Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    14—“Katika Roho Na Nguvu Za Eliya”

    Kwa muda mrefu wa karne nyingi zilizopita, habari zilizoandikwa za maisha ya Eliya na kazi yake, zimeleta uamsho mkuu kwa watumishi wa Mungu, walioitwa kuitetea kweli katika kizazi kipotofu. Na kwetu sisi, “tuliofikiliwa na miisho ya zamani,” (1 Wakorintho 10:11), maneno haya ni muhimu sana.MwI 143.1

    Historia imerudiwa. Leo ulimwenguni kuna Ahabu wengi na Yezebeli wengi. Kizazi hiki ni chenye kuabudu miungu, sawasawa na kizazi cha wakati wa Eliya. Huenda madhabahu ya kuabudia hayaonekani; hata sanamu zilizosimamishwa ili ziabudiwe huenda hazionekani kwa macho; hata hivyo, watu maelfu huabudu miungu ya dunia hii, yaani miungu ya utajiri, heshima, anasa na masimulizi ya kuburudisha, ambayo hayagusi moyo wa mtu na kuuamsha. Watu wengi mno wanamfikiri Mungu vingine kabisa, jinsi asivyo; nao kwa kweli wanatumikia miungu ya uongo, kama wale waliokuwa wakiabudu Baali. Wengi, hata miongoni mwa wakristo wamejiunga na mivuto ile iliyo kinyume cha Mungu na ukweli wake. Na kwa njia hiyo wamegeuka kutoka katika njia ya Mungu, na kufuata njia za wanadamu na kuzitukuza.MwI 143.2

    Roho iliyomo dunia wakati wetu huu ni roho ya ukafiri na Watu huonekana kana kwamba wanaijua kweli ya neno la ngu sana, lakini kwa kweli ni vipofu wa kupindukia. Mawazo kibinadamu hutukuzwa badala ya mpango wa Mungu netani huwashawishi watu wasimtii Mungu, akiwaahidi Kwamba, kule kutoyatii mashauri ya Mungu, kutawapatia maendeleo makubwa na ujuzi utakaowafanya wawe kama miungu. Roho ya kuyapinga maendeleo makubwa na ujuzi utakaowafanya wawe kama miungu. Roho ya kuyapinga maneno ya Mungu inadhihirika wazi duniani, roho ya kuabudu sanamu, ambayo huyatukuza maarifa ya mwanadamu kuliko Mungu. Watu wameachia mawazo yao yatiwe giza, kwa hiyo wamechanganyikiwa kwa vile walivyojiunga na ulimwengu na kawaida zake, hata hawapambanui kati ya nuru na giza, na kati ya kweli na uongo Wamejitenga mbali sana na njia ya wima, mpaka wakashikamana na maongozi ya watu wanaojiita wataalam, wakauacha ukweli wa BibliaMwI 144.1

    Mwito wa Mungu wa kusihi, ahadi zilizomo katika Biblia, na adhabu ir.ayotangazwa juu ya wakaidi wote na wenye kuabudu sanamu, hayo yote hayawezi kuyeyusha mioyo yao migumu. Imani kama ile ya Paulo, Petro, na Yohana, wao huiona kuwa ni hadithi za zamani zisizo na maana yo yote kwa mtu wa kisasa.MwI 144.2

    Huko mwanzoni Mungu alimpa mwanadamu sheria yake iwe njia ya kumletea raha na kumpatia uzima wa milele. Tumaini la Shetani ni kumpotosha mwanadamu ili aiasi sheria hii, ili apinge kusudi la Mungu; naye daima amekuwa akikazana kuyapotosha mafundisho ya Mungu na kuyahafifisha. Shabaha yake kuu imekuwa kujaribu kuibadili sheria yenyewe, ili kusudi wanadamu waivunje wakati wanapodhani kuwa wanaishika na kuitii.MwI 144.3

    Mwandishi mmoja amefananisha jaribio la kubadili sheria ya Mungu na tendo baya lililotendwa zamani, la kubadili kibao kilichoandikwa na kusimamishwa kwenye njia panda, kuonyesha upande njia zinakokwenda, kikageuzwa na kuelekezwa kwingine. Taabu na mahangaiko yaliyoletwa na tendo hili yalikuwa makubwa.MwI 144.4

    Kibao cha kuonyesha njia ya mbinguni kiliwekwa na Mungu ili kiwasaidie wasafiri wa ulimwengu huu. Mkono mmoja wa kibao hiki unaonyesha utii wa hiari kwa Mungu Mwumbaji, kama barabara inayokwenda kwenye heri na kwenye uzima; wakati mkono wa pili wa kibao huonyesha ukaidi na kutotii kama barabara inayokwenda kwenye uharibifu na mauti. Njia iliyokwenda kwenye raha ilionyeshwa wazi wazi kama njia iliyokuwa ikienda kwenye miji ya kukimbilia, wakati wa Israeli. Lakini wakati wetu huu, ambao ni mwovu, adui wa mema yote, amegeuza kibao na kukielekeza upande mwingine na watu makundi makundi, wamekoseshwa wakafuata njia mbaya.MwI 145.1

    Bwana aliwaagiza Waisraeli kwa kinywa cha Musa, akisema: “Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi. Basi mtaishika hiyo Sabato kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa. . . . Kila mtu atakayefanya kazi yo yote katika siku ya Sabato hakika yake atauawa. Kwa ajili ya haya wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele. Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika.” Kutoka 31:13-17.MwI 145.2

    Kwa maneno haya Bwana anadhihirisha wazi kwamba, njia ya kuuingia mji wa Mungu ni kuyatii maagizo yake; lakini mtu wa dhambi amegeuza kibao cha njiani akakielekeza upande mwingine, ambao sio wa kweli. Ameanzisha Sabato ya uongo na kuwafikirisha watu kwamba, wanapopumzika siku hiyo wanatii sheria ya Mungu Mwumbaji.MwI 145.3

    Mungu amenena kwamba, siku ya Saba ni Sabato ya Bwana Mungu. Wakati “mbingu na nchi zilipomalizika,” aliitukuza siku hiyo iwe ukumbusho wa kazi yake ya kuumba. Alistarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa.” Mwanzo 2:1-3.MwI 145.4

    Wakati wa kutoka huko Misri, Sabato ilidhihirishwa wazi kwa watu wa Mungu. Wakati walipokuwa wangali utumwani, wasimamizi wao katika kazi walijaribu kuwalazimisha wafanye kazi na siku ya Sabato kwa njia ya kuongeza kazi zaidi kila juma. Hali ya kazi yao ilizidi kuwa ngumu zaidi na zaidi. Lakini Waisraeli walikombolewa, wakaletwa mahali ambapo walikuwa huru kuyatii maagizo ya Bwana bila udhia wo wote. Sheria ilinenwa huko Sinai, ikaandikwa pia katika “mbao mbili za mawe zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu.” Kutoka 31:18. Na kwa muda wa miaka arobaini ya kuzunguka kwao jangwani, daima Waisraeli walikuwa wakikumbushwa juu ya siku takatifu ya Bwana ya kupumzika, kwa njia ya kuzuia manna isiwepo kila siku ya saba, na kuihifadhi ile iliyokusanywa siku ya sita, ambayo ni siku ya maandalio ili isioze.MwI 145.5

    Kabla Waisraeli hawajaingia katika nchi ya ahadi, walikumbushwa na Musa “kuishika siku ya Sabato na kuitakasa.” Kumbukumbu la Torati 5:12. Bwana alikusudia kwamba, kwa njia ya kuishika amri ya Sabato kwa uaminifu, Waisraeli wangekumbushwa daima juu ya Mungu kwamba, ndiye Mwumbaji wao na Mwokozi wao.MwI 147.1

    Kama wangeshika Sabato kwa nia halisi, ibada ya sanamu ingetoweka. Lakini kama agizo la Bwana kuhusu Sabato likidharauliwa, Mungu pia atasahauliwa, nao wataanza kuabudu miungu mingine. Mungu alinena: “Niliwapa Sabato zangu ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, Bwana, ndimi niwatakasaye.” Lakini “walizikataa hukumu zangu, wala hawakuenda katika amri zangu, wakazitia unajisi Sabato zangu, kwa maana mioyo yao iliandama vinyago vyao Katika kusihi kwake ili wamrudie alielekeza mawazo yao hasa waone umuhimu wa kuitakasa Sabato. Alisema, “Mimi ni Bwana Mungu wenu; endeni katika amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzitenda; zitakaseni Sabato zangu, nazo zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.” Ezekieli 20:12, 16, 19, 20.MwI 147.2

    Bwana alipowasihi watu wa Yuda wajihadhari na uovu uliosababisha kuchukuliwa mateka na Wababeli baadaye, alisema: “Umezitia unajisi Sabato zangu.” “Kwa sababu hiyo nimemwaga ghadhabu yangu juu yao; nimewateketeza kwa moto wa hasira yangu; nami nimeileta njia yao wenyewe juu ya vichwa vyao.” Ezekieli 22:8, 31.MwI 147.3

    Wakati wa Nehemia, Bwana alipowarudisha watu Yerusalemu, uvunjaji wa Sabato ulikaripiwa vikali, kwa maneno haya: “Je! sivyo hivyo walivyofanya baba zenu; na Mungu wetu, je! hakuyaleta mabaya haya yote juu yetu, na juu ya mji huu? Nanyi hata hivyo mwazidi kuleta ghadhabu juu ya Israeli kwa kuinajisi Sabato!” Neh. 13:18.MwI 148.1

    Wakati Kristo alipokuwa hapa duniani, alikazia juu ya ulazima wa kuitunza Sabato. Katika mafundisho yake yote alionyesha heshima kwa Sabato ambayo ilianzishwa na yeye mwenyewe. Siku hizo Kristo alizoishi duniani, Sabato ilikuwa imepotoshwa mno, hata utunzaji wake, haukuonyesha tabia ya Mungu, bali tabia ya kujipenda nafsi. Kristo alifafanua mafundisho ya uongo, ambayo kwayo waliokuwa wakijidai kwamba wanamtumikia Mungu, walionekana kuwa waongo.MwI 148.2

    Ingawa Kristo alikuwa akishambuliwa kwa maneno na Waongozi wa Mafarisayo na Waandishi, ambao walikuwa wakorofi sana, lakini yeye hakujaribu hata kidogo kushirikiana nao katika kutunza Sabato, bali aliitunza vema kama inavyoagizwa katika sheria ya Mungu.MwI 148.3

    Alinena dhahiri kwa lugha wazi kuhusu sheria ya Mungu, kwa maneno haya: “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.” Mathayo 5:17-19.MwI 148.4

    Wakati wa mgawanyiko wa ukristo, adui mkuu, anayechukia mema yote, ameyaelekeza mashambulio yake kwenye amri ya nne, yaani ya Sabato. Shetani asema “Nitapingana na makusudi ya Mungu. Nitawawezesha wafuasi wangu, waweze kuiondoa Sabato ya siku ya saba, ambavo ni ukumbusho wa uumbaji wa Mungu. Basi nitauonyesha ulim- wengu kwamba, siku ile iliyotakaswa na kubarikiwa na Mungu imebadilishwa. Hivyo siku hiyo isahauliwe na watu. Nitaifutilia mbali katika kumbukumbu. Badala yake nitaweka siku tu ya kawaida, ambayo haikuamriwa na Mungu, siku ambayo siyo ishara kati ya Mungu na watu wake. Nitawafanya watu watakaoikubali waiwekee utukufu na utakatifu ule Mungu aliowekea siku ya saba.MwI 148.5

    Kwa njia ya mjumbe wangu, nitajitukuza sana. Siku ya kwanza ya juma itatukuzwa sana, na Waprotestanti wote wataipokea kwa nia Sabato hii ya uongo kana kwamba ni Sabato ya kweli. Kwa njia ya kuacha kutunza Sabato ya kweli ambayo ilianzishwa na Mungu mwenyewe, nitaifanya sheria yake idharauliwe kabisa. Neno lisemalo kwamba, “Iwe ishara kati yangu na wao,” litaeleweka kana kwamba lilinenwa juu ya Sabato ya jumapili, niliyoianzisha mimi.MwI 149.1

    Hivyo ndivyo nitakavyowapata watu wote wa ulim- wenguni. Nitakuwa mtawala wa dunia. Nitaongoza nia na mawazo ya watu mpaka waidharau Sabato ya kweli ya Mungu. Ishara? Nitafanya kule kutunza Sabato ya kweli kuonekane kwamba ni ishara ya uasi, mbele ya watawala wa nchi. Sheria za nchi zitatungwa kali sana ili kuwaogofya watu wasiitunze Sabato ya siku ya saba. Kwa ajili ya hofu kwamba watakosa riziki na mavazi, watakuwa tayari kuungana na ulimwengu ili kumwasi Mungu na sheria yake. Na nchi yote itakuwa chini ya utawala wangu.”MwI 149.2

    Kwa njia ya kuanzisha Sabato ya uongo, adui Shetani alidhani kuwa atabadili sheria ya Mungu na wakati. Walakini, je, kweli amefaulu kuibadili sheria ya Mungu? Maneno ya Kutoka 31:13, 17 ndiyo yanatoa jawabu. Mungu ambaye ni yule yule jana na leo na hata milele anazungumzia Sabato ya siku ya saba akisema: “Ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote” . . . “Ni ishara. . . ya milele.” Kutoka 31:13, 17. Kibao kile kilichopotoshwa huwaelekeza wasafiri upande usio wa kweli, lakini Mungu ni yule asiyebadilika. Yeye ni Mungu Mwenyezi wa Israeli. “Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama, yeye huvinyanyua visima kama ni kitu kidogo sana. Lebanoni nayo hautoshi kwa kuni, wala wanyama wake hawatoshi kwa kafara. Mataifa yote huwa kama si kitu mbele zake; huhesabiwa kwake kuwa duni ya si kitu, na ubatili.” Isaya 40:15-17. Naye anaona wivu kwa ajili ya kuivunja sheria yake sasa, sawasawa na jinsi alivyokuwa wakati wa Ahabu na Eliya.MwI 149.3

    Lakini sheria inadharauliwaje! Tazameni ulimwengu leo unamwasi Mungu wazi wazi. Kweli hiki ni kizazi kikaidi kisichokuwa na shukrani, kizazi kinafiki, chenye hila, chenye majivuno na kuasi. Watu hudharau Biblia na kuchukia ukweli. Yesu huona kuwa sheria yake inakataliwa, upendo wake unadharauliwa, Wajumbe wake wanatendewa kijeuri. Yeye amewabembeleza kwa huruma, lakini wao hawakumkubalj. Amewatolea maonyo, lakini hawakuyajali. Mahekalu matakatifu, ambayo ni mioyo ya wanadamu, yamegeuzwa na kufanywa kuwa mahali pa mambo machafu. Uchoyo na kujipenda nafsi, kijicho, kiburi na majivuno, ukorofi na uovu wote unapendwa sana na kutunzwa.MwI 150.1

    Watu wengi hawa hawasiti kulidhihaki neno la Mungu. Na wote wanaoliamini jinsi lilivyo huonekana kama vichekesho tu. Hali ya kudharau sheria na utaratibu inazidi sana, nayo hutokana na kuziasi amri za Mungu. Maasi na uhalifu nchini hutokana na kule kuasi na kuiacha njia nyofu ya utii kwa maagizo ya Yehova. Lo, ni hali ya kuhurumiwa ya kiasi gani waliyo nayo makutano wenye kuabudu sanamu, huku wakiitafuta amani na raha bila kuiona.MwI 150.2

    Lo, ulimwengu umeidharau amri ya Sabato kiasi gani. Ona jinsi wanavyowayawaya watu wale waliothubutu kuhalalisha siku ya kwanza ya juma kuwa sheria ilindayo, na wakati ule ule kuhalalisha vileo pia. Wakijifanya wajuzi kuliko yale yaliyoandikwa, hujaribu kulazimisha dhamiri za watu, wanaporuhusu maovu yawaharibu watu walioumbwa kwa sura ya Mungu. Shetani mwenyewe ndiye anayeruhusu mambo ya jinsi hiyo. Anajua kuwa laana ya Mungu itawakalia wale wanaotukuza sheria za wanadamu kuliko sheria ya Mungu; naye hujitahidi kadiri awezavyo kuwaongoza watu wafuate njia pana iendayo uharibifuni.MwI 150.3

    Kwa muda mrefu wanadamu wamekuwa wakitukuza mawazo ya watu na kufuata mafundisho yao, hivyo karibu ulimwengu mzima umekuwa ukiabudu sanamu. Na yule aliyejitahidi kuibadili sheria ya Mungu, anatumia kila namna ya udanganyifu ili kuwafanya watu wawe kinyume na Mungu na kuipinga ishara ile iliyowekwa na Mungu ili kuwatambulisha wenye haki. Lakini Bwana kila mara hataacha sheria yake ivunjwe na kudharauliwa na wakaidi. Wakati unakuja, ambapo, “Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye Bwana, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.” Isaya 2:11. Wenye mashaka wanaweza kuiona sheria ya Mungu kwa namna ya dharau, mzaha na kutojali. Roho ya ulimwengu inaweza kuwachafua watu wengi na kubakiza wachache, kazi ya Mungu inaweza kuendelea tu kwa njia ya jitihada kubwa na kujinyima kwa daima, walakini mwishowe ukweli utafaulu kwa shangwe kuu.MwI 150.4

    Katika kufunga kazi ya Mungu duniani, kiwango cha sheria yake kitatukuka. Dini za uongo zinaweza kuenea pote, maovu yanaweza kuwako kila mahali, upendo wa watu wengi utaweza kupoa, msalaba wa Kalwari unaweza ukakosa kutambuliwa, giza nene kama nguo nyeusi inayofunikia jeneza la maiti linaweza kuenea mahali pote; ulimwengu wote na majeshi yake unaweza kuipinga kweli; njama kwa njama zinaweza kufanywa juu ya watu wa Mungu; lakini wakati wa hatari kuu Mungu wa Eliya atainua wanadamu ambao ni vyombo vyake, wauchukue ujumbe ambao hautanyamazishwa na kitu cho chote. Katika miji miovu ya dunia, na mahali ambapo wanadamu wamek- wenda mbali sana na Mungu, sauti kali ya karlpia itasikika. Watu wa Mungu watakanusha kwa ujasiri kabisa mwungano wa kanisa pamoja na ulimwengu. Watawasihi watu kwa bidii watoke katika njia ya kutukuza siku uliyowekwa na wanadamu, warudi kumwabudu Mungu katika Sabato ya kweli.” Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji. . . . Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake.” Ufunuo 14:7-10.MwI 151.1

    Mungu hatavunja agano lake, au kuondoa kitu cho chote alichotamka na kinywa chake. Neno lake litasimama imara milele kama vile kiti chake cha enzi kisivyoweza kubadilika. Katika hukumu agano hili litaletwa, lililoandikwa dhahiri na chanda cha Mungu, na ulimwengu utapasishwa hukumu mbele ya Mwenyezi, ili kila mtu apokee stahili yake.MwI 152.1

    Leo, kama ilivyokuwa siku za Eliya, mpaka kati ya watu wanaoshika amri za Mungu, na wale wanaoabudu miungu ya uongo, umekwisha kuwekwa wazi. Siku zile Eliya alipaaza sauti na kusema, “Mtasitasita katikati ya mawazo mawili hata Iini ? Bwana akiwa ndiye Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! Mfuateni yeye.” 1 Wafalme 18:21. Na ujumbe wa siku hizi ni huu: “Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu. . . . Tokeni kwake, enyl watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.” Ufunuo 18:2, 4, 5.MwI 152.2

    Wakati hauko mbali, ambapo kila mtu atajaribiwa. Tutalazimishwa kushika Sabato ya uongo. Shindano litakuwa kati ya amri ya Mungu na maagizo ya wanadamu. Wale ambao wamejisogeza katika kanuni za ulimwengu kidogokidogo, wataanguka katika majaribu hayo yajayo, kuliko kudhihakiwa, kutukanwa, kutishiwa kifungo na kuuawa. Wakati huo dhahabu itatengana na takataka. Utawa halisi utatambulikana wazi, ukiwa tofauti na utawa wa kuigiza. Wengi ambao sasa wanang'aa kama nyota na sisi tunashangaa kwa imani waliyo nayo, watazimika na kutoweka gizani. Wale waliojipamba kwa mavazi ya kanisa tu, wala hawakuvikwa vazi la haki ya Kristo, wataonekana kwa aibu wakiwa uchi.MwI 152.3

    Miongoni mwa wenyeji wa duniani, ambao wametawanyika pande zote za nchi, wako watu ambao hawajapiga magoti yao mbele ya Baali. Watu waaminifu hawa watang'aa na kutoa nuru yao wakati wa giza kuu la dunia, sawasawa na nyota za mbinguni zinavyong'aa wakati wa giza Katika Afrika, ambayo ni nchi ya waabudu sanamu; katika Ulaya ambayo ni nchi ya Ukatoliki; katika Amerika ya Kusini; katika China; katika India; katika visiwa vya bahari na pande zote za giza duniani, Mungu anao wateule wake watakaong'aa katika giza kuu, wakiudhihirishia ulimwengu ulioasi uwezo wa Mungu uwezao kubadili maisha ya watu wanaoitii sheria yake. Watu hao hata sasa wanaonekana katika kila taifa, kati ya kila kabila na lugha; na wakati wa uasi mkuu, Shetani atakapofanya bidii yake yote ili “awafanye wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa” wapokee alama ya kuonyesha heshima yao kwa sabato ya uongo, ambao ni jumapili, au la sivyo, wauawe. Waaminifu hawa “wasio na lawama, wala udanganyifu, wana wa Mungu wasio na ila, watang'aa kama mianga katika ulimwengu.” Ufunuo 13:16; Wafilipi 2:15. Kadiri giza la usiku litakavyozidi, ndivyo nao watakavyong'aa.MwI 152.4

    Eliya ilimpasa kufanya kazi tofauti kadiri gani katika kuwahesabu Waisraeli wakati hukumu za Mungu zilipokuwa zikiwaangukia waasi. Yeye alipotaja hesabu ya wenye haki, ambao ni waaminifu alisema: “Nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu waiondoe.” Neno la Bwana lilimshangaza, liliponenwa: “Nimejisazia katika Israeli watu elfu saba, kila goti lisilomwinamia Baali.” 1 Wafalme 19:14, 18.MwI 153.1

    Leo mtu ye yote asijaribu kuhesabu Waisraeli, yaani Wakristo walio waaminifu; ila tu kila mtu awe na moyo wa nyama, moyo wenye huruma, moyo unaofanana na moyo wa Kristo, moyo unaowatafuta wapotevu na kuwaleta kwenye wokovu.MwI 153.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents