Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    10—Sauti Ya Karipio Kali

    Eliya aliendelea kujificha milimani karibu na kijito cha Kerithi, kwa muda wa miezi mingi Kwa muda huo wote alilish- wa kwa njia ya mwujiza. Baadaye, kwa ajili ya ukavu wa nchi, kijito kilipokauka, Mungu alimwagiza mtumishi wake akajifiche katika nchi ya watu wa mataifa. Mungu alimwambia, “Ondoka, uende Sarepta. ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe.”MwI 99.1

    Mwanamke huyu hakuwa Mwisraeli. Hakupata bahati ya kufurahia mibaraka kama ile taifa teule la Kiisraeli liliyofurahia. Lakini alikuwa mcha Mungu, na aliendelea katika njia ya Mungu kulingana na nuru aliyokuwa nayo. Na sasa Eliya alipokosa hifadhi katika Israeli, Mungu alimpeleka kwa mwanamke huyu ili apate kuhifadhiwa nyumbani mwake.MwI 99.2

    “Basi akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni mwa mji, kumbe! mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, “Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa.” Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, “Niletee nakuomba; kipande cha mkate mkononi mwako.”MwI 99.3

    Katika nyumba hii ya kimaskini, njaa ilitia huzuni sana, na riziki yao ndogo iliyobaki, ilionekana kuwa inazimisha moyo wa huruma. Kuja kwa Eliya siku ile ile ambayo mwanake alikuwa amekata tamaa ya kuishi, imani yake ilijaribiwa vikubwa. Je, ataamini kuwa Mungu wa mbinguni atampatia riziki, au la! Lakini hata katika hali ya kutisha namna hii, aliyokuwa nayo, alishuhudia imani yake, kwa kukubali ombi la mgeni huyu anayeomba mkate, ambao ni riziki yake ya mwisho.MwI 100.1

    Katika kumjibu Eliya kwa ombi lake la maji na mkate, mjane alisema, Kama Bwana, Mungu wako aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.” Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao. Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka. wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi.”MwI 100.2

    Hakuna jambo kuu la kuipima imani ya mtu kuliko hili. Mjane huyu alikuwa amezoea kuwatendea mema wageni, na kuwakaribisha. Na sasa bila kujali tabu itakayompata yeye na mtoto, akiweka tumaini lake kwa Mungu awezaye kumpatia haja zake zote, alikabili jambo hili kuu, yaani, “akafanya kama alivyosema Eliya.”MwI 100.3

    Mwanamke huyu wa Kifoiniki alionyesha ukarimu wa ajabu kwa nabii wa Mungu, na imani yake ilipata thawabu kwa ajabu. “Yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake wakala siku nyingi. Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa kinywa cha Eliya.MwI 100.4

    “Ikiwa, baada ya hayo, mwana wake yule mwanamke, bibi wa nyumba ile, akaugua; ugonjwa wake ukazidi hata akawa hana pumzi tena. Akamwambia Eliya, “Nina nini nawe, Ee mtu wa Mungu?” Je, umenijia ili dhambi yangu ikumbukwe, ukamwue mwanangu?MwI 100.5

    Akamwambia, “Nipe mwanao.” Akamtoa katika kifua chake, akamchukua juu chumbani mle alimokaa mwenyewe, akamlaza kitandani pake. . . Akajinyosha juu ya mtoto mara tatu, akamwomba Bwana. . . . Bwana akaisikia sauti ya Eliya; na roho ya mtoto ikamrudia, akafufuka.MwI 100.6

    “Eliya akamtwaa mtoto, akamchukua toka orofani mpaka chini ya nyumba ile, akampa mama yake. Eliya akanena, “Tazama, mwanao yu hai.” Mwanamke akamwambia Eliya, “Sasa najua ya kuwa wewe ndiwe mtu wa Mungu, na ya kuwa neno la Bwana kinywani mwako ni kweli.”MwI 101.1

    Mjane wa Sarepta alikubali kula mkate wake pamoja na Eliya, na matokeo yake yalikuwa kuponya maisha yake na ya mwanawe. Vivyo hivyo, wote wale wanaowahurumia wenye shida na wahitaji wakati wa matatizo yao, na kuwasaidia, Mungu ameahidi kuwabariki vikubwa sana. Mungu ni yule yule, hajabadilika. Uwezo wake ni ule ule kama ulivyokuwa siku za Eliya. Maneno yaliyotamkwa na Mwokozi kwamba, “Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii” ni ya kweli mpaka leo. Mathayo 10:41.MwI 101.2

    “Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.” Waebrania 13:2. Maneno haya hayajapungua ukweli wake hata kidogo, ingawa yalinenwa zamani. Baba yetu wa mbinguni mpaka leo huwafungulia watoto wake njia za kupatia mibaraka kwa kukarimu wahitaji; na wale wanaotimiza wajibu huo, hupata furaha kuu. Ahadi ya Mungu ni hii: “Kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri. Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.” lsaya 58:10 11.MwI 101.3

    Kuhusu watumishi wake waaminifu wa leo, Kristo anasema, “Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma.” Hakuna tendo jema lo lote litendwalo kwa jina lake Yesu, ambalo litapita bila kutambuliwa mbinguni, na kupata thawabu. Kuhusu matendo mema hayo, Kristo alitaja hata matendo madogo mno yanayotendewa wana wa Mungu, “Na mtu awaye yote, atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa,“—yaani wadogo katika imani na katika kumjua Mungu,” — ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawambia, haitampotea kamwe thawabu yake. Mathayo 10:40, 42.MwI 101.4

    Muda wote wa ukame wa nchi Eliya alikuwa akiomba sana ili mioyo ya Waisraeli ipate kubadilika na kumwelekea Mungu. Nabii alingoja kwa uvumilivu wakati mkono wa Bwana ulipokuwa juu ya nchi ili kuzidisha dhiki yao. Alipoona mateso na masumbuko yakiongezeka sana kila upande, roho yake iliumia kwa masikitiko, naye alitamani awe na uwezo wa kufanya matengenezo ya dini upesi. Lakini Mungu alikuwa akiendesha kazi yake mwenyewe, na jambo lililompasa nabii kufanya ni kuomba tu na kungojea wakati utakapofika wa kutenda kitu.MwI 102.1

    Uasi uliokuwa umeenea sana wakati wa utawala wa Ahabu, ni matokeo ya kutenda maovu ya siku nyingi. Waisraeli walikuwa wakijitenga na Mungu hatua kwa hatua, na mwaka kwa mwaka. Kwa vizazi na vizazi walikuwa wakikataa kutengeneza mapito yao, ili yawe katika njia ya haki, mpaka mwishoni kundi kubwa likaasi kabisa na kujiweka wenyewe chini ya uongozi wa mwovu.MwI 102.2

    Kadiri ya karne moja iliyopita, Waisraeli walikuwa wakifurahi na kumwimbia Mungu wakati wa utawala wa Daudi, nao walimtumikia Mungu kwa moyo mmoja. Hebu, sikia jinsi walivyokuwa wakimsifu Mungu:MwI 102.3

    “Ee Mungu wa wokovu wetu, . . .
    Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha.
    Umeijilia nchi na kuisitawisha, umeitajirisha sana.
    Mto wa Mungu umejaa maji;
    Wawaruzuku watu nafaka, maana ndiwe uitengenezaye ardhi.
    Wailainisha nchi kwa manyunyu; waibariki mimea yake
    Umeuvika mwaka taji ya wema wako; mapito yako
    yadondoza unono.
    Huyadondokea malisho ya nyikani, na vilima vya jifunga furaha.
    Na malisho yamevikwa kondoo, na mabonde yamepambwa nafaka,
    Yanashangilia, naam, yanaimba.”
    MwI 102.4

    Zaburi 65:5, 8-13

    Hapo mwanzo Waisraeli walimtambua na kumkiri Mungu kuwa ndiye aliyeuweka msingi wa dunia. Waliimba kwa imani na kusema:MwI 103.1

    “Uliiweka nchi juu ya misingi yake,
    Uliifunika kwa vilindi kama vazi,
    Maji yalikuwa yakisimama juu ya milima.
    Kwa kukemea kwako yakakimbia,
    Kwa sauti ya radi yako yakaenda zake kasi,
    Yakapanda milima, yakatelemka mabondeni,
    Mpaka mahali ulipoyatengenezea.
    Umeweka mpaka yasiupite,
    wala yasirudi kuifunikiza nchi.”
    MwI 103.2

    Zaburi 104:5-9.

    Ni uwezo mkuu wa Mwenyezi Mungu tu ndio unaovi- shikilia vitu vyote vya duniani, bahari, na angani na kuviongoza, na kuviweka kwa utaratibu, kila kitu mahali pake. Na vitu vyote hivi huvitumia kwa ajili ya manufaa ya viumbe vyake. “Hazina yake nzuri,” huitoa bure, “kwa kutoa mvua . . . kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mikono ya mtu. Kumbukumbu la Torati 28:12.MwI 103.3

    “Hupeleka chemchemi katika mabonde;
    Zamnywesha kila mnyama wa kondeni;
    Punda-mwitu huzima kiu yao.
    Kandokando hukaa ndege wa angani;
    Kati ya matawi hutoa sauti zao. . . .
    Huyameesha majani kwa makundi,
    Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu;
    Ili atoe chakula katika nchi,
    Na divai imfurahishe mtu moyo wake.
    Aung'aze uso wake kwa mafuta,
    Na mkate umburudishe mtu moyo wake.
    Ee Bwana, jinsi yalivyo mengi matendo yako!
    Kwa hekima umevifanya vyote pia.
    Dunia imejaa mali zako. Bahari iko kule, kubwa na upana,
    Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika,
    Viumbe hai vidogo kwa vikubwa. . . .
    Hao wote wanakungoja Wewe, Uwape chakula chao kwa wakati wake.
    Wewe huwapa, wao wanakiokota;
    Wewe waukunjua mkono wako, wao wanashiba mema.”
    MwI 103.4

    Zaburi 104:10-15, 24-28.

    Waisraeli walikuwa na sababu tele za kushangilia. Nchi ambayo Bwana aliwaleta ndani yake ilikuwa nchi ijaayo maziwa na asali. Wakati walipokuwa wakitangatanga jangwani, Mungu alikuwa amewaahidi kuwa atawaongoza na kuwafikisha katika nchi bora, ambamo hawatahitaji cho chote, wala hapatakuwa na upungufu wa mvua. Alikuwa amewahakikishia, akisema, Nchi mwingiayo kuimiliki, si mfano wa nchi ya Misri mlikotoka, uliyokuwa ukipanda mbegu zako humo na kuinywesheleza kwa mguu wako, kama shamba la mboga; lakini nchi mwivukiayo kuimiliki ni nchi ya vilima na mabonde, nayo hunyweshwa maji ya mvua ya mbinguni; nayo ni nchi itunzwayo na Bwana, Mungu wako; macho ya Bwana, Mungu wako ya juu yake, tangu mwanzo wa mwaka hata mwisho wa mwaka.” Kumbukumbu la Torati 11:10-12.MwI 104.1

    Ahadi ya kuhusu wingi wa mvua ilitolewa kwa masharti, kwamba ikiwa watatii. Bwana alinena, “Tena itakuwa, mtakaposikiza kwa bidii maagizo yangu niwaagizayo leo, kwa kumpenda Bwana, Mungu wenu, na kumtumikia kwa mioyo yenu vote na roho zenu zote, ndipo nitakapowapa mvua ya nchi yenu kwa wakati wake, mvua ya masika na mvua ya vuli, upate kuvuna nafaka yako, na divai yako, na matuta yao. Nami nitakupa nyasi katika mavue yako kulisha wanyama wako wa mifugo, nawe utakula na kushiba.MwI 104.2

    “Jitunzeni nafsi zenu, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka, na kutumikia miungu mingine na kuiabudu; hasira za Bwana zikawaka juu yenu, naye akafunga mbingu kusiwe na mvua, wala nchi isitoe matunda yake; mkaangamia kwa upesi mtoke katika nchi nzuri awapayo Bwana.” Mafungu 13-17.MwI 104.3

    Mungu aliendelea kuonya: “Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma. Bwana atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia kutoka mbinguni hata uangamie.” Kumbukumbu la Torati 28:15, 23, 24.MwI 104.4

    Haya ni miongoni mwa mashauri bora Yehova aliyowapa Waisraeli wa kale: “Yawekeni maneno yangu mioyoni mwenu na rohoni mwenu; yafungeni yawe dalili juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yenu. Nayo wafunzeni vijana wenu kwa kuyazungumza uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo na uondokapo.” Kumbukumbu la Torati 11:18, 19. Maagizo haya yalikuwa dhahiri kabisa. Walakini kadiri karne zilivyopita, na kizazi kwa kizazi hakikujali maagizo haya yahusuyo hali yao ya kiroho, mafuriko ya uasi mkuu yalifutilia mbali kila jambo lihusulo neema ya Mungu kwao.MwI 105.1

    Hivyo basi ilikuwa lazima Mungu awaadhibu vikali watu wake. Utabiri wa Eliya ulikuwa unatimia kikamilifu. Kwa muda wa miaka mitatu, Eliya, mjumbe wa kutangaza ajali kwa watu, alikuwa akitafutwa mji kwa mji, na taifa kwa taifa. Wafalme wengi wa nchi jirani walikuwa wameapa kwa Ahabu kwamba hawana habari zo zote za nabii wa jinsi hiyo. Hata hivyo utafutaji wa Eliya uliendelea tu, maana Yezebeli na manabii wa Baali waMmchukia Eliya kiasi cha kufa; kwa hiyo hawakupumzika mpaka watakapompata. Hata hivyo hapakuwa na mvua.MwI 105.2

    Mwishowe, “baada ya siku nyingi, neno la Bwana likamjia Eliya, Enenda ukajionyeshe kwa Ahabu; nami nitaleta mvua juu ya nchi.”MwI 105.3

    Eliya alitii agizo, “akaenda ili ajionyeshe kwa Ahabu.’ Wakati ule nabii alipoanza safari ya kwenda Samaria kwa Ahabu, Ahabu naye alikuwa amepanga kwamba Obadia, msimamizi wa nyumba yake, aondoke kwenda kutafuta vijito vyenye maji ili kuwanywesha wanyama wake waliokuwa wakifa kwa njaa na kiu. Ukame wa nchi uliokumba watu wote, hata watu wa nyumba ya mfalme Ahabu pia walikumbwa. Mfalme Ahabu akiwa na wasiwasi juu ya wanyama wake, aliondoka pia pamoja na mtumishi wake kwenda kutafuta mahali penye maji. “Basi wakaigawanya nchi, ili wapite katika nchi yote; Ahabu akaenda zake njia moja peke yake, na Obadia akaenda zake njia nyingine peke yake.”MwI 105.4

    “Na Obadia alipokuwa njiani, kumbe! Eliya akakutana naye Akamtambua, akaanguka kifudifudi, akanena, “Je! ni wewe, bwana wangu Eliya?”MwI 106.1

    Wakati wote wa uasi mkuu wa Israeli Obadia alidumu kuwa mwaminifu kwa Mungu. Bwana wake, mfalme Ahabu hakuweza kumgeuza auache uaminifu wake kwa Mungu aliye hai. Na sasa anapewa heshima na Eliya aliyemwambia, “Enenda, umwambie bwana wako, Tazama, Eliya yupo.”MwI 106.2

    Obadia alisema kwa hofu kuu kwamba, “Nimekosa nini, hata unitie mimi mtumishi wako mkononi mwa Ahabu, aniue?” Kumpelekea Ahabu habari kama hizo, hakika ilikuwa ni kutafuta kifo. Obadia akaendelea kusema, “Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, hakuna taifa wala ufalme ambao bwana wangu hakutuma watu akutafute; na waliposema, “Hayupo,” akawaapisha ule ufalme, na taifa, ya kwamba hawakukuona. Nawe sasa wasema, “Enenda, umwambie bwana wako,” Tazama, Eliya yupo. Na itakuwa, mara mimi nikiondoka kwako roho ya Bwana atakuchukua uende nisikojua; nami nitakapok- wenda kumwambia Ahabu, naye asipokuona, ataniua.”MwI 106.3

    Obadia alimsihi sana nabii Eliya asikazane kumtuma kwa Ahabu, alisema, “Lakini mimi mtumishi wako namcha Bwana tangu ujana wangu. Je, bwana wangu hakuambiwa nilivyofanya hapo Yezebeli alipowaua manabii wa Bwana? Jinsi nilivyowaficha manabii wa Bwana, watu mia, hamsini hamsini katika pango, nikawalisha chakula na kuwapa maji? Nawe sasa wasema, Enenda umwambie bwana wako, Tazama, Eliya yupo, basi ataniua.”MwI 106.4

    Nabii Eliya alimwapia Obadia kwamba, haitakuwa kama anavyohofu. Alisema, “Kama Bwana wa majeshi aishivyo ambaye ninasimama mbele zake, hakika nitajionyesha kwake leo.” Obadia alipohakikishiwa hivyo, “akaenda zake amwone Ahabu, akamwambia.”MwI 106.5

    Akishikwa na mshangao pamoja na hofu, Ahabu alim- sikiliza mtu yule ambaye anamwogopa na kumchukia, ambaye amemtafuta sana kila mahali. Ahabu alijua kuwa Eliya hawezi kuhatarisha maisha yake kwa kukutana naye wakati huo. Ila aliwaza, “Je, nabii huyu anataka kutangaza ole mwingine? Mfalme aliogopa. Alikumbuka mkono wa Yeroboamu uliokaukiana. Wakati huu Ahabu hakuweza kukataa agizo lo lote la nabii, wala hakuthubutu kumnyoshea mkono. Hivyo basi mfalme, akifuatana na kundi la walinzi wake, alienda kumlaki nabii Eliya, huku akiwa na wasiwasi.MwI 106.6

    Mfalme na nabii wakakutana uso kwa uso. Ingawa Ahabu alikuwa na chuki kuu kwa Eliya, lakini aliposimama mbele yake, alikuwa dhaifu, mwoga sana. Maneno yake ya kwanza aliyoyatamka kwa Eliya, “Je, ni wewe, Ewe mtaabishaji Israeli?'‘ Yalidhihirisha hali na mawazo yake bila kufahamu. Alijua kuwa ni kwa neno la Mungu ndivyo mbingu zimekuwa kama shaba, hata hivyo akatafuta njia ya kumtupia nabii lawama, kwa ajili ya adhabu iliyoanguka juu ya nchiMwI 107.1

    Ni kawaida kwa mkosaii ve yote kutupa lawama kwa wajumbe wa Mungu kwa ajili ya matokeo ya makosa yao kwa kuziasi kanuni za haki. Watu wanaojikabidhi mikononi mwa Ibilisi, hawawezi kuona mambo kwa wazi kama Mungu anavyoyaona. Kioo cha ukweli kikiwekwa mbele yao, hughadhabika kwa ajili ya kudhihirishwa ukweli ulivyo. Hukataa kutubu kwa ajili ya kupofushwa na dhambi; hudhani kuwa waiumbe wa Mungu waliodhihirisha ukweli ndio waliogeuka adui wao, kwa hiyo wanastahili kulaumiwa sana.MwI 107.2

    Eliya akisimama mbele ya mfalme Ahabu, mwenye dhamiri safi, hakujaribu kujitetea, au kumsifu Ahabu. Wala hakujaribu kutuliza hasira ya mfalme kwa kumwambia kwamba ukame wa nchi karibu utakoma. Hakuwa na maneno ya kuomba samahani. Akiwa na uchungu na wivu kwa ajili ya Bwana, alimrudishia mfalme maneno bila hofu, akisema, “Si mimi niliyewataabisha Israeli; bali ni wewe, na nyumba ya baba yako, kwa kuwa mmeziacha amri za Bwana; nawe umewafuata mabaali.”MwI 107.3

    Leo kunahitajika sauti ya karipio kali; kwa kuwa maovu mengi yamewatenga watu na Mungu wao. Ukafiri unazidi kuenea kila mahali. Sauti za watu maelfu husikika zikisema, “Hatumtaki huyu atutawale.” Luka 19:14. Mahubiri laini yanayohubiriwa mara kwa mara hayapenyi na kudumu katika mioyo ya watu; maana tarumbeta ipigwayo haitangazi jambo maalum. Watu hawachomwi mioyo yao kwa ujumbe wa neno la Mungu lenye ukweli.MwI 107.4

    Kuna wakristo wengi, ambao kama wangejifunua jinsi walivyo hasa, wangesema hivi, Iko haja gani ya kuhubiri ujumbe na kutaja mambo dhahiri jinsi yalivyo? Pia wangejiuliza hivi, Yohana Mbatizaji alikuwa na haja gani ya kuhubiri na kuwaambia Mafarisayo: “Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?” Luka 3:7. Kwa nini aliichochea hasira ya Herodia kwa kumwambia Herode kwamba, haikuwa halali kwake kuishi na mke wa nduguye? Aliyekuwa mtangulizi wa Kristo alipoteza uhai wake kwa ajili ya kuusema ukweli jinsi ulivyo. Kwa nini hakuendesha kazi yake bila kuwaingilia wale wanaoishi katika dhambi na kutaja dhambi zao?MwI 108.1

    Hivyo watu wapaswao kusimama kama wajumbe halali wa kuitetea sheria ya Mungu, wameshindana kwa maneno mpaka busara iletayo faida zaidi katika mwenendo wao kung'ang'ania mabisano yatakayowapa ushindi kisheria kuingia mahali pa uaminifu na dhambi huendelea bila makaripio. Je, sauti halali ya uaminifu itasikika lini kanisani ikikemea dhambi.?MwI 108.2

    Wewe ndiwe mtu huyo.” 2 Samweli 12:7. Maneno dhahiri kama haya yaliyosemwa na Nathani kwa mfalme Daudi, siku hizi nusikika kwa nadra sana yakitajwa mimbarani, au katika magazeti. Kama yasingeadimika, tungeweza kuona uwezo wa Mungu ukionekana dhahiri kwa watu. Wajumbe wa Mungu wasilalamike kwamba kazi yao haina matokeo, wala haizai matunda; ila yawapasa kutubu, na kuacha tabia yao ya kujipendekeza kwa wanadamu inayofanya waifiche kweli.MwI 108.3

    Wachungaji ambao hujipendekeza kwa wanadamu, wakisema, Amani, amani, ambavyo Mungu hakusema amani, yawapasa wajinyenyekeze mbele za Mungu, huku wakiomba samahani kwa kutokuwa waaminifu kwao, na kwa kutokuwa na ushujaa. Kule kuhafifisha ujumbe wa Mungu, na kuusema kwa namna hafifu, hakuonyeshi kwamba wanawapenda watu, ila huonyesha kuwa, wanafuata nia zao tu, pa kupenda starehe. Upendo wa kweli kwanza humheshimu Mungu, halafu hushughulika na wokovu wa wanadamu. Watu walio na upendo halisi hawaepi ukweli, ili kujiepusha na mashambulio yatakayofuata, baada ya kusema ukweli jinsi ulivyo. Watu wanapokuwa katika hatari ya kuangamia, wajumbe wa Mungu hawatajihadhari jinsi ya kusema ili kujilinda, lakini watasema maneno yote watakayoamuriwa kusema, bila kutoa udhuru au kufunikafunika dhambiMwI 108.4

    Yampasa kila mchungaji, ambaye ni mjumbe wa Mungu, afahamu utakatifu wa kazi yake na mwito wake kwa kazi hiyo, apate kuonyesha ushujaa kama ule Eliya aliokuwa nao! Wachungaji, ambao ni wajumbe wa Mungu wa mbinguni wanashikilia madaraka muhimu sana, ambayo ni matakatifu, na yenye heshima kuu. Yawapasa “kukaripia. kukemea, na kuonya kwa uvumilivu wote.” 2 Timotheo 4:2. Wao, badala ya Kristo, hawana budi kufanya kazi kama mawakili wa siri za mbinguni, huku wakiwatia shime walio waaminifu, na kuwaonya wasiokuwa waaminifu. Kwao, kawaida zinazofuatwa na walimwengu hazina kazi. Haiwapasi kamwe kupotoka, na kuiacha njia ile Yesu aliyowaagiza kufuata. Hawana budi kwenda mbele katika imani, huku wakikumbuka kuwa wanazungukwa na wingu kubwa la mashahidi. Haiwapasi kunena maneno vao wenyewe, bali maneno walivoagizwa na Mfalme Mkuu kuliko wakuu wa dunia. Ujumbe wao, na uwe: “Ndivyo asemavyo Bwana.” Mungu anaita watu kama Eliya, Nathani, na Yohana Mbatizaji, watu ambao watashika kazi yake ya kutoa ujumbe kwa uaminifu, bila kujali mambo yatakayowapata; watu watakaoinena kweli jinsi ilivyo kwa ujasiri, ijapokuwa itawagharimu vyote walivyo navyo.MwI 109.1

    Mungu hawezi kuwatumia watu ambao ni woga. watu ambao wakati wa hatari wanaogopa kusimama imara na kuitetea kweli. Anawaita watu watakaosimama imara katika vita, wakishindana juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Watu kama hao ndio watakaoambiwa maneno haya mwishoni: “Vema, mtumwa mwema na uaminifu . . . ingia katika furaha ya Bwana wako.” Matt. 25:23.MwI 109.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents