Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    8—Uasi Wa Taifa Zima

    Tangu wakati wa kifo cha Yeroboamu mpaka kutokea kwa nabii Eliya mbele ya Ahabu, Waisraeli walikuwa wakididimia kiroho mfulizo. Wakitawaliwa na wafalme wasiomcha Mungu, ambao walikubali kuingiza ibada ya sanamu katika nchi, watu wengi sana walizama maovuni, wala hawakutambua wajibu wao kwa Mungu wao tena, maana walikuwa wameambatana na ibada ya sanamu tu.MwI 81.1

    Nadabu, mwana wa Yeroboamu, alitawala juu ya Israeli miezi michache tu. Maisha yake maovu yalikomeshwa na njama iliyoongozwa na Baasha, mmoja wa majemadari wake Walipomwua, Baasha alishika utawala. Nadabu aliuawa pamoja na jamaa yote ya Yeroboamu. “Hakumwachia Yeroboamu mwenye pumzi ye yote, hata alipomharibu sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa mtumishi wake Ahiya Mshiloni, kwa sababu ya makosa yake Yeroboamu aliyoyakosa; ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli.” 1 Wafalme 15:29, 30.MwI 81.2

    Hivyo ndivyo nyumba ya Yeroboamu ilivyoangamia. Ibada ya sanamu aliyoingiza katika Israeli, iliwapatilizia wote walioiandama, na hukumu za mbinguni zikawaangukia. Walakini, hata hivyo, wafalme waliomfuata,— Baasha, Ela, Zimri, na Omri — kipindi cha miaka arubaini, wote waliendelea katika njia ya uovu.MwI 81.3

    Muda huo wote wa uovu mkuu katika ufalme wa Israeli, Asa alikuwa akitawala katika ufalme wa Yuda. Kwa muda wa miaka mingi, “Basi, Asa akafanya yaliyo mema, yaliyo ya adili, machoni pa Bwana, Mungu wake; maana aliziondoa madhabahu za kigeni, na mahali mahali pa juu, akazivunja nguzo, akayakatakata maashera; akawaamuru Yuda wamtafute Bwana, Mungu wa baba zao, na kuzitenda torati na amri. Tena akaondoa kutoka miji yote ya Yuda mahali mahali pa juu na sanamu za jua; ufalme ukastarehe mbele yake.” 2 Mambo ya Nyakati 14:2-5.MwI 82.1

    Imani ya Asa ilijaribiwa vikali sana, wakati “Zera Mkushi alipotoka juu yao, mwenye jeshi elfu elfu, na magari mia tatu. Katika msukosuko huu, Asa hakutumainia miji yenye ngome mathubuti iliyomo katika ufalme wake, wala hakutumaini watu mashujaa waliokuwa katika jeshi lake.” Mafungu 6-9. Tumaini la mfalme lilikuwa kwa Yehova, Bwana wa majeshi, ambaye, kwa jina lake ukombozi uliwatokea Waisraeli wa kale. Baada ya kuwapanga askari wake vitani, aliutafuta msaada wa Bwana Mungu.MwI 82.2

    Majeshi ya adui sasa yakamkabili uso kwa uso. Wakati huo ulikuwa wa jaribu kali kwa wale wanaomtumikia Mungu. Je, walikuwa wameungama kila dhambi? Je, watu wote wa Yuda walikuwa wakimtumaini Mungu kwa kweli? Mawazo na maswali ya jinsi hii yalikuwamo mioyoni mwa viongozi. Kwa kuonekana kibinadamu, jeshi hili la Misri, litafyagilia mbali kila kitu kinachosimama mbele yake. Lakini wakati wa amani Asa hakustarehe na kujiburudisha kwa anasa; alikuwa amejitayarisha kwa matukio yo yote ya ghafula. Alikuwa na jeshi lililojiandaa vema kwa vita; alikuwa amefanya bidii kuwashauri watu wake wawe na amani na Mungu. Na sasa, ingawa jeshi lake lilikuwa dogo kwa kulinganisha na jeshi la adul zake, imani yake kwa Mungu anayemtumaini, haikupungua kitu.MwI 82.3

    Kwa kuwa mfalme alipatana na Mungu, na kuafikiana vema wakati wa amani, aliweza sasa kumwegemea wakati huu wa matatizo. Maombi yake aliyoomba yanaonyesha kwamba, yeye alijuana na Mungu vizuri. Maana aliomba, akisema: “Bwana, hapana kuliko wewe aliye wa kusaidia, kati yake yeye aliye hodari, na yeye asiye na nguvu; utusaidie, Ee Bwana, Mungu wetu; kwa kuwa sisi twakutegemea wewe, na kwa jina lako tumekuja juu ya jamii kubwa hii Ee Bwana, wewe ndiwe Mungu wetu, asikushinde mwanadamu.” Fungu la 11.MwI 82.4

    Sala iliyoombwa na Asa inafaa sana kwa kila mkristo aombe. Tunapigana, si juu ya damu na nyama, ila tunashindana na falme na mamlaka . . . juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Soma Waefeso 6 12. Katika mashindano ya maisha, hatuna budi kupambana na majeshi maovu, ambao ni wajumbe wa Ibilisi waliojipanga tayari kushindana na haki. Tumaini letu halimo katika mwanadamu, bali limo katika Mungu aliye hai. Lazima tuamini kweli kwamba, uwezo wake wa Mungu, ukiungana na juhudi za kibinadamu, utafaulu na kuleta utukufu kwa jina lake. Tukijivika silaha za haki yake tutafaulu katika mashindano na kila adui.MwI 83.1

    Imani ya mfalme Asa ilipata thawabu. “Basi, Bwana akawapiga Wakushi mbele ya Asa, na mbele ya Yuda; na Wakushi wakakimbia. Asa na watu waliokuwa pamoja naye wakawafuata mpaka Gerari; nao wengi wakaanguka wa Wakushi hata wasiweze kupona; kwa sababu waliangamizwa mbele za Bwana, na mbele ya jeshi lake.” 2 Mambo ya Nyakati 14:12, 13.MwI 83.2

    Wakati washindaji wa Yuda na Benyamini walipokuwa wakirudi Yerusalemu, “Ndipo Roho ya Mungu ikamjia Azaria mwana wa Obedi, naye akatoka ili amlaki Asa, akamwambia, Nisikieni Ee Asa, na Yuda wote na Benyamini; Bwana yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi. Nanyi jipeni nguvu, wala mikono yenu isilegee; kwa maana kazi yenu itakuwa na ijara.” 2 Mambo ya Nyak ati 14:1, 2, 7.MwI 83.3

    Baada ya kutiwa moyo kwa maneno haya Asa alianza matengenezo mengine katika Yuda mara moja. Akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi ya Yuda na Benyamini, na katika miji aliyoitwaa milimani mwa Efraimu; akaifanyiza tena madhabahu ya Bwana, iliyokuwako mbele ya ukumbi wa Bwana.MwI 83.4

    Akakusanya Yuda wote na Benyamini, na hao wageni waliokaa kwao, wa Efraimu na wa Manase na wa Simeoni, kwa kuwa walimwangukia wengi katika Israeli, walipoona kwamba; Bwana, Mungu wake, alikuwa pamoja naye. Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu, katika mwaka wa kumi na tano wa kumiliki kwake Asa. Wakamchinjia Bwana siku ile, katika nyara walizozileta, dhabihu za ng'ombe mia saba, na kondoo elfu saba. Wakafanya agano, ya kuwa watamtafuta Bwana, Mungu wa baba zao, kwa mioyo yao yote, na kwa roho zao zote. Naye ameonekana kwao; naye Bwana akawastarehesha pande zote.” 2 Mambo ya Nyakati 15:8-12, 15.MwI 84.1

    Habari ya uaminifu wa Asa wa muda mrefu, na ushirikiano wake na Mungu, ulichafuliwa na makosa aliyoyafanya, wakati aliposhindwa kutia tumaini lake kamili kwa Mungu. Wakati fulani, mfalme wa Israeli alipoishambulia Yuda, na kuteka Rama, mji wenye boma mathubuti, uliokuwa umbali na yerusalemu kiasi cha maili tano, Asa alitafuta msaada wa wokovu kwa njia ya kuungana na Benhadadi, mfalme wa Shamu. Kosa hili la kutomtumaini Mungu wakati wa shida, lilikemewa na nabii Hanani aliyemtokea Asa akiwa na ujumbe huu: “Kwa kuwa umemtegemea mfalme wa Shamu, wala hukumtegemea Bwana, Mungu wako, kwa hiyo limeokoka jeshi la mfalme wa Shamu mkononi mwako. Je! hao Wakushi na Walubi hawakuwa jeshi kubwa mno, wenye magari na wapanda farasi wengi sana? Lakini kwa kuwa ulimtegemea Bwana, aliwatia mkononi mwake. Kwa maana macho ya Bwana hukimbiakimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo, umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.” 2 Mambo ya Nyakati 16:7-9.MwI 84.2

    Badala ya kujinyenyekeza mbele ya Mungu kwa ajili ya kosa hilo, “Asa akamkasirikia mwonaji, akamtia nyumbani mwa mkatale; maana amemghadhabikia kwa sababu ya neno hilo. Na Asa akawaonea baadhi ya watu wakati ule ule.” Fungu la 10.MwI 84.3

    “Katika mwaka wa thelathini na kenda wa kumiliki kwake, Asa akashikwa na ugonjwa wa miguu; ugonjwa wake ukazidi sana; lakini hakumtafuta Bwana katika ugonjwa wake, bali waganga.” Fungu la 12. Mfalme akafa katika mwaka wa arobaini na mmoja wa kumiliki kwake, Vehoshafati mwanawe akamiliki mahali pake.MwI 84.4

    Miaka miwili kabla ya kufa kwake Asa, Ahabu alianza kumiliki katika ufalme wa Israeli. Tangu mwanzo wa kumiliki kwake, uasi wa kutisha ulionekana dhahiri. Baba yake Omri, aliyeujenga mji wa Samaria, “akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, akatenda maovu kuliko wote waliomtangulia.” 1 Wafalme 16:25. Dhambi ya Ahabu ilikuwa kubwa mno. “Ahabu akazidi kumghadhibisha Bwana, Mungu wa Israeli, kuliko wafalme wote wa Israeli waliomtangulia.” Fungu la 33. Akafanya “kama ingalikuwa neno dogo tu kuyaendea makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati.’” Fungu la 31. Hakutosheka kufuata ibada ya sanamu iliyoanzishwa huko Bethelina Dani, lakini kwa ushupavu wake akawaingiza watu wote katika ushenzi mzito mno; kwa njia ya kuifuta ibada halali ya Mungu, na kusimamisha ibada ya Baali.MwI 85.1

    Ahabu aliingiza ibada hii ya Baali kutoka kwa Yezebeli, binti Ethabaali, mfalme wa Sidoni, aliyemwoa na kufuata miungu yake ya Baali. “Akamjengea Baali madhabahu katika nyumba ya Baali, aliyoijenga huko Samaria.” 1 Wafalme 16:31, 32.MwI 85.2

    Si kwamba Ahabu aliingiza ibada ya Baali huko Samaria, mji mkuu wa serikali peke yake, bali kwa kufuata maongozi ya Yezebeli mkewe, alijenga madhabahu nyingi huko na huko katika mahali pa juu, ambapo wote waliohusika na ibada hiyo waliiendesha mpaka Waisraeli wote wakashawishika na kufuata ibada ya Baali. “Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza . . . atende maovu machoni pa Bwana, ambaye Yezebeli mkewe alimchochea. Akachukiza mno, kwa kuzifuata sanamu sawasawa na yote waliyoyafanya Waamori, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.” 1 Wafalme 21:25, 26.MwI 85.3

    Ahabu alikuwa mfisadi sana. Alipounganika na mwanamke mwovu, ambaye alikuwa na tabia mbovu, wakaoana, jambo hilo halikumletea hatari yeye mwenyewe tu, bali liliangamiza taifa zima pia. Akiwa hakuwa na msimamo thabiti, wala hakufuata kanuni bora, aliyumbishwayumbishwa na mkewe Yezebeli, aliyekuwa na tabia shupavu, ya ukaidi. Hali yake ya kujipendeza haikuweza kufurahia mipango ya Mungu kwa taifa la Israeli, wala mwenyewe hakuweza kuona wajibu wake, kama kiongozi kwa taifa teule.MwI 85.4

    Chini ya uongozi wa Ahabu wenye kupoozesha Waisraeli walitanga mbali sana na Mungu, wakaharibika kabisa mbele za Mungu. Kwa muda wa miaka mingi sana walikuwa gizani, wala hofu ya Mungu haikuwamo ndani yao; hata ikaonekana kuwa hakuna mtu athubutuye kusimama mbele yao na kupinga njia zao za uovu. Giza la uasi mkuu liliifunikiza nchi nzima. Sanamu za Baali na Ashtorethi zilikuwa zimeenezwa kila mahali. Mahekalu ya kuabudia sanamu, ambazo ni kazi za mikono ya wanadamu, yalijaa tele nchini. Hewa ilijaa mioshi ya makafara yaliyokuwa yakitolewa kwa sanamu za uongo, na miungu ya uongo. Vilimani na mabondeni palikuwa na makelele ya kilevi yaliyokuwa yakitoka kwa makuhani waliokuwa wakitoa kafara zao kwa jua, na mwezi na nyota.MwI 86.1

    Kwa njia ya Yezebeli na makuhani wake wapotovu, watu walifundishwa kwamba sanamu za miungu ambazo zimeenezwa kila mahali nchini, zilikuwa miungu yenye uwezo wa kuamuru vitu vya asili ili vitende kazi zao, yaani matetemeko ya nchi mioto, mafuriko na tufani. Baraka zote za mbinguni, yaani mito ya maji itiririkayo taratibu, chemchemi na visima vya maji matulivu, umande na mvua inayorutubisha nchi, ili itoe mazao yake, yote hayo, yalielezwa kwamba, yalitokea kwa ajili ya huruma za Baali na Ashtorethi, badala ya Mungu atupaye mibaraka yake. Watu wakasahau kuwa, milima na mabonde, vijito vya maji na chemchemi, vilikuwa mikononi mwa Mungu aliye hai, ambaye hutawala jua, na mawingu ya mbinguni, na uwezo na sheria zote za asili.MwI 86.2

    Mungu alituma maonyo kwa watu waasi hao, mfalme na watu wote, kwa njia ya wajumbe wake waaminifu, lakini maonyo hayo hayakujaliwa hata kidogo. Maelezo yote ya wajumbe wa Mungu yaliyoelezwa kwamba Mungu aliye hai ndiye Mungu pekee, hayakujaliwa. Hata walipoieleza sheria yake aliyowapa, hawakujali hata kidogo. Watu wakiendea gizani, walithamini ibada ya sanamu ambayo mfalme na wakuu wote walifuata, wakajitoa katika ulevi na uasherati bila kikomo, wakaabudu miungu kwa juhudi kabisa. Katika upumbavu wao, wakamkataa Mungu kabisa, na ibada yake. Nuru waliyomulikiwa na Mungu imezimika, kukawa giza tupu.MwI 86.3

    Lo, utukufu wa Mungu umefarakana nao! Watu wateule wa Mungu hawajazama maovuni kama hawa. “Manabii wa Baali walikuwa mia nne na hamsini, na wale manabii wa Ashera mia nne.” 1 Wafalme 18:19. Uwezo wa Mungu peke yake unaweza kuwaokoa taifa katika uangamivu. Israeli wamefarakana na Mungu kwa hiari, lakini hata hivyo, kwa huruma za Mungu, bado angali anawatafuta wapotevu dhambini, na alikuwa tayari kuwatumia nabii mashuhuri kabisa; ambaye atawarudisha wengi kwa Mungu wa baba zao.MwI 87.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents