Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    16—Anguko La Nyumba Ya Ahabu

    Mvuto mwovu Yezebeli aliomwambukiza Ahabu ulidumu kuendelea mpaka mwisho wa utawala wake, nao ulizaa matunda ya uasi wa aibu, ambayo haijaonekana katika historia takatifu. “Hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa Bwana, ambaye Yezebeli mkewe alimchochea.”MwI 167.1

    Hali ya asili ya Ahabu ya choyo na kujipenda, ilitiwa nguvu na Yezebeli mkewe ili atimize mapenzi ya moyo wake mpaka baadaye akatawaliwa na choyo na kuzidi kutenda maovu. Hakuweza kujizuia katika lo lote, ila jambo alilolitamani alijipa haki ya kulipata.MwI 167.2

    Tabia hii mbovu iliyomtawala Ahabu na kuleta msiba kwa ufalme katika watawala waliofuata, inadhihirika katika tukio lililotukia wakati Eliya alipokuwa angali nabii katika Israeli. Karibu na jumba lake la kifalme, palikuwako na shamba la Nabothi Myezreeli. Ahabu akalitamani shamba hilo. Alikusudia kulinunua, au kubadilishana na Nabothi, ampe shamba lingine. Alimwambia Nabothi “Nipe shamba lako la mizabibu, nilifanye shamba la mboga, maana ni karibu na nyumba yangu; nami nitakupa badala yake shamba la mizabibu lililo zuri zaidi; au ukipenda, nitakupa fedha sawasawa na thamani yake.”MwI 167.3

    Nabothi alilithamini shamba hilo zaidi kwa sababu ni urithi wa baba zake; kwa hiyo akakataa kulitoa. Nabothi alisema, “Bwana apishe mbali nikupe wewe urithi wa baba zangu.” Kufuata sheria ya walawi, hakuna ruhusa kutoa nchi kwa njia ya kuuza, au kubadili; kila Mwisraeli ilimpasa “kushikamana kila mtu na urithi wa kabila ya baba zake.” Hesabu 36:7.MwI 168.1

    Kukataa kwa Nabothi kulimwuguza mfalme. “Basi Ahabu akaenda nyumbani kwake, ana moyo mzito, tena amekasirika, kwa sababu ya neno lile aliloambiwa na Nabothi Myezreeli. . . . Akajilaza kitandani pake, akageuza uso wake, akakataa kula.”MwI 168.2

    Baadaye Yezebeli akagundua sababu ya hayo yote, akaudhika sana, kwamba mtu anawezaje kukataa matakwa ya mfalme, akamhakikishia Ahabu kwamba atakomesha masikitiko yake, na moyo wake utachangamka. Akatamka na kusema, “Je! sasa wewe unaumiliki ufalme wa Israeli? Ondoka, ule chakula, moyo wako ufurahi; mimi nitakupa shamba la mizabubi la Nabothi Myezreeli.”MwI 168.3

    Ahabu hakujali, kwamba mkewe atatumia njia gani kulipata hilo shamba. Mara moja Yezebeli alianza kushughulika na mipango yake miovu. Aliandika barua kwa jina la mfalme, akazitia muhuri wa mfalme, halafu akazituma kwa wazee na wakuu wa mji ule anamokaa Nabothi, kusema: “Pigeni mbiu ya watu kufunga, mkamweke Nabothi juu mbele ya watu; mkainue watu wawili, watu wasiofaa, ili wa-mshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe ili afe.”MwI 168.4

    Agizo hilo lilitiiwa. “Wale wazee wa mji wake na walio wenye nguvu. . . . wakafanya kama Yezebeli alivyowaagiza, kama ilivyoandikwa katika nyaraka alizowapelekea.” Kisha Yezebeli akaenda kwa mfalme, akamwambia aondoke akalichukue shamba. Ahabu akaondoka kwenda kulichukua shamba bila kupeleleza mambo yalivyo, akafuata tu maneno ya Yezebeli kama kipofu, maana alitamani mno.MwI 168.5

    Mfalme hakuachwa alitumie shamba alilolipata kwa dhuluma na kumwaga damu, bila kukemewa. “Neno la Bwana likamjia Eliya Mtishbi, kusema, Ondoka, ushuke, ukutane na Ahabu, mfalme wa Israeli, akaaye katika Samaria; yuko katika shamba la mizabibu la Nabothi, ndiko alikoshukia ili alitamalaki. Ukamwambie ukisema, Bwana asema hivi: Je, umeua, ukatamalaki?” Bwana alimwagiza nabii atangaze adhabu ya kutisha zaidi kwa Ahabu.MwI 168.6

    Nabii aliharakisha kutimiza agizo la Mungu. Mfalme mwenye hatia alipokutana na mjumbe mkali wa Bwana katika shamba la mizabibu, alimsemea kwa sauti ya kutetemeka, akasema: “Je, umenipata ewe adui yangu?”MwI 169.1

    Bila kusita, mjumbe wa Bwana akasema: “Nimekupata, kwa sababu umejiuza utende yaliyo mabaya machoni pa Bwana: Angalia, nitaleta mabaya juu yako; nami nitakuangamiza kabisa, nitamkutia Ahabu kila mume, aliyefungwa na aliyeachwa katika Israeli.” Hakuna huruma yo yote Ahabu atakayopata.MwI 169.2

    Nyumba ya ahabu itaangamizwa kabisa, sasa sawa na nyumba ya Yeroboamu mwana wa Nebati, na kama nyumba ya Baasha mwana wa Ahiya, “kwa ajili ya chukizo ulilonichukiza, hata ukanighadhabisha, ukawakosesha Israeli.”MwI 169.3

    Kuhusu Yezebeli, Bwana alitamka: “Mbwa watamla Yezebeli katika kiwanja cha Yezreeli. Mtu wa nyumba ya Ahabu afaye mjini, mbwa watamla, na yeye afaye mashambani ndege wa angani watamla.”MwI 169.4

    Mfalme aliposikia ujumbe huu wa kuogofya, “akayararua mavazi yake, akavaa magunia mwilini mwake, akafunga, akajilaza juu ya magunia, akaenda kwa upole. Neno la Bwana likaja kwa Eliya Mtishbi, kusema, Huoni jinsi Ahabu alivyojidhili mbele yangu? Basi, kwa sababu amejidhili mbele yangu, sitayaleta yale mabaya katika siku zake; ila katika siku za mwanawe nitayaleta mabaya hayo juu ya nyumba yake.”MwI 169.5

    Baada ya karibu miaka mitatu, Ahabu alikufa vitani akipigana na Washami. Ahazia aliyetawala baada yake, “akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, akaiendea njia ya babaye, na njia ya mamaye, na njia ya Yeroboamu mwana wa Nebati, aliyewakosesha Israeli. Akamtumikia Baali, akamwabudu, akamghadhabisha Bwana, Mungu wa Israeli, kwa mfano wa mambo yote aliyoyafanya Ahabu baba yake.” 1 Wafalme 22:52, 53. Lakini adhabu ilifuata upesi kwa mfalme mwasi. Msiba wa vita vya Wamoabu, halafu ajali ile ambayo yeye mwenyewe alihatarisha maisha, yote hayo yalithubutisha ghadhabu ya Mungu kwake.MwI 169.6

    Ahazia “akaanguka katika dirisha la chumba chake,” na kuumia vibaya sana. Akiogopa mambo yatakayotokea kwa ajili ya kuanguka huko, alituma baadhi ya watumishi wake ili kuulizia kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekrom, kwamba atapona au la. Ilidhaniwa kwamba mungu wa Ekroni atatoa jawabu, kwa njia ya Makuhani wake. Kwamba anaweza kubashiri mambo ya mbele. Watu wengi walikuwa wakienda kuulizia habari; lakini majawabu yaliyopatikana na maelezo yote yalikuwa yakitoka kwa Mkuu wa giza — Ibilisi.MwI 170.1

    Watumishi wa Ahazia walikutana na mtu wa Mungu, ambaye aliwarudisha kwa Mfalme, wakiwa na Ujumbe huu: “Je, ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-Zebubu mungu wa Ekroni? Basi sasa, Bwana asema hivi: Hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.” Nabii alipomaliza kutoa Ujumbe wake aliondoka.MwI 170.2

    Watumishi walirudi kwa haraka na kwa mshangao mpaka kwa Mfalme, wakamkariria maneno ya mtu wa Mungu. Mfalme aliwauliza: “Alikuwa mtu wa namna gani?” Nao wakamjibu: “Alikuwa amevaa vazi la manyoya, tena amejifunga shuka ya ngozi kiunoni mwake. Naye akasema: Ndiye yule Eliya Mtishbi.” Alijua kuwa kama ni Eliya aliyekutana na watumishi wake, na kuwaambia maneno yale, hakika yatatimia. Akiwa na wasiwasi sana, na akijaribu kuepusha adhabu hiyo isitimilizwe, alituma watu kumwita nabii.MwI 170.3

    Ahazia alituma Askari mara mbili wakijaribu kumtisha Eliya, na mara mbili walipata adhabu kutoka kwa Mungu. Kikosi cha tatu cha Askari kilijinyenyekea mbele ya Mungu, na mkuu wao alipomkaribia Eliya, “akapiga magoti mbele ya Eliya, akamsihi sana, akamwambia, Ee mtu wa Mungu, nakusihi, roho yangu, na roho za watumishi wako hawa hamsini, ziwe na thamani machoni pake.”MwI 170.4

    “Malaika wa Bwana akamwambia Eliya, shuka pamoja naye, usimwogope. Akaondoka, akashuka pamoja naye hata kwa Mfalme. Akamwambia, Bwana asema hivi: Kwa kuwa umetuma wajumbe waulize kwa Baal-Zebubu, mungu wa Ekroni, Je, ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, uulize neno lake? Kwa hiyo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.”MwI 170.5

    Ahazia alishuhudia matendo makuu ya Mungu wakati wa utawala wa baba yake. Alikuwa ameona ushuhuda wa kutisha, kuhusu Waisraeli waasi, jinsi Mungu alivyowatendea wale walioidharau sheria yake. Mambo ya kutisha yote hayo, kwa ahazia yalikuwa kama mchezo tu. Badala ya kujinyenyekeza mbele ya Bwana, alifuata Baali, kitendo ambacho kilionyesha ukaidi wake mkuu. Ahazia alikufa katika hali hiyo ya uasi, bila kutubu, “sawasawa na neno la Bwana alilolinena Eliya.”MwI 171.1

    Habari ya dhambi za mfalme Ahazia na adhabu aliyopata, hutoa maonyo kwa wote kwamba, hakuna mchezo kwa kuasi bila hofu. Wanadamu leo wanaweza wakawa hawaheshimu miungu ya mataifa, walakini watu maelfu huabudu katika mahekalu ya Shetani kama alivyofanya mfalme wa Israeli. Roho ya kuabudu sanamu imeenea ulimwenguni kote leo, ingawaje kwa ajili ya elimu na sayansi, inaonekana tofauti kidogo na jinsi ilivyokuwa wakati Ahazia alipokwenda kuuliza kwa mungu wa Ekroni. Kila siku ipitayo huzuni huongezeka kwa vile inavyoonekana kwa watu kutolijali neno la unabii lililo imara; ila badala yake hufuata madanganyo ya Kishetani, yaani elimu ya uongo.MwI 171.2

    Leo siri ya ibada ya sanamu ya kimataifa imeachwa, na badala yake zinafuatwa njia za kushirikisha mambo ya siri na maajabu ya kiroho ambayo huongozwa na Shetani. Mafunuo haya ya kiajabu-ajabu hukubaliwa na watu maelfu ambao hukataa kufuata nuru ya neno la Mungu, au maongozi ya Roho wake. Watu hawa wenye kuamini roho za kiajabu-ajabu wanaweza kuwacheka wanajimu na wenye roho za uaguzi wa zamani; lakini mdanganyaji mkuu huwacheka tu na kushangilia kwa vile wanavyokubali kufuata madanganyo yake, ingawa ni kwa umbo jingine kuliko watu wa zamaniMwI 171.3

    Wako watu wengi wasiotaka kuongozwa na roho ya uaguzi, lakini roho ile ile inapokuja kwa umbo jingine huwa tayari kuifuata. Wengine hupotoshwa na mafundisho ya sayansi ya Kikristo na mafundisho ya dini ya namna nyingine nyingine.MwI 171.4

    Wajumbe wa dini hizi za roho hujidai kuwa wanao uwezo wa kuponya. Husema kuwa uwezo huo umo katika mawazo ya mtu, nao hufanya kazi kwa namna ya nguvu za umeme na sumaku, nao huuita, “dawa za huruma.” Sio watu wachache wanaowafuata waponyaji hawa, badala ya kumwendea na kumtumaini Mungu aliye hai na waganga halisi waliofundishwa uganga barabara. Mama mtoto, anayemwangalia mtoto wake aliye katika hali ya kufa, husema: “Sina la kufanya. Je, hakuna mganga mwenye uwezo wa kumponya mwanangu?” Ndipo anapoambiwa habari za mponyaji wa ajabu anayeponya watu kwa miujiza, naye hutumainia mganga wa jinsi hiyo, na kumkabidhi mtoto wake mikononi mwa mtu kama huyo, ambaye kwa kweli ni kama kumkabidhi kwa Shetani hasa. Kuna mifano mingi ya mambo ya jinsi hii, ambayo inathubutisha kwamba, hali ya baadaye ya mtoto kama huyo huwa ikitawaliwa na uwezo wa Shetani, ambavyo huwa vigumu kuvunja hali hiyo.MwI 172.1

    Mungu alikuwa na sababu ya kutopendezwa na ukaidi wa Ahazia. Maana, je, ni jambo gani ambalo hakulitenda ili kuwaelekeza Waisraeli katika njia ya unyofu? Kwa muda wa miaka yote, Mungu amekuwa akijidhihirisha kwa watu wake kwa upendo wa fadhili zisizokuwa na kifani. Tangu mwanzo ameonyesha kwamba, “furaha yake ilikuwa pamoja na wanadamu.” Mithali 8:31. Yeye amekuwa msaada ulio karibu sana kwa watu wote waliomwita kwa uelekevu wa moyo. Na sasa mfalme wa Israeli anapomwacha Mungu na kwenda kutafuta msaada kwa miungu ya mataifa, ambayo ni adui wa Mungu, anawatangazia wote kuwa, anaiamini miungu zaidi ya anavyomwamini Mungu wa mbinguni. Kwa njia hiyo hiyo watu humdharau Mungu, wanapogeukia kwa uwezo wa giza. Je, ikiwa kitendo cha Ahazia kilimkasirisha, itakuwaje kwa watu wanaojua ukweli halisi halafu wanachagua kuenenda gizani pia?MwI 172.2

    Wale wanaokubali kufuata uchawi wa Shetani, wanaweza kudhani kuwa wamepata mafanikio makubwa; lakini je, wakiwa katika hali hiyo wako salama, au uchaguzi wao huo ni wa busara? Je, kama maisha yakirefishwa, itakuwaje? Je, kama wakifanikiwa kwa muda kitambo, mwishoni itawafaa kama wakidharau mapenzi ya Mungu? Faida na mapato yote ya namna hiyo, mwisho yataonekana kuwa ni hasara tupu. Hatuwezi kuvunja uzio ambao Mungu aliuweka kutulinda na uwezo wa Shetani kikaidi bila kupata hasara.MwI 172.3

    Kwa kuwa Ahazia hakuwa na mwana, Yehoramu ndugu yake alitawala mahali pake. Alitawala makabila yale kumi kwa muda wa miaka kumi na miwili Kwa muda huo wote, mama yake Yezebeli alikuwa angali hai, naye aliendelea na hali yake ya uovu tu kwa taifa hilo. Ibada ya sanamu ilikuwa ikifuatwa na watu wengi. Yehoramu mwenyewe, “akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana; ila si kama Baba yake na kama mama yake; maana akaiondoa ile nguzo ya baali aliyoifanya baba yake. Pamoja na hayo alishikamana na dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo kwa hizo aliwakosesha Israeli; wala hakuziacha.” 2 Wafalme 3:2, 3.MwI 173.1

    Wakati huo wa utawala wa Yehoramu, ndipo Yehoshafati alipokufa, na mwanawe, aliyeitwa Yehoramu pia, alitawala badala yake katika Ufalme wa Yuda. Kwa ajili ya kumwoa binti Ahabu na Yezebeli, Yehoramu mfalme wa Yuda alifanya ujamaa na mfalme wa Israeli; na katika utawala wake alifuata Baali “Kama walivyofanya nyumba ya Ahabu.” “Tena ndiye aliyefanya mahali pa juu milimani pa Yuda, na kuwaendesha katika uasherati wenyeji wa Yerusalemu, na kuwakosesha Yuda.” 2 Mambo ya Nyakati 21:6, 11.MwI 173.2

    Mfalme wa Yuda hakuachwa aendelee katika uasi huo bila kukemewa Eliya Nabii bado hajachukuliwa mbinguni, naye asingekaa kimya wakati ufalme wa Yuda ulipofuata njia ile ile iliyofuatwa na ufalme wa Israeli hata ukafikia ukingo wa kuangamia Nabii Eliya alimtumia Yehoramu mfalme wa Yuda waraka wenye ujumbe huu: “Bwana Mungu wa Daudi, baba yako, asema hivi: Kwa sababu hukuziendea njia za Yehoshafati baba yako, wala njia za Asa mfalme wa Yuda; lakini umeiendea njia ya wafalme wa Israeli, ukawaendesha katika uasherati Yuda na wenyeji wa Yerusalemu, kama walivyofanya nyumba ya Ahabu; tena umewaua ndugu zako wa nyumba ya baba yako, waliokuwa wema kuliko wewe; tazama, Bwana atawapiga pigo kubwa watu wako, na watoto wako, na wake zako, na mali yako yote; nawe utakuwa na ugonjwa mkuu.”MwI 173.3

    Ili kusudi kuyatimiza maneno ya unabii huu, “Bwana akawaamsha roho Wafilisti, na Waarabu waliowaelekea Wakushi juu ya Yehoramu. Nao wakakwea juu ya nchi ya Yuda, wakaipenya, wakaichukua mali yote iliyoonekana nyumbani mwa mfalme, na wanae pia, na wakeze, asisaziwe mwana hata mmoja, ila Ahazia (Azaria) aliyekuwa mdogo miongoni mwa wanawe. Na bsada ya hayo yote Bwana akampiga matumbo kwa ugonjwa usioponyeka. Ikawa baada ya siku, ikiisha miaka miwili. . .akafa, akiugua vibaya. Na ahazia mwanawe akatawala mahali pake.” 2 Mambo ya Nyakati 21:12-19; 2 Wafalme 8:24.MwI 174.1

    Yehoramu mwana wa Ahabu alikuwa angali akitawala ufalme wa Israeli, wakati mpwa wake Ahazia, alipotawalishwa juu ya ufalme wa Yuda. Ahazi alitawala mwaka mmoja tu, na wakati huo wote, alifuata mashauri ya Athalia mama yake. “Yeye naye akaziendea njia za nyumba ya Ahabu; kwa kuwa mamaye alikuwa mshauri wake katika kufanya maovu Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana.” 2 Mambo ya Nyakati 22:3, 4; 2 Wafalme 8:27. Yezebeli, nyanya yake alikuwa bado anaishi, naye alijiunga kamili na Yehoramu wa Israeli, mjomba wake.MwI 174.2

    Ahazia, mfalme wa Yuda mara akapata msiba wa mauti. Watu wa nyumba ya Ahabu waliobaki, ndio waliokuwa washauri wake. “Kwa kuwa hao walikuwa washauri wake, alipokwisha kufa babaye, hata aangamie.” 2 Mambo ya Nyakati 22:3, 4. Wakati Ahazia alipokwenda kumsalimu mjomba wake huko Yezreeli, Elisha nabii aliagizwa na Mungu amtume mmojawao wa wana wa manabii kwenda Ramothgileadi, ili amtie Yehu mafuta awe mfalme wa Israeli. Wakati huo majeshi ya Yuda na ya Israeli, kwa pamoja yalikuwa yakipigana na majeshi ya Washamu huko Ramothgileadi. Mfalme Yehoramu alikuwa amejeruhiwa katika mapigano, akarudi nyumbani huko Yezreeli, na kumwacha Yehu asimamie majeshi yote yanayopigana na Washamu.MwI 174.3

    Wakati Yehu alipotiwa mafuta, mtumishi wa Elisha alitamka: “Nimekutia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa Bwana, yaani, juu ya Israeli. Halafu akamwagiza kinaganaga agizo la mbinguni, akisema: “Bwana asema hivi, “Nawe utawapiga nyumba ya Ahabu Bwana wako, ili nijilipize kisasi cha damu ya watumishi wangu manabii na damu ya watumishi wote wa Bwana, mkononi mwa Yezebeli. Kwa maana nyumba Vote ya Ahabu wataangamia.” 2 Wafalme 9:6-8.MwI 174.4

    Baada ya kutangazwa kuwa mfalme na jeshi, Yehu aliharakisha kwenda Yezreeli, ambapo ataanza kazi yake, kutekeleza agizo la mbinguni juu ya wote wenye shingo gumu, wanaoendelea kutenda maovu kwa makusudi, na kuwakosesha wengine pia. Yehoramu wa Israeli, Ahazia wa Yuda, Yezebeli mama malkia, Yehu akawapiga wote waliosalia wa nyumba ya Ahabu katika Yezreeli, na hao wakuu wake wote, na rafiki zake, na makuhani wake, hata hakumwachia aliyesalia hata mmoja. Manabii wote wa Baali, na watumishi wake wote na makuhani wake wote wamwabuduo, na madhabahu zote za Baali huko Samaria, wote wakaliwa na upanga. Ndivyo Yehu alivyoharibu Baali katika Israeli.” 2 Wafalme 10:11, 19, 23.MwI 175.1

    Habari ya utekelezaji huu mkuu ilimfikia Athalia binti wa Yezebeli, ambaye alikuwa malkia wa Yuda. Alipoona kuwa mwanawe Ahazia, mfalme wa Yuda amekufa, “akainuka akawangamiza wazao wote wa kifalme wa nyumba ya Yuda.” Katika maangamizo haya uzao wote wa Daudi, ambao ndio waliokuwa na haki ya kutawala, walifutwa wote, kasoro mtoto mchanga mmoja aitwaye Yoashi, ambaye mke wa Yehoiada, kuhani mkuu alimficha katika ua wa hekalu. Mtoto alifichwa kwa muda wa miaka sita, wakati “Athalia alipoitawala nchi.” 2 Mambo ya Nyakati 22:10, 12.MwI 175.2

    Mwisho wa miaka hii sita, “Walawi na Yuda wote, (2 Mambo ya Nyakati 23:8) wakaungana na Yehoiada kuhani mkuu, wakamtawaza mtoto Yoashi na kumtangaza kuwa ndiye mfalme wao. “Wakapiga makofi, wakasema, Mfalme na aishi 2 Wafalme 11:12.MwI 175.3

    “Na Athalia aliposikia sauti ya watu, na ya walinzi, na ya hao waliomsifu mfalme, akaingia kwa watu nyumbani mwa Bwana.” 2 Mambo ya Nyakati 23:12. “Akatazama, na tazama, mfalme amesimama karibu na nguzo kama ilivyo desturi, nao wakuu na wapiga baragumu karibu na mfalme; na watu wote wa nchi wakafurahi, wakapiga baragumu. Ndipo Athalia akararua mavazi yake, akalia, Fitina, Fitina!” 2 Wafalme 11:14. Lakini Yehoiada akawaamuru wakuu wamkamate pamoja na wafuasi wake wakawatoa hekaluni mpaka mahali pa machinjio, wakawaulia mbali.MwI 175.4

    Hivyo mtu wa mwisho wa nyumba ya Ahabu aliangamizwa. Mvuto wake mwovu uliosababishwa na kuoana kwake na Yezebeli uliendelea mpaka mzao wake wa mwisho alipoangamizwa. Hata katika nchi ya Yuda, mahali ambapo ibada ya Mungu wa kweli haikuachwa, Athalia alifaulu kupotosha watu wengi. Mara moja baada ya kumwangamiza malkia huyo mwasi, “watu wote wa nchi wakaiendea nyumba ya Baali, wakaiangusha; madhabahu zake na sanamu zake wakazivunja-vunja kabisa, na Matani kuhani wa Baali wakamwua mbele ya madhabahu.” Fungu 18.MwI 177.1

    Matengenezo ya dini yalifuata. Wale waliomkiri Yoashi kuwa mfalme wao, “Walifanya agano kwamba, watakuwa watu wa Bwana.” Na sasa, kwa kuwa uovu ulioletwa katika Yuda na binti wa Yezebeli umeondolewa, na makuhani wa Baali wame- angamizwa, na hekalu lao limebomolewa, “wakafurahi watu wote wa nchi, na mji ukatulia.” 2 Mambo ya Nyakati 23: 16, 21.MwI 177.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents