Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    15—Yehoshafati

    Kabla Yehoshafati hajatawalishwa mwenye umri wa miaka thelathini na mitano, alikuwa na bahati nzuri ya kuishi na mfalme mwema. Asa, ambaye karibu kwa kila hali “alifanya yaliyo mema machoni pa Mungu.” Wafalme 15:11 Kwa muda wa utawala wake wenye mafanikio wa miaka ishirini na mitano, Yehoshafati “akaiendea njia yote ya Asa babaya, wala hakugeuka.”MwI 155.1

    Katika juhudi yake ya kutawala kwa busara, Yehoshafati alijitahidi kuwaongoza raia zake waepukane na ibada ya sanamu. Lakini wengi wa watu wake, “wakaendelea kutoa dhabihu wakafukiza uvumba katika mahali pa juu.” 1 Wafalme 22:43. Mfalme hakubomoa mahali pa juu mara moja; lakini tangu mwanzo wa utawala wake alijaribu kuwakinga watu wa Yuda wasiingize uovu uliokuwa ukifanywa na watu wa kaskazini chini ya utawala wa Ahabu, ambaye waliishi pamoja naye miaka mingi. Yehoshafati mwenyewe alikuwa mcha Mungu. “Asiyatafute mabaali, lakini alimtafuta Mungu wa baba yake, akaenda katika amri zake, wala si katika matendo ya Israeli.” Kwa ajili ya unyofu wake Bwana alikuwa pamoja naye, “akauthibitisha ufalme mkononi mwake.” 2 Mambo ya Nyakati 17:3-5.MwI 155.2

    “Yehoshafati akaletewa zawadi na Yuda wote; basi akawa na mali na heshima tele. Ukainuliwa moyo wake katika njia za Bwana.” Muda ulivyoendelea, na matengenezo ya dini yalivyoendelea, mfalme “akapaondoa mahali mahali pa juu ya maashera katika Yuda.” Mafungu 5, 6. “Tena mahanithi waliosalia, hao waliosalia siku za Asa baba yake, akawaondoa katika nchi.” 1 Wafalme 22:46. Hivyo kwa taratibu wenyeji wa Yuda wakaepushwa na hatari nyingi zilizotishia kudhuru hali yao ya kiroho, na maendeleo yao.MwI 156.1

    Katika ufalme mzima, watu walikuwa na haja ya mafun- disho kuhusu sheria ya Mungu. Usalama wao ulikuwa katika kuielewa sheria hii Kwa kushikamana na mafundisho ya sheria hii, ndipo watakuwa waaminifu kwa Mungu na kwa wanadamu pia. Yehoshafati akifahamu hayo, alichukua hatua thabiti ya kuwafundisha watu wake maandiko matakatifu. Wakuu waliokuwa wakisimamia mambo mbali mbali waliagizwa wapange mambo ili kuwezesha makuhani watoe mafundisho ya kiroho bila udhia. Kwa agizo hilo la mfalme, wakufunzi hawa, wakifanya kazi chini ya wasimamizi, “akazunguka katika miji yote ya Yuda, wakafundisha kati ya watu.” 2 Nyaka. 17:7-9. Kwa jinsi watu wengi walivyojitahidi kufahamu matakwa ya Mungu, na kutupilia dhambi mbali, matengenezo ya dim yalifaulu.MwI 156.2

    Kwa mpango huu wa busara Yehoshafati alioupanga kwa ajili ya kuinua hali ya kiroho ya raia zake, alifaulu sana kama mtawala afaaye. Kule kuzitii amri za Mungu huleta faida kuu. Kule kushikamana na matakwa ya Mungu huleta uwezo wa kubadili maisha na kuleta hali ya amani kati ya watu. Kama mafundisho ya neno la Mungu yangefanywa yatawale maisha ya watu, kama mawazo ya watu na nia zao vingetekwa nyara nayo maovu yanayoenea sasa katika maisha ya watu, kitaifa na kimtu binafsi yasingepata nafasi. Kutoka kwa kila nyumba watu wangekuwa na uwezo wa kiroho na kuwa watu waadilifu. Kwa njia hiyo taifa zima na watu binafsi wangejengwa katika msingi ulio imaraMwI 156.3

    Kwa miaka mingi Yehoshafati aliishi kwa amani, bila kuchokozwa na mataifa yaliyomzunguka. “Hofu ya Bwana ikaziangukia falme za nchi zote zilizozunguka Yuda.” Fungu la 10. Kutoka Ufilisti, mfalme aliletewa kodi na zawadi; kutoka Uarabuni makundi makubwa ya kondoo na mbuzi yaliletwa. “Ukuu wake Yehoshafati ukazidi sana; akajenga katika Yuda ngome na miji ya hazina. . . . Watu wa vita, watu washujaa. . . . Hao ndio waliomngojea mfalme, zaidi ya hao mfalme aliowaweka katika miji yenye maboma katika Yuda yote.” Mafungu 12-19. Kwa jinsi alivyofanikiwa kuwa na “mali tele na heshima,” aliweza kuwa na mvuto mkubwa kuelekea katika uk- weli wa neno la Mungu na haki. 2 Mambo ya Nyakati 18:1.MwI 156.4

    Baada ya kupita miaka kadhaa, tangu ashike utawala, wakati huo akiwa katika kilele cha mafanikio, Yehoshafati aliridhika kumwoza mwanawe Yehoramu Athalia binti Ahabu na Yezebeli. Kwa ajili ya ndoa hii, falme mbili hizi zilifanya mwungano, yaani ufalme wa Yuda ukafanya mwungano na ufalme wa Israeli, kinyume cha matakwa ya Mungu. Mwungano huo ulileta maafa kwa mfalme mwenyewe na kwa raia zake pia.MwI 157.1

    Wakati fulani Yehoshafati alikwenda kumtembelea mfalme wa Israeli, yaani Ahabu, huko Samaria. Mfalme huyu aliyetoka Yerusalemu alikaribishwa kwa heshima kuu, na kabla ya kumalizika ziara yake, mfalme Ahabu alimwomba ili amsaidie kupigana na Washami (Syria). Ahabu alitumaini kwamba, kule kuunganisha majeshi yao pamoja atafaulu kuuteka mji wa Ramoth-Gileadi, mmojawapo wa miji ya zamani sana, yenye ngome, ambao aliupigania na kudai kuwa ulikuwa wa Israeli.MwI 157.2

    Ingawa Yehoshafati aliahidi kumwunga mkono Ahabu katika vita hivyo, lakini alipowaza vema, aliona kuwa yapasa kumtegemea Bwana katika shughuli hiyo. Kwa hiyo alimshauri Ahabu akisema: “Uulize leo, nakusihi, ambao ni manabii wa uongo wa huko Samaria, akawauliza, akisema: “Je, tuende Ramoth-Cileadi vitani, au niache? Wakasema, Kwea; kwa kuwa Mungu atautia mkononi mwa mfalme.” Mafungu 4, 5.MwI 157.3

    Yehoshafati hakuridhika na hayo, akataka kujua zaidi juu ya mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo akauliza: “Je, hayuko hapa nabii wa Bwana tena, ili tumwulize?” Fungu 6. Ahabu akasema, “Yuko mtu mmoja, ambaye tungeweza kumwuliza Bwana kwa yeye, yaani Mikaya mwana wa Imla, lakini namchukia, kwa sababu hanibashirii mema, ila mabaya.” 1 Wafalme 22:8. Yehoshafati alikaza kwamba, mtu wa Mungu budi aitwe ili aulizwe. Alipokuja na kuapishwa na Ahabu, kwamba, asiseme jingine, ila la kweli tu, Mikaya alisema, “Naliwaona Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji. Na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani.” Mafungu 16, 17.MwI 157.4

    Maneno hayo ya nabii yangetosha kumwonyesha mfalme kwamba, mpango wao hauna kibali cha mbinguni. Walakini hakuna aliyejali maonyo hayo. Ahabu alikuwa amepanga mambo yake, naye alikusudia kuyatekeleza. Yehoshafati naye alikuwa amemtamkia Ahabu maneno yake akisema: “Nasi tutakuwa pamoja nawe vitani.” Na baada ya kutamka hivyo ilikuwa vigumu kugeuza usemi tena. 2 Mambo ya Nyakati 18:3. “Basi mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda wakak- wea mpaka Ramoth-Gileadi.” 1 Wafalme 22:29.MwI 159.1

    Wakati wa mapigano yaliyofuata, Ahabu alipigwa mshale, na wakati wa jioni alifariki. “Ikapigwa mbiu jeshini, jua likich- wa, kusema: Kila mtu aende mjini kwake, na kila mtu shambani kwake.” Fungu 36. Hivyo, maneno ya nabii Mikaya yakatimia.MwI 159.2

    Mfalme Yehoshafati alirudi kwake Yerusalemu kutoka katika vita hii yenye msiba. Alipokaribia mji, Yehu nabii alimlaki akiwa na ujumbe huu: “Je, imekupasa kuwasaidia waovu, na kuwapenda wamchukiao Bwana? Kwa ajili ya hayo ghadhabu i juu yako itokayo kwa Bwana. Walakini yameonekana mema ndani yako, kwa kuwa umeyaondoa maashera katika nchi, na moyo wako umeukaza kumtafuta Mungu.” 2 Mambo ya Nyakati 19:2, 3.MwI 159.3

    Miaka ya mwisho ya Yehoshafati ilitumika katika kuliimarisha taifa la Yuda kiroho na kijeshi. “Akatoka tena kwenda kati ya watu toka Beer-sheba mpaka milima ya Efraimu, akawarudisha kwa Bwana, Mungu wa baba zao.” Fungu la 4.MwI 159.4

    Jambo mojawapo muhimu Yehoshafati alilofanya ni kule kujenga mahakama ya kuhukumia haki za watu. “Akasimamisha makadhi katika nchi, katikati ya miji yote yenye maboma ya Yuda, mji kwa mji; akawaambia hao makadhi, Angalieni myafanyao; kwa kuwa hamfanyii mwanadamu hukumu, ila Bwana; naye yupo pamoja nanyi katika neno la hukumu. Basi sasa hofu ya Bwana na iwe juu yenu; angalieni mkaifanye; kwa maana kwa Bwana, Mungu wetu, hapana uovu, wala kujali nafsi za watu, wala kupokea zawadi.” Mafungu 5-7MwI 159.5

    Mahakama ya hukumu yaliendeshwa barabara, kwa njia ya kuwa na mahakama ya rufani huko Yerusalemu, ambako Yehoshafati “alisimamisha Walawi, na makuhani, na wakuu wa mbari za mababa wa Israeli wawe kwa hukumu ya Bwana, na kwa mateto.” Fungu 8.MwI 160.1

    Mfalme aliwaagiza waamuzi hawa wawe waaminifu. “Ndivyo mtakavyotenda kwa hofu ya Bwana, kwa uaminifu, na kwa moyo kamili. Na kila mara watakapowajia na teto ndugu zenu wakaao mijini mwao, kati ya damu na damu, kati ya torati na amri, sheria na hukumu, mtawaonya wasiingie hatiani mbele za Bwana, mkajiliwa na ghadhabu ninyi na ndugu zenu; fanyeni haya wala hamtakuwa na hatia.MwI 160.2

    Tena angalieni, Amaria, kuhani mkuu, yu juu yenu kwa maneno yote ya Bwana; naye Zebadia, mwana wa Ishmaeli jemadari wa nyumba ya Yuda, kwa maneno yote ya mfalme Walawi nao watakuwa wasimamizi mbele yenu. Jitieni nguvu, mtende, naye Bwana awe pamoja nao walio wema.” Mafungu 9-11.MwI 160.3

    Mpango huu uliopangwa kwa uangalifu kwa ajili ya kulinda haki na uhuru wa raia, Yehoshafati alisisitiza kwamba kila binadamu hupokea haki yake kutoka kwa Mungu atawalaye pote. “Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; katikati ya miungu anahukumu.” Na watu ambao huwekwa kuwa waamuzi chini yake hawana budi kumtetea “maskini na yatima,” lazima kumtendea “haki aliyeonewa na fukara.” Na “kuwaopoa mikononi mwa wadhalimu.” Zaburi 82:1, 3, 4.MwI 160.4

    Karibu na mwisho wa utawala wa Yehoshafati, nchi ya Yuda ilishambuliwa na jeshi lililowatetemesha wenyeji wote wa Yuda. “Wana wa Moabi, na wana wa Amoni, na pamoja nao baadhi ya Wameuni, wakaja juu ya Yehoshafati vitani.” Habari ya shambulio hilo ilimfikia mfalme kwa njia ya mjumbe aliyekuja na maneno haya: “Wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shambu toka ng'ambo ya bahari; na tazama wako katika Hasasontamari (Engedi).” 2 Mambo ya Nyakati 20:1, 2.MwI 160.5

    Yehoshafati alikuwa mtu shujaa na mwenye moyo mkuu. Kwa muda wa miaka mingi alikuwa akiliimarisha jeshi lake na miji yenye maboma. Alikuwa amejitayarisha kukutana na adui ye yote; walakini katika tatizo hili hakutegemea nguvu ya kimwili. Hakutumaini jeshi la askari lililofundishwa vema, wala miji yenye maboma. Bali alimtumaini Mungu wa Israeli, kwamba ndiye anayeweza kushinda majeshi haya ya waabudu sanamu yaliyokuwa yakijitapa kwamba yataiangamiza Yuda, mbele ya mataifa.MwI 161.1

    Vehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake amtafute Bwana; akatangaza mbiu ya watu kufunga katika Yuda yote. Yuda wakakusanyika pamoja ili wamtafute Bwana; hata kutoka miji yote ya Yuda wakaja kumtafuta Bwana.”MwI 161.2

    Yehoshafati akisimama katika ukumbi wa hekalu, mbele ya watu wake, aliomba maombi ya moyo, akimsihi Mungu na kudai ahadi zake, na kukiri kwamba Israeli wote hawana uwezo, alisema: “Ee Bwana, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu ye yote kusimama kinyume chako. Si wewe Ee, Mungu wetu uliyewafukuza wenyeji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, ukawapa wazao wa Ibrahimu rafiki yako hata milele? Nao walikaa humo, wamekujengea patakatifu na jina lako humo, wakisema, Yakitujia mabaya, upanga, hukumu, au tauni au njaa, tutasimama mbele ya nyumba hii na mbele zako, na kukulilia katika shida yetu, wewe utasikia na kuokoa. Na sasa, tazama, wana wa Amoni na Moabi, na wa mlima Seiri, ambao hukuwaacha Israeli waingie katika nchi yao, walipotoka nchi ya Misri, lakini wakawageukia mbali, wasiwaharibu; tazama jinsi wanavyotulipa, wakija kututupa toka milki yako, uliuoturithisha. Ee Mungu wetu, Je, hutawahukumu? Maana sisi hatuna uwezo juu ya jamii kubwa hii wanaotujia juu yetu, wala hatujui tufanyeje; lakini macho yetu yatazama kwako.” Mafungu 3-12.MwI 161.3

    Yehoshafati aliweza kusema kwa ujasiri kwamba: “Macho vetu yatazama kwako.” Kwa muda wa miaka mingi alikuwa amefundisha watu wamtumaini Mungu ambaye kwa miaka ya zamani aliwaokoa wateule wake na uharibifu; na sasa wakati ufalme umo hatarini, Yehoshafati hakuachwa asimame mwenyewe. “Wakasimama Yuda wote mbele za Bwana, pamoja na wadogo wao, na wake zao, na watoto wao.” Fungu 13. Walifunga na kuomba kwa umoja na kwa umoja walimsihi Bwana awachafue adui zao, ili jina la Yehova lipate kutukuzwa. “Ee Mungu usinyamaze, wala usitulie,MwI 161.4

    Maana adui zako wanafanya ghasia,
    Nao wakuchukiao wameviinamia vichwa vyao.
    Juu ya watu wako wanefanya hila,
    Na kushauriana juu va uliowaficha.
    Wamesema, Njooni tu wakatilie mbali wasiwe taifa.
    Na jina la Israeli hal kumbukwa tena.
    Maana wanashauriana kwa moyo mmoja,
    Juu yako wanafanya na agano.
    Hema za Edomu na Waishmaeli,
    Na Moabi na Wahagari Gebalia na Amoni na Amaleki. . .
    Uwatende kama Midiani, kama Sisera,
    Kama Yabini penye kijito Kishoni. . . .
    Waaibike, wafadhaike milele,
    Naam, watahayarike na kupotea.
    Wajue ya kuwa wewe, uitwaye jina lako YEHOVA,
    Ndiwe peke yako uliye juu, juu ya nchi yote.
    MwI 162.1

    ” Zaburi 83.

    Watu wote pamoja na mfalme wao walipojidhili mbele za Mungu, na kumwomba msaada, Roho wa Bwana akamjia Yahazieli, Mlawi wa wana wa Asafu, naye akasema: “Sikieni, Yuda wote, nanyi mkaao Yerusalemu, na wewe mfalme Yehoshafati; Bwana awaambia hivi: Msiogope, wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili, kwani vita si yenu, bali ni ya Bwana, Mungu. Kesho shukeni juu yao; tazameni wanakwea kwa kupandia sisi; nanyi mtawapata penye mwisho wa bonde; mbele ya jangwa la Yerueli. Hamtahitaji kupigana vita, jipangeni simameni, mkauone wokovu wa Bwana ulio pamoja nanyi, enyi Yuda na Yerusalemu; msiogope wala msifadhaike; kesho tokeni juu yao, kwa kuwa Bwana yu pamoja nanyi.MwI 162.2

    Yehoshafati akainama kichwa kifudifudi, wakaanguka mbele za Bwana Yuda wote, na wakaao Yerusalemu, wakamsujudia Bwana. Na Walawi wana wa Wakohathi, na wana wa Wakorahi, wakasimama ili wamsifu Bwana, Mungu wa Israeli, kwa sauti kuu sana.MwI 162.3

    Keshoye asubuhi mapema, wakaondoka kwenda katika iangwa la Tekoa ili kupigana. Walipokuwa wakienda Yehoshafati alisema: “Nisikieni enyi Yuda, nanyi wenyeji wa Yerusalemu; Mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa. Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia Bwana, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu.” 2 Mambo ya Nyakati 20:14-21. Waimbaji hawa hawa walitangulia mbele ya jeshi wakiinua sauti zao katika kumsifu Mungu kwa nyimbo kwa ajili ya ahadi yake ya ushindi.MwI 163.1

    Hii ilikuwa njia ya pekee ya kwenda kupigana vita, katika kukutana na jeshi la adui watu walikuwa wakimhimidi Mungu tu. Huo ndio uliokuwa wimbo wao wa vita. Walikuwa na uzuri wa utakatifu. Walipomsifu Mungu kwa moyo, walipata kuwa na ujasiri na ushujaa. Je, hali kama hiyo haitawatia nguvu askari wanaoitetea kweli siku hizi?MwI 163.2

    “Bwana akaweka waviziao juu ya wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, waliokuja juu ya Yuda; nao wakapigwa. Kwani wana wa Amoni na wana wa Moabu waliwaondokea wenyeji wa mlima Seiri kuwaulia mbali; na kuwaharibu, nao walipokwisha kuwakomesha hao wakaao Seiri, wakajitia kuharibu kila mtu mwenziwe. Hata Yuda walipofika mnara wa kulindia wa jangwani, wakalitazama hilo jeshi, nao, angalia, walikuwa maiti walioanguka nchi, wala hapana aliyeokoka.” Mafungu 22-24.MwI 163.3

    Katika shida hii Bwana ndiye alikuwa nguvu ya Yuda, na yeye ndiye nguvu ya watu wake hata leo. Hatupaswi kuwategemea wakuu, au kuwaweka wanadamu mahali pa Mungu. Lazima tukumbuke kuwa wanadamu ni wakosefu wenye kumangamanga. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu mwenye nguvu zote, ndiye mnara wetu wa ulinzi. Kwa kila tatrzo lazima tujisikie kuwa vita ni ya Bwana. Uwezo wake haukomi, na yale yanayoonekana kuwa hayawezekani, yatawezekana dhahiri.MwI 163.4

    “Ee Mungu wa wokovu wetu, utuokoe,
    Utukusanye kwa kututoa katika mataifa,
    Tulishukuru jina lako takatifu,
    Tuzifanyie shangwe sifa zako.”
    MwI 164.1

    Jeshi la Yuda likarudi na nyara nyingi mno. “Kisha wakarudi. . . . Yerusalemu kwa furaha; kwa kuwa Bwana amewafurahisha juu ya adui zao. Wakafika Yerusalemu wenye vinanda na vinubi na mapanda kwenda nyumbani kwa Bwana.” 2 Mambo ya Nyakati 20:27, 28. Furaha yao ilikuwa kubwa sana, nayo ilisababishwa na mambo makuu Bwana aliyowatendea; walipotii agizo lile, kwamba: “Simameni, mkauone wokovu wa Bwana. . . . Msiogope, wala msifadhaike.” Fungu la 17. Walimtegemea kabisa Mungu, naye akawawia ngome halisi, na Mkombozi wao. Ndipo wakaimba kwa hakika wimbo huu: “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,MwI 164.2

    Msaada . . . tele wakati wa mateso. . . .
    Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.
    Acheni, mjue ya kuwa mimi ni Mungu.
    Nitatukuzwa katika mataifa,
    Nitatukuzwa katika nchi.
    Bwana wa majeshi yu pamoja nasi
    Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.”
    MwI 164.3

    Zaburi 46.

    “Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu
    Ndivyo na sifa zako hata miisho ya dunia.
    Mkono wako wa kuume umejaa haki
    Na ufurahi mlima Sayuni
    Binti za Yuda na washangilie
    Kwa sababu ya hukumu zako. . . .
    Kwa maana ndivyo alivyo, Mungu, Mungu wetu,
    Milele na milele, yeye ndiye atakayetuongoza.”
    MwI 164.4

    Zaburi 48:10-14.

    Kwa ajili ya imani ya mfalme wa Yuda na jeshi lake, “Ikawa hofu ya Mungu juu ya falme zote za nchi, waliposikia ya kuwa Bwana amepigana juu ya adui za Israeli. Basi ukatulia ufalme wake Yehoshafati, kwa sababu Bwana Mungu wake amemstarehesha pande zote.”MwI 164.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents