Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura 13—Kufurahia Mungu

  WATU wa Mungu wameitwa wajumbe wa Kristo, kwa kutangaza wema wa Bwana na rehema zake. Kwa vile Yesu alivyotudhihirishia sifa za Baba, hivyo na sisi imetupasa kuwadhihirishia wengine wasiomjua Kristo jinsi alivyo mwenye upendo, na mwenye huruma. Yesu alisema, “Kama ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma wao ulimwenguni.” Mimi ndani yao, na wewe ndani yangu,. . . . ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma.” Yoh. 17:18, 2, 3. Mtume Paulo huwaambia wanafunzi wa Yesu, Mnadhihirishwa kuwa ni barua ya Kristo,” inavyojulikana “na kusomwa na watu wote.” 2 Wakor. 3:3, 2. Kila mmoja wa watoto wake ni kama barua Yesu anayoipeleka ulimwenguni. Kama wewe ni mfuasi wa Kristo, u barua yake anayoipeleka kwa jamaa zako, mji wako na mtaa unaokaa. Yesu akaapo ndani yako, anataka kusema kwa mioyo yao wasiomjua. Pengine hawasomi Biblia na kusikia sauti yake humo; hawatambui upendo wa Mungu kwa kuumba kwake. Lakini kama wewe ni mjumbe wake wa kweli, pengine kwa sababu ya mwenendo wako mwema na matendo yako mema, wataongozwa wapate kujua kidogo wema wake ua kuvutwa kwake Yesu, hata kumpenda na kumtumikia.KY 120.1

  Wakristo wamewekwa kuwaangazia wengine njia iendayo mbinguni; kuwaonyesha nuru itokayo kwa Kristo. Mienendo yao na sifa zao vyapasa kuwa safi, kuwajulisha wengine hakika ya Kristo na namna ya kumhudumia.KY 121.1

  Nasi tukiwa wajumbe wa Kristo kweli tutakuwa watu wa furaha. Wakristo ambao huzoea kuwa na mioyo mizito, wagunao na kunung’unika, huonyesha wengine mfano usio wa kweli juu ya Mungu na maisha ya kikristo. Wale ambao mienendo yao na desturi zao zinafanya wengine kudhani kwamba Mungu hapendezwi kama watu wake wanafurahi, hao nao wanamshuhudia uwongo Baba yetu aliye mbinguni.KY 121.2

  Shetani husimanga sana anapoweza kuwatilia watu wa Mungu fikara za kutoamini na kufa moyo. Hufurahi sana tukiona mashaka mioyoni juu ya Mungu jinsi anavyotupenda na kuweza kutuokoa. Ni kazi ya Shetani kumtangazia Mungu kuwa hana huruma na rehema. Hujaribu kuutia moyo wa binadamu fikara za uwongo juu ya Mungu; nasi mara nyingi twasikiliza habari zile za uwongo, na kutomheshimu Mungu kwa ajili ya kutomwamini na kumnung’unikia. Shetani hujaribu kuwatia watu fikara kuwa njia ya kikristo ni ya taabu na shida. Tena Mkristo kama anaonyesha mashaka haya katika maisha yake, ni kama kusema yu pamoja na Shetani.KY 121.3

  Wengi hufikiri sana juu ya makosa yao, upungufu wao na dhiki zao, hao nao mioyo yao hujaa huzuni na uchungu. Je, katika maisha yako hujapata mambo yafaayo kuyafurahia? Hata nyakati zingine hujaona furaha moyoni mwako kwa ajili ya mvuto na uongozi wa Roho ya Mungu? Hata hujaona uzuri wa ahadi za Mungu?KY 122.1

  Kudumu kufikiri mambo haya yanayoutia moyo uchungu na kukata tamaa, ni kama kukusanya miiba na viwavi vinavyotuchoma na kutuuma, bila kuona maua na matunda jinsi yalivyo mazuri na ya kufurahisha moyo. Yule ambaye amekata tamaa, moyo wake umekufa ganzi, haoni nuru ya Mungu moyoni mwake, pia huwatia wengine giza njiani mwao.KY 122.2

  Tumshukuru Mungu kwa vile ambavyo ametuhakikishia upendo wake kwa njia nyingi zitupasazo kuzifikiri mara kwa mara; Mwana wa Mungu jinsi alivyoacha utukufu wake, na kuwa katika mfano wa kibinadamu ili apate kutuokoa katika mamlaka ya Shetani; jinsi alivyomshinda Shetani, na kuinua binadamu toka katika hali ya uhalifu ambao aliuangukia kwa ajili ya dhambi, na kutupatanisha tena na Mungu; naye binadamu akivumilia na kustahimili hata mwisho kwa kumwamini Mwokozi, jinsi atakavyovikwa nguo nyeupe, yaani haki itokayo kwa Mungu, kwa imani—hayo ni mambo ambayo Mungu ataka tuyafikirie.KY 122.3

  Ikionekana kwetu kana kwamba tuko katika hali ya kutosadiki upendo wa Mungu na ahadi zake, tunamdharau Mungu na kumhuzunisha Roho wake Mtakatifu. Mama fulani angeonaje kama watoto wake wangemnung’unikia mara kwa mara kama asiyetaka kuwatendea vizuri, naye hudumu kuwakifiri na kuwatendea mema? Na sisi je, Baba yetu aliye mbinguni ataonaje kama tunamdharau kwa upendo wake jinsi alivyomtoa Mwana wake wa pekee ili tupate uzima? Mtume Paulo alisema, “Yeve asiyemwachilia Mwana wake yeye, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi, atakosaje kutukarimia na vitu vyote pamoja naye?” Warumi 8:32. Hata hivyo kuna wengi ambao kwa matendo yao, si kwa maneno hasa, huwa wanasema, “Maneno haya ya Mungu hayanihusu mimi. Pengine awapenda wengine, lakini si mimi.”KY 123.1

  Katika kufanya hivyo unajihatarisha moyo wako mwenyewe; kwa kuwa kila mara unaposema maneno ya kushuku na kutoamini, unazidi kujithibitisha katika kutoamini; tena si wewe mwenyewe tu ambaye unajihatarisha kwa tendo hili; hata na wale ambao wanasikia maneno yako watavutwa kuwa na shaka pia, tena pengine haitawezekana kubatilisha matokeo ya maneno yako jinsi yatakavyokuwa mwishowe. Wewe mwenyewe labda utaweza kuokoka katika mtego wa udanganyifu wa Shetani, lakini wale waliovutwa nawe, pengine hawataweza kuondolewa mawazo yale uliyowatilia mioyoni mwao. Hivyo inatupasa sana kusema mambo yale tu yatakayozidisha nguvu na uzima wa kiroho!KY 123.2

  Watu wote hupata majaribu: mambo ya kutia majonzi na huzuni, ambayo ni vigumu kuyastahimili; na mivuto ya Shetani, ambayo ni vigumu kuipinga. Tusiwasimulie wanadamu wenzetu taabu zetu na mambo ya kuwatilia mashaka mioyoni mwao; ila tumwonyeshe Mungu shida zetu zote katika sala zetu. Kwa namna ya maisha na maneno yetu, wengine waweza kutiwa moyo na kuzidishiwa nguvu, ama waweza kuingiliwa na mashaka na kuzuiliwa wasimtake Kristo na ukweli wake.KY 124.1

  Ni kweli Mwokozi wetu alikuwa mtu wa huzuni, ajuaye taabu, kwa kuwa alichukua huzuni zote za wanadamu. Lakini ijapokuwa hivyo, moyo wake ulikuwa mtulivu, nao ulikuwa kama chemchemi ya uzima; po pote alipokwenda, aliwatilia watu raha, amani, furaha na shangwe mioyoni mwao. Alikuwa mtu wa moyo wa juhudi, asiye na chuki, wala mwenye uso mzito kamwe. Maisha yao wanaomfuata Mwokozi yatakuwa na kusudi jema; watafaha- mu jinsi walivyo na mzigo wa kuwa mfano wake mbele ya wengine. Hawatatoa ubishi na upuzi au kufanyiza mzaha, kwa kuwa dini ya Yesu ni yenye adibu na ya utaratibu: ni dini ya amani. Dini hii haizimi furaha wala kuzuia ukunjufu au vicheko vya upendo. Kristo hakuja kuhudumiwa bali kuhudumu; upendo wake ukiwamo moyoni tutafuata mfano wake.KY 124.2

  Tukifikiri sana juu ya makosa ya wengine, ukali wao na matendo yao yasiyo na haki, haitawezekana kwetu kuwapenda jinsi Kristo alivyotupenda sisi. I lakini tukifikiri zaidi juu ya pendo la ajabu na huruma ambayo Kristo anatuonyesha, haitakuwa vigumu kwetu kuonyesha roho ile ile kwa wengine. Tungependana na kuheshimiana ingawa tunajuana kuwa tunayo makosa. Tungejifunza kujidhili na kuwa na unyenyekevu na kuyavumilia makosa ya wengine kwa upole mwingi. Hivyo nia ya kujipendeza nafsi zetu itaondolewa na tutajawa na ukarimu wa moyo.KY 125.1

  Mtunga Zaburi asema, “Umwamini Bwana, ukatende mema; ukae kwa nchi, ukaishike amini.” Zab. 37:3. “Umwamini Bwana.” Kila siku inaleta taabu na mahangaiko yake; nasi tu wepesi kuzungumza na wenzetu juu ya shida zetu na majaribu yetu, kana kwamba hatuna Mwokozi atupendaye, aliye mwepesi kusikia haja zetu zote, naye yu karibu sana kutusaidia katika shida.KY 125.2

  Wengine huzoea kuwa na hofu na kutazamia shida isiyokuwapo bado. Siku zote sisi huzungukwa na vitu vinavyoonyesha upendo wake; kila siku hufurahishwa na wingi wa majaliwa ya Mungu; lakini wengine wetu husahau mibaraka ya sasa hivi, na huzoea kufikiri mabaya wanayodhani labda yatakuja.KY 126.1

  Je, imetupasa kutokuwa na shukrani na amini hivi? Yesu ndiye rafiki yetu. Wa mbinguni wote hutufikiri sisi. Tusife moyo; tumtwike Bwana taabu zetu zote, nasi tuwe na amani na uchangamfu. Tumwombe Mungu hekima na akili katika kufanya shughuli zetu, ili tusipate hasara na misiba. Yesu ameahidi msaada wake, lakini inatupasa pia tufanye juhudi sisi wenyewe. Mungu hapendi ili tutaabike. Bwana wetu hatudanganyi. Hasemi, “Msiogope; hamtapata kuhatarishwa kamwe.” Si kusudi lake kuwatoa watu wake katika dunia palipo dhambi na maovu, lakini huwaonyesha mahali pa kukimbilia kwa kupata msaada. Aliwaombea wafuasi wake hivi: “Siombi uwatoe katika ulimwengu, bali uwalinde na yule mwovu.” Alisema pia’ “Ulimwenguni mtapata shida: lakini jipeni moyo: mimi nimeushinda ulimwengu.” Yoh. 17:15; 16:33.KY 126.2

  Katika mafundisho yake mlimani, Kristo aliwafundisha wafuasi wake kwamba ni lazima kumtumaini Mungu. Mafundisho haya yali- kusudiwa kusaidia watu wa Mungu siku zote hata siku hizi ili wajipe moyo. Mwokozi aliwaonyesha ndege za anga, jinsi waimbavyo bila kufadhaika moyo; “hawapandi, wala hawavuni.” Lakini Baba aliye mbinguni awalisha. Ndipo Mwokozi anauliza, “Ninyi je! si bora kupita hao?” Mattayo 6:26. Baba mkuu hufunua mkono wake, huviruzuku viumbe vyake vyote mahitaji yao. Ndege hawana budi kudonoa punje za nafaka na vitu vinginevyo vinavyokuwa chakula chao. Imekuwa juu yao kuokota vitu vya kutengeneza viota vyao. Wamelazimishwa kuwalisha watoto wao. Hao nao huondoka kufanya kazi yao na wimbo kwa kuwa “Baba yenu wa mbinguni awalisha hao.” Na “ninyi je! si bora kupita hao?” Naye alituumba sisi katika mfano wake mwenyewe, naye angekosa kuturuzuku mahitaji yetu kama tunamtumainia?KY 126.3

  Kristo alielekeza nia za wafuasi wake kwa maua ya mashamba, jinsi yameavyo. Alisema kwamba “hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama moja la hayo.” Naye Yesu auliza, “Lakini Mungu akiyavika hivi majani ya mashamba, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je, hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?” Mattayo 6:28, 30. Fundisho hili la Kristo linakaripia masumbufu na mahangaiko ya moyo usio na amani.KY 127.1

  Mungu ataka watu wake wote wawe na moyo wa furaha na utulivu, na usikivu. Yesu alisema, “Amani nawaachieni; amani yangu nawatolea; si kama ulimwengu utoavyo, mimi nawatolea. Msifadhaike mioyo yenu, wala msiwe na woga.” “Haya nimewaambieni, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.” Yoh. 14:27; 15:11.KY 127.2

  Furaha inayotakiwa na mtu fulani kwa ajili ya kujipendeza mwenyewe tu, bila kufanya yanayompasa, hiyo ndiyo furaha isiyofaa, isiyo na faida, furaha isiyodumu. Lakini katika kumhudumia Mungu, Mkristo aweza kupata furaha na kuridhishwa moyo. Ingawa tunakosa anasa za maisha haya, twaweza kuona furaha moyoni katika kutumainia maisha yajayo ya milele.KY 128.1

  Lakini hata hapa duniani Wakristo waweza kufurahi katika kumshiriki Kristo na kuongea naye; waweza kujua upendo wake, na kufarijiwa moyoni. Kila siku katika maisha haya ya sasa twaweza kuzidi kumkaribia Yesu na kuzidi kujua upendo wake jinsi ulivyo kwetu. Tusiutupe ujasiri wetu; bali tushikamane sana “na ujasiri wetu, . . . kwa kutumaini mpaka mwisho.” Waeb. 10:35; 3:6. “Hata sasa Bwana ametusaidia,” pia atatusaidia mpaka mwisho. Ni heri tudumu kufikiri mambo yaliyo ukumbusho kwetu, jinsi Bwana alivyotusaidia na kutuokoa mkononi mwake aliye mharabu. Tukizoea kukumbuka jinsi Mungu alivyotuhurumia—machozi ambayo ameyafuta katika macho yetu, maumivu yetu aliyovatuliza, jinsi alivyotuondolea fadhaa na hofu mioyoni mwetu, jinsi alivyoturuzuku mahitaji yetu, na mibaraka yake ambayo tumeipata— tutajipa moyo kwa kujiweza kustahimili yote yatakayotupata katika siku zijazo.KY 128.2

  Katika mashindano ya yule mwovu yatakayokuwa kwa siku zijazo, twajua ya kwamba tutafadhaika moyoni; lakini kwa vile tunavyofikiri mambo yaliyopita na kusema, “Hata sasa Bwana ametusaidia,” twaweza kutazamia mambo yatakayokuja na kujua hivi: “Na kadiri ya siku kadhalika nguvu zako.” 1 Sam. 7:12; Kumbu. 33:25. Majaribu hayatakuwa makali kushinda nguvu tutakayopewa kuyastahimili. Kwa hiyo tushike kazi yetu jinsi ilivyo, na kutumaini kwamba tukipatwa na jambo lo lote, bila shaka tutapewa nguvu kwa kadiri ya jaribio lile ili tuweze kustahimili.KY 129.1

  Hatimaye milango ya mbinguni itafunguliwa kuwakaribisha wana wa Mungu, naye Mfalme wa utukufu atawaambia, “Njooni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu.” Mattayo 25:34.KY 129.2

  Ndipo waliokorabolewa watakaribishwa hapo Yesu anapowaandalia. Hapo majirani zao hawatakuwa waovu wa dunia, waongo, makafiri, wasio na usafi na wenye kutoamini; bali watashirikiana nao waliomshinda Shetani, wenye kufanana na Mungu na kuwa na sifa kamili. Kila tamaa ya dhambi, kila ukosefu na hila ambavyo tunavyo katika hali yetu ya sasa, vitakuwa vimefutwa na damu ya Kristo; hao nao watapata uzuri usio na kiasi na kuwa na utukufu wa Kristo. Watakuwa na sifa kamilifu kwake; watasimama mbele ya “kiti cha enzi, cheupe, kikubwa,” wakiwa hawana hila na mawaa.KY 129.3

  Kwa sababu ya utukufu wa urithi uliowekwa kwake, “mtu atatoa nini badala ya roho yake?” Mattayo 16:26. Hata amekuwa maskini, mwana wa Mungu huwa na utajiri na heshima ambavyo haviwezi kupatikana kwa dunia. Moyo uliokombolewa na kusafishwa dhambi, na kujitoa kumtumikia Mungu, umekuwa wa thamani kubwa isiyokadiriwa; iko furaha mbele ya Mungu na malaika zake kwa mwenye dhambi mmoja atubuye, furaha inayoonyeshwa kwa nyimbo za shangwe.KY 130.1

  Nitaonana na Yesu, uso kwa uso kweli;
  Siku ile shangwe tele nikimwona Mwokozi.
  Tutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni;
  Na kwa utukufu wake nitamwona milele.
  Sasa siwezi kujua jinsi alivyo hasa;
  Bali atakapokuja, nitamwona halisi.
  Mbele yake yafukuzwa machozi na huzuni;
  Kipotovu kitanyoshwa, fumbo litafumbuka.
  Uso kwa uso! Hakika palepale furaha;
  Nitafurahi kabisa nikimwona Mwokozi.
  KY 130.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents