Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    7— Yeroboamu

    Akiwekwa KitiniMwI 73.1

    Akitawalishwa juu ya makabila kumi yaliyoasi kuwa nchi ya nyumba ya Daudi, Yeroboamu alikuwa na madaraka makuu ya kuleta matengenezo halisi kuhusu utawala na mambo ya dini pia. Yeye hapo kwanza alikuwa mtumishi wa mfalme Sulemani. Alipokuwa chini ya uongozi wa Sulemani, alionyesha hali nzuri na welekevu wa mambo mema Mambo aliyojifunza kwa Sulemani kwa muda mrefu, yalimweze ha kutawala kwa busara. Lakini Yeroboamu alishindwa kumtumaini MunguMwI 73.2

    Wasiwasi ya Yeroboamu ilikuwa juu ya raia zake, kwamba, wakati ujao huenda wakashawishika kutaka watawaliwe na mfalme wa jamaa ya Daudi. Akafikirifikiri kuwa, kama raia zake wa makabila kumi, wataendelea kwenda Yerusalemu kila mara kwa ajili ya mikutano ya dini na kafara zitakiwazo, huenda wakavutwa na kutaka kujiunga na utawala wa Yerusalemu. Akishauriana na wazee wake, Yeroboamu alikusudia kuchukua hatua kubwa itakayowazuia watu wasiasi na kutaka kuungana na Yerusalemu. Alikusudi kufanya hivyo kwa njia ya kuanzisha vituo viwili vya ibada ya dini katika utawala wake. Kimoja kilianzishwa huko Betheli na kingine huko Dani. Katika vituo hivi viwili, ndipo ibada zote zingefanyika kwa makabila haya kumi, badala ya kwenda Yerusalemu kama Mungu alivyoagiza.MwI 73.3

    Katika mpango huu, Yeroboamu alitafuta jambo la kuwavutia watu, akatafuta kitu kitakachosimamishwa na kuonekana, kana kwamba kinasimama badala ya Mungu asiyeonekana Kwa hiyo akaamuru watengeneze mifano ya ndama mbili za dhahabu, na kuwekwa mahali pa juu pa ibada. Kwa njia hii ya kufanya mfano wa Mungu, Yeroboamu alihalifu amri ya Mungu isemayo: “Usijifanyie sanamau ya kuchonga. . . Usivisujudie wala kuvitumikia.” Kutoka 20:4, 5.MwI 74.1

    Hivyo Yeroboamu alijitahidi sana kuwafanya makabila yale kumi yasahau mambo ya Yerusalemu. Kwa njia ya shughuli hizo, alisahamu kufuata kanuni halali, hata akashindwa kutambua ubaya wa mpango wake. Hakufahamu juu ya uovu aliokuwa akiwaongoza watu wa Mungu kuuingia. Alikuwa akiingiza ibada ya sanamu katika taifa la Mungu bila kufahamu. Ibada ya namna hiyo ndiyo iliyozoelewa sana na Waisraeli wakati walipokuwa Misri kama watumwa. Kule kukaa kwa Yeroboamu katika nchi ya Misri, kungemfanya ajihadhari kuingiza ibada ya sanamu katika nchi ya Waisraeli, ambayo ilikuwa ikifanywa na mataifa yote yasiyomjua Mungu.MwI 74.2

    Lakini kule kujitahidi kwake kuwazuia Waisraeli wasiende Yuda kuabudu, kulimfanya achukue hatua ya kipumbavu namna hiyo. Aliwaambia watu: “Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri.” 1 Wafalme 12:28. Hivyo wakaongozwa kusujudia sanamu ya dhahabu, na kujifunza kufanya ibada ya namna ya kigeni.MwI 74.3

    Mfalme akajaribu kuwashawishi Walawi waliokuwa katika utawala wake, ili wahudumu katika mpango huu mpya, kama makuhani, huko Betheli na Dani, lakini hakufaulu, walikataa. “Akafanya na watu wo wote, watu wasio wa wana wa Lawi, kuwa makuhani.” Fungu 31. Watu walipohisi juu ya matokeo ya baadaye ya mpango huo, wengi waliokuwa waaminifu, pamoja na jamii kubwa ya Walawi, walikimbilia Yerusalemu kum- wabudu Mungu kama alivyopanga yeye mwenyewe.MwI 74.4

    Yeroboamu akaamuru kushika sikukuu katika mwezi wa nane, siku ya kumi na tano ya mwezi, mfano wa sikukuu iliyokuwa katika Yuda, akapanda juu ili kuiendea madhabahu. Akafanya vivyo katika Betheli akiwatolea dhabihu wale ng'ombe aliowafanya; akawaweka katika Betheli wale makuhani wa mahali pa juu alipokuwa amepafanya.” Fungu la 32.MwI 75.1

    Ukaidi wa mfalme juu ya Mungu wa kuacha maagizo yake kando na kufuata mambo mengine, haukuachwa upite bila kuadhibiwa. Hata wakati ule alipokuwa akihudumu juu ya madhabahu, akichoma kafara na uvumba wakati wa kuzindua madhabahu ya namna ya kigeni aliyoyajenga huko Betheli, mara akatokea mtu wa Mungu kutoka katika ufalme wa Yuda, alikuwa ametumwa ili akanushe ibada ngeni hiyo aliyokuwa ikianzishwa. nabii “akapiga kelele juu ya madhabahu . . . akasema, Ee madhabahu, madhabahu, Bwana asema hivi: Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako.MwI 75.2

    “Akatoa ishara siku ile ile, akasema, “Hii ndiyo ishara aliyoinena Bwana, Tazama, madhabahu itapasuka, na majivu yaliyo juu yake yatamwagika.” Mara hiyo “madhabahu ikapasuka, majivu ya madhabahuni yakamwagika, sawasawa na ishara aliyoitoa mtu wa Mungu kwa neno la Bwana.” 1 Wafalme 13:2, 3, 5.MwI 75.3

    Yeroboamu alipoona mambo haya, akawa mkaidi zaidi, moyo wake ukajazwa na chuki kwa Mungu, akajaribu kumzuia nabii aliyetoa ujumbe huo. Kwa ghadhabu nyingi, mfalme pale madhabahuni, aliunyosha mkono wake, akasema, “Mkamateni.” Tendo lake la harara, lilikemewa pale pale. Mkono ulionyoshwa kwa ghadhabu ili wamkamate mtu wa Mungu, ukapooza, wala haukuwa na nguvu za kurudi mahali pake.MwI 75.4

    Mfalme, akiwa na fadhaa nyingi, alimsihi nabii ili am- wombee kwa Mungu. Alisema, “Umsihi sasa Bwana, Mungu wako, ukaniombee, ili nirudishiwe mkono wangu tena. Yule mtu wa Mungu akamwomba Bwana, mkono wa mfalme ukarudishwa tena, ukawa kama ulivyokuwa kwanza.” Fungu 6.MwI 75.5

    Yeroboamu alijibidisha bure kuzindua na kuingiza ibada ya sanamu iliyo kinyume cha ibada ya kweli ya Mungu inayofanywa huko Yerusalemu. Ujumbe ule wa nabii wa Mungu uliletwa kumtubisha Yeroboamu, ili aache makusudi yake maovu, ambayo yalikuwa na shabaha ya kuwageuzia watu mbali na Mungu. Lakini alishupaza moyo wake, akaazimu kuendelea na makusudi yake maovu.MwI 76.1

    Kwenye siku kuu ya Betheli, mioyo ya Waisraeli haikuwa migumu. Wengi walikuwa tayari kuitikia maongozi ya Roho Mtakatifu. Bwana alikusudia kuwa, wale wenye shingo ngumu, ambao hawataki kuacha njia za uovu, uasi wao lazima ukomeshwe kabla haujaenea sana. Alimtuma mjumbe wake kujitia kati ya ibada yao mbovu, na kuwadhihirishia wote, mfalme na watu wake, matokeo ya baadaye yatakavyokuwa. Kupasuka kwa madhabahu kulikuwa ishara ya chuki ya Mungu kwa tendo hilo, ambalo ni chukizo lililoletwa katika Israeli.MwI 76.2

    Bwana hutafuta kuokoa, si kuangamiza. Yeye hupendezwa kuwaokoa wenye dhambi. Asema: “Kama mimi niishivyo, asema Bwana Mungu, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu.” Ezekieli 33:11. Kwa njia ya kusihi na kuonya Bwana huwaita wapotovu waache njia zao za upotovu, wamgeukie Yeye wapate kuishi. Huwapa wajumbe wake ujasiri mkuu wa kutoa maonyo, ili wanaosikia wapate kuogopa na kutubu. Mjumbe wa Mungu alimkaripia mfalme kwa ujasiri mkuu jinsi gani! Ujasiri huu ulifaa; maana uovu huo uliokuwako haukuweza kukaripiwa kwa njia nyingine, ila hiyo. Bwana alimjalia mjumbe wake kuwa na ujasiri ili maneno yaliyotamkwa hapo yaweze kudumu katika mioyo ya wote walioyasikia. Haiwapasi wajumbe wa Bwana kuziogopa nyuso za watu, bali yawapasa kusimama imara wakiitetea kweli Kadiri wanavyomtegemea Mungu, hawana sababu ya kuogopa; maana aliyewaagiza kufanya kazi hiyo, anawahakikshia pia kuwa atawalinda.MwI 76.3

    Nabii alipomaliza kutoa ujumbe wake alikuwa tayari kurudi wakati Yeroboamu alipomwambia, “Karibu nyumbani kwangu ujiburudishe, nami nitakuwapa thawabu. Mtu wa Mungu akamwambia mfalme, Ujaponipa nusu ya nyumba yako, sitaingia pamoja nawe, wala sitakula chakula, wala sitakunywa maji mahali hapa; maana ndivyo nilivyoagizwa kwa neno la Bwana, kusema, Usile chakula cho chote, wala usinywe maji, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia ” 1 Wafalme 13:7-9.MwI 76.4

    Ingefaa sana kama nabii angeshikilia kusudi lake la kurudi Uyahudi bila kuchelewa. Alipokuwa akisafiri kurudi kwao kwa kupita njia nyingine, alikuwa na mtu mzee aliyedai kuwa hata yeye ni nabii, ambaye alimdanganya mtu wa Mungu, akisema, “Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la Bwana, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji.” Mzee yule alisisitiza tena na tena, mpaka mtu wa Mungu akashawishika, na kurudi.MwI 77.1

    Kwa kuwa nabii wa kweli wa Mungu alishawishwa, akafuata shauri ambalo Mungu hakumwagiza, Mungu alikubali apate adhabu ya uasi. Wakati alipokuwa akiketi pamoja na yule aliyemrudisha huko Betheli, nyumbani mwake, neno la Mungu likamjia yule nabii wa uongo, “akamlilia yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda, akinena, Bwana asema hivi, Kwa sababu umeiasi kauli ya Bwana, wala hukuishika amri ile aliyokuamuru Bwana, Mungu wako . . . maiti yako haitaliingia kaburi la baba zako.” Mafungu 18-22.MwI 77.2

    Unabii huu wa hukumu ulitimizwa baada ya muda si mrefu. “Basi, ikiwa, alipokwisha kula chakula na kunywa maji. . . akamtandikia punda. Na alipokuwa amekwenda zake, simba akamwua. Maiti yake ikatupwa njiani, na yule punda akasimama karibu naye; na yule simba naye akasimama karibu na maiti. Na tazama, watu wakapita wakauona mzoga umetupwa njiani . . . wakaenda wakatoa habari katika mji yule alimokaa yule nabii mzee. Na yule nabii aliyemrudisha njiani alipopata habari, akasema, Ndiye yule mtu wa Mungu, aliyeasi kauli ya Bwana.” Mafungu 23-26.MwI 77.3

    Adhabu iliyomkumba nabii yule ambaye hakuwa mwaminifu ni ushuhuda mwingine wa kuonyesha kwamba unabii uliotolewa kuhusu madhabahu ulikuwa wa kweli. Kama nabii yule asiyetii, angekwenda salama baada ya kutoa unabii na kula chakula huko Betheli, Yeroboamu naye angefanya jambo hilo kama kisingizio cha uasi wake. Katika kupasuka kwa madhabahu, na mkono uliopooza, pamoja na adhabu ya nabii asiyetii amri ya Mungu, Yeroboamu hana budi kujifunza. Ubaya wa kumchukiza Mungu; na adhabu zilizotolewa lazima zim- fundishe kutoendelea kutenda maovu. Lakini bila kujali wala kutubu, Yeroboamu “akafanya tena makuhani wa mahali pa juu, wa watu wo wote. Kila aliyetaka akamfanya wakfu, ili wawepo makuhani wa mahali pa juu! Hivyo basi hakutenda dhambi kuu yeye mwenyewe, bali “aliwakosesha Israeli” pia. “Jambo hilo likawa dhambi kwa nyumba ya Yeroboamu, hata kuiharibu, na kuifuta usoni pa nchi.” 1 Wafalme 13:33, 34; 14:16.MwI 77.4

    Karibu na mwisho wa utawala wake wenye matatizo uliodumu miaka ishirini na miwili, Yeroboamu akapata pigo vitani na Abiya aliyetawala badala ya Rehoboamu. “Wala Yeroboamu hakupata nguvu tena siku za Abiya; kisha Bwana akampiga, akafa.” 2 Mambo ya Nyakati 13:20.MwI 78.1

    Uasi mkuu ulioletwa na Yeroboamu, ulizidi kukua zaidi na zaidi, mpaka mwishowe. ukauangamiza kabisa ufalme wote wa Israeli. Hata kabla ya kufa kwa Yeroboamu, Abiya, nabii mzee wa Shilo, ambaye alitabiri miaka mingi iliyopita kuhusu kutawala kwa Yeroboamu, alisema, “Kwa kuwa Bwawna atawapiga Israeli kama manyasi yatikiswapo majini, naye atawang'oa Israeli katika nchi hii njema, aliyowapa baba zao, naye atawatawanya ng'ambo ya Mto; kwa sababu wamejifanyia maashera yao, wakimkasirisha Bwana. Naye atawatoa Israeli kwa ajili ya makosa ya Yeroboamu, aliyoyakosa, ambayo kwa hayo amewakosesha Israeli.” 1 Wafalme 14:15, 16.MwI 78.2

    Hata hivyo Bwana hakuwatupa Israeli kabla hajawa- shughulikia kwanza, ili wamrudie. Kwa muda wa miaka mingi, wakati wafalme wengi walipotawala, na kuwaongoza Waisraeli katika njia za giza, Mungu aliwatumia ujumbe . . ujumbe, ili kuwasihi wauache uasi wao. Kwa njia ya manabii wake, aliwapa nafasi ya kusahihisha uasi wao, na kumrudia yeye. Miaka ile iliyofuata, baada ya kuurarua ufalme, mwito wa kusihi kutoka kwa vinywa vya Hosea na Amosi na Obadia ulisikika nchini. Ufalme wa Israeli haukuachwa kamwe usipate ushuhuda wa nguvu za Mungu za kuokoa, kutoka dhambini. Hata katika uasi mkuu, wakati wa giza, wengine walidumu kuwa waaminifu. Walishikamana na Mungu, Mtawala Mkuu, wakaishi katikati ya ibada ya sanamu. bila mawaa. Watu hao waaminifu walihesabiwa katika mabaki ya Mungu ambayo kwayo makusudi ya Yehova yatatimizwa mwishowe.MwI 78.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents