Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura 9—Kazi na Maisha, Jinsi Vinavyohusiana

  MUNGU ndiye asili ya uzima na mwanga na furaha kwa ulimwengu wote. Mibaraka inatoka kwake kwa viumbe vyake vyote. Na mahali po pote ukiwapo uzima wa Mungu mioyoni mwa wanadamu, itakuwa kama mito ya maji ya uzima ule, kuwatokea na kuwasaidia na kuwabariki wengine.KY 83.1

  Ilikuwa furaha ya Mwokozi wetu kuwainua na kuwakomboa wanadamu wapotevu. Kwa hiyo hakuyahesabu maisha yake kuwa ni kitu cha thamani kwake, lakini “kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu.” Waeb. 12:2. Hivyo pia malaika hushughulika katika kazi ya kufurahisha wengine. Hiyo ndiyo furaha yao. Kazi ile ambayo wengine hudhani ni kazi ya namna ya kuwavunjia heshima na cheo, yaani kuwahudumia na kuwasaidia walio chini yao na wenye hali mbaya, ndiyo kazi wanayoifanya malaika wakaao mahali pasipo dhambi kabisa. Ile nia ya Kristo ya kutojipendeza nafsi yake, bali kufikiria na kusaidia wengine, ndiyo nia inayoenea kote mbinguni, tena ni asili ya furaha yao wa mbinguni. Hiyo ndiyo nia watakayokuwa nayo wafuasi wa Kristo, na namna ya kazi watakayoifanya.KY 83.2

  Upendo wa Kristo ukiwamo moyoni, hauwezi kufunikika, bali utatambulika kwa wote tunaokutana nao. Kumpenda Yesu kutabainishwa katika kutamani kutenda kama alivyotenda yeye, kwa kusaidia na kubariki walimwengu wengine. Tutakuwa na moyo wa upendo, na huruma, na kushiriki katika hali ya wengine wote walio viumbe vya Baba yetu aliye mbinguni.KY 84.1

  Mwokozi alipokuwa hapa duniani, hakukaa raha mustarehe na kujipendeza mwenyewe; bali alifanya bidii kuwaokoa wanadamu wapotevu. Tangu kuzaliwa kwake mpaka kusulubiwa kwake Kalwari, alifuata njia ya kujinyima. Alisema ya kwamba Mwana wa Adamu hakuja “kuhudumiwa, bali kuhudumu, na kutoa roho yake kuwa dia ya wengi.” Mattayo 20:28. Hilo ndilo kusudi kuu la maisha yake, kufanya mapenzi ya Mungu na kumaliza kazi yake. Hakufikiri kamwe juu ya kujipendeza nafsi yake mwenyewe.KY 84.2

  Vivyo hivyo wale wanaomshiriki Kristo watakuwa tayari kujinyima ili wengine wapate kujua jinsi Yesu alivyokufa kwa ajili yao, nao pia washirikiane naye. Hiyo ndiyo roho inaooynekana kwa yule anayeongoka kweli. Mara anapomjua Kristo, husikia moyoni kwamba ameshurutishwa kuwajulisha wengine kuwa Yesu ni rafiiki wake mwema. Ikiwa tumesikia wema wa Bwana wetu, basi, tuwaonyeshe wenzetu, ili wao pia wavutwe kwa Yesu, na kumjua “Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Yoh. 1:29.KY 84.3

  Tukijitahidi hivyo kusaidia wengine tutabarikiwa sisi pia. Mungu alikusudia hivi alipotupa sisi sehemu ya kazi ya kuokoa watu. Kuwa watenda kazi pamoja na Mungu ni heshima iliyo kuu na furaha iliyo kubwa zaidi ya yote wanayoweza wanadamu kupewa na Mungu.KY 85.1

  Mungu angaliweza kuwapa malaika kazi ya kuwahubiria wanadamu Injili. Lakini kwa upendo wake alituchagua tuwe watenda kazi pamoja naye, pamoja na Kristo na malaika, ili tushiriki mibaraka, furaha, na kuchangamshwa roho kwa jinsi inavyopatikana katika huduma hii. Tena kila tendo la kujinyima kwa kuwasaidia wengine, humzidishia moyo wa ukarimu yule mwenye kujinyima, naye huzidi kupatana na kushirikiana na Mwokozi; “maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yetu, alipokuwa tajiri, ili ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.” 2 Wakor. 8:9. Tena kwa kadiri tunavyotimiza kusudi la Mungu juu yetu, ndivyo tutakavyopata furaha na baraka katika maisha yetu.KY 85.2

  Kama utafanya kazi kama Kristo alivyokusudia wafuasi wake wafanye, na kuwavuta watu kwake, utaona haja ya kuzidi kumjua Mungu moyoni mwako, na kuzidisha maarifa katika mambo ya Mungu, nawe utaona “njaa na kiu ya haki.” Utaendelea kumwomba Mungu, tena kuamini kwako kutazidi kuthibitika. Kama unapata kujaribiwa utashurutishwa kusoma Neno la Mungu na kumwomba zaidi. Hivyo utazidi kumjua Kristo, na kupata neema yake na kuwa mwaminifu wake katika maisha yako; hasa utazidi kufanana na Kristo, tena utapata raha na furaha zaidi moyoni mwako.KY 86.1

  Wale wanaojaribu kuwa Wakirsto na kupata mibaraka yake bila kumfanyia kazi yo yote, hufanana na watu wanaotaka kupata chakula na kukaa bure bila kufanya kazi. Mtu anayekataa kuvinyosha viungo vyake kwa kutenda kazi, atapotewa na nguvu ile aliyo nayo. Vivyo hivyo Mkristo anayekataa kuutumia uwezo ule aliopewa na Mungu, hukosa kukua na kuwa kama mtu mzima katika Kristo, hata na yeye pia atapotewa na uwezo wa kiroho aliokuwa nao zamani.KY 86.2

  Mungu ameweka kanisa la Kristo kuwa kama wakili wake kwa kuwaokoa watu. Kazi yake: ni kueneza Injili duniani pote. Sharti hiyo imekuwa juu ya Wakristo wote. Kama tumejua upendo wa Kristo, basi tunawiwa deni na wote wasiomjua Kristo. Mungu ametupa nuru, si kwa kujisaidia sisi wenyewe tu, ila pia tumulikie wale wengine wasiomjua.KY 86.3

  Wafuasi wa Kristo wangaliamka na kufanya wajibu wao, kungekuwako watu elfu wa kuhubiri Injili mahali palipo na mhubiri mmoja tu sasa. Na hata wale wasioweza wenyewe kuwa watenda kazi wa Mungu, wangesaidia kazi kwa fedha zao na maombi yao. Tena kazi ya kueneza Injili na kuwajulisha watu kuwa Kristo ndiye Mwokozi wao, ingeendelea na kufanywa kwa moyo wa bidii sana.KY 87.1

  Si lazima twende katika nchi ngeni za makafiri, kumfanyia Kristo kazi, ikiwa wajibu wetu uko huko kwetu. Twaweza kumtumikia Kristo nyumbani mwetu, kanisani kwetu, kwa wenzetu, majirani zetu, hata na wale tunaokutana nao katika kazi yetu.KY 87.2

  Katika maisha yake hapa duniani, Yesu alipitisha miaka mingi katika kufanya kazi ya useremala pamoja na babake mjini Nazareti. Tena alimwamini Mungu katika kufanya kazi ile kama alivyokuwa akiwaponya wagonjwa na kutembea juu ya maji ya Galilaya. Hivyo na sisi pia, hata ikiwa tumehesabiwa kuwa tu watu duni na kufanya kazi iliyo chini, twaweza kutembea na Yesu na kumtumikia.KY 87.3

  Mtume Paulo asema, “Kila mtu . . . na akae katika hali hiyo hiyo aliyoitwa.” 1 Wakor. 7:24. Mfanyi biashara anaweza kufanya kazi yake kwa namna awezavyo kumtukuza Mungu kwa ajili ya uaminifu wake. Ikiwa yu mfuasi wa kweli wa Kristo, dini yake itaonekana katika mambo yake yote, na atawadhihirishia watu namna ya roho ya Kristo. Mwashi, au mfanyi kazi yo yote, inampasa kuwa mwenye bidii tena mwaminifu katika kazi yake, na hivyo atakuwa mjumbe mwaminifu wa Kristo. Kila mtu anayejiita kwa jina la Kristo inampasa kutenda kazi kwa namna iliyo sawa, ili wengine wapate kuyaona matendo yake mema wakamtukuze Mungu aliye Muumba tena Mwokozi wetu.KY 87.4

  Wengi hujisingizia wasitumie akili zao katika kufanya kazi ya Kristo, kwa sababu kuna watu wengine wanayo akili iliyo bora zaidi. Watu wengi hudhani ya kwamba wale tuwenye akili nyingi ndio ambao wametakiwa kujitoa na akili zao katika kumtumikia Mungu. Pia wengi hudhani ya kwamba ni baadhi tu va watu, yaani wanaopendelewa zaidi na kuwa Katika hali nzuri, ambao hupewa akili na talanta; na wengine wametengwa mbali, hao nao hawapati kutiwa kushiriki kazi ya Mungu na neema yake. Lakini haikuelezwa hivyo katika mfano uliotolewa na Kristo. Bwana wa nyumba alipowaita watumishi wake, alimpa kila mmoja kazi yake.KY 88.1

  Kwa moyo wa kupenda, twaweza kuifanya hata kazi iliyo chini kabisa na kuifanya “kama kwa Bwana.” Wakol.3:23. Upendo wa Mungu ukiwamo moyoni, utaonekana katika maisha.KY 89.1

  Usingojee jambo lililo kuu wala kutumaini kupata akili nyingi kabla ya kumtumikia Mungu. Tena usifikiri juu ya wengine jinsi watakavyokudhania. Kama maisha yako na matendo yako ya siku zote huushuhudia wema wako na uaminifu wako, na kuwasadikisha wengine ya kwamba unataka kuwatendea valiyo mema, kazi yako haitapotea bure. Hata na wafuasi wa Yesu wanaohesabiwa kuwa ni watu duni, wanaweza kusaidia wengine na kuwaletea baraka. Kama wanaendelea kufanya kwa uaminifu kazi ile wanayopewa na Mungu, maisha yao hayatakuwa bure. Watazidi kufanana na Kristo mioyoni mwao; huwa wafanyi kazi pamoja na Mungu katika maisha ya sasa, na vivyo hivyo wanatayarishwa kumhudumia Mungu mbinguni, na kupata furaha kuu katika uzima ujao.KY 89.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents