Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura 5—Kujitoa Kuwa wa Mungu

  MUNGU ameahidi hivi: “Nanyi mtanitafuta, na kuona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.” Yer. 29:13.KY 45.1

  Isipokuwa moyo mzima umetolewa kuwa wa Mungu, mtu hawezi kugeuzwa kuwa katika hali ya kufanana na Mungu. Kwa hali yetu ya kibinadamu tumetengwa mbali na Mungu. Roho Mtakatifu ameeleza hali yetu kuwa ni hii: “wafu kwa sababu ya makosa yenu na dhambi zenu;” “kichwa chote kigonjwa, moyo wote umezimia;” “hamna uzima.” Waef. 2:1; Isa. 1:5, 6. Mungu hutaka kutuponya na kutuweka huru. Kufanya hivyo ni kugeuza hali yetu kabisa, na kuifanya dhamiri yetu yote kuwa mpya; tena hayawezekani hayo ila sisi tukijitoa kabisa kuwa wake Mungu.KY 45.2

  Kupigana kule ambako mtu hupigana na nafsi yake mwenyewe, ni vita vikubwa kuliko vyote. Kujitoa hivyo na kujisalimisha mkononi mwa Mungu, hakuwezekani bila mashindano moyoni; lakini isipokuwa mtu amejitoa na kujiweka chini ya mamlaka ya Mungu, hawezi kabisa kusafishwa na kuwa katika hali ya utakatifu.KY 45.3

  Mungu hawashurutishi watu wamtii, bila kwanza kuwaonyesha sababu ya maana yake, ili tupime kwa akili zetu jinsi ilivyo na kuchagua sisi wenyewe namna ya kufanya. “Njooni, tufanyane huja, asema Bwana.” Isa. 1:18. Mungu halazimishi watu. Anataka tumtii na kumcha kwa hiari yetu wenyewe, si kwa lazima. Anataka tujitoe kwake sisi wenyewe, ili kwa Roho yake afanye kusudi lake mioyoni mwetu. Imekuwa juu yetu sisi kuchagua kwa hiari yetu ili tuondolewe katika utumwa wa dhambi, na kuwekwa huru kuwa wana wa Mungu.KY 46.1

  Na pia, tukijitoa kwa Mungu, hivyo imetupasa kuacha vyote vinavyotaka kututenga mbali na Mungu. Mwokozi asema, “Kila mmoja wenu asiyeviacha vitu vyote alivyo navyo hawezi kuwa mwanafunzi wangu.” Luka. 14:33. Hata jambo gani, liwalo lote, linalotuvuta macho kutoka kwa Mungu, lazima tuliache kabisa. Kupenda mali, kutaka fedha, ni kama minyororo inayofunga wengine kwa Shetani. Wengine hupenda sifa na heshima ya watu, na mambo na anasa ya dunia. Imekuwa ni lazima kuikatakata minyororo hiyo yote. Hatuwezi kumpenda Mungu kwa moyo nusu, na nusu kuipenda dunia na mambo yake. Hatuwezi kuitwa watoto wa Mungu mpaka tutakapokuwa wake kabisa. Kuna wengine wanaosema kwamba wanamtumikia Mungu, na huku hujitegemea nguvu zao wenyewe kwa kufuata sheria za Mungu na kujipatia sifa njema na wokovu. Hawawi wakiamshwa mioyoni na kufahamu upendo wa Kristo kama inavyopasa; bali hujaribu kufuata mambo ya kikristo wakidhani kwamba kwa njia hiyo wataweza kujipatia mahali mbinguni. Dini ya namna hiyo haifai kitu.KY 46.2

  Inapokuwa Kristo anakaa rnoyoni, roho inajaa upendo wake, hupenda kuongea naye, huambatana naye; hivyo pia mtu anajisahau nafsi yake kabisa na tamaa zake. Wale ambao hubidishwa moyoni kwa ajili ya upendo wa Kristo jinsi alivyojitoa kabisa kwa ajili yao, hawafikiri kumtii Mungu kwa kad ri ya kutosha kukubaliwa naye; bali hutaka kufikilia kile kipeo cha Kristo kwa kufuata matakwa yote ya Mwokozi wao.KY 47.1

  Je, umeona ya kwamba kujitoa kwa Kristo ni kujinyima kupita kiasi? Jiulize hivi: “Kristo amefanya nini kwa ajili yangu?” Mwana wa Mungu alijitoa kabisa—maisha yake, kupendwa kwake, na kupata maumivu— ili apate kutukomboa. Na sisi je, wabaya wasiofaa kupendwa sana hivi, twawezaje kumkataa mioyoni mwetu? Tangu mwanzo wa maisha yetu tumepata mibaraka yake. Tungewezaje kumwangalia Yule aliyeumizwa kwa ajili ya dhambi zetu, na huku kutokubali upendo wake na dhabihu yake? Tukifikiri na kufahamu jinsi Yesu alivyojishusha kwa ajili yetu, sisi tungewezaje kunung’unika kupata uzima kwa njia ya kushindana na kujinyima na kujishusha mioyo?KY 47.2

  Kosa la wengi wanaojisifu mioyoni mwao ni kusema hivi: “Mbona imenipasa kutubu na kujishusha moyo ili nijue kwa yakini kwamba nimekubaliwa na Mungu?” Mtazame Kristo. Yeye alikuwa mahali pasipo dhambi kabisa, tena zaidi ya hayo, alikuwa Mfalme wa mbinguni; lakini kwa ajili ya binadamu alihesabiwa kuwa ni mwenye dhambi. Alihesabiwa “pamoja na wakosao: ila dhambi za wengi akazichukua yeye, akawaombea wakosao. Isa. 53:12.KY 48.1

  Lakini sisi je, hata tukijitoa kabisa kwa ajili ya Kristo, tumetoa nini? Moyo uliochafuka kwa dhambi, ili Yesu autengeneze na kuusafisha kwa damu yake, na kutuokoa kwa upendo wake mkuu. Hata hivyo wanadamu huona kwamba ni vigumu kujitoa kwake kabisa. Kusema hivyo ni haya tupu.KY 48.2

  Mungu hataki tuache kitucho chote ambacho kingekuwa na faida kwetu. Katika mambo yote, Mungu anataka tu ili tuwe na hali njema. Wote ambao hawajamchagua Kristo bado, laiti wangefahamu ya kwamba mambo ya dunia wanayoyataka, hayafai, kitu yakilinganishwa na vitu vizuri ambavyo Kristo anataka kuwapa. Yule afuataye njia iliyokatazwa na Mungu, hawezi kabisa kupata furaha ya kweli. Njia ya kufanya dhambi ni njia ya taabu na uharibifu.KY 48.3

  Si vizuri kufikiri ya kwamba Mungu hupenda kuona watoto wake wakipata kuumizwa na kuona uchungu. Anataka ili watoto wake wapate furaha tu. Baba yetu aliye mbinguni anataka tuache kujaribu kujifurahisha na anasa za dunia, ambazo huleta maumivu na kulegea moyo kwa ajili ya kutopata raha na furaha jinsi inavyotazamiwa; na pia anasa zile zitatufungia mlango wa furaha ya mbinguni. Mwokozi hukubali watu jinsi walivyo, pamoja na mahitaji yao, upungufu wao, na udhaifu wao; tena pamoja na kuwasafisha moyo na kuwakomboa kwa damu yake, pia ataridhisha mioyo ya wote watakaomjia kwa ajili ya mkate wa uzima. Matakwa yake ni haya; tufanye mambo hayo tu yatakayotuongoza katika njia ya kweli, ili tufikilie kipeo cha furaha kisichoweza kufikiliwa na wale wasiomtii Mungu. Na kama Kristo anakaa ndani, hivyo ndivyo moyo huwa na furaha ya kweli.KY 49.1

  Wengi wanauliza hivi: “Nawezaje kujitoa kwake Mungu?” Kweli umetaka kujitoa kwake, lakini umekuwa dhaifu katika dhamiri yako, una mashaka moyoni, umefungwa na mazoezi na matendo ya dhambi. Huwezi kutimiza ahadi na maazimio yako. Huwezi kutawala fikara zako, nia yako, wala mapenzi yako. Tena kama unafikiria hayo yote, unashuka moyo na kudhani ya kwamba hutakubaliwa na Mungu; lakini usikate tamaa. Jambo kubwa la kufahamu ni hili: Mungu ametupa sisi uwezo wa kuchagua kwa hiari zetu jinsi tutakavyofanya. Wewe mwenyewe huwezi kugeuza moyo wako; huwezi kwa nguvu zako mpaka Mungu upendo wa moyo wako; lakini waweza kuchagua kama unataka kumtii Mungu na kufanya mapenzi yake. Mpe nia yako na dhamiri yako ili apate kuitawala; ndipo Mungu atakapoweza kufanya kazi yako moyoni mwako, ili kutaka kwako na kutenda kwako kupatane na kusudi lake jema. Hivyo utajiweka chini ya mamlaka ya Kristo; upendo wako utavutwa kwake, utapatana na Kristo katika fikara zako.KY 49.2

  Kutaka mema na usafi ni vizuri; lakini kutaka tu haifai kitu. Wengi watapotea wakiwa wanatamani tu kuwa Wakristo, kwa kuwa wanakosa kujiweka chini ya mamlaka ya Mungu katika dhamiri zao; huchelewa kuchagua kabisa ya kwamba watakuwa Wakristo sasa.KY 50.1

  Ukitumia nia na dhamiri yako kwa njia ya kweli, hali ya maisha yako itageuka kabisa. Kama ukijiweka chini ya mamlaka ya Kristo, unajiunga na uwezo wa kupita uwezo mwingi- ne wo wote. Utakuwa na nguvu itokayo juu iwezayo kukuimarisha kabisa; tena kwa njia ya kujitoa na kujiweka chini ya mamlaka ya Mungu kila siku, utajaliwa kushi maisha mapya, maisha ya kumwamini Mungu daima.KY 50.2

  Naendea msalaba, miye mnyonge na mpofu,
  Yapitayo naacha, nipone msalabani.

  Nakulilia sana: nalemewa na dhambi;
  Pole Yesu asema: “Nitazifuta zote.

  Natoa vyote kwako, nafasi nazo nguvu,
  Roho yangu na mwili viwe vyako milele.

  Kwa damu yake sasa nimegeuka roho,
  Nikaziacha tamaa, nimtafute Yesu tu.

  Nakutumaini tu, Ewe Mwana wa Mungu;
  Nainamia kwako; niponye Mponya wangu.

  Yesu yuaja tena! Nimepevuka kwake,
  Kila chembe kamili; msifuni yeye Mponya.
  KY 51.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents