Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    19—Nabii Wa Amani

    Kwa hali fulani kazi ya nabii Elisha ilitofautiana na ile ya Eliya. Eliya aliagizwa kutoka malaumu na kuhukumu. Yeye alikuwa mwenye sauti ya kukemea isiyo na hofu yo yote, ikiwaita wafalme na watu wote kugeuka na kuacha njia zao ovu. Kazi ya Elisha, kidogo ilikuwa ya amani. Kazi yake ilikuwa kujenga na kuimarisha kazi ile Eliya aliyoanza; yaani kuwafundisha watu njia ya Bwana. Anatajwa kuwa alikuwa mtu aliyewasogolea watu karibu zaidi, akizungukwa na wana wa manabii, na kwa miujiza aliyokuwa akitenda, aliwahudumia watu kwa kuwafurahisha.MwI 197.1

    Elisha alikuwa mtu mwenye roho njema, ya upole, lakini pia alikuwa mkali kama inavyoelezwa wakati alipodhihakiwa na vijana wakaidi akiwa njiani kwenda Betheli. Vijana hawa walikuwa wamesikia habari za kutwaliwa kwa Eliya, nao wakalifanya jambo hilo kama la kujichangamsha, wakisema: “Paa wewe mwenye upaa! Paa wewe mwenye upaa!” Katika makelele yao ya kumdhihaki Elisha aligeuka, na kwa uwezo wa Mungu aliwalaani. Hukumu ya mara moja iliyowafika, ilitoka kwa Mungu.” “Wakatoka dubu wawili wa kike mwituni, wakawararua vijana arobaini na wawili miongoni mwao.” 2 Wafalme 2:23, 24.MwI 197.2

    Kama Elisha angalinyamaza bila kuchukua hatua yo yote juu ya mzaha huo, watu wangeliendelea kumdhihaki, na kazi yake ya muhimu kwa taifa lililokuwa hatarini, ingalishindwa kufaulu. Hatua moja hiyo aliyochukua ilitosha kumfanya aheshimiwe na watu siku zote za maisha yake. Kwa muda wa miaka hamsini alitoka na kuingia katika mji wa Betheli, na katika nchi yote, akienda mji kwa mji, akiwapita vijana wengi wakizurura-zurura bila kazi; lakini hakuna aliyethubutu kumdhihaki, au kumdharau na kudharau kazi yake kama nabii wa Mungu.MwI 198.1

    Hata wema lazima uwe na kikomo. Madaraka lazima yahifadhike kwa msimamo thabiti wa kiongozi, au sivyo yatadhihakiwa tu na watu wengi na kudharauliwa. Kile wazazi na waongozi wanachokiita huruma kwa watoto wao, wakiwa- bembeleza tu daima ni uovu mkubwa mno wanaowafanyia vijana. Kwa kila nyumba na jamaa lazima viwemo kanuni thabiti ambazo lazima zifuatwe bila kuyumbayumba.MwI 198.2

    Heshima iliyowapungukia vijana wale waliomcheka Elisha, ndiyo neema inayohitajiwa sasa, na lazima vijana wetu wawe nayo. Kila mtoto lazima afundishwe kamili kumcha Mungu na kuheshimu kikweli. Jina lake lisitajwe ovyo ovyo kimchezo. Malaika wanapolitaja husetiri nyuso zao. Sisi je, wenye dhambi, tungelitajaje jina hilo kuu.MwI 198.3

    Heshima lazima ionyeshwe kwa wajumbe wa Mungu, Wachungaji, walimu, na wazazi, ambao hufanya kazi yake badala yake hapa duniani. Watu hao wanapoheshimiwa, Mungu hutukuzwa.MwI 198.4

    Adabu pia ni mojawapo ya neema za Roho, na ni lazima ikuzwe kabisa na kila mtu. Adabu inao uwezo wa kulainisha maisha, ambavyo pasipo hiyo maisha yangekuwa katika hali mbaya mno. Watu wanaojidai kuwa wafuasi wa Kristo, na wakati uleule ni watundu, wakaidi, wenye roho mbaya, wasiokuwa na adabu, hawamjui Yesu hata kidogo, wala hawakujifunza kwake. Wanaweza kuwa waaminifu na wasiogeukageuka; lakini uaminifu huo hautakuwa badala ya utu wema na fadhili.MwI 198.5

    Roho njema iliyomwezesha Elisha kuwa na mvuto bora, hata akawavuta watu wengi katika Israeli inadhihirishwa katika kisa cha jamaa iliyoishi huko Shunemu, jinsi alivyoishi kwa hali ya wema. Katika safari zake za kupitapita katika nchi, “Hata ikawa siku moja, Elisha alikwenda Shunemu; na huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo; naye akamshurutisha aje ale chakula. Ikawa alipopita njia ile, huingia kula chakula.” Mama wa nyumba hiyo aliona kuwa Elisha ni “Mtu mtakatifu wa Mungu,” na akamwambia mumewe, “Nakuomba, tumfanyie chumba kidogo ukutani; na ndani yake tumwekee kitanda, na meza, na kiti, na kinara cha taa; na itakuwa, atujiapo, ataingia humo.” Kila mara Elisha alikuja na kukaa katika chumba hiki, naye alikuwa na shukrani sana kukaa mahali patulivu namna hii. Hata Mungu hakufumba macho kwa ukarimu wa mwanamke huyu. Hakuwa na mtoto. Na sasa Mungu anamjalia kupata mtoto wa kiume kwa ajili ya ukarimu wake.MwI 199.1

    Miaka ilipita. Mtoto alikuwa mkubwa sasa wa kwenda mashambani pamoja na babake. Siku moja alipigwa na ugonjwa. “Akamwambia baba yake, kichwa changuf kichwa changu! “Baba akamwambia mtumishi ampeleke kwa mama yake. “Akamchukua, akampeleka kwa mama yake, naye akakaa magotini mwake hata adhuhuri, kisha akafa. Mamaye akapanda juu, akamlaza juu ya kitanda cha yule mtu wa Mungu, akamfungia mlango, akatoka.”MwI 199.2

    Katika huzuni yake, yule mama Mshunemu alikusudia kumwendea Elisha amsaidie. Wakati huo Nabii Elisha alikuwa kwenye mlima wa Karmeli, yule mama akifuatana na mtumishi wake, walianza safari mara moja.MwI 199.3

    “Ikawa yule mtu wa Mungu alipomwona, kwa mbali, akamwambia Gehazi mtumishi wake, tazama Mshunami yule kule. Tafadhali piga mbio sasa kwenda kumlaki, ukamwambie, Hujambo? Mume wako hajambo? Mtoto hajambo? Mtumishi akafanya kama alivyoagizwa, lakini mama huyu hakusema neno mpaka alipofika kwa Elisha ndipo akaeleza matatizo yake. Elisha aliposikia habari hiyo ya huzuni alimwambia Gehazi: “Jikaze viuno, ukachukue fimbo yangu mkononi mwako, ukaende zako, ukikutana na mtu usimsalimu; na mtu akikusalimu; usimjibu; ukaweke fimbo yangu juu ya uso wa mtoto.”MwI 199.4

    Lakini mama hakuridhika mpaka Elisha aende pamoja naye. Alitamka: “Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha.” “Basi akaondoka akamfuata.” Na Gehazi akawatangulia, akaiweka ile fimbo juu ya uso wa mtoto, lakini hapakuwa na sauti, wala majibu. Basi akarudi ili kumlaki, akamwambia, akisema, Mtoto hakuamka.”MwI 201.1

    Walipofika nyumbani, Elisha aliingia chumbani, alimolazwa mtoto aliyekufa, “akajifungia mlango, yeye na yule mtoto wote wawili, akamwomba Bwana. Akapanda juu ya kitanda, akajilaza juu ya mtoto, akaweka kinywa chake juu ya kinywa chake, na macho yake juu ya macho yake, na mikono yake juu ya mikono yake; akajinyosha juu yake; mwili wake yule mtoto akaanza kupata joto. Kisha akarudi. akatembea nyumbani, huko na huko mara moja; akapanda akajinyosha juu yake; na yule mtoto akapiga chafya mara saba na mtoto. akafumbua macho yake.”MwI 201.2

    Elisha akamwita Gehazi, akamwambia amwite mama yake. “Na anpofika kwake, Elisha akasema, Haya! mchukue mwanao. Ndipo akaingia, akamwangukia miguu akainama mpaka nchi kisha akamchukua mwanawe, akatoka.”MwI 201.3

    Hivyo basi imani ya mwanamke huyu ilipata thawabu, Kristo ambaye ni Mkuu wa Uzima, alimrudishia mtoto wake. Vivyo hivyo, watu wake waaminifu watapata thawabu, wakati atakapokuja. Mauti haitakuwa na uchungu wake tena, wala kaburi ushindi wake. Ndipo atawarudishia watu wake watoto wao walionyakuliwa kwao na kifo, “Bwana asema hivi, Sauti imesikiwa Rama, kilio na maombolezo mengi; Raheli akiwalilia watoto wake; asikubali kufarijiwa kwa watoto wake, kwa kuwa hawako. Bwaha asema hivi, Zuia sauti yako, usilie na macho yako yasitoke machozi, maana kazi yako itapata thawabu. nao watakuja tena toka nchi ya adui. Tena liko tumaini kwa siku zako za mwisho, asema Bwana; na watoto wako watarejea hata mpaka wao wenyewe.” Yeremia 31:15-17.MwI 201.4

    Yesu hutufariji kwa ajili ya kufiwa na ujumbe huu wa tumaini. “Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti, ewe mauti, ya wapi mapigo yako? ewe kaburi ku wapi kuharibu kwako?” Hosea 13:14. “Na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti na za kuzimu.” Ufu. 1:18. “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.” 1 Wathesaloniki 4:16, 17. Kazi ya Elisha miongoni mwa watu ilifanana kabisa na ile ya Mwokozi wa wanadamu, yaani kuponya na kufundisha. Katika muda mrefu wa kazi ya Elisha, alijitahidi sana kuendeleza kazi ya elimu iliyokuwa ikiendeshwa katika shule za manabii. Kwa maongozi ya Mungu, maneno aliyowafundisha vijana hao yalinata mawazoni kwa msaada wa Roho Mtakatifu, hivyo basi kwa njia za dalili nyingi alithubutika kuwa mtumishi wa Yehova.MwI 201.5

    Ilikuwa ni katika mojawapo ya ziara zake huko Gilgali kwenye shule, ndipo alipoponya sufuria la maboga. “Na kulikuwa na njaa katika nchi; na hao wana wa manabii walikuwa wakikaa mbele yake. Akamwambia mtumishi wake, Teleka sufuria kubwa, ukaona mtangomwitu, kwa maana hawakuyajua. Basi wakawapakulia hao watu ili wale. Ikawa, walipokuwa katika kula chakula, wakapiga kelele, wakasema, Mauti imo sufuriani, Ee, mtu wa Mungu. Wala hawakuweza kula. Lakini yeye akasema, Leteni unga. Naye akautupa ndani ya sufuria, akasema, Wapakulie watu ili wale. Wala hakikuwamo kitu kibaya sufuriani.”MwI 202.1

    Hata huko Gilgali pia wakati wa njaa Elisha aliwalisha watu mia moja kwa chakula kidogo alicholetewa na mtu wa “Baal- shalisha, “mikate ishirini ya shayiri, na masuke mabichi ya ngano guniani.” Walikuwapo watu hapo wenye njaa. Sadaka ya malimbuko ilipokuja, alimwambia mtumishi wake, “Uwape watu ili wale. Na mtumishi wake akasema, Je, niwaandikie hiki watu mia? Lakini akasema, Uwape watu ili wale; kwa kuwa Bwana asema hivi, Watakula na kusaza. Basi akawaandikia, nao wakala, wakasaza, sawasawa na neno la Bwana.”MwI 202.2

    Lo, hisani ya Kristo, kwa njia ya mtumishi wake ilidhihirishwaje, kwa kuwalisha wenye njaa! Tangu wakati huo Bwana Yesu ametenda miujiza ya kuwaruzuku wanadamu, ingawa si kwa njia wanayoona wazi. Kama tukiwa na utambuzi wa kiroho, tutaelewa wazi kuliko tunavyofahamu sasa jinsi Mungu anavyowaruzuku wanadamu.MwI 202.3

    Neema ya Mungu ndiyo inayoongeza kitu kidogo kikawa cha kutosha. Mkono wa Mungu huongeza kitu mara mia. Kutoka katika hazina yake huandaa meza nyikani. Kwa njia ya kugusa na mkono wake huzidisha vitu vilivyo vichache vikawa vingi vya kuwatosheleza watu wote. Uwezo wake ndio ulioizidisha mikate na masuke mikononi mwa wana wa manabii.MwI 203.1

    Siku zile za kazi ya Kristo duniani, alipofanya mwujiza wa namna hiyo wa kuwalisha makutano ya watu, hali ya kutokuwa na imani kwa wanafunzi wake ilionekana sawa kama ilivyoonekana kwa mtumishi wa nabii wa zamani yaani Elisha. Mtumishi wa Elisha alisema, “Je, niwaandikie hiki watu mia?” Na Yesu alipowaamuru wanafunzi wake wawaandike makutano, walimjibu wakisema, “Hatuna kitu zaidi ya mikate mitano na samaki wawili, tusipokwenda tukawanunulie watu hawa wote vyakula.” Luka 9:13. Je, kwa watu wengi kuna hali gani?MwI 203.2

    Fundisho hili linawahusu watoto wa Mungu wa vizazi vyote. Bwana anapoagiza kazi fulani ifanyike watu wasitie hoja zao na kuulizauliza juu ya matokeo yake. Vitu walivyo navyo vinaweza kuonekana kuwa havitoshi kitu, lakini mikononi mwa Bwana, vitazidi na kufurika. “Basi akawaandikia, nao wakala, wakasaza, sawasawa na neno la Bwana.”MwI 203.3

    Haja kuu ya kanisa leo ni kufahamu wazi uhusiano uliopo baina ya Mungu na watu wake aliowanunua kwa kipaji cha Mwana wake, na kuwa na imani juu ya maendeleo ya kazi yake duniani. Mtu asilielie kwa ajili ya upungufu wa vitu au uwezo wake. Huo ni upotezaji wa wakati. Hali ya kuonekana kwa mambo kwa nje nje, kunaweza kukatisha tamaa, lakini juhudi na kumtegemea Mungu, kutaleta kufaulu. Vitu vinavyoletwa kwake kwa imani na maombi, yeye mwenyewe atavizidisha kama alivyozidisha vyakula walivyopewa wana wa manabii, ha kwa wale makutano wenye njaa.MwI 203.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents