Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    20—Naamani

    “Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake Bwana alikua amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.”MwI 205.1

    Ben-hadadi,, mfalme wa Shamu (Syria) alikuwa amewashinda Waisraeli vitani, katika vita iliyomwangamiza Ahabu. Tangu wakati huo Washami waliteka sehemu kubwa ya nchi ya Waisraeli, na katika mashambuliano hayo, Washami walimteka binti mdogo wa Kiisraeli, ambaye alipelekwa kumhudumia “mkewe Naamani.”MwI 205.2

    Binti huyu, ingawa ni mtumwa, tena yuko mbali sana na kwao, alikuwa shahidi mwaminifu wa Mungu, akitimiza kusudi lile ambalo Mungu aliwachagua Waisraeli walitimize. Wakati alipokuwa akihudumu katika nyumba hiyo ya watu wa mataifa, alimhurumia sana bwana wake akikumbuka miujiza ya kuponya iliyofanywa na Elisha katika nchi ya kwao. “Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake.'‘ Alijua kuwa uwezo wa mbinguni ulikuwa.na Elisha, naye aliamini kua Naamani angeweza kuponywa kwa uwezo huu.MwI 205.3

    Maisha ya msichana huyo katika nyumba ya watu wa mataifa hawa, na jinsi alivyotenda ndio ushuhuda wa dhahiri kuonyesha namna mafundisho ya nyumbani wakati wa utoto yalivyo muhimu. Hakuna kazi kuu zaidi waliyokabidhiwa wazazi (baba na mama) kuliko kuwafundisha watoto wao. Wazazi yawapasa kuweka msingi halisi wa tabia za watoto wao. Kwa njia ya wao kuwa vielelezo, na kwa mafundisho yao, maisha ya usoni ya watoto wao hutegemea.MwI 206.1

    Wa heri wazazi wale ambao maisha yao huwa vielelezo vya unyofu wa kweli wa Mungu ili yaweze kuamsha nia za watoto katika ahadi za Mungu na utii wa maagizo yake. Wazazi ambao fadhili zao, na haki yao, na uvumilivu wao hudhihirisha upendo, na haki na uvumilivu wa Mungu kwa watoto wao, na ambao huafundisha watoto kuwapenda, kuwatii na kuwategemea, huwa wanawafundisha kumpenda, kumwamini na kumtii Baba wa mbinguni. Wazazi wanaowapa watoto wao zawadi ya namna hiyo, huwa wamewapatia hazina yenye thamani kuu zaidi ya hazina zote, ambayo ni hazina ya milele.MwI 206.2

    Hatufahamu kuwa watoto wetu watafanya kazi gani watakapokua. Huenda watafanya kazi za kawaida tu karibu na nyumbani kwao; huenda wakawa wakulima; au huenda wakatumwa mbali katika nchi nyingine kuhubiri injili; lakini kwa vyo vyote vile, ni mamoja, yote ni kazi ya Mungu, wakiwahudumia watu duniani. Lazima apate mafundisho yatakayowafanya kusimama imara upande wa Kristo, huku akitoa huduma isiyo na choyo na ubinafsi.MwI 206.3

    Wazazi wa msichana huyo wa Kiebrania, walivyomfundisha juu ya Mungu, hawakufahamu juu ya mambo yake ya usoni, na mahali atakapokuwa. Lakini wao walimfundisha kwa uaminifu sana; na alipokuwa nyumbani mwa jemadari wa jeshi la Washami, alikua shahidi mwaminifu wa Mungu, ambaye alikua akimcha.MwI 206.4

    Naamani aliupata ujumbe, ambao binti alimwambia mkewe, naye baada ya kupata kibali cha mfalme wake, alianza safari ya kutafuta uponyaji, huku akichukua “talanta kumi za fedha, na vipande vya dhahabu elfu sita, na mavazi kumi.” Pia alichukua barua ya mfalme wa Shamu kumpelekea mfalme wa Israeli, ambayo iliandikwa maneno haya: “Tazama, nimemtuma mtumishi wangu Naamani kwako, ili upate kumponya ukoma wake.” “Mfalme wa Israeli alipousoma waraka, alirarua mavazi yake, akasema, Je! mimi ni Mungu, niue na kuhuisha hata mtu huyu akanipelekea mtu imponye ukoma wake? Fahamuni, basi, nakusihini, mwone ya kuwa mtu huyu anataka kugombana nami.” Habari za mambo hayo ziIimfikia Elisha, naye akatuma ujumbe kwa mfalme, kusema, “Mbona umeyararua mavazi yako? Na aje sasa kwangu mimi, naye atajua ya kuwa yuko nabii katika Israeli.”MwI 206.5

    “Basi Naamani akaja na farasi wake na magari yake, akasimama mlahgoni pa nyumba ya Elisha.” Nabii akamtumia mjumbe, kusema, Enenda ukaoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itakurudia, nawe utakuwa safi.”MwI 208.1

    Naamani alikuwa akitazamia mwujiza wa wazi kutoka mbinguni. Kwa hiyo alisema. “Tazama, nilidhania, bila shaka atatoka kwangu, na kusimama, na kuomba kwa jina la Bwana, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma. Je! Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora kuliko maji yote ya Israeli? Je! siwezi kujiosha ndani yake, na kuwa safi? Akageuka, akaondoka kwa hasira.”MwI 208.2

    Moyo wa kiburi wa Naamani ulimzuia asifuate mashauri ya nabii Elisha. Mito iliyotajwa na jemadari wa Kishami ilikuwa inazungukwa na mwitu mzuri, au vichaka, ambavyo watu wengi walikuwa wakimiminika humo ili kuabudu miungu yao. Miungu hiyo ilikuwa imejengewa kandokando ya mito hiyo. Kwenda na kuoga katika mito hiyo kusingeshusha kiburi cha Naamani. Kupona kwake kulitegemea jinsi atakavyofuata mashauri ya nabii. Kuyatii mashauri hayo, ndiko tu kungeleta matokeo mazuri.MwI 208.3

    Watumishi wa Naamani walimsihi afuate mashauri ya Elisha. Walisema, Baba yangu, kama yule nabii angelikuambia kutenda jambo kubwa usingalilitenda? Je! si zaidi basi, akikuambia, Jioshe, uwe safi?” Imani ya Namaani ilijaribiwa sana, wakati kulikuwa na mshindano moyoni mwake baina ya kiburi na unyenyekevu. Lakini imani ilifaulu, na mwenye majivuno huyu wa Shami alikubali kunyenyekea ili kufuata mapenzi ya Mungu. Akajichovya mara saba mtoni Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu, Imam yake ilipata thawabu. Nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi.”MwI 208.4

    Kwa furaha na shukrani, “akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja akasimama mbele yake, akasema, “Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli.”MwI 209.1

    Kama ilivyokuwa kawaida ya siku hizo, Naamani sasa alimsihi Elisha apokee zawadi. Lakini nabii alikataa. Haikuwa haki kupokea zawadi kwa mbaraka uliotolewa na Mungu. Akasema, “Kama Bwana aishivyo . . sipokei kitu.” Yule mtu wa Shamu alimsihi sana apokee, lakini alikataa.MwI 209.2

    “Naamani akasema, Kama sivyo, lakini mtumwa wako apewe mzigo mmoja wa udongo wa baghala wawili, kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa Bwana. Jambo hili Bwana amwachilie mtumwa wako, bwana wangu akiingia nyumbani mwa Rimoni ili aabudu humo, naye akitegemea mkononi mwangu, nami nikijiinama nyumbani mwa Rimoni, hapo ninapojiinama nyumbani mwa Rimoni, Bwana amwachilie mtumwa wako jambo hili. Akamwambia Enenda kwa amani. Basi akamwondokea mbali kidogo.”MwI 209.3

    Cehazi, mtumishi wa Elisha alikuwa amepata nafasi ya kukuza tabia ya utaua kwa kuishi nyumbani mwa Elisha miaka mingi hiyo. Ilikuwa nafasi yake kuwa mtu amchaye Bwana, kwa bahati aliyopata ya kujifunza kwa Elisha Karama bora ya mbinguni imekuwa karibu sana naye. walakini pamoja na bahati hizo zote, Cehazi aligeuka kuwa mtamanifu wa mali za dunia hii Na sasa roho ya choyo na tamaa iliyojificha ndani yak ilimshinda hata akaangukia katika jaribu. Akajisemea nami mwake, “Tazama, bwana wangu amewachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta mimi nitamfuata mbio, nipokee kitu kwake Basi Cehazi akapanga mpango wa kisirisiri, “akamfuata Naamani.”MwI 209.4

    “Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio anakuja nyuma yake alishuka garini amlaki, akasema. “Jel ni amani? Akasema, Amani! Halafu ndipo Cehazi alinena maneno ya uongo wa makusudi, akasema: “Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana wa manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili.” Naamani akafurahi sana kusikia ombi hilo, “akafunga talanta mbili za fedha, badala ya moja, na “mavazi mawili,” akamtwika Gehazi na akawaagiza watumishi wake wamchukulie mali hiyo.MwI 209.5

    Gehazi alipokaribia nyumba ya Elisha, aliwarudisha wale watumishi, akavitwaa vitu vile akavificha mahala. Alipomaliza shughuli hiyo, “akaingia, akasimama mbele ya bwana wake.” Ili kujitakasa, akasema uongo wa pili tena. Nabii alipomwuliza, “Watoka wapi Gehazi?” Gehazi alijibu, “Mtumwa wako hakuenda mahali.”MwI 210.1

    Ndipo maneno makali ya kukemea yakafuata, kuonyesha kuwa Elisha alifahamu yote. Alimwuliza, “Je! moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! huu ndio wakati wa kupokea kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi? Basi, ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.”MwI 210.2

    Jambo hili linatoa fundisho muhimu sana, kuhusu mtu aliyebahatisha kupata nafasi ya upendeleo kama huo. Jambo la Gehazi lilikuwa la kumkwaza Naamani, mtu aliyepata bahati ya kugundua nuru ya kweli, na mvuto wa kumwelekea Mungu. Udanganyifu uliofanywa na Gehazi hauna udhuru. Katika maisha yake yaliyobaki aliendelea kuwa na ukoma, wenye laana ya Mungu, huku akitengwa mbali na wenzake.MwI 210.3

    “Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa, wala asemaye uongo hataokoka.” Mit. 19:5. Watu wanaweza kudhani kuwa kuficha vitendo vyao viovu machoni pa watu inafaa, lakini machoni pa Mungu wako wazi. “Lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.” Waebrania 4:13. Gehazi alidhani kuwa atamdanganya Elisha, lakini Mungu alimfunulia nabii wake maneno yote Gehazi aliyomwambia Naamani, na mambo yote yaliyofanyika.MwI 210.4

    Kweli ni ya Mungu, na udanganyifu wote wa hali zote ni wa Shetani; na mtu ye yote anayejiondoa katika njia ya wima, hujiweka katika kiwanja cha yule mwovu. Wala waliojifunza na kujua mapenzi ya Mungu, hawana ushirika na matendo yasiyozaa, ya giza.” Waefeso 5:11. Katika usemi, na katika hali yote ya maisha watakuwa watu wa kawaida wa kweli, wasiokuwa vigeugeu, maana wao wanajiandaa kushirikiana na watakatifu, ambao katika vinywa vyao hakuna hila. Soma Ufunuo 14:5.MwI 210.5

    Karne nyingi zilipokwisha kupita baada ya kuponya kwa Naamani, imani yake ilitajwa na Mwokozi kama kielelezo cha wote wanaomtumikia Mungu. Mwokozi alisema, “Tena, palikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli zamani za nabii Elisha, wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu.” Luka 4:27. Mungu aliwaacha wenye ukoma wengi katika Israeli kwa ajili ya kutokuamini kwao, walijizuilia mema mengi. Mtu wa mataifa ambaye alikuwa mtu wa haki, na mwenye kutaka msaada, machoni pa Mungu alistahili kupata baraka za mbinguni kuliko waisraeli waliokuwa wagonjwa, ambao walipata bahati ya Mungu na kuidharau. Mungu hufanya kazi kwa wale wanaothamini mashauri yake, ambao hufuatana na ujuzi wa mbinguni waliojaliwa kuupata.MwI 211.1

    Leo, katika kila nchi kuna watu wanyofu rohoni mwao, na kwa watu hao nuru ya mbinguni huwaangazia. Kama wakidumu kufuata nuru hiyo kwa uaminifu, wataongezewa nuru kuu zaidi, mpaka itawalazimu kukiri kama Naamani wa zamani alivyokiri, na kusema, “Hakuna Mungu duniani mwote, ila Mungu Mwumbaji.”MwI 211.2

    Kwa kila mtu wa kweli, “ambaye anakwenda katika giza, wala hakuna nuru,” mwito unamjia na kusema, “Naye alitumainie jina la Bwana, na kumtegemea Mungu wake.” “Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye. Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo ya haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako.” Isaya 50:10; Isaya 64:4, 5.MwI 211.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents