Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    2—Hekalu Na Kuzinduliwa Kwake

    Mpango wa Daudi wa siku nyingi wa kumjengea Bwana hekalu, ulikamilishwa na Sulemani. Kwa muda wa miaka saba mji wa Yerusalemu ulikuwa umejaa watu waliokuwa wakishughulika na ujenzi wa hekalu, wengine waki- sawazisha uwanja, wengine wakijenga msingi, wengine wakijenga nguzo za ukuta—“Mawe makubwa, mawe ya thamani, ili wauweke msingi wa nyumba kwa mawe yaliyochongwa” — wengine kuchonga mbao kubwa zilizoletwa kutoka katika mwitu wa Lebanoni, na wengine kusimamisha jengo lenyewe. 1 Wafalme 5:17.MwI 17.1

    Watu maelfu walishughulika na jengo hili kwa vifaa vili- vyotayarishwa tayari, yaani mbao na mawe. Kazi hii iliongozwa na Hiramu mtu wa Tiro, “Mtu mstadi, mwenye akili . . . ajuaye sana kazi ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, ya chuma, ya mawe, na ya mti, ya urujuani, ya samawi, na ya kitani safi, na ya nyekundu.” 2 Mambo ya Nyakati 2:13, 14.MwI 17.2

    Hivyo jengo lililojengwa juu ya mlima wa Moria likaen- delea bila kusikika kelele yo yote, “ikajengwa kwa mawe yaliyokwisha kuchongwa chimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma cho chote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba,” matengenezo yote yalikamilika jinsi Daudi alivyomwagiza mwanawe, “vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu.” 1 Wafalme 6.7; 2 Mambo ya Nyakati 4:19. Vyombo hivyo ni madhabahu ya kufukizia uvumba, meza ya mikate ya wonyesho, kinara na taa, pamoja na vyombo vinavyohusiana na huduma ya makuhani katika patakatifu, vyote hivyo, “ndivyo dhahabu bora.” 2 Mambo ya Nyakati 4:21. Vyombo vya shaba — madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, birika kubwa lililoshikiliwa na maksai kumi na wawili wa ng'ombe, na mabirika madogo pamoja na vyombo vingine vingi — “katika uwanda wa Yordani ndipo mfalme alipovisubu, katika udongo mzito kati ya Sukothi na Sereda.” 2 Mambo ya Nyakati 4:17. Vifaa hivi vilitengenezwa kwa wingi ili pasiwepo na upungufu wo wote.MwI 17.3

    Jumba ambalo Sulemani na wasaidizi wake walilomjengea Mungu ili kumwabudia, lilikuwa zuri mno la fahari kabisa kupita yote. Jumba hilo, likiwa limepambwa kwa vito vya thamani, likiwa limezungukwa na uwanja mkubwa wenye njia za kupitia kulifikia, likiwa limezungukwa na nguzo za mierezi zenye kunakishwa kwa dhahabu safi, IiIistahili kabisa kuwa kanisa la Mungu hapa duniani, ambalo kwa miaka yote limejengwa kwa mfano wa lile la mbinguni, likijengwa kwa vitu vilivyofananishwa na “dhahabu au fedha au mawe ya thamani,” zilizonakishwa kwa kupamba hekalu.” 1 Wakorintho 3:12; Zaburi 144:12. Katika Hekalu hili la kiroho “Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana.” Waefeso 2:20, 21.MwI 18.1

    Mwishowe, hekalu lililopangwa kujengwa na Daudi. likajengwa na mwanawe Sulemani lilimalizika. “Na yote yaliyomwingia Sulemani moyoni ayafanye nyumbani mwa Bwana. . . akayafanikisha,” 2 Mambo ya Nyakati 7:11. Na sasa, ili kusudi hekalu hili lililoko juu ya mlima wa Moria liwe kama Daudi alivyokusudia tangu zamani maskani “si kwa mwanadamu, ila kwa Bwana, Mungu” (1 Mambo ya Nyakati 29:1), kilibaki kitu kimoja tu, ndiyo sherehe ya kulizindua na kuliweka wakfu kwa Yehova na ibada yake.MwI 18.2

    Mahali pale hekalu lilipojengwa palihesabiwa kuwa mahali patakatifu tangu zamani. Hapo ndipo Ibrahimu, baba wa waaminifu, alipoonyesha imani yake kwa kukubali kumtoa mwanawe wa pekee kuwa kafara, kama Yehova alivyomwagiza. Hapo ndipo Mungu alipofanya upya agano na Ibrahimu kwamba atambariki, agano ambalo huhusu ahadi ya Masihi atakayekuja kuwaokoa wanadamu kwa njia ya kafara yake mwenyewe, ambaye ni Mwana wa Mungu aliye juu. Soma Mwanzo 22:9, 16-18.MwI 19.1

    Hapo ndipo Daudi alipotoa kafara ya kuteketezwa na kafara ya amani ili kuzuia tauni iliyokuwa ikiendeshwa na malaika, na Mungu alimjibu kwa moto kutoka mbinguni. Soma 1 Mambo ya Nyakati 21. Na sasa mara nyingine tena watu wa Mungu wamekusanyika hapo ili kumwabudu, na kufanya agano lao na Mungu upya.MwI 19.2

    Siku iliyochaguliwa kwa sherehe hiyo ilikuwa ya kufaa sana—mwezi wa saba, ambapo ilikuwa kawaida ya watu kukusanyika Yerusalemu ili kuadhimisha siku kuu ya vibanda. Siku kuu hii ilikuwa ya furaha sana. Maana shughuli ya mavuno huwa imekwisha, na kazi za mwaka mpya huwa hazijaanza bado. Kwa hiyo watu walikuwa huru bila kusongwa na kitu, wapate kufurahia mambo ya dini.MwI 19.3

    Siku ilipofika, makundi ya wana wa Israeli pamoja na wageni wengine kutoka kwa mataifa mengine walikusanyika kwenye uwanja wa hekalu. Lo, kilikuwa kivumbi. Sulemani pamoja na wazee wa Israeli na watu wakuu, walikuwa wamerudi kutoka upande mwingine wa mji kuleta sanduku la agano. “Ile hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwamo Hemani” vilikuwa vimehamishwa kutoka milima ya Gibeoni kupata maskani ya kudumu katika jumba tukufu lililojengwa kuingia mahali pa hema. (Soma 2 Mambo ya Nyakati 5:5).MwI 19.4

    Wakati wa kulileta sanduku takatifu hekaluni, ambamo zimo mbao mbili za mawe zenye amri za Mungu alizoandika yeye mwenyewe, Sulemani alifanya kama baba yake Daudi alivyofanya. Kila hatua sita walitoa kafara. Kwa furaha na shangwe ya nyimbo na maadhimisho makuu, “Makuhani wakaliingiza sanduku la agano la Bwana mahali pake katika chumba cha ndani cha nyumba, patakatifu pa patakatifu.” 2 Mambo ya Nyakati 5:7. Walipotoka ndani walijipanga mahali pao. Waimbaji wana wa Lawi, wakiwa katika mavazi yao rasmi, mavazi meupe, wenye matoazi na vinanda na vinubi, walijipanga upande wa mashariki mwisho wa madhabahu, pamoja nao kulikuwa na makuhani mia moja na ishirini wenye matarumbeta. Soma 2 Mambo ya Nyakati 5:12.MwI 19.5

    “Hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru Bwana; nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya Bwana, hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao, kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa Bwana.” 2 Mambo ya Nyakati 5:13, 14.MwI 20.1

    Sulemani akielewa umuhimu wa wingu hilo, alinena, “Bwana alisema ya kwamba atakaa katika giza nene. Lakini nimekujengea nyumba ya kukaa, iwe mahali pa makao yako milele.” 2 Mambo ya Nyakati 6:1, 2.MwI 20.2

    “Bwana ametamalaki, mataifa wanatetemeka;
    Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika.
    Bwana katika Sayuni ni mkuu.
    Naye ametukuka juu ya mataifa yote.
    Na walishukuru jina lake kuu la kuhofiwa.
    Ndiye Mtakatifu. . . .
    Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu;
    Sujuduni penye kiti cha miguu yake;
    MwI 20.3

    Ndiye mtakatifu.” Zaburi 99:1-5.

    “Sulemani alikuwa amefanya mimbari ya shaba, urefu wake mikono mitano, na upana wake mikono mitano, na kwenda juu kwake mikono mitatu na kuisimamisha katikati ya ua.” Juu ya mimbari hii Sulemani alisimama akanyosha mikono yake, akawabariki wote mkutano mzima. “Na mkutano wote wa Israeli wakasimama.” 2 Mambo ya Nyakati 6:13, 3.MwI 20.4

    Sulemani akasema, “Bwana, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenena kwa kinywa chake na baba yangu Daudi . . . akasema. . . . Nimeuchagua Yerusalemu, jina langu liwe humo.” 2 Mambo ya Nyakati 6:4-6. Kisha Sulemani akapiga magoti kuomba sala ya kuzindua jengo, huku akisikiwa na watu wote. Akiinyosha mikono yake kuelekea mbinguni, hali mkutano wote umeinamisha vichwa vyao, aliomba akisema, “Ee Bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe, mbinguni, wala duniani; ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako waendao mbele zako kwa moyo wao wote.MwI 20.5

    Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; siuze nyumba hii niliyoijenga! Walakini um- wangalie mtumwa wako anayoyaomba, na kusihi, Ee Bwana, Mungu wangu, usikie kilio na maombi anayoyaomba mtumwa wako mbele zako; ili macho yako yafumbuke kwa nyumba hii mchana na usiku, mahali uliponena, ndipo utakapoliweka jina lako; usikie maombi atakayoomba mtumwa wako, na watu wako Israeli, watakapoomba wakikabili mahali hapa, naam, usikie toka makaoni mwako, toka mbinguni, nawe usikiapo, samehe. . . .MwI 21.1

    Ikiwa watu wako Israeli, wamepigwa mbele ya adui zao, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakirejea kwako, na kulikiri jina lako, wakikuomba na kukusihi nyumbani humu; basi usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watu wako Israeli, na kuwarejeza tena katika nchi uliyowapa wao na baba zao.MwI 21.2

    Ikiwa mbingu zimefungwa, hata hakuna mvua, kwa sababu wamekukosa wewe; kama wakiomba wakikabili mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kuiacha dhambi yao, uwatesapo; basi usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watumwa wako, na ya watu wako Israeli; uwafundishapo njia njema iwapasayo waiendee; ukainyeshee mvua nchi yao, uliyowapa watu wako iwe urithi.MwI 21.3

    Ikiwa nchi imeingia njaa, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewahusuru katika nchi ya miji yao; au ukiwapo msiba wo wote, au uele wo wote; yo yote atakayoyaomba na kusihi mtu awaye yote, au watu wako Israeli wote pamoja, watakaojua kila mtu pigo lake mwenyewe, na msiba wake mwenyewe, akiinyoshea mikono nyumba hii; basi usikie huko mbinguni, ukaapo, ukasamehe, ukampatilize kila mtu kwa kadiri ya njia zake zote; wewe um- juaye moyo ... ili wakuche wewe, waziendee njia zako, siku zote watakazoishi katika nchi uliyowapa baba zetu.MwI 21.4

    Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako kuu, na mkono wako ulio hodari, na mkono wako ulionyoshwa; hao watakapokuja na kuomba wakiielekea nyumba hii; basi usikie huko mbinguni, toka makaoni mwako, ukatende yote atakayokuomba huyo mgeni; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe, kama watu wako Israeli, tena wajue ya kuwa nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa jina lako.MwI 22.1

    Ikiwa watu wako wametoka kupigana na adui zao, utakakowatuma ko kote, wakikuomba kuuelekea mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako; basi uyasikie huko mbinguni wayaombayo, na kusihi, ukaitetee haki yao.MwI 22.2

    Wakikukosa, (maana hakuna mtu asiyekosa) hata uwakasirikie, na kuwatia mikononi mwa adui zao, wawahamishe, na kuwachukua mateka mpaka nchi iliyo mbali au iliyo karibu; basi wakikumbuka katika nchi walikohamishwa, na kutubu, na kukusihi katika nchi ya uhamisho wao, wakisema, Tumekosa, tumetenda kwa ukaidi, tumefanya maovu; wakurudiapo kwa mioyo yao yote, na kwa nia zao zote, katika nchi ya uhamisho wao, adui walikowahamisha, wakiomba na kuielekea nchi uliyowapa baba zao, na mji huu uliouchagua, na nyumba hii niliyoijenga kwa jina lako; basi uyasikie toka mbinguni, toka makaoni mwako, wayaombayo na kesihi, ukaitetee haki yao; ukawasamehe watu wako, waliokosa juu yako.MwI 22.3

    Na sasa, Ee Mungu wangu, macho yako yafumbuke, nakusihi, masikio yako yakasikilize maombi yaombwayo mahali hapa. Sasa, Ee Bwana, Mungu uondoke, uende kwenye raha yako, wewe na sanduku la nguvu zako; makuhani wako, Ee Bwana, Mungu, wavikwe wokovu, watakatifu wako na washangilie mema. Ee Bwana, Mungu, usiurudishe nyuma uso wa masihi wako; uzikumbuke fadhili za Daudi mtumishi wako.” 2 Mambo ya Nyakati 6:14-42.MwI 22.4

    Sulemani alipomaliza kuomba, “Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukateketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu.” Makuhani hawakuweza kuingia hekaluni, yaani nyumbani mwa Bwana, “Kwa kuwa utukufu wa Bwana umeijaza nyumba ya Bwana. Wakatazama wana wa Israeli wote. ... utukufu wa Bwana ulipokuwapo juu ya nyumba wakasujudu kifulifuli hata nchi sakafuni, wakaabudu, wakamshukuru Bwana, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele.”MwI 24.1

    “Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za Bwana. . . . Ndivyo mfalme na watu wote walivyoifanya wakfu nyumba ya Mungu.” 2 Mambo ya Nyakati 7:1-5. “Sulemani akafanya sikukuu, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa sana, toka maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Misri, muda wa siku saba. Hata siku ya nane wakaita kusanyiko la makini; kwa maana walishika kuitakasa madhabahu siku ya saba, na sikukuu siku saba. Akawaruhusu watu. . . .kwao, wakifurahi na kuchangamka mioyoni kwa wema wote Bwana aliomfanyia Daudi, na Sulemani, na Israeli, watu wake.” 2 Mambo ya Nyakati 7:8-10.MwI 24.2

    Mfalme alifanya kila jambo kadiri ya uwezo wake ili kuwavuta watu wajitoe kamili kwa Mungu wapate kumtumikia na kulitukuza jina lake takatifu. Na sasa tena, kama vile huko Cibeoni, mfalme alipata kibali kwa Mungu, na hakikisho la kumbariki. Katika njozi ya usiku, Bwana alimtokea akiwa na ujumbe huu: “Nimesikia uliyoyaomba, na mahali hapa nimejichagulia kuwa nyumba ya dhabihu. Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.MwI 24.3

    Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa. Maana sasa nimeichagua nyumba hii na kuitakasa, ili kwamba jina langu lipate kuwako huko milele; yatakuwako na macho yangu, na moyo wangu daima.” 2 Mambo ya Nyakati 7:12-16.MwI 24.4

    Kama Waisraeli wangedumu kuwa waaminifu kwa Mungu, jengo hili mashuhuri lingesimama milele, kuwa ushuhuda wa daima jinsi Mungu anavyowapendelea watu wake. Mungu asema, “Na wageni, walioandamana na Bwana ili wamhudumu, na kulipenda jina la Bwana, kuwa watumishi wake; kila aishikaye Sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu; nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.” Isaya 56:6, 7.MwI 25.1

    Pamoja na uthibitisho huo wa kibali, Bwana alimdhihirishia mfalme Sulemani wajibu wake hivi:MwI 25.2

    “Nawe ukienda mbele yangu kama alivyokwenda Daudi baba yako, ufanye sawasawa na yote niliyokuamuru na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu; ndipo nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyoagana na Daudi baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kutawala katika Israeli.” 2 Mambo ya Nyakati 7:17, 18.MwI 25.3

    Kama Sulemani angeendelea kumtumikia Mungu kwa moyo mnyofu, ufalme wake ungeeneza mvuto bora kwa mataifa yaliyowazunguka, mataifa ambayo yalikuwa yamevutiwa na hali ya utawala wa Daudi, baba yake, na pia na hali ya utawala wake wakati wa mwanzo, na maneno yake yenye hekima. Mungu akiona majaribu ya kutisha yanayoambatana na ufanisi na heshima ya dunia, alimwonya Sulemani juu ya kuasi, na matokeo mabaya yanayofuata dhambi. Akamwambia kuwa, hata hekalu maridadi ambalo limewekwa wakfu hivi karibuni litakuwa, “mithali na tukano katikati ya watu wote”, kama Waisraeli wata mwacha “Mungu wa baba zao.” 2 Mambo ya Nyakati 7:20, 22.MwI 25.4

    Sulemani aliishika kazi ya utawala kwa moyo mkuu, kwa sababu ya uthibitisho aliopewa na Mungu kwa kuyakubali maombi yake Hicho kilikuwa kipindi muhimu katika maisha yake, wakati ambapo “Wafalme wote wa dunia,” walipoanza “kumtafuta uso wake Sulemani, ili waisikie hekima yake, Mungu aliyomtia moyoni.” 2 Nyakati 9:23. Wengi walimjia ili kuona narnna ya utawala wake ulivyo, na kujifunza namna ya kuamua mambo magumu.MwI 25.5

    Watu hao walipokuwa wakija kwa Sulemani, alipata nafasi kuwafundisha habari za Mungu aliyeumba vitu vyote, nao wakarudi kwao wakifahamu zaidi habari za Mungu wa Waisraeli, na jinsi anavyowapenda wanadamu. Walipoangalia viumbe waliweza kuona kazi ya Mungu na upendo wake, pia wakaona namna tabia yake ilivyo. Hivyo wengi walimwamini na kumwabudu.MwI 26.1

    Unyenyekevu wa Sulemani wakati alipoanza kuchukua mzigo wa utawala, wakati alipokiri mbele za Mungu, “Mimi ni mtoto mdogo tu” (1 Wafalme 3:7), alipokuwa akimpenda Mungu kwa moyo, na kuheshimu mambo matakatifu — yote hayo yalidhihirika wakati aliposhughulika kumjengea Mungu nyumba, na wakati alipopiga magoti akitoa sala ya kuweka wakfu hekali. Wafuasi wa Kristo wa leo hawana budi kujihadhari sana wasije wakapungukiwa na roho ya kuheshimu mambo matakatifu, na kicho halisi. Maandiko matakatifu hufundisha namna inavyowapasa wanadamu kuishi na muumba wao— lazima waishi kwa unyenyekevu na kicho, kwa njia ya imani katika mpatanishi, yaani Yesu Kristo. Mtunga Zaburi husema:MwI 26.2

    “Kwa kuwa Bwana ni Mungu mkuu,
    Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote. . . .
    Njoni, tuabudu, tusujudu,
    Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba.”
    MwI 26.3

    Tukisali katika chumba chetu au kanisani, inatulazimu kupiga magoti mbele za Mungu. Po pote tuombapo ni haki kupiga magoti. Yesu ambaye ni kielelezo chetu, “akapiga magoti akaomba.” Luka 22:41. Kuhusu wanafunzi wake imeandikwa kwamba, hata Petro pia “akapiga magoti akaomba.” Matendo 9:40. Paulo anasema, “Kwa hiyo nampigia Baba magoti.” Waefeso 3:14. Ezra alipokuwa akiungama dhambi za Waisraeli alipiga magoti. Soma Ezra 9:5. Danieli alikuwa “akipiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake.” Danieli 6:10.MwI 26.4

    Kicho halisi cha Mungu huwapo wakati tunapoelewa jinsi alivyo Mkuu mno bila kifani, na tunapofahamu kuwa yuko pale tunapokusanyika. Kule kuelewa mambo hayo, ingawa hayaonekani kwa macho kungemfanya kila mtu kuwa na kicho. Mahali pa sala na wakati wa sala ni vitu vitakatifu, vyenye kuheshimiwa na kwa sababu Mungu yuko hapo. Jinsi tunavyoonyesha heshima kwa nje, hali kadhalika heshima hiyo inavyoongezeka mioyoni pia Mtunga Zaburi asema: “Jina lake ni takatifu la kuogopwa.” Zaburi 111:9. Malaika wanapolitaja jina hilo hufunika nyuso zao. Je, sisi wenye dhambi tulioanguka maovuni, tunalitajaje jina hilo kuu!MwI 27.1

    Ingefaa sote, wakubwa kwa vijana tufikirie sana maneno ya maandiko matakatifu yanayosema mambo kuhusu mahali Mungu alipo. Mungu alimwamuru Musa pale penye kichaka kilichokuwa kikiwaka moto, akasema, “Vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapa unaposimama ni nchi takatifu.” Kutoka 3:5. Yakobo, alipokwisha kuona njozi ya malaika, alisema, “Kweli Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. . . . Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni.” Mwanzo 28:16, 17.MwI 27.2

    Mambo ambayo Sulemani aliyasema wakati wa kuzindua hekalu, yalikusudiwa kuondoa mawazo ya ushirikina yanayofikiriwa na watu wa mataifa, na kugeuza fikira zote kwa Mungu Muumbaji. Mungu wa mbinguni hafanani na miungu ya watu wa mataifa, ambao hukaa katika vihekalu vinavyojengwa na mikono ya watu; Mungu wa mbinguni sivyo alivyo; walakini hukubali kukutana na wanadamu kwa njia ya roho wake, wanapokusanyika katika majengo yaliyowekwa wakfu kwa ajili Ya kumwabudu yeye.MwI 27.3

    Baada ya karni nyingi, mtume Paulo alifundisha mambo yale yale, aliposema, “Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono; wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote . . . . ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa- papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu. Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu.” Matendo 17:24-28.MwI 27.4

    “Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao,
    Watu aliowachagua kuwa urithi wake.
    Toka mbinguni Bwana huchungulia,
    Huwatazama wanadamu wote pia.
    Toka mahali pake aketipo
    Huwaangalia wote wakaao duniani.”

    “Bwana ameweka kiti chake cha enzi mbinguni,
    Na ufalme wake unavitawala vitu vyote.”

    “Ee Mungu, njia yako i katika utakatifu;
    Ni nani aliye mungu mkuu kama Mungu?
    Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu;
    Uliudhihirisha uwezo wako kati ya mataifa.”
    MwI 28.1

    Zaburi 33:12-14; 103:19; 77:13, 14.

    Ingawa Mungu hakai katika mahekalu yaliyofanywa kwa mikono, lakini hukubali kukutana na watu wake wanapokusanyika. Ameahidi kuwa wanapokusanyika ili kumtafuta na kuungama dhambi zao, na kuombeana, atakutana pamoja nao kwa njia ya Roho wake. Lakini wale wanaokusanyika ili kumtafuta, lazima waweke mbali kila aina ya uovu. Wasipomwabudu katika roho na kweli na kwa uzuri wa utakatifu, kukusanyika kwao huwa kwa bure. Bwana ananena kuhusu jambo hilo.” “Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure.” Mathayo 15:8, 9. Wale wanaomwabudu Mungu yawapasa kumwabudu katika “roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.” Yohana 4:23.MwI 28.2

    Lakini Bwana yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.” Habakuki 2:20.MwI 28.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents