Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    13—“Unafanya Nini Hapa?”

    Utoro wa Eliya mpaka mlima wa Horebu, ingawa haukuiulikana kwa mwanadamu ye yote, lakini ulijulikana kwa Mungu: na nabii huyu aliyechoka na kukata tamaa kabisa, hakuachwa ashindane peke yake na nguvu za giza zilizokuwa zikimsonga. Pale penye lango la pango, ambamo Eliya aliingia, Mungu alikutana naye, kwa njia ya Malaika aliyetumwa kwake ili amweleze mambo yote Mungu anayokusudia kwa Israeli.MwI 133.1

    Eliya hawezi kukamilisha kazi yake kwa watu waliodanganyika na kuabudu Baali, mpaka kwanza yeye mwenyewe ajifunze namna ya kumtegemea Mungu halisi. Ule ushindi uliopatikana juu ya mlima wa Karmeli ulikuwa mwanzo tu wa mambo makuu yatakayotendeka: walakini wakati mlango ulipofunguliwa kwa Eliya ili atende mambo makuu zaidi, alitoroka kwa kuogopa matisho ya Yezebeli. Mtu wa Mungu lazima afahamishwe udhaifu alio nao wakati huu, kulinganisha na hali Mungu atakayomjalia kuwa nayo wakati ujao.MwI 133.2

    Mungu alikutana na mtumishi wake aliyejaribiwa vikubwa, na swali hili. Unafanya nini hapa Eliya? Mimi nilikutuma katika kijito cha Kerithi, na baadaye nikakutuma kwa mjane wa Sarepta. Nikakuagiza kuwa urudi katika nchi ya Israeli, ukasimame mbele ya waabudu sanamu juu ya mlima Karmeli, nilikukaza mwili ukaweza kupiga mbio mbele ya gari la mfalme, ukamwongoza mpaka akafika Yezraeli. Na sasa, ni nani aliyekutuma huku jangwani? Kazi uliyokuja kufanya hapa ni kazi gani?”MwI 133.3

    Eliya akalalamika kwa uchungu wa roho yake, akasema Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana, Mungu wa majeshi: kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano, yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga: nami nimesalia, mimi peke yangu: nao wanitafuta roho yangu, waiondoe.”MwI 134.1

    Malaika akimwita nabii atoke pangoni, alimwagiza asimame mbele ya Bwana mlimani, ili asikilize sauti yake: “Na tazama, Bwana akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunjavunja miamba mbele za Bwana: lakini Bwana hakuwamo katika upepo ule: na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini Bwana hakuwamo katika lile tetemeko la nchi: na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto: lakini Bwana hakwamo katika moto ule: na baada ya moto, sauti ndogo, ya utulivu. Ikawa Eliya alipoisikia alijifunika uso wake katika mavazi yake, akatoka, akasimama mlangoni mwa pango.”MwI 134.2

    Mungu hakujidhihirisha kwa mtumishi wake kwa njia ya nguvu kuu na vishindo, bali kwa sauti tulivu. Alitaka kum- fundisha Eliya kwamba, kazi yake na makusudi yake havifanyiki kwa njia ya vishindo, na makelele mengi ya kuvutia watu, kila mara. Wakati Eliya alipokuwa anamngoja Bwana, tufani kuu ilivuma, umeme ukametameta, na moto mkali ukapita ukiteketeza kila kitu; lakini Bwana hakuwamo katika vitu hivyo vyote. Halafu ikaja sauti ndogo ya utulivu, ndipo nabii akajifunika uso wake mbele za Bwana. Harara alizokuwa nazo zikanyamazishwa kimya, moyo wake ukalainika, ukatulia. Akafahamu kwamba kumtegemea Mungu halisi, huleta msaada wakati wa mahitaji.MwI 134.3

    Ukweli wa neno la Mungu hauongoi watu kwa kuwa umehubiriwa na mtu mtaalam. Sio ufundi wa maneno. na ujuzi wa kuhubiri, kwamba ndio unaogusa mioyo ya watu. la, sivyo, bali ni kwa mvuto wa Roho Mtakatifu, anayefanya kazi yake kimya-kimya katika maisha ya watu, na kusababisha mapinduzi ya tabia. Ni sauti tulivu ya Mungu, ndiyo yenye uwezo wa kubadili nia za watu na maisha yao.MwI 134.4

    Sauti hiyo ilimwuliza tena Eliya swali: “Unafanya nini hapa Eliya?” Tena nabii Eliya alijibu: “Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana, Mungu wa majeshi: kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako na kuwaua manabii wako kwa upanga nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe.” Bwana akamjibu Eliya kwamba, wakosaji wote katika Israeli, lazima waadhibiwe. Lazima wachaguliwe watu watakaotekeleza adhabu hiyo kwa waabudu sanamu katika ufalme wote. Shughuli kali lazima itendeke, na kila mtu apate nafasi ya kuchagua msimamo wake kwa upande wa Mungu wa kweli. Eliya hana budi kurudi katika nchi ya Israeli, ili ashirikiane na wengine katika shughuli ya matengenezo.MwI 135.1

    Bwana akamwamuru Eliya, akisema, “Enenda, urudi njia ya jangwa la Dameski; ukifika, mtie mafuta Hazaeli awe mfalme wa Shamu, Yehu mwana wa Nimshi mtie mafuta awe Mfalme wa Israeli; na Elisha mwana wa Shafati wa Abeli-Mehola mtie mafuta awe nabii mahali pako. Na itakuwa, atakayeokoka na upanga wa Hazaeli, Yehu atamwua; na atakayeokoka na panga wa Yehu, Elisha atamwua.”MwI 135.2

    Eliya alidhani kwamba, yeye peke yake ndiye anayem- wabudu Mungu wa kweli katika Israeli nzima. Lakini Mungu anayeona na kujua mioyo ya watu wote, alimweleza nabii kuwa, wako wengi sana, ambao wameshika uaminifu wao, muda wote wa uasi mkuu. Bwana alisema, “Nimejisazia katika Israeli watu elfu saba, kila goti lisilomwinamia Baali, na kila kinywa kisichombusu.”MwI 135.3

    “Tunapata mafundisho mengi kutokana na mambo ya Eliya wakati aliposhindwa na mashaka akakata tamaa; hasa katika kizazi hiki. Watumishi wa Mungu wajifunze kwa makini jinsi inavyowezekana kujitenga na kweli kwa urahisi Uasi ulioenea siku hizi ni sawasawa na wa wakati wa nabii Eliya, kwa Israeli. Leo makundi-makundi yanamfuata Baali kwa njia ya kuwatukuza wanadamu kuliko Mungu, na kwa njia ya kuwatukuza Viongozi wao, na kutumikia mali, yaani utajiri, pamoja na kutukuza mafun-disho ya sayansi kuliko neno la Mungu. Mashaka na kutokuamini kwao huharibu roho zao, kiasi cha kulitupilia mbali neno la Mungu, na kushikamana na mafundisho madanganyifu ya wanadamu.MwI 135.4

    Siku hizi mafundisho hutolewa waziwazi kwamba, tumefikia kipeo cha kuthamini ujuzi wa kibinadamu kuliko Biblia, ambalo ni neno la Mungu. Sheria ya Mungu, ambayo ni kiwango cha ukamilifu hudharauliwa wazi, kwamba haina kazi yo yote. Adui Shetani ambaye huchukia kweli yote, huwadanganya wanadamu kwa uchawi wake wapate kuwatukuza wataalam badala ya Mungu, nao husahau mambo Mungu aliyopanga ili kuwaletea wanadamu furaha na wokovu.MwI 136.1

    Hata hivyo, ingawa uasi umeenea jinsi hiyo, si kwamba umewakumba watu wote. Sio watu wote waliomo ulimwenguni, kwamba ni wafedhuli na waovu; si wote wanaomwunga mkono Shetani. Mungu anao watu maelfu ambao hawakumsujudia Baali; wengi wanaotamani kuelewa habari za Kristo na sheria ya Mungu; wengi wanaotamani kabisa kabisa kwamba Yesu atakuja tena karibuni, ili kukomesha utawala wa dhambi na mauti. Pia wako wengi ambao wamekuwa wakimwabudu Baali kwa kutojua, ambao Roho wa Mungu anawashughulikia.MwI 136.2

    Watu kama hawa wanahitaji msaada kutoka kwa wale waliomjua Mungu na uwezo wa neno lake. Wakati kama huu, kila mtoto wa Mungu hana budi kujitahidi kuwasaidia wale waliomo gizani. Watu ambao wanaifahamu kweli ya Biblia, wanaposhughulika kuwasaidia wale wasiojua kitu, malaika wa Bwana hushirikiana nao katika kazi hiyo. Na ikiwa malaika hufuatana nao hakuna hofu yo yote. Matokeo ya kazi ya watu hawa waaminifu, yatakuwa mazuri sana, maana watawageuza watu waliokuwa wakiabudu sanamu, wapate kumwabudu Mungu aliye hai. Wengi wataacha kufuata mafundisho ya kibinadamu, na kumgeukia Mungu na sheria yake.MwI 136.3

    Wale walio waaminifu wanatakiwa wafanye bidii bila kukoma ili kuwaita walio gizani; maana Shetani anajitahidi sana kupotosha na kuharibu makusudi ya Mungu, yanayotokana na utij. Huwafanya wengine wasijali mwito na kazi yao takatifu, ila watosheke tu na kufurahia maisha haya. Huwafanya wakae raha mustarehe; au washughulike na mapato ya ulimwengu huu tu, hata wahame kwenda mahali pengine badala ya kuishi pale ili wawe nuru. Wengine huwakatisha tamaa kiasi cha kutoroka na kuacha kazi yao inayowahusu, kwa ajili ya matatizo au mateso. Lakini wote wa namna hiyo, mbingu huwatazama kwa huruma sana. Kila mtoto wa Mungu ambaye amenyamazishwa na Shetani, hata hawezi kutoa sauti yake, swali hili humfuata: “Unafanya nini hapa?” Mimi niliwaamuru mwende katika ulimwengu wote, mkaihubiri injili ili kuwatayarisha watu kwa siku ile ya Mungu. Kwa nini mko hapa? Nani aliyewaagiza mje huku?MwI 136.4

    Furaha iliyowekwa mbele ya Kristo, ambayo ilifanya apite katika mateso bila wasiwasi na kutoa kafara kamilifu, ni ile ya kuwaona wenye dhambi wakiokolewa. Furaha ya jinsi hii, ndiyo inapasa kuwa kwa kila mfuasi wake, na kumhimiza. Wale wanaotambua hivyo, hata kama ni kidogo maana ya wokovu kwao wenyewe na kwa majirani zao ndipo watatambua haja kuu ya binadamu. Watajazwa na huruma nyingi, watakapoona jinsi maelfu ya wanadamu yanavyozama maovuni, huku wakitembea katika bonde la uvuli wa uharibifu wa maisha yao, kiroho na kimwili pia.MwI 137.1

    Kwa kila jamaa na kwa kila mtu binafsi, swali hili huja: “Unafanya nini hapa?” Katika makanisa mengi kuna jamaa ambao wanao ujuzi wa kweli ya Mungu, ambao wangepanua mvuto wao, kwa kuhamia mahali ambapo watu wa huko hawana habari na ukweli huu, nao wangewahudumia watu hao. Mungu anawaita wakristo wahamie mahali penye giza ya kiroho, ili wakamulike hapo. Kujibu mwito huu, kunatakiwa kujitoa kwa kujinyima. Wakati wengine wanapongojea kwanza mpaka kila tatizo linyoshwe, ndipo waende, watu wengi watakufa bila kuwa na tumaini lo lote la uzima, au kuwa na Mungu. Watu wengi huenda mahali penye shida sana kwa ajili ya kutafuta mali ya dunia hii, au kwa ajili ya uchunguzi wa kisayansi. Je, walio tayari kufanya hivyo kwa ajili ya Kristo wako wapi?MwI 137.2

    Watu wa Mungu wakikumbana na matatizo mazito hata wakakata tamaa, na wakati huo bila kupata faida yo yote, wajue kwamba hilo si jambo geni au jipya. Wakumbuke kwamba, nabii mkuu kabisa katika manabii alitoroka, akamkimbia mwanamke aliyeghadhabika, ili apate kujiponya. Akiwa mkimbizi, mchovu kwa ajili ya safari, mwenye kukata tamaa, akiwa na wasiwasi rohoni kiasi cha kuzimia, Eliya aliomba ajifie. Alijifunza fundisho muhimu, wakati matumaini yote yalipotoweka, na kazi yake aliyoishughulikia maisha yote, ikaonekana kana kwamba imeanguka. Katika saa ya kushindwa kwake, njia zote zimetoweka, ndipo alijifunza kumtegemea Mungu wakati akiwa katika kutapatapa bila kuwa na mbele wala nyuma.MwI 138.1

    Wale wanaotumia nguvu zao zote katika kazi ya Mungu katika maisha yote, halafu wakapambana na jaribu lenye kuwakatisha tamaa, hebu wajipatie ujasiri kutokana na mambo ya Eliya. Ulinzi wa Mungu ulio kamili, upendo wake, uwezo wake, hudhihirishwa kwa watumishi wake, waliotoa maisha yao yote kwa kazi yake, ambao badala ya kutiwa moyo na wenzao, wanalaumiwa tu, na kazi yao inaonekana kama uchofu, na ambao wanapotoa shauri lo lote halijaliwi, na kazi yao ya kufanya matengenezo ya dini inakutana na chuki na mapingamiziMwI 138.2

    Wakati wa udhaifu mwingi, ndipo Shetani humshambulia mtu vikali kabisa. Hivyo ndivyo alivyotumaini kumshinda Mwana wa Mungu; maana kwa njia hiyo amewashinda watu wengi sana. Wakati wa mashaka, na imani inapopungua, na kufifia, ndipo watu huanguka majaribuni, ambavyo walikuwa imara kwa siku nyingi. Musa, akiwa amechoka na safari ya kutangatanga miaka arobaini, huku akihangaika na watu wasiosimama katika imani, aliteleza muda kitambo tu, akajitenga na Mungu, na uwezo wake. Alishindwa pale mpakani mwa nchi ya ahadi Ndivyo ilivyokuwa na Eliya pia. Mtu aliyesimama katika imani wakati wote wa ukame wa nchi na njaa kuu, mtu aliyesimama kijasiri mbele ya Ahabu, mtu aliyesimama imara siku ile ya kujaribiwa imani katika mlima wa Karmeli, akasimama kama shahidi mwaminifu mbele ya taifa lote la Israeli, akimtetea Mungu wa kweli, kitambo tu cha wasiwasi akaruhusu hofu ya kifo imwondolee imani yake kwa Mungu.MwI 138.3

    Hali kadhalika na siku hizi. Tunapozungukwa na mashaka, hali ya mambo ikitutia wasiwasi, au shida yo yote ikituingilia, Shetani hutafuta njia wakati huo ili kutupeperushia mbali na Mungu. Wakati huo hutupangia makosa yetu yote, na kutufikirisha kuwa uhusiano wetu na Mungu umeharibika, kwa hiyo ni kazi bure kuzidi kumwamini, ndipo huwa na mashaka kuhusu upendo wa Mungu kwetu. Hutumaini kututenganisha na Mungu kwa njia hiyo.MwI 139.1

    Wale wanaosimama katika msitari wa mbele katika vita, ambao wanahimizwa na Roho Mtakatifu kutenda mambo maalum, watajikuta pia wamo mashakani wakati hali fulani ikiwapata. Kukata tamaa kunaweza kuitikisa imani ya mtu shujaa kabisa na kuidhoofisha. Lakini Mungu afahamu, hivyo huendelea kuwa na huruma na upendo kwa mtu wa namna hiyo, aliyekata tamaa. Mungu husoma nia na makusudi ya moyo. Waongozi katika kazi ya Mungu wanapaswa kujifunza fundisho kwamba, wakati mambo yakiwawia magumu, yenye giza, yenye kutatiza, hawana budi kusubiri kwa uvumilivu, na kutegemea uongozi wa Mungu bila kuwa na mashaka. Mbingu haitawaacha bila msaada wakati wa dhiki na shida yao. Hakuna kitu kinachoonekana kana kwamba hakina msaada wo wote, lakini kikiwa imara, kuliko mtu anayeweka matumaini yake yote kwa Mungu.MwI 139.2

    Si kwamba ni wenye madaraka makuu katika kazi ya Mungu tu, ndio wanaopaswa kujifunza kutokana na mambo ya Eliya, kwamba, wakati wa majaribu wamtegemee Mungu kabisa. Aliyekuwa nguvu ya Eliya, ndiye anayemshikilia kila mtoto wa Mungu anayeshindana na majaribu ya kila namna. Mungu hutaka kila mtu awe mwaminifu kwake, naye humpa uwezo kwa kadiri ya mahitaji yake. Mtu mwenyewe hana uwezo wo wote, lakini kwake Mungu, mtu huwa na uwezo wa kushinda majaribu na kuwasaidia wengine pia wapate kushinda. Kamwe Shetani hawezi kumshinda mtu yule anayemfanya Mungu kuwa ngome yake. “Mmoja ataniambia, kwa Bwana, peke yake, iko haki na nguvu.” Isaya 45:24.MwI 139.3

    Mkristo mwenzangu, Shetani anajua udhaifu wako; kwa hiyo ambatana na Yesu. Kaa katika pendo la Mungu ndipo utashinda kila jaribu. Haki ya Kristo peke yake yaweza kukupatia uwezo wa kupinga mawimbi ya uovu yanayofurika ulimwenguni. Uwe mwenye imani. Imani hufanya mizigo kuwa miepesi, na kukupa utulivu katika wasiwasi. Siri ya kutatulia matatizo ni kudumu kumtegemea Mungu. Tembea kwa imani katika mapito aliyokuagiza. Majaribu yatakuja, lakini usitishwe, endelea mbele. Majaribu yataimarisha imani yako, na kukufanya ufae kwa kazi yake. Maandiko matakatifu yameandikwa, si kwamba tuyasome tu, na kushangaa, lakini imani waliyokuwa nayo watumishi wa Mungu wa zamani, hata sisi tuwe nayo. Bwana atatenda mambo kwa wenye imani wa sasa, kama alivyotenda kwa wale wa zamani bila kupungua.MwI 140.1

    Neno linanenwa kwetu, kama lilivyonenwa kwa Petro, kwamba, “Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike.” Luka 22:31, 32.MwI 140.2

    Kamwe Kristo hatawaacha watu aliowafia. Sisi tunaweza kushindwa na majaribu tukamwacha, lakini Kristo hawezi kamwe kumtupa mtu ye yote aliyemwaga damu yake kwa ajili yake. Kama macho yetu ya kiroho yangepata njozi tungewaona watu waliolemewa na mizigo wakisumbuka chini ya mateso ya kila namna, wakiwa wamekata tamaa kabisa, wakingojea tu kifo. Tungeweza kuwaona malaika wakipitapita haraka kwenda kuwasaidia watu wanaojaribiwa, wakiwafukuza majeshi ya mwovu yanayo wazunguka, huko wakiwaimarisha hawa na kuwaweka katika msingi imara. Vita inayopiganwa kati ya majeshi ya malaika wema na waovu ni ya hakika, sawa na vita vinavyopiganiwa hapa duniani kati ya mataifa. Vita hivyo vya kiroho ndivyo huamua mwisho wa kila mwanadamu kwamba ni mwema au mbaya.MwI 140.3

    Katika njozi ya nabii Ezekieli, kulikuwa na kuonekana kwa mkono chini ya mabawa ya Kerubi. Jambo hili huwafundisha watu, ambao ni watumishi wa Mungu kwamba, uwezo wa Mungu ndio unaoleta ushindi. Watu wale Mungu anaowatumia kufanya kazi yake wasidhani kwamba, kazi ya Mungu inawategemea wao ili kuimaliza. Wanadamu wadhaifu hawawezi kuachiwa madaraka haya makuu. Mungu ambaye hasinzii, anayefanya kazi daima bila kukoma, ataendesha kazi yake mpaka itimilike, na kukamilika.MwI 140.4

    Yeye atayabatilisha makusudi ya wanadamu waovu, naye atayachafuachafua mashauri yote ya watu yanayokusudiwa kuwadhuru watu wake. Veye ambaye ni Mfalme, Bwana wa majeshi, aketiye kati ya makerubi, kati ya mashindano na fujo ya mataifa, huwahifadhi watoto wake. Wakati ngome za wafalme zitakapopinduliwa wakati mishale ya ghadhabu kali itakapochoma mpaka mioyoni mwa adui zake, watu wake watakuwa salama mikononi mwake.MwI 141.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents