Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura 4—Kuungama Dhambi

    MWENYE kusetiri makosa yake hatasitawi: kila aziungamaye na kuziacha atarehemiwa.” Methali 28:13.KY 39.1

    Masharti yanayompasa mtu kufanya ili apate rehema ya Mungu si magumu, ni ya haki na ya maana. Bwana Mungu hataki tufanye mambo mazito ili tusamehewe dhambi; hasemi tufanye malipo makubwa kwa ajili ya dhambi zetu; asema tu kwamba anayeungama dhambi zake na kuziacha, ndiye atakayerehemiwa.KY 39.2

    Mtume Yakobo asema, “Ungameni makosa yenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana: mpate kuponywa.” Yak. 5:16. Ungama dhambi zako hasa kwa Mungu, ambaye yeye tu ndiye awezaye kuzisamehe; lakini makosa ambayo umewafanyia wanadamu, basi uyaungame mbele ya wanadamu. Hivi ikiwa umemfanyia fulani yasiyofaa na kumchukiza kwa njia yo yote, nenda kwake na kuungama kosa lile ulilomfanyia, naye amepasiwa kulisamehe kabisa. Nyuma yake imekupasa kuomba msamaha kwa Mungu, kwa sababu huyo mwenzako ni kiumbe cha Mungu, na kumfanyia mwanadamu mako- sa ni kufanya makosa machoni pa Mungu pia. Hivyo kwa njia ya kuomba, mambo hufika mbele ya Mwombezi wetu, Kuhani Mkuu wetu ambaye “alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila dhambi,” naye awezaye “kuyachukua mambo yetu ya udhaifu,” huweza kutusafisha uchafu wote wa dhambi.KY 39.3

    Wale ambao hawajajishusha moyo mbele ya Mungu na kuziungama dhambi zao na kukiri kwamba wametiwa hatiani, hao nao hawajafanya bado jambo la kwanza lipasalo ili wapate kukubaliwa na Mungu. Isipokuwa tumemtubia Mungu kwa kweli, na kuchukizwa kabisa na maovu yetu, tumekuwa katika hali ya kutoomba kweli kwa kupata kusamehewa dhambi zetu; hivyo hatujapata kweli amani ya Mungu rohoni mwetu. Mtu akikiri dhambi zake, kukiri kwake lazima kuwa kwa moyoni; mtu akimtupia Mungu roho yake yote, Mungu atamhurumia kweli. “Bwana yuko karibu yao wenye moyo uliovunjika, wenye roho iliyopondeka huwaokoa.” Zaburi 34:18.KY 40.1

    Katika kuungama kwa kweli, imepasa kukiri dhambi au kosa hasa jinsi lilivyo. Pengine ni dhambi ambazo zimefaa kukiri wa kwa siri mbele ya Mungu tu; pengine ni tendo baya lifaalo kukiriwa kwa mtu mmoja tu, yule aliyehasiriwa kwa tendo lile; au pengine ni kosa lifaalo kukiriwa kwa wazi hadhara ya watu; hata ni dhambi au kosa la namna gani, mwenye kufanya kosa lazima kukiri kosa lile lile ambalo amelifanya.KY 40.2

    Zamani wakati wa Samweli, Waisraeli walimwasi Mungu; tena waliona taabu kwa ajili ya dhambi zao. Walikuwa hawamwamini Mungu jinsi alivyokuwa na uwezo na akili kwa kuwatawala vizuri. Walimtupia Mfalme Mkubwa kisogo, nao walitaka kutawaliwa kwa jinsi yalivyotawaliwa mataifa mengine yaliyokuwa karibu nao. Na kabla ya kukubaliwa tena na Mungu, wakakiri hivi: “Tumeziongeza dhambi zetu kwa uovu wa kututakia mfalme.” 1 Sam. 12:19. Kosa lile ambalo kwalo walitiwa hatiani, liliwalazimu kulikiri hasa.KY 41.1

    Kukiri kutupu hakutakubaliwa na Mungu bila kutubu kwa kweli na kugeuka moyo na matendo na maisha; kila kitu kinachomchukiza Mungu lazima kutolewa ili mwenendo uwe safi machoni pake. Kazi iliyo wajibu wetu imeelezwa dhahiri hivi: “Osheni, safikeni; wekeeni mbali uovu wa matendo yenu toka machoni pangu; acheni kutenda maovu; jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu, msaidieni mwenye kuonewa, mhukumieni yatima, mteteeni mjane.” Isa. 1:16,17. “Mwovu atakaporudisha amana, akitoa tena aliyoitwaa kwa unyang’anyi, akiendea sheria za uzima, asipotenda maovu; kuishi ataishi hatakufa.” Ezek. 33:15. Mtume Paulo alisema hivi juu ya kutubu: “Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko mbele za Mungu kwalitenda bidii ya namna gani ndani yenu: naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na hofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi. Kwa kila njia mmejionyesha kuwa safi katika jambo hilo.” 2 Wakor. 7:11.KY 41.2

    Kama maovu yametia giza macho ya kiroho, mwenye dhambi hawezi kutambua hali yake jinsi alivyo na upungufu, na jinsi makosa yake yanavyokuwa mabaya sana; tena isipokuwa atajitoa ili Roho Mtakatifu afanye kazi moyoni mwake, basi atadumu kuwa na giza la kiroho. Kukiri kwake si kwa kweli wala kwa haki. Anapoungama kosa lake hujisingizia akisema kwamba laiti mambo yasingalikuwa hivi na hivi, asingalifanya hivi na hivi, na hivyo asingalipata kukaripiwa.KY 42.1

    Adamu na Hawa walipokwisha kula matunda yaliyokatazwa, waliona haya na hofu kuu. Mara ya kwanza walifikiri namna ya kujitetea kosa lao, ili waepukane na hukumu ya kifo. Mungu alipowauliza habari za kosa lao, Adamu akawa kama anamlaumu Mungu, akisema, “Mwanamke uliyenipa kuwa nami, ndiye aliyenipa ya mti, nikala.” Yule mwanamke alimshtaki nyoka akisema, “‘Nyoka alinidanganya, nikala.” Mwanzo 3:12,13. Inaonekana kwamba wote wawili walikuwa wanamsingizia Mungu, Adamu kwa kuwa Mungu alimpa mwa- namke; tena Hawa kwa ajili ya kumwumba nyoka na kumwacha aingie katika bustani ya Aden. Ile roho ya kujifanya kuwa na haki ilianzishwa na yule baba wa uwongo, nayo huonekana kwa wanadamu wote. Kukiri namna hii na kujisingizia liaifai kitu, wala hakukubaliwi na Mungu. Katika kutubu na kukiri kwa kweli, mtu hukubali kwamba ametiwa hatiani bila kujisingizia wala kutaka kujifanya mwenye haki. Huomba kama yule mtoza ushuru alivyoomba, na kusema, “Mungu uniwie radhi mimi mwenye dhambi;” asitake hata kuinua macho yake mbinguni. Hao nao wanaokiri makosa yao kwa namna walivyotiwa hatiani, watapata msamaha, kwa kuwa Yesu atawaombea kwa ajili ya damu yake aliyomwagika kwao wenye kutubu.KY 42.2

    Katika Neno la Mungu twasoma habari juu ya wengine wenye kutubu kwa kweli, na kujishusha mioyo na kuziungama dhambi, wala hawakuwa na moyo wa kujisingizia ama kujifanya wenye haki. Fikiri jinsi alivyosema Paulo, asitake kamwe kujiteteea makosa yake;“Niliwafunga wengi miongoni mwa watakatifu ndani ya magereza, nikiisha kupewa amri na makuhani wakuu; na walipouawa nalitoa. idhini yangu. Na mara nyingi katika masunagogi mengi naliwaadhibu, nikawashurutisha kukufuru; nikawaonea hasira kama nina wazimu, nikawaudhi hata katika miji ya ugenini.” Matendo 26:10, 11. Lakini hakuogopa kusema, “Yesu Kristo alikuja ulimwenguni, awaokoe wenye dhambi; na mimi wa kwanza wao.” 1 Tim. 1:15. Alijiona kuwa ni mwenye dhambi zaidi ya wengine wote.KY 43.1

    Yule mnyenyekevu mwenye kupondeka moyo na kutubu kwa kweli, yeye atafahamu kidogo upendo wa Mungu, na dhabihu iliyofanywa Kalwari jinsi ilivyo na thamani kubwa sana. Tena jinsi mtoto atakavyoungama makosa yake mbele ya baba yake anayempenda, hivyo ndivyo mweye kutubn atakavyomletea Mungu dhambi zake zote; kama ilivyoandikwa, “Tukiziungama dhambi zetu, yu amini na wa haki atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha udhalimu wote. Yoh. 1:9KY 44.1

    Ninaye Rafiki, naye alinipenda mbele;
    Kwa kamba za pendo zake nimefungwa milele;
    Aukaza moyo wangu, nisitengane naye:
    Mimi wake, Yeye wangu; ndimi naye milele.

    Ninaye Rafiki ndiye aliyenifilia;
    Alimwaga damu yake kwa watu wote pia;
    Sina kitu mimi tena, nikiwa navyo tele;
    Pia vyote ni amana, ndimi wake milele.

    Ninaye Rafiki, naye yuna na moyo mwema:
    Ni Mlwalimu, Kiongozi, Mlinzi wa daima;
    Ni nani wa kunitenga na Mepnzi wa mbele?
    Kwake nimetia nanga, ndimi wake milele.
    KY 44.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents