Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    3—Majivuno Ya Ufanisi

    Wakati Sulemani alipotii sheria ya Mungu na kuheshimu mambo matakatifu ya mbinguni, Mungu alikuwa pamoja naye, akimpa hekima ya kutawala kwa haki na huruma. Kwanza alipopata mali na heshima, alidumu kuwa mnyenyekevu, kwa hiyo mvuto wake ulikuwa mkubwa. “Sulemani akatawala juu ya falme zote toka Mto (Euphrates) mpaka nchi ya Wafilisti, na hata mpaka wa Misri . . . Naye alikuwa na amani pande zake zote. Yuda na Israeli wakakaa salama, kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake. . . . siku zote za Sulemani.” 1 Wafalme 4.21-25.MwI 31.1

    Lakini baada ya maelekeo makuu ya kufaulu, maisha yake yakatiwa giza kwa ajili ya uasi wake. Habari zake za baadaye zinakuwa za masikitiko mno, kwamba mtu ambaye aliitwa jina la Yedida, yaani, “Mpendwa wa Bwana” (2 Samweli 12:25) —mtu ambaye aliheshimiwa na Mungu kwa njia ya ajabu, ambavyo hekima yake iliushangaza ulimwengu, mtu aliyewaongoza wengine wamtukuze Mungu wa mbinguni, Mungu wa Israeli, akageuka kabisa, akaacha kumwabudu Mungu, akageukia sanamu za watu wa mataifa, akaziabudu.MwI 31.2

    Miaka mamia kabla Sulemani hajakuwako, Bwana aliona hatari itakayowapata watu watakaochaguliwa kuwa watawala wa Israeli; hivyo alimpa Musa maagizo kuhusu mambo hayo. Musa aliagizwa atoe mwongozo kwamba, mtu atakayekuwa mtawala wa Israeli itampasa “ajiandikie nakala ya torati hii katika chuo. . . . na awe nayo, asome humo siku zoteMwI 32.1

    atakazoishi; ili apate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi, kwa kuyafanya; moyo wake usije ukainuliwa juu ya ndugu zake, wala asikengeuke katika maagizo, kwa mkono wa kuume wala wa kushoto; ili apate kuzifanya siku zake kuwa nyingi katika ufalme wake, yeye na wanawe, katikati ya Israeli.” Kum- bukumbu la Torati 17:18-20.MwI 32.2

    Pamoja na maagizo hayo, Bwana alitoa maonyo hasa juu ya mtu atakayetiwa mafuta ili awe mfalme, “asijizidishie wake ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na dhahabu kuwa nyingi mno.” Fungu la 17.MwI 32.3

    Sulemani aliyajua maonyo hayo, na kwa muda fulani aliyajali. Nia yake ilikuwa kuishi na kutawala kwa kufuata maagizo yaliyotolewa huko Sinai. Njia zake za kuendeshea mambo ya utawala zilikuwa tofauti kabisa na za mataifa yaliyowazunguka, yaani mataifa yale yasiyomcha Mungu, yenye kukanyaga sheria zake.MwI 32.4

    Ili kusudi afanye uhusiano mzuri na ufalme uliokuwa upande wa kusini mwa Israeli, Sulemani alithubutu kuingia upande uliopigiwa marufuku. Shetani alijua matokeo ya mtu kuwa mtiifu; wakati wa mwanzo wa utawala wake, alipokuwa anashikana na kanuni za mbinguni kulikuwa na kufaulu kwa ajabu, hivyo Shetani alitafuta njia ya kumfanya aziasi kanuni hizo, apate kumtenga na Mungu. Ibilisi alifaulu katika juhudi yake, maana maandiko yanatuambia, “Sulemani akafanya ujamaa na Farao, mfalme wa Misri, akamwoa binti yake Farao, akamleta mjini mwa Daudi.” 1 Wafalme 3:1.MwI 32.5

    Tukiangatia ndoa hii kwa hali ya kibinadamu, tunaona kuwa ilifaulu, ingawa ilikuwa kinyume cha mpango wa Mungu; maana binti huyo wa kimataifa aliongoka, akaanza kumwabudu Mungu pamoja na mumewe. Zaidi ya hayo Farao aliwafanyia kazi Waisraeli, kwa maana, “Farao, mfalme wa Misri, alikuwa amepanda akautwaa Gezeri, na kuuteketeza kwa moto, akawaua Wakanaani waliokaa mjini, akampa zawadi binti yake, mkewe Sulemani.” 1 Wafalme 9:16. Sulemani aliujenga tena mji huu, kwa hiyo ni dhahiri kuwa ufalme wake ulienea na kuimarika pwanipwani mwa Bahari ya Kati. Lakini kule kufanya mapatano na watu wa mataifa na kuyaimarisha kwa kifungo cha ndoa, Sulemani alikuwa amedharau mausia yote aliyopewa na Mungu, ili kuendeleza usafi na utakatifu wa taifa la Mungu. Kule kutumaini kuwa angemgeuza binti huyo wa Kimisri awe mwaminifu, ambako Sulemani aliona kuwa inafaa, haukuwa udhuru wa maana ili afanye dhambi hiyo.MwI 32.6

    Kwa muda, Mungu alichukuliana na kosa baya hili kwa ajili Ya rehema zake nyingi; na mfalme, kwa busara katika mwenendo wake, angeweza kusimamisha na kurekebisha maovu ambayo yameletwa na kutokuwa na busara kwake. Lakini Sulemani alianza kwenda kando kutoka kwenye asili ya nguvu zake na utukufu wake. Hali ya kujitukuza ilivyozidi kushinda nia njema, ndivyo hali ya kujitegemea ilivyozidi, ndipo akatafuta kufanya kazi ya Mungu kwa mpango wake mwenyewe. Akafikiri kuwa, akiungana na mataifa yaliyom- zunguka kisiasa na kibiashara, ataweza kuwavuta wamwelekee Mungu wa kweli. Hivyo basi akafanya mwungano usio halali wa mataifa ya kishenzi. Katika miungano hiyo, ndoa za mabinti wa kimataifa zilifungwa pia. Kwa ajili ya mila za mataifa majirani aliacha amri za Mungu.MwI 33.1

    Sulemani alijivuna na kusema kwamba hekima yake na nguvu za mvuto wake zitawaongoza wake zake wa kimataifa waache ibada ya sanamu na kumgeukia Mungu wa kweli, na kwamba mwungano huu na mataifa mengine utawaleta washiriki dini ya Israeli Tumaini la bure! Kosa la Sulemani la kudhani kuwa alikuwa na uwezo mwingi wa kupinga desturi za kimataifa zisimnase, lilikuwa kubwa mno. Tena kosa kubwa jingine ni kule kudhani kuwa kwa vile yeye alivyovunja maagizo matakatifu ya Mungu, ati atawafanya wengine wayatii. Huu ni udanganyifu wa kudhuru sana.MwI 33.2

    Ule mwungano wa mfalme Sulemani pamoja na mataifa yasiyoamini, ulimletea sifa, heshima na utajiri wa ulimwengu huu. Aliwezeshwa kuleta dhahabu kutoka Ofiri na fedha kutoka Tarshishi kwa wingi sana. “Mfalme akafanya fedha na dhahabu kuwa kama mawe humo Yerusalemu, na mierezi akaifanya kuwa kama mikuyu iliyomo Shefela, kwa kuwa mingi.” 2 Mambo ya Nyakati 1:15. Sulemani akiwa tajiri kiasi hicho, huku akizungukwa na majaribu yote, watu walimjia kwa wingi utajiri pamoja na majaribio ambayo hufuatana nao uliwajia watu wengi wakati ule wa Sulemani; . . . dhahabu safi ya tabia ilikuwa imeacha kung'aa ikaharibika.MwI 33.3

    Hivyo punde kwa punde Sulemani akaasi pole pole bila kujua, mpaka akawa amekuwa mbali na Mungu. Kidogo kiodgo, akaanza kupotoka na kutoutegemea uongozi wa Mungu na mibaraka yake, badala yake akategemea uwezo wake mwenyewe. Kidogo kidogo akaacha kumtii Mungu, ambavyo utii huo ndio unaowafanya Israeli kuwa watu wa pekee, akaambatana na desturi za mataifa zaidi na zaidi. Akishindwa na majaribu kuhusu ufanisi wake na heshima yake, alisahau kabisa asili ya ufanisi huo. Akiwa na hamu ya kuwazidi mataifa yote katika ukuu, uwezo na utukufu, alipotoka, akawa mbahili, akaacha makusudi ya kutumia vipawa vya mbinguni kwa utukufu wa Mungu. Fedha ambazo zingewekwa katika hazina ya Mungu kwa matumizi matakatifu, kwa maskini na kuen- delezea haki ya Mungu duniani, alizitumia katika makusudi ya kukifu tamaa zake.MwI 34.1

    Akishughulika mno na tamaa ya kuwapita mataifa mengine kwa mambo ya nje, mfalme aliachilia mbali mambo ya adili na ubora wa tabia. Aliuza heshima yake na utu wake, ili aonyeshe fahari yake ulimwenguni. Fedha nyingi mno alizochuma kwa njia ya biashara na nchi nyingi, iliongezewa kodi nzito iliyotozwa raia. Hivyo basi, kiburi, kutaka makuu, kutapanya mali, na anasa vilizaa matunda katika kuwakatili watu na kuwatoza isivyo haki. Unyofu na huruma alizokuwa nazo, na utu wema aliokuwa akiwatendea watu wakati wa miaka ya kwanza ya utawala wake, sasa vilibadilika. Akaacha unyofu na huruma, kama iwapasavyo watawala, akageuka kuwa mjeuri, na mdhalimu kabisa. Mtu aliyekuwa mwenye rehema, amchaye Mungu, mlinzi wa watu, akabadilika kuwa mtesaji na jeuri. Makodi ya namna mbalimbali yalitozwa watu, ili fedha zipatikane za kuendeleza anasa ya kifalme.MwI 34.2

    Watu walianza kunung'unika. Heshima waliyokuwa nayo kwa mfalme wao hapo kwanza, ilibadilika kuwa chuki na karaha. Kukinga wale watakaotawala juu ya Israeli wasitumie uweso wao wenyewe, Mungu aliwaonya wasijisidishie farasi wengi. Lakini bila kujali agizo hilo, “nao farasi, aliokuwa nao Sulemani wakaletwa toka Misri.” 2 Mambo ya Nyakati 1:16. Wakamletea Sulemani farasi kutoka Misri, na kutoka nchi zote. 2 Mambo ya Nyakati 9:28. “Sulemani akakusanya magari na wapandao farasi; naye alikuwa na magari elfu na mia nne, na wapandao farasi kumi na mbili elfu, aliwaweka katika miji ya magari, na pamoja na mfalme huko Yerusalemu.” 1 Wafalme 10:26.MwI 35.1

    Mfalme aliendelea kuhesabu anasa na starehe pamoja na kusifiwa na ulimwengu kuwa ndiyo alama ya ukuu. Akavitegemea vitu hivyo zaidi na zaidi. Akakusanya wanawake wenye sura nzuri kutoka Misri, Foeniki, Edomu, Moabu na kati ya nchi nyingine nyingi. Wanawake hawa walikuwa mamia. Dini zao zilikuwa za kuabudu sanamu, nao walikuwa wamezoezwa kufuata kanuni za ukatili na ufisadi katika ibada zao. Mfalme akipumbazwa na uzuri wao, aliachilia mbali wajibu wake kwa Mungu na kwa ufalme wake.MwI 35.2

    Wake zake walikuwa na mvuto mkubwa sana kwake, pole pole, mwisho wakamteka, hata akakubali kuabudu miungu yao pamoja nao. Sulemani alidharau mafundisho yaliyotolewa na Mungu ili kuwalinda kutokana na uasi, na sasa amejitoa kabisa kuabudu sanamu, “Maana ikiwa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake. Kwa kuwa Sulemani akam- fuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni, na Milkomu, chukizo la Waamoni.” 1 Wafalme 11:4, 5.MwI 35.3

    Upande wa kusini wa mlima wa mizeituni kuelekeana na mlima wa Moria, ambako hekalu zuri sana la Yehova lilisimamishwa, Sulemani alijenga majengo ya ajabu ya kutumika kwa ibada ya sanamu, yakiheshimiwa kama matakatifu. Ili kusudi kuwapendeza wake zake, aliweka sanamu kubwa za kusubu, za miti na mawe, katikati ya mihadasi na mizeituni. Hapo kwenye madhabahu ya miungu ya kimataifa, “Kemoshi, chukizo la Wamoabi, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni,” ndipo ibada ya kutisha ya kimizimu illpofanyika Fungu 7.MwI 35.4

    Mwenendo wa uasi wa Sulemani ulileta adhabu ya kweli. Kule kujitenga na Mungu na kushikamana na waabudu sanamu, ndiko kulisababisha uharibifu wake. Alipoutupa ushirikiano wake na Mungu, alipotewa na uwezo wa kujitawala. Maadili yake yalitoweka. Uwezo wake wa kufikiri ukafifia, akachomwa moto dhamiri yake. Mtu ambaye hapo mwanzoni alionyesha hekima kubwa katika kuamua na kutetea mtoto aliyekuwa karibu kuangamia na kumrudisha kwa mama yake (Soma 1 Wafalme 3:16-28) alizama maovuni kabisa, kiasi cha kukubali kusimamisha sanamu, na kuitolea kafara za watoto walio hai. Mtu ambaye katika ujana wake alijaliwa kuwa na busara na akili, mtu ambaye katika utu uzima wake aliongozwa kuandika,MwI 36.1

    “Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti,” Mithali 14:12, ndiye miaka yake ya mwisho, aliye jitenga mbali kabisa na usafi wote wa maisha na kuwa mtu mfisadi, mwasharati, akifanya machukizo ya kuabudu miungu ya Kemoshi na Moleki na Ashtorethi. Mtu ambaye siku ya kuzindua hekalu aliwaambia watu wake akisema, “Mioyo yenu na iwe kamili kwa Bwana, Mungu wetu,” yeye mwenyewe akawa kikwazo kwa moyo wake na maisha yake, akiyakanusha maneno yake mwenyewe. Alikosa kuuelewa uhuru. Alijaribu kwa gharama kubwa, kuunganisha nuru na giza, wema na ubaya, usafi na uchafu, Kristo na Beliali.MwI 36.2

    Kutoka kuwa mmoja wa wafalme wakuu wenye sifa, Sulemani aligeuka mpotovu, akawa mtumwa wa wengine. Tabia yake, ambayo hapo zamani ilikuwa nyofu ya kiutu uzima, ikawa hafifu na ya anasa. Imani aliyokuwa nayo juu ya Mungu ikageuka kuwa hali ya kutoamini kwamba kuna Mungu. Kutokuamini kuliharibu furaha yake, kukadhoofisha msimamo wake, na kushusha hali yake chini kabisa. Haki na unyofu aliokuwa navyo mwanzoni mwa kutawala kwake, vikabadilika kuwa udhalimu na ujeuri. Lo, hali hafifu kiasi gani hiyo! Mungu aweza kuwashughulikia kidogo sana watu ambao hawam- tumaini.MwI 36.3

    Kwa muda wote wa miaka hiyo ya uasi, hali ya kiroho ya Waisraeli ilizidi kudidimia. Basi ingekuwaje vingine, iwapo mfalme wao amejiunga na wajumbe wa Shetani? Hali hiyo ilisababisha kudidimia huko. Kwa njia ya wajumbe hao wa Shetani, adui alipata nafasi ya kuwatatanisha Waisraeli kuhusu ibada ya kweli na ya uongo, kwa hiyo katika kutangatanga kwao, walianguka maovuni kwa urahisi. Kufanya biashara na mataifa mengine kuliwashirikisha na watu ambao hawamchi Mungu, wala hawana upendo kwa Mungu, hivyo ushirika huo ulipunguza upendo wao kwa ilififia mno, wala hawakupam- banua tena tabia yake takatifu ilivyo. Wakikataa kufuata njia ya utii, waligeuka na kumtumikia adui wa haki. Kuoana na waabudu sanamu kukawa ni kitu cha kawaida kwao. Mwisho Waisraeli hawakuona kuwa kuabudu sanamu ni jambo baya la kutisha. Ndoa ya mitara ikakubalika sana. Mama wa kimataifa waliwafuusa watoto wao mitambiko ya kimizimu. Baadhi ya watu waliokuwa na dini safi ya Mungu, waliiachia mbali, wakafuata ibada ya sanamu yenye giza kuu.MwI 37.1

    Yawapasa Wakristo kujitenga kabisa na ulimwengu, na mivuto yake. Mungu aweza kabisa kutulinda katika ulimwengu, nasi hatupaswi kuuiga ulimwengu. Upendo wake kwetu hauna mashaka yo yote. Daima huwalinda watoto wake kamili bila kupunguka kitu. Lakini anachotaka kwao ni utii kamili usiogawanyika. “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili, kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kum- tumikia Mungu na mali.” Math. 6:24.MwI 37.2

    Sulemani alitunukiwa hekima ya ajabu lakini ulimwengu ulimvuta kando, akatengana na Mungu. Watu wa siku hizi hawana nguvu kuliko yeye, huelekea maelekeo yale yale yaliyomwangusha. Kama Mungu alivyonwonya Sulemani juu ya hatari iliyomkabili, hali kadhalika, leo Mungu huwaonya watoto wake wasijihatarishe kwa kufanya urafiki na ulimwengu. Anawasihi akisema, “Tokeni kati yao, mkatengwe nao. . . , msiguse kitu kilicho kichafu, nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike.” 2 Wakorintho 6:17, 18.MwI 37.3

    Katika ufanisi hatari kuwa imejibanza humo. Siku zote, utajiri na heshima na cheo vimeambatana na hatari inayodhuru mambo ya kiroho na unyenyekevu. Hakuna shida kuchukua kikombe kitupu, lakini kikiwa kimejaa na kufurika, hutaka uangalifu mwingi ili kuweza kukichukua bila kumwagika. Mateso na taabu huleta masikitiko, lakini ufanisi ndio ulio na hatari kubwa ya kuangamiza maisha ya kiroho. Nia ya kibinadamu isipoambatana na mapenzi ya Mungu daima, mwanadamu asipotakaswa kwa ile kweli, ufanisi utaamsha hali potovu ya kujivuna.MwI 38.1

    Katika bonde la shida, mahali wanadamu wanapotegemea msaada wa Mungu peke yake, uongozi wake kwa kila hatua, ndipo penye usalama. Lakini watu wanaosimama kileleni, kwenye vimo vya juu, ambao kwa ajili ya vyeo vyao hujidhania kuwa wanayo hekima kubwa—watu hawa huwamo katika hatari kubwa mno. Wasipomwegemea Mungu kamili, hakika yao, wataanguka.MwI 38.2

    Po pote kiburi na kutaka makuu vinapositawi, maisha huchafuliwa; maana majivuno hayahitaji kitu cho chote, hufunga moyo kinyume cha mibaraka ya mbinguni. Mtu am- baye shabaha yake ni kujitukuza atajikuta amekaukiwa na neema ya Mungu, ambayo kwayo tunapata utajiri na furaha ya kweli Lakini mtu anayetoa yote na kufanya yote kwa ajili ya Kristo, atafahamu utimizo wa ahadi hii. “Baraka ya Bwana hutajirisha, wala hachanganyi huzuni nayo.” Mithali 10:22. Neema ya Kristo Mwokozi huondoa mahangaiko yote na kutaka makuu kutoka katika moyo, na hugeuza moyo wa chuki kuwa wenye upendo, na kutoamini kuwa kutumaini. Anaposema, “Nifuateni,” huvunja nguvu zote za ulimwengu. Sauti yake hufukuza choyo chote na kutaka makuu kwote kutoka moyoni, na wanadamu huinuka kumfuata kwa uhuru kamili.MwI 38.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents