Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    11—Karmeli

    Eliya akiwa anasimama mbele ya Ahabu, alidai kwamba Waisraeli wote pamoja na manabii wa Baali na Ashtorethi wakutane naye juu ya mlima wa Karmeli. Akaamuru, akisema, “Basi sasa upeleke watu, unikusanyie jamii ya Israeli katika mlima wa Karmeli na wale manabii wa Baali mia nne na hamsini, na wale manabii wa Ashera mia nne, walao chakula mezani pa Yezebeli.”MwI 111.1

    Amri hii ilitolewa na mtu aliyeonekana kana kwamba anasimama mbele za Mungu; na Ahabu aliitii mara moja, kana kwamba nabii ndiye aliyekuwa mfalme, na Ahabu raia. Wajumbe walitumwa kwa haraka, wakaenda katika nchi yote, kuwaalika watu wote wakutane na Eliya pamoja na manabii wa Baali na Ashtorethi. Katika kila mji na kijiji, watu walijitayarisha kwa mkutano huo, kwa siku iliyopangwa. Kadiri watu walivyosafiri kwenda mahali pa mkutano, mioyo ya watu wengi ilikuwa na wasiwasi. Kuna jambo la pekee linalokuja; au sivyo, kwa nini watu wote wakusanyike huko Karmeli? Je, kuna hatari gani nyingine inayotaka kutuangukia?MwI 111.2

    Kabla ukame haujaipiga nchi, mlima wa Karmeli ulikuwa ukipendeza sana; chemchemi za maji zilianzia huko zikafanya Mbele ya makutano na makuhani wa Baali vijito vinavyotiririka daima; na mitelemko yake ilikuwa ikipendeza kwa ajili ya maua yake na mwitu mzuri. Na sasa uzuri huo wote umeumbuka kwa ajili ya laana ya ukame. Madhabahu zilizojengwa huko kwa ajili ya kuabudia Baali na Ashtorethi, zilikuwa zikisimama kwenye miti isiokuwa na majani. Katika kilele kimojawapo kilicho kirefu, palikuwa na magofu ya madhabahu ya Bwana Mungu.MwI 111.3

    Mlima wa Karmeli uliinuka juu kabisa; na vilele vyake viliweza kuonekana toka pande zote za nchi. Chini ya mlima palikuwa mahali pengi pafaapo, ambapo watu wakisimama hapo wanaweza kuona vizuri mambo yanayotendeka juu kileleni. Mungu alikuwa amedharauliwa na waabudu sanamu hawa kwa kufanya ibada zao katika mwitu huo; na sasa Eliya alipachagua mahali hapo ili kuonyesha uwezo wa Mungu na kulitukuza jina lake.MwI 112.1

    Asubuhi mapema ya siku iliyopangwa, makundi makundi ya Waisraeli walioasi, walikusanyika mlimani wakiwa na hamu kuu ya kuona mambo yatakayotokea. Manabii wa Yezebeli walikwenda huko wakiwa na mavazi yao rasmi. Mfalme Ahabu alitokea mwenye fahari kuu, akakaa mbele ya makuhani wake. Alipofika, waabudu sanamu hao wakamkaribisha kwa vifijo. Lakini hata hivyo mioyoni mwa makuhani palikuwa na wasiwasi kwa ajili ya neno la nabii Eliya, ambalo limefunga mbingu kwa miaka mitatu na nusu. Walikuwa na matazamio ya jambo fulani baya, kuwa litatokea. Miungu yao waliyokuwa wakiitumaini haikuweza kukanusha neno la Eliya la kuilaani nchi na kuifanya kame. Ibada zao za kiwazimu, sala zao, kilio chao, kafara zao za daima, na mambo yao yote waliyoyafanya ili kuleta mvua hayakufua dafu.MwI 112.2

    Eliya akiangaliana na mfalme Ahabu na manabii wa uongo, na kuzungukwa na majeshi ya Israeli, alisimama akiwa mtu mmoja tu ambaye anamdhihirisha Mungu na kumtukuza. Mtu ambaye watu wote wa ufalme wa Ahabu walimlaumu kwa ajili ya dhiki iliyowapata, sasa yuko mbele yao waziwazi, bila ulinzi wo wote, mbele ya Ahabu, manabii wa Baali na Ashtorethi, watu wa vita, na watu maelfu wakimzunguka. Lakini nabii Eliya hayuko peke yake. Juu yake na kandokando yake wako walinzi wa mbinguni, wakimlinda, malaika ambao uwezo wao ni mkuu.MwI 112.3

    Nabii alisimama mbele ya jeshi kubwa hili bila wasiwasi wala woga, akijua wajibu wake na kazi aliyopewa kufanya na Mfalme wa wafalme. Uso wake uling'aa kwa ajili ya kujitoa kwake Watu walingojea kwa shauku kile atakachosema. Kwanza akiangalia madhabahu ya Bwana iliyobomokabomoka, halafu akiangalia makutano, Eliya alipaaza sauti kama parapanda, akisema: “Mtasitasita katikati ya mawazo mawili hata Iini? Bwana akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! mfuateni yeye.”MwI 113.1

    Watu hawakumjibu neno lo lote. Hakuna hata mtu mmoja katika mkutano mkubwa ule aliyethubutu kumkiri Mungu. Udanganyifu mkuu unaofanana na wingu zito jeusi uliwafunikiza Israeli, ukawafanya kuwa vipofu. Uasi huu haukuwafunikiza wote mara moja, lakini uliwafunika taratibu kwa kadiri ile waliyokataa kujali maonyo yaliyotumwa kwao na Mungu. Kila mara walipojitenga na haki, na kila mara walipokataa kutubu, walizidi kuzama zaidi na kuwa mbali na mbinguni. Na sasa wakati huu wa shida walizidi kushupaza mioyo yao na kukataa kujitia upande wa Mungu.MwI 113.2

    Bwana huchukizwa na hali ya kutojali, na kutokuwa mwaminifu wakati wa shida, katika kazi yake. Malimwengu yote yanaangalia kwa hamu kuu mashindano ya mwisho yanavyoendelea katikati ya wema na uovu. Watu wa Mungu wamekaribia mipaka ya ulimwengu wa milele; kwa hiyo, ni jambo gani lililo muhimu kwao zaidi ya yote, Mungu anao mashujaa wa imani, hata sasa anao, watu wanaofanana na Yusufu, Eliya na Danieli, ambao hawaonei aibu kuwaita watu wake wa pekee. Mungu huwamwagia mibaraka watu wake wenye matendo, watu ambao hawapotoshwi, na kuacha mstari wa wajibu wao; lakini kwa juhudi ya Mungu, huuliza swali hili: “Ni nani aliye upande wa Bwana? (Kutoka 32:26). Watu ambao hawataridhika kuuliza swali hilo tu, bali watakaowaita watu walio upande wa Bwana wajidhihirishe kwa Bwana wa mab- wana, na Mfalme wa wafalme. Watu kama hao huunganika na Bwana katika mipango yao na katika mapenzi yao, sheria ya Bwana huwa mwongozo wao. Kwa ajili ya kumpenda, huwa— tayari hata kufa kwa ajili yake. Kazi yao ni ya kupokea nuru kutoka mbinguni na kuumulikia ulimwengu dhahiri. Neno lao kuu ni, Uaminifu kwa Mungu.”MwI 113.3

    Wakati Israeli walipokuwa wakisitasita mlimani Karmeli, Eliya alipaaza sauti yake tena akasema: “Mimi nimesalia, mimi peke yangu, nabii wa Bwana; lakini manabii wa Baali ni watu mia nne na hamsini. Kwa hiyo na watutolee ng'ombe wawili; wao na wajichagulie ng'ombe mmoja, wamkatekate na kum- weka juu ya kuni, wasitie moto chini nami nitamtengeneza huyo ng'ombe wa pili, na kumweka juu ya kuni, wala sitatia moto chini. Nanyi ombeni kwa jina la mungu wenu, nami nitaomba kwa jina la Bwana; na Mungu yule ajibuye kwa moto, na awe ndiye Mungu ”MwI 114.1

    Makusudio ya Eliya yalikuwa ya wima ambayo watu wasingeweza kuepa, kwa hiyo walipata ujasiri wa kujibu, na kusema, “Maneno haya ni mazuri.” Manabii wa Baali hawakutoa sauti zao kwa ajili ya kutokubali kwao; lakini Eliya akiwaelekea, alisema; “Jichagulieni ng'ombe moja, mkam- tengenze kwanza; maana ninyi ndio wengi; mkaliitie jina la mungu wenu, wala msitie moto chini.”MwI 114.2

    Manabii wa uongo, wakionekana kwa nje kama watu mashujaa wenye majivuno, haIi katika mioyo yao dhamiri zao zikiwashuhudia kuwa wana hatia, walitengeneza madhabahu yao, wakaanza kumsihi Baali awasaidie, huku wakirukaruka, wakigaagaa chini, wakipiga yowe, waking'oa nywele zao, na kujikatakata miili yao kwa visu.MwI 114.3

    Saa za asubuhi zilipita, adhuhuri ikafika, hata hivyo hapakuwa na dalili yo yote ya kuonyesha kuwa Baali anasikia maombi ya watu wake waliodanganyika. Hakuna sauti yo yote, wala jawabu kwa sala hizo za kiwazimu. Kafara yao ilidumu kuwa vilevile bila kuteketezwa.MwI 114.4

    Walipokuwa wakiendelea na sala zao za kiwazimu, baadhi ya makuhani, walikuwa wakijaribu kufanya uchawi ili moto uwake bila kupulizwa na mtu, hivyo wapate kuwaaminisha watu kuwa Baali ameleta moto. Lakini Eliya alikuwa akiwachunguza sana; na makuhani hao wakitumaini kuwa wanaweza kugundua hila ya kuwasha moto, waliendelea huku wakiomba.MwI 114.5

    “Ikawa, wakati wa adhuhuri, Eliya akawafanyia dhihaka akasema, Mwiteni kwa sauti kuu; maana ni mungu huyo; labda anazungumza, au ana shughuli, au anasafiri, au labda amelala, sharti aamshwe. Wakapiga kelele, wakajikatakata kwa visu na nyembe kama ilivyo desturi yao, hata damu ikawachuruzika. Ikawa, wakati wa adhuhuri ulipopita, wakatabiri hata wakati wa kutoa dhabihu ya jioni; lakini hapakuwa na sauti, wala aliyejibu, wala aliyeaangalia.”MwI 115.1

    Shetani angefurahi sana kuwasaidia watu ambao amewadanganya hata wakakubali kumtumikia yeye. Angefurahi sana kuwatumia moto kwa njia ya umeme ili uteketeze kafara yao. Lakini Mwenyezi Mungu amemwekea mipaka ya uwezo wake, ambayo hawezi kuipita, kwa hiyo hakuweza kuleta hata cheche moja la moto katika madhabahu ya Baali.MwI 115.2

    Mwishowe sauti za makuhani ziliziba kwa sababu ya kupiga kelele, mavazi yao yakawa na madoadoa ya damu ya miili yao, waliyojikatakata, wakapigwa butaa, hali wamekata tamaa kabisa. Hali yao ya msisimko wa kiwazimu ikatoweka, sasa wakageuka kulaani miungu yao ya jua. Eliya alikuwa akiwaangalia kwa makini, maana alifahamu kuwa, kama makuhani hawa wakifanya ujanja, hata kuwasha moto kwenye madhabahu yao, angeraruliwa vipande vipande.MwI 115.3

    Jioni ikakaribia. Manabii wa Baali wako hoi, wamebung'aa. Kila mara mmoja anatoa shauri hili na mwingine shauri lile, mpaka mwishowe wakakaa tu bila kufanya lo lote. Makelele yao yakanyamaza kimya, hayakusikika tena huko mlimani Karmeli. Wakaacha mashindano yao na Eliya.MwI 115.4

    Mchana kutwa watu walikuwa wakiangalia mambo ya makuhani walioshindwa kuleta moto. Walikuwa wakiwaangalia jinsi walivyokuwa wakipiga makelele, huku wakirukaruka na kujiviringisha huko na huku kuzunguka madhabahu yao, kana kwamba wanakusanya miali ya jua ili iwawashie moto. Watu walikuwa wakiangalia kwa hofu jinsi makuhani hao walivyojijeruhi kwa kujikatakata, wakaona jinsi ibada ya sanamu ilivyo upumbavu mtupu. Wengi katika kundi hilo Iililokusanyika walichoka kuona maonyesho ya kishetani, wakawa wanangoja kwa hamu sana kuona mambo ya Eliya.MwI 115.5

    Wakati huo ulikuwa wa kutoa dhabihu ya jioni, na Eliya akawaambia watu, “Nikaribieni mimi.” Watu walipomkaribia huku wakitetemeka, akageuka kuangalia madhabahu iliyobomokabomoka, ambayo watu walimwabudia Mungu hapo zamani. Kwake yeye magofu haya ni yenye thamani zaidi kuliko madhabahu malidadi ya Baali. Eliya akaitengeneza madhabahu iliyobomoka. Kule kuitengeneza, Eliya alionyesha heshima aliyokuwa nayo kwa agano, ambalo Mungu alifanya na Waisraeli wakati wa kuvuka mto wa Yordani na kuingia Kanaani. Akichagua mawe kumi na mawili kwa hesabu ya wana wa Israeli, alijenga madhabahu kwa jina la Bwana.MwI 116.1

    Makuhani wa Baali wakiwa wamechoka mno, na nguvu zimewaishia, kwa juhudi zao za bure walizofanya, walingoja kuona kile Eliya atakachofanya. Walimchukia nabii Eliya kwa ajili ya kuihafifisha miungu yao, lakini walimwogopa kwa ajili ya uwezo wake. Watu waliendelea kungoja wakati Eliya alipokuwa akitayarisha, huku mioyo yao imejaa hofu. Hali tulivu ya nabii ilitofautiana sana na hali ya harara ya manabii wa Baali ambao walikuwa kama waenda wazimu.MwI 116.2

    Madhabahu ya Bwana ikawa tayari, nabii akafanya mfereji kando yake, alipokwisha kupanga kuni na kuweka kafara juu yake, aliwaamuru watu kujaza maji mengi juu yake. Akasema, “Jazeni mapipa manne maji, mkayamwage juu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya kuni. Akasema, Fanyeni mara ya pili. Wakafanya mara ya pili Akasema, Fanyeni mara ya tatu. Wakafanya mara ya tatu. Yale maji yakaizunguka madhabahu; akaujaza mfereji maji.”MwI 116.3

    Eliya akiwakumbusha watu juu ya hali yao ya uasi iliyosababisha adhabu ya Mungu kuipiga nchi aliwaita wamrudie Mungu wao na wa baba zao kwa kutubu na kuacha njia zao mbaya ili hukumu ya Mungu iondolewe. Kisha akiinua mikono yake kuelekea juu, aliinamisha kichwa chake na kutoa sala fupi. Manabii wa Baali wamekuwa wakiomba na kurukaruka na kufanya ghasia za kila namna; lakini Eliya alipoomba, hakupiga kelele za kijinga, wala sauti yake haikusikika ikitamka maneno ya upuzi huko mlimani Karmeli. Aliomba kama mtu ajuaye kuwa Mungu yuko hapo, akiona mambo yote ya hapo na akisikiliza maombi yake. Manabii wa Baali waliomba kijeuri, kwa kupayukapayuka; lakini Eliya aliomba kwa heshima na kicho, akimwomba Mungu ajitukuze juu ya Baali, ili Israeli wapate kuongozwa na kumrudia yeye.MwI 116.4

    Nabii Eliya alisema, Bwana, Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli, na ya kuwa mimi ni mtumishi wako, na ya kuwa nimetanya mambo haya yote kwa neno lako. Unisikie, Ee Bwana, unisikie, ili watu hawa wajue ya kuwa wewe, Bwana ndiwe Mungu, na ya kuwa wewe umewageuza mioyo wakurudie.”MwI 118.1

    Watu wote wakawa kimya kabisa. Makuhani wa baali wakatetemeka kwa hofu. Dhamiri zao zikawashuhudia kuwa wana hatia, hivyo walitazamia adhabu iwaangukie.MwI 118.2

    Mara moja, baada ya sala ya Eliya kumalizika, miali ya moto yenye kung'aa kama umeme, ilishuka kutoka mbinguni ikateketeza dhabihu iliyowekwa madhabahuni, ikaramba na maji yaliyokuwa yamejaa katika mfereji, hata mawe ya madhabahu pia yaliteketezwa. Mng'ao wa moto uliangaza mlima wote, ukawatia watu kiwi katika macho yao. Chini, katika mabonde ya mlima, mahali watu wengine wengi walipokusanyika kuanagalia mambo yanayotendeka juu ya mlima, waliuona moto wazi wazi uliposhuka kutoka juu, nao walishangaa mno. Moto huo ulifanana na nguzo za moto uliowatenganisha Waisraeli na Wamisiri katika bahari ya Shamu.MwI 118.3

    Watu waliokuwa juu ya mlima waliinama mbele za Mungu, wakasujudu. Hawakuthubutu kuangalia moto ulioshuka kutoka mbinguni. Walihofu kwamba, hata wao pia watapitiwa na moto na kuteketezwa. Wakijikuta kuwa na hatia, katika mienendo yao, mara moja. wakamkiri Mungu wa Eliya, kwamba ndiye Mungu wa baba zao anayestahili kuabudiwa, kwa hiyo wakapaaza sauti zao kwa pamoja wakisema, “Bwana ndiye Mungu, Bwana ndiye Mungu.” Sauti hizo zilisikika dhahiri katika mlima wote na katika mabonde, wametubu. Mwisho wameona jinsi walivyomdharau Mungu na kumwacha. Tofauti ya kuabudu Baali na kumwabudu Mungu ikadhihirika wazi. Wakaona kuwa Mungu ana haki kuzuia mvua isinyeshe mpaka watakapotubu na kumrudia. Sasa wanakiri kwa moyo kwamba, Mungu wa Eliya ndiye Mungu Mkuu kuliko miungu yote.MwI 118.4

    Makuhani wa Baali waliangalia mambo hayo kwa hofu kuu, jinsi Mungu alivyodhihirisha uwezo wake. Walakini hata katika mshangao wao na wakiona utukufu wa Mungu mbele yao, walikataa kutubu, wala kuacha njia zao ovu. Walidumu tu kuwa manabii wa Baali. Kwa hiyo wakajionyesha kuwa wanastahili kuangamizwa.MwI 119.1

    Ili kusudi Waisraeli waliotubu walindwe wasiambukizwe uovu tena na watu wale waliowafundisha kuabudu Baali, Eliya akaambiwa na Bwana awaangamize walimu hawa wa uongo. Tangu hapo hasira ya watu ilikuwa imeamshwa juu ya watu hawa waliowapotosha na Eliya alipoamuru kwamba, “Wakamateni hao manabii wa Baali, asiokoke hata mmoja., watu walitii mara moja. Wakawakamata manabii hao, wakawapeleka kwenye kijito cha Kishoni, pale pale, siku ile ile ya kukata shauri kumrudia Mungu, manabii wa Baali wakauliwa mbali Hakuna hata mmoja aliyeachwa kuishi.MwI 119.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents