumika katika Biblia, usemi “ufalme wa Mungu” unatumika kumaanisha ufalme wa neema na ufalme wa utukufu. Ufalme wa neema umeelezwa na Paulo katika Waraka kwa Waebrania. Baada ya kumtaja Kristo, Mwombezi mwenye huruma ambaye anaguswa na “mambo yetu ya udhaifu,” mtume anasema: “Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema” (Waebrania 4:15, 16). Kiti cha neema huwakilisha ufalme wa neema; kuwepo kwa kiti cha neema humaanisha kuwepo kwa ufalme. Katika mingi ya mifano Yake Kristo alitumia usemi “ufalme wa mbinguni” kueleza kazi ya neema ya Mungu katika mioyo ya watu.PKSw 265.5

    Hivyo, kiti cha utukufu huwakilisha ufalme wa utukufu; na ufalme huu umetajwa katika maneno ya Mwokozi: “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake” (Mathayo 25:31, 32). Ufalme huu ni wa wakati ujao bado. Ufalme wa utukufu hautasimikwa mpaka wakati wa ujio wa pili wa Kristo.PKSw 266.1

    Ufalme wa neema ulianzishwa mara tu baada ya anguko la mwanadamu, wakati mpango ulipobuniwa wa kumkomboa mwanadamu mwenye hatia. Tangu hapo ufalme wa neema uliendelea kuwepo katika kusudi na ahadi ya Mungu; na kwa njia ya imani, wanadamu waliweza kuwa raia wa ufalme huo. Lakini kwa kweli ufalme wa neema haukuanza mpaka kifo cha Kristo kilipotokea. Hata baada ya kuanza utume Wake wa duniani, Mwokozi, ikiwa angechoshwa na ukaidi na utovu wa shukurani wa wanadamu, angeweza kubadilika na kuacha kujitoa kafara pale Kalvari. Akiwa katika Bustani ya Gethsemane kikombe cha mateso kilitetemeka mkononi Mwake. Hata wakati huo angeweza kufuta jasho la damu kutoka katika uso Wake na kuwaacha wanadamu wenye hatia waangamie katika uovu wao. Ikiwa angefanya hivyo, kusingekuwepo ukombozi wa wanadamu walioanguka dhambini. Lakini Mwokozi aliposalimisha uhai Wake na kukata roho, na wakati alipopumua pumzi Yake ya mwisho aliposema kwa sauti kuu, “Imekwisha,” hapo ndipo utimilifu wa mpango wa ukombozi ulipothibitishwa kikamilifu. Ahadi ya wokovu iliyotolewa kwa jozi ya wenye dhambi katika bustani ya Edeni ilithibitishwa. Ufalme wa neema, ambao kabla ya hapo ulikuwepo kwa njia ya ahadi ya Mungu, ulisimikwa.PKSw 266.2

    Hivyo basi, kifo cha Kristo—tukio ambalo wanafunzi waliliona kuwa mwisho wa tumaini lao—ndicho kilifanya tumaini lao kuwa la hakika milele. Wakati ambapo kiliwafanya waumie sana na wakate tamaa kuliko kawaida, kilikuwa kilele cha uthibitisho kuwa imani yao ilikuwa sahihi. Tukio ambalo liliwajaza huzuni na kukata tamaa kwingi ndilo lilifungua mlango wa tumaini kwa kila mtoto wa Adamu, na ambalo ni kitovu cha maisha ya baadaye na furaha ya milele ya watu wa Mungu waaminifu katika zama zote.PKSw 267.1

    Makusudi ya rehema ya milele yalikuwa yamefikia utimilifu wake, licha ya wanafunzi kukatishwa tamaa. Pamoja na mioyo yao kuwa imeongolewa na neema ya Mungu na nguvu ya mafundisho Yake, ambaye “aliongea katika namna ambayo hakuna mtu aliyewahi kuongea kama Yeye,” lakini dhahabu safi ya upendo wao kwa Yesu, ilichanganyika na madini hafifu ya muunganiko wa kiburi cha kidunia na tamaa za kibinafsi. Hata katika chumba cha Pasaka, wakati wa saa ile muhimu ambapo Bwana wao tayari alikuwa akiingia katika kivuli cha Gethsemane, kulikuwepo “mashindano miongoni mwao, juu ya nani miongoni mwao alikuwa mkuu kuliko wote” (Luka 22:24). Njozi zao zilijazwa na kiti cha enzi, taji, na utukufu, ilhali mbele yao walikabiliwa na aibu na uchungu wa bustanini Gethsemane, ukumbi wa hukumu, na msalaba wa Kalvari. Ilikuwa kiburi chao cha moyoni, kiu yao ya utukufu wa ulimwenguni, ambavyo viliwafanya wang'ang'anie sana mafundisho ya uongo ya wakati wao, na kushindwa kuelewa maneno ya Yesu yaliyoonesha uhalisia wa ufalme Wake, na yaliyotabiri uchungu Wake na kifo Chake. Na makosa haya yalisababisha majaribu—makali lakini muhimu—yaliyoruhusiwa ili kuwasahihisha. Ingawa wanafunzi hawakuelewa maana ya ujumbe wao, na walishindwa kutambua matarajio yao, pamoja na hayo walihubiri onyo walilopewa na Mungu, na Bwana aliwazawadia kwa imani yao na aliheshimu utii wao. Walikabidhiwa kazi ya kutangaza kwa mataifa yote injili tukufu ya Bwana wao aliyefufuka. Ilikuwa ni kwa kusudi la kuwaandaa kwa ajili ya kazi hii ambapo uzoefu ulioonekana kuwa mchungu kwao uliruhusiwa.PKSw 267.2

    Baada ya ufufuo, Yesu aliwatokea wanafunzi wakiwa njiani kuelekea Emau, na, “akianza na Musa na manabii wote, aliwaeleza kutoka katika Maandiko mambo yote yaliyomhusu Yeye Mwenyewe” (Luka 24:27). Mioyo ya wanafunzi ilisisimuliwa. Imani yao iliwashwa upya. “Walizaliwa upya katika tumaini hai” hata kabla Yesu hajajifunua kwao. Ilikuwa kusudi Lake kuwaangazia ufahamu wao na kuimarisha imani yao katika“neno la uhakika la unabii.” Alitamani ukweli uoteshe mizizi yake katika akili zao, sio tu kwa sababu uliungwa mkono na ushuhuda Wake binafsi, bali kwa sababu ya ushahidi usio na maswali uliowasilishwa na mifano na vivuli vya sheria ya kaida, na unabii wa Agano la Kale. Ulihitajika kwa ajili ya wafuasi wa Kristo ili wawe na imani iliyoelimishwa, siyo tu kwa ajili yao wenyewe, bali ili waweze kupeleka elimu ya Injili ya Kristo kwa ulimwengu. Na kama hatua ya kwanza ya kutoa elimu hii, Yesu alielekeza wanafunzi kwa “Musa na manabii wote.” LakiniPKSw 267.3

    Badiliko kubwa kiasi gani lilitokea katika mioyo ya wanafunzi walipoona kwa mara nyingine uso mpendwa wa Bwana wao! (Luka 24:32). Katika maana timilifu na kamilifu kuliko hapo awali“walikuwa wamemwona Yeye, ambaye Musa katika torati, na manabii, waliandika.” Mashaka, uchungu, kukata tamaa, vilitoweka, na badala yake, uhakika kamili, na imani isiyokuwa na mawingu, vilitawala. Hakuna cha kushangaza kuona kuwa baada ya kupaa Kwake “walidumu katika hekalu, wakimsifu na kumtukuza Mungu.” Watu, wakijua tu kifo cha kutisha cha Mwokozi, walitazamia kuona katika nyuso zao mwonekano wa huzuni, kuchanganyikiwa, na kushindwa; lakini waliona furaha na ushindi. Maandalizi makubwa kiasi gani waliyopewa wanafunzi hawa kwa ajili ya kazi iliyokuwa mbele yao! Walikuwa wamepitia katika majaribu mazito waliyoweza kuyapitia, na waliona jinsi, njozi yao ilivyokuwa imepotea, neno la Mungu lilikuwa limetekelezwa kwa ushindi mkubwa. Kuanzia wakati huo na kuendelea mbele ni kitu gani kingedhoofisha imani yao au kuhafifisha bidii ya upendo wao? Katika huzuni kubwa kabisa walipata “faraja iliyo imara,” tumaini ambalo lilikuwa kama “nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu” (Waebrania 6:18, 19). Walikuwa mashuhuda wa hekima na mamlaka ya Mungu, na “kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote,” kisingeweza kuwatenga na “upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.” “Katika mambo hayo yote,” walisema, “tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda” (Warumi 8:38, 39, 37). “Bali Neno la Bwana hudumu hata milele” (1 Petro 1:25). Na “ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea” (Warumi 8:34). Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai.PKSw 268.1

    Bwana asema: “Watu wangu hawatatahayari kamwe” (Yoeli 2:26). “Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha” (Zaburi 30:5). Siku ya ufufuo, wakati hawa wanafunzi walipokutana na Mwokozi wao, na mioyo yao ikawaka ndani yao waliposikiliza maneno Yake; wakati walipoona kichwa na mikono na nyayo zilizochubuliwa kwa ajili yao; wakati, kabla ya kupaa Kwake, Yesu alipowaongoza hadi Bethania, na kuinua mikono Yake ili kuwabariki, akawaagiza akisema, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri injili,” akaongeza kusema, “Tazama, niko pamoja nanyi siku zote” (Marko 16:15; Mathayo 28:20); wakati Siku ya Pentekoste Mfariji aliyeahidiwa aliposhuka na nguvu itokayo juu ikatolewa na roho za waumini zikasisimka kwa uwepo halisi wa Bwana wao aliyepaa—ndipo, hata kama, kama njia Yake ilivyokuwa, njia yao iliwaongoza hadi kufikia kujitoa kafara na kufa kifo cha wafia dini, wangeacha huduma ya injili ya neema Yake, pamoja na “taji ya haki” itakayopokelewa wakati wa ujio Wake, na kupokea utukufu wa kiti cha enzi cha kidunia, ambacho kilikuwa tumaini la uanafunzi wao wa awali? Yeye ambaye “anaweza kufanya mengi zaidi ya vyote tunavyoweza kuomba au kufikiria,” aliwapa, pamoja na kushiriki mateso Yake, ushirika wa furaha Yake—furaha ya “kuleta watoto wengi katika utukufu,” furaha isiyoelezeka, “uzito wa milele wa utukufu,” ambayo, Paulo anaieleza akisema, “mateso yetu mepesi, ambayo ni ya kitambo,” “hayawezi kulinganishwa nayo.”PKSw 268.2

    Uzoefu wa wanafunzi waliohubiri “injili ya ufalme” wakati wa ujio wa kwanza wa Kristo, unafanana na uzoefu wa wale waliotangaza ujumbe wa ujio Wake wa pili. Kama vile wanafunzi wa Kristo walivyozunguka wakihubiri kuwa, “Wakati umewadia, ufalme wa Mungu umekaribia,” kadhalika Miller na wenzake walitangaza kuwa kipindi kirefu na cha mwisho kinachoelezwa katika Biblia kilikaribia kwisha, kuwa hukumu ilikuwa imekuja, na ufalme wa milele ulikuwa umekaribia kufika. Mahubiri ya wanafunzi kuhusiana na wakati yalijengwa juu ya majuma sabini ya Danieli 9. Ujumbe uliohubiriwa na Miller na wenzake ulitangaza kukoma kwa siku 2300 za Danieli 8:14, ambazo majuma sabini ni sehemu yake. Mahubiri ya kila mmoja yalijengwa juu ya utimizwaji wa sehemu mbalimbali za kipindi kilekile kirefu cha kiunabii.PKSw 269.1

    Kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa Yesu, William Miller na wenzake, nao hawakuelewa kikamilifu maana halisi ya ujumbe walioutangaza. Makosa yaliyojengeka kwa muda mrefu katika kanisa yaliwazuia kufikia tafsiri sahihi ya kipengele muhimu katika unabii. Kwa hiyo, ingawa walitangaza ujumbe ambao Mungu aliwapa waupeleke ulimwenguni, lakini kwa sababu ya kutokuelewa vizuri maana yake walipata uzoefu wa kukatisha tamaa sana.PKSw 269.2

    Katika kufafanua Danieli 8:14, “Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa,” Miller, kama ilivyokwisha kuelezwa, alijenga tafsiri yake juu ya fundisho lililoaminiwa na watu wote katika wakati wake kuwa dunia ilikuwa patakatifu, na aliamini kuwa kutakasa patakatifu kuliwakilisha kusafisha dunia kwa moto wakati wa ujio wa Bwana. Kwa hiyo, alipogundua kuwa mwisho wa siku 2300 ulikuwa umebainishwa katika unabii, alihitimisha kuwa unabii huu ulitaja wakati mahsusi wa ujio wa pili. Kosa hili lilitokana na kuamini mtazamo wa watu walio wengi wa wakati wake kuhusu patakatifu ni nini hasa.PKSw 269.3

    Katika mfumo wa mifano, ambayo ilikuwa kivuli cha kafara na ukuhani wa Kristo, utakasaji wa patakatifu ilikuwa huduma ya mwisho iliyofanywa na kuhani mkuu katika mzunguko wa mwaka mzima wa huduma. Ilikuwa ndiyo kazi ya mwisho ya upataisho—uondoshaji wa dhambi kutoka katika Israeli. Ilikuwa mfano wa kazi ya mwisho katika huduma ya Kuhani wetu Mkuu mbinguni, katika kuondoa au kufuta dhambi za watu Wake, zilizoandikwa katika kumbukumbu za mbinguni.PKSw 270.1

    Huduma hii inahusisha kazi ya uchunguzi, kazi ya hukumu; na inatangulia muda mfupi kabla ya ujio wa Kristo katika mawingu ya mbinguni akiwa na nguvu na utukufu mwingi; kwa kuwa anapokuja, kila kesi itakuwa imeamriwa. Yesu alisema: “Ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo” (Ufunuo 22:12). Ni kazi hii ya hukumu, inayotangulia muda mfupi kabla ya ujio wa pili wa Kristo, mbayo inatangazwa katika ujumbe wa malaika wa kwanza wa Ufunuo 14:7: “Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu Yake imekuja.” Waliotangaza onyo hili walitoa ujumbe sahihi kwa wakati sahihi. Lakini kama wanafunzi wa awali walivyotangaza, “Wakati umewadia, na ufalme umekaribia,” kwa kuzingatia unabii wa Danieli 9, wakati walishindwa kuelewa kuwa kifo cha Masihi kilitabiriwa katika andiko hilo hilo, kadhalika Miller na wenzake walihubiri ujumbe wa Danieli 8:14 na Ufunuo 14:7, na walishindwa kuona kuwa kulikuwepo na ujumbe mwingine uliotolewa katika Ufunuo 14, ambao pia ulipaswa kuhubiriwa kabla ya ujio wa Bwana. Kama vile wanafunzi walivyokosea kuhusu ufalme uliopaswa kusimikwa mwishoni mwa majuma sabini, kadhalika Waadventista walikosea kuhusiana na tukio ambalo lilipaswa kutokea mwishoni mwa siku 2300. Katika matukio yote mawili kulikuwepo na kukubali, au kufuata, makosa yaliyokuwepo wakati huo na makosa hayo yalipofusha akili zao wakashindwa kuuona ukweli. Makundi yote mawili yalitimiza mapenzi ya Mungu kwa kuhubiri ujumbe ambao alitaka uhubiriwe, na makundi yote mawili, kwa kutokuelewa vizuri ujumbe wao, matarajio yao yalikwama.PKSw 270.2

    Lakini Mungu alitimiza kusudi Lake jema la kuruhusu onyo la hukumu litolewe kama lilivyokuwa. Siku kuu ilikuwa karibu, na katika uongozi Wake watu walipimwa kwa mtihani wa wakati mahsusi, ili kuwafunulia kile kilichokuwa mioyoni mwao. Ujumbe ulikusudiwa kulipima na kulisafisha kanisa. Waliongozwa kuona ikiwa upendo wao ulikuwa umeelekezwa kwa ulimwengu huu au kwa Kristo aliyeko mbinguni. Walidai kumpenda Mwokozi; sasa iliwapasa kuthibitisha upendo wao. Je, walikuwa tayari kuachana na matumaini na tamaa za ulimwengu huu, na kukaribisha kwa furaha ujio wa Bwana wao? Ujumbe ulikusudiwa kuwawezesha kutambua hali yao halisi ya kiroho; ulitumwa kuwaamsha wamtafute Bwana kwa toba na kujinyenyekesha.PKSw 270.3

    Kukatishwa tamaa kwao pia, japokuwa kulikuwa ni matokeo ya kutokuelewa vizuri ujumbe ambao waliuhubiri, kulikusudiwa kutumiwe na Mungu kuleta jambo jema. Kungepima mioyo ya wale waliodai kupokea onyo. Katika kukatishwa tamaa kwao wangetupilia mbali uzoefu wao haraka haraka na kuondoa imani yao kwa neno la Mungu au, kwa kuomba na kujinyenyekesha, wangetafuta ili wagundue ni wapi walishindwa kuelewa kiini cha unabii? Ni wangapi walisukumwa na hofu, au mhemko au msisimko? Wangapi walikuwa wamejitoa nusu-nusu na wasioamini? Watu wengi walidai kupenda ujio wa Bwana. Walipotakiwa kustahimili matusi na dharau za ulimwengu, na jaribu la kuchelewa na kukatishwa tamaa, wangeacha imani yao? Kwa kuwa hawakuelewa mara moja jinsi Mungu alivyokuwa akishughulika nao, wangetupilia mbali ukweli uliothibitishwa kwa ushuhuda dhahiri wa neno la Mungu?PKSw 271.1

    Jaribu hili lingefunua nguvu ya wale ambao kwa imani ya kweli walitii kile walichoamini kuwa fundisho la neno na Roho wa Mungu. Lingewafundisha, kwa namna ambayo ni uzoefu kama huo peke yake ungeweza kuwafundisha, hatari ya kupokea na kukubali nadharia na tafsiri za watu, badala ya kuifanya Biblia kujitafsiri yenyewe. Kwa watoto wa imani, mashaka na huzuni iliyotokana na kosa lao ingeleta masahihisho yaliyotakiwa. Wangeongozwa kujifunza kwa maandiko ya kiunabii kwa umakini zaidi. Walijifunza kuchunguza kwa uangalifu zaidi msingi wa imani yao, na kutupilia mbali kila kitu, hata kama kinakubaliwa watu wengi kiasi gani katika ulimwengu wa Kikristo, ambacho hakikujengwa juu ya Maandiko ya ukweli.PKSw 271.2

    Kwa hawa waumini, kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa awali, kile ambacho katika saa ya majaribu kilionekana kuwa giza kwa ufahamu wao baadaye kingeweza kuwa dhahiri. Wakati ambapo wangeona “lengo la Bwana“wangejua kuwa, licha ya jaribu lililotokana na makosa yao, makusudi Yake ya upendo kwao yalikuwa yakitimizwa hatua kwa hatua. Wangejifunza kwa uzoefu uliobarikiwa kuwa Yeye ni “mwenye huruma nyingi, na rehema tele;” kuwa njia Zake zote “ni za rehema na ukweli kwa wale wanaotunza agano Lake na shuhuda Zake.”PKSw 271.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents