Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    6—Kuraruliwa Kwa Ufalme

    “Naye Sulemani akalala na baba zake, akazikwa katika mji wa Daudi baba yake; na Rehoboamu mwanawe akatawala mahali pake.” 1 Wafalme 11:43.MwI 63.1

    Mara tu baada ya . . . , Rehoboamu alipanda kwenda Shekemu, ambapo alitazamia kutawazwa mbele ya makabila yote ya Israeli. “Maana Israeli wote walikuwa wamekuja Shekemu, ili wamfanye mfalme.” 2 Mambo ya Nyakati 10:1.MwI 63.2

    Miongoni mwa waliohudhuria, alikuwamo Yeroboamu mwana wa Nebati . . . ni yule yule, ambaye katika utawala wa Sulemani alijulikana kama “mtu hodari, shujaa,” ambaye nabii Ahiya Mshloni alimtolea ujumbe, akisema, “Nitaurarua ufalme, na kuuondoa katika mkono wa Sulemani, nami nitakupa wewe kabila kumi.” 1 Wafalme 11:28, 31.MwI 63.3

    Kwa njia ya mjumbe wake, Bwana alimwambia Yeroboamu kwamba ataurarua ufalme na kuugawanya. Mgawanyiko huu hauna budi kutokea. Maana amenena, “Kwa sababu wameniacha mimi wakaabudu Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni, na Kemoshi, mungu wa Wamoabi, na Milkomu, mungu wa wana wa Amoni, wala hawakuenda katika njia zangu, kutenda mema machoni pangu, kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, kama Daudi.” Fungu la 33.MwI 63.4

    Yeroboamu alikuwa ameambiwa kwamba, mgawanyiko huu wa ufalme hautatokea kabla ya kumalizika kwa utawala wa Sulemani. Bwana alikuwa amenena, “Sitauondoa ufalme wote katika mkono wake; lakini nitamfanya awe mkuu siku zote za maisha yake, kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi niliyem- chagua; kwa maana alizishika amri zangu na sheria zangu, lakini nitauondoa ufalme katika mkono wa mwanawe, nami nitakupa wewe kabila kumi.” Mafungu 34, 35.MwI 64.1

    Ingawa Sulemani alitamani kumtayarisha mwanawe Rehoboamu, ili aweze kukabili mambo yaliyosemwa na nabii wa Mungu kuhusu ufalme kwa hekima hakufaulu kumvuta mwanawe kutoka katika hali mbaya, aliyoiga tangu utoto wake. Rehoboamu alipata tabia mbaya ya kutangatanga kutokana na mvuto wa mama yake, Mwamoni. Kwa muda alijitoa kum- tumikia Mungu, na kafanikiwa kiasi fulani, lakini hakuwa mwenye nia imara, mwishowe akashikamana na mivuto minyonge aliyozoea tangu utotoni. Maovu yaliyotokea katika maisha ya Rehoboamu, mpaka yakampeperushia mbali, kiasi cha kupotea na kumwasi Mungu yanadhihirisha matokeo ya kutisha ya mwungano wa Sulemani na wanawake wenye kuabudu sanamu.MwI 64.2

    Makabila ya Israeli yalikuwa yameteseka sana chini ya utawala mbaya wa Sulemani. Maisha ya anasa ya mfalme yalisababisha kuwatoza watu kodi kubwa mno na utumishi mzito kutoka kwa raia. Hayo yote yalitokea wakati wa uasi wake. Kwa hiyo kabla ya kuendelea na sherehe ya kutawazwa, waongozi wote walipenda kufahamu kwanza, kama mfalme mpya atawapunguzia watu mzigo huo au la. “Yeroboamu akaja na Israeli wote, wakamwambia Rehoboamu, wakasema, Baba yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa upunguze utumwa mgumu wa baba yako na kongwa lake zito alilotutwika, nasi tutakutumikia.”MwI 64.3

    Akitaka kupata shauri kwa washauri wake kwanza, kabla ya kupanga kanuni zake, Rehoboamu aliwajibu akasema, “Mnirudie baada ya siku tatu.” Watu wakaenda zao.MwI 64.4

    “Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee, waliosimama mbele ya Sulemani baba yake, alipokuwa hai bado, akasema, Mwanipa shauri gani la kuwajibu watu hawa? Wakamwambia, wakasema, Ukiwa mwema kwao watu hawa, na kuwapendeza, na kuwaambia maneno mazuri, ndipo watakapokuwa watumishi wako siku zote.” 2 Mambo ya Nyakati 10:3-7.MwI 65.1

    Asiporidhika, Rehoboamu akageuka kwa vijana wa rika moja naye, waliopitisha ujana wao pamoja, akawauliza akisema, “Mwanipa shauri gani ili tuwajibu watu hawa, waliosema nami, wakinena, Utufanyie jepesi kongwa lile alilotutwika baba yako?” 1 Wafalme 12:9. Vijana walimshauri kwamba, asiruhusu raia kumchezeachezea, awadhihirishie wazi kwamba, hatakubali kuingiliwa katika mipango yake.MwI 65.2

    Akiutumaini uwezo wake na ukuu wake, Rehoboamu akatupilia mbali shauri alilopewa na wazee, akafuata shauri la vijana. Basi ikafika siku waliyoagana na watu “Yeroboamu na vatu wote wakamfikia Rehoboamu,” ili kusudi wasikie kanuni takayofuatwa katika ufalme huo. “Mfalme akawajibu watu vale kwa ukali”. . . . Akasema, “Baba yangu alilifanya zito ongwa leni, bali mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu liwapiga kwa mijeledi, bali mimi nitawapigeni kwa nge.” lafungu 12-14MwI 65.3

    Kama Rehoboamu na washauri wake wasio na busara angefahamu mpango wa Mungu kwa Israeli, wangesikiliza aombi ya watu juu ya mageuzo kadhaa katika taratibu za falme. Lakini katika nafasi iliyoafikia huko Shekemu, katika kutano mkuu. wakashindwa kutimiza wajibu wao, na kwa yo mvuto wao ukawa hafifu mbele ya mkutano mkuu. Kule kazia na kuongezea hali ngumu kwa ile iliyokuwapo siku za lemani, kulikuwa kinyume cha mapenzi ya Mungu na oango wake kwa Israeli, na kuliwatatanisha watu katika hali o. Katika jaribio hilo lisilo na busara la mfalme na washauri ake kutumia uwezo wake, mfalme na washauri wake alidhihirisha roho ya kiburi na majivuno kwa ajili ya cheo na amlaka.MwI 65.4

    Bwana hakumruhusu Rehoboamu kufikiliza makusudi yake. Miongoni mwa makabila hayo, kulikuwako na watu walioudhika mno kwa ajili ya mzigo mzito waliotwikwa wakati wa utawala wa Sulemani, na watu hawa sasa hawakuwa na jingine, ila kuiasi nyumba ya Daudi tu. “Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hakuwasikia, hao watu walimjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya! nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Ee, Daudi. Hivyo Israeli wakaenda zao hemani kwao.” Fungu la 16.MwI 66.1

    Uharibifu uliofanywa kwa usemi wa harara wa Rehoboamu, haukuweza kuponyeka. Kwa hiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, yaligawanyika, kabila la Yuda na la Benyamini, yaliyoishi upande wa kusini wa ufalme, yalibakia chini ya Rehoboamu; ambavyo makabila kumi yaliyoishi upande wa kaskazini yalijitenga, yakawa na ufalme wake, nayo yalijulikana kama ufalme wa Israeli, chini ya Yeroboamu. Hivyo basi, unabii wa nabii ukatimia kuhusu kuraruliwa kwa ufalme. “Maana jambo hili lilitoka kwa Bwana.” Fungu la 15.MwI 66.2

    Rehobaomu alipoona kuwa makabila kumi yamejitenga naye, akaondoka kupigana vita. “Adoramu,” mmojawapo wa watu mashuhuri, “aliyekuwa juu ya shokoa,” alijaribu kuwapatanisha. Lakini msuluhishi huyo alitendewa tendo la kumdhihirishia Rehoboamu kuwa hatakiwi. “Nao Israeli wote wakampiga kwa mawe hata akafa.” Akiona kitendo hicho, “Rehoboamu akafanya haraka kupanda katika gari, ili akimbilie Yerusalemu.” Fungu la 18.MwI 66.3

    Huko Yerusalemu, Rehoboamu “akakusanya nyumba yote ya Yuda, pamoja na kabila ya Benyamini, watu wateule mia na themanini elfu, waliokuwa watu wa vita, ili wapigane na nyumba ya Israeli, waurudishe ufalme tena kwa Rehoboamu mwana wa Sulemani. Lakini likaja neno la Mungu kwa Shemaya mtu wa Mungu, kusema, Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, na jamaa yote ya Yuda na Benyamini, na watu waliosalia, ukisema, Bwana asema hivi, Msiende, wala msipigane na ndugu zenu wana wa Israeli; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakalisikiliza neno la Bwana, wakarudi, wakaenda zao, sawa sawa na neno la Bwana.” Mafungu ya 2124.MwI 66.4

    Kwa muda wa miaka mitatu Rehoboamu alijaribu kujifaidia kwa ajili ya matukio ya huzuni yaliyompata; katika jitahada yake, alifanikiwa. “Akajenga miji yenye ngome katika Yuda. Akazifanya imara hizo ngome, akaweka majemadari humo, na akiba ya vyakula, na mafuta, na mvinyo. Akaifanya kuwa na nguvu nyingi mno.” 2 Mamboya Nyakati 11:5, 11, 12. Lakini siri ya kufanikiwa kwa Yuda mwanzoni mwa utawala wa Rehoboamu, hakukutokana na mambo hayo ya kuimarisha ngome. Mafanikio yao yalitokana na kule kumkiri Mungu kuwa ndiyo Mtawala Mkuu Hiyo ndiyo ilikuwa siri ya kufanikiwa kwa Yuda na Benyamini. Watu waliomcha Mungu kutoka upande wa kaskazini, walijiunga nao, hivyo hesabu yao ikaongezeka. Maandiko yanasema, “Na kutoka katika kabila zote za Israeli, wakaandamwa na hao waliojikaza nia kumtafuta Bwana, Mungu wa Israeli, wakaja Yerusalemu, ili wamtolee dhabihu Bwana, Mungu wa baba zao. Hivyo wakaufanya imara kwa miaka mitatu ufalme wa Yuda, na kumtia nguvu Rehoboamu mwana wa Sulemani; kwa maana muda wa miaka mitatu wakaiendea njia ya Daudi na Sulemani.” Mafungu 16, 17.MwI 67.1

    Kwa njia hii Rehoboamu alikuwa na nafasi ya kurekebisha makosa aliyofanya mwanzoni, ikiwa atadumu kuwa hivyo, pia angepata kutawala kwa busara zaidi. Lakini maandiko yanasimulia kuwa, Rehoboamu ambaye amrithi Sulemani katika kutawala, alishindwa kabisa kuandamana na Yehova. Ijapokuwa kwa asili yake alikuwa mkaidi, mwenye kujitosheleza, na mwenye kuambatana na ibada ya sanamu, walakini, kama angemgeukia Mungu kwa moyo wake wote, angeweza kukuza tabia yenye imani na kujiweka upande wa Mungu matakwa yake. Lakini kwa kadiri siku zilivyozidi kupita, ndivyo mfalme alivyozidi kutegemea mali zake na cheo chake, na miji yenye ngome alizoimarisha. Pole pole alizidi kushindwa na hitilafu alizozirithi, mpaka akawa mwabudu sanamu kamili. “Ikiwa ulipothibitika ufalme wa Rehoboamu, naye amepata nguvu, aliacha torati ya Bwana, na Israeli wote pamoja naye.” 2 Mambo ya Nyakati 12:1.MwI 67.2

    Lo, maneno haya, “Na Israeli wote pamoja naye,” ni yenye huzuni mno kupita kiasi! Watu ambao Mungu aliwachagua wawe nuru kwa mataifa yaliyowazunguka, wakageukia mbali kutoka kwa chemchemi ya nguvu zao, wakatafuta njia ya kufanana na mataifa waliopakana nayo. Kama ilivyokuwa kwa Sulemani, ndivyo ilivyokuwa kwa Rehoboamu pia, yaani mvuto wake mwovu ulipoteza watu wengi. Jinsi ilivyokuwa kwa wafalme hao wawili, ndivyo ilivyo hata leo. Mtu ye yote anayejitoa kutenda maovu, mvuto wake hauwezi kuishia kwakeMwI 68.1

    mwenyewe, bali huwapoteza wengine pia. Hakuna mtu anayeishi kwa ajili yake mwenyewe. Hakuna mtu atendaye maovu anayepotea yeye mwenyewe bila kukokota wengine Maisha ya kila mtu huweza kuwa nuru ya kuwamulikia na kuwachargamsha wengine, au huwa giza la kuwaangamiza na kuwakatisna tamaa wengine. Kila mmoia wetu huwaongoza wengine na kuwaelekeza juu kwenye maisha ya furaha na uzima wa milele, au huwaongoza kuelekea chini kwenye huzuni na kifo cha milele. Na ikiwa kwa matendo yetu huwakosesha wengine na kuwashupaza ili watende maovu, sisi pia hushirikiana nao katika maovu hayo.MwI 68.2

    Mungu hakuachilia uasi wa mfalme wa Yuda upite bila kuadhibiwa. Ikawa katika mwaka wa tano wa mfalme Rehoboamu, akapanda Shishaki, mfalme wa Misri, juu ya Yerusalemu; kwa kuwa walikuwa wamemwasi Bwana; mwenye magari elfu moja na mia mbili, na wapanda farasi sitini elfu; na watu wasiohesabika, waliotoka Misri pamoja naye. . . Akaitwaa miji yenye maboma iliyokuwa ya Yuda, akaja Yerusalemu.MwI 68.3

    Ndipo akaja Shemaya nabii kwa Rehoboamu, na kwa wakuu wa Yuda, waliokusanyika Yerusalemu kwa sababu ya Shishaki, akawaambia, Bwana asema hivi, Ninyi mmeniacha mimi, kwa hiyo nami nimewaacha ninyi mkononi mwa Shishaki.” Mafungu 2 - 5.MwI 68.4

    Watu walikuwa hawajazama kabisa katika maovu kiasi cha kukaidi hukumu za Mungu. Katika hasara waliyopata kwa kuvamiwa na Shishaki, walitambua ya kuwa huo ni mkono wa Mungu, kwa hiyo, kwa muda fulani walijinyenyekeza chini ya Mungu, na kukiri kuwa, Bwana ndiyo mwenye haki.”MwI 68.5

    Naye Bwana alipoona ya kwamba wamejinyenyekeza, neno la Bwana likamjia Shemaya, kusema, Wamejinyenyekeza; sitawaharibu; lakini nitwapa wokovu punde, wala ghadhabu yangu haitamwagika juu ya Yerusalemu kwa mkono wa Shishaki. Walakini watamtumikia; ili wapate kujua utumwa wangu, na huo utumwa wa falme za nchi.MwI 68.6

    Basi Shishaki, mfalme wa Misri, akapanda juu ya Yerusalemu, akazichukua hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao za dhahabu alizozifanya Sulemani. Mfalme Rehoboamu akafanya ngao za shaba mahali pake, akawakabidhi wakuu wa walinzi, waliongoja mlangoni pa nyumba ya mfalme. . . Naye alipojinyenyekeza, ghadhabu ya Bwana ikamgeukia mbali, asimharibu kabisa; tena, yalionekana katika Yuda mambo mema.” Mafungu 6 - 12.MwI 69.1

    Lakini mkono wa uharibifu ulipoondolewa kwao, na taifa likaanza kustawi tena, wengi walizisahau hofu zao, wakageuka kuabudu sanamu na udhalimu mwingi. Miongoni mwa watu waliosahau, alikuwamo Reheboamu pia. Ingawa aliji- nyenyekeza kwa ajili ya hatari iliyomjia, alishindwa kubadili maisha yake kwa hayo. Akisahau fundisho hilo ambalo Mungu alikuwa akimfundisha, aliyarudia maovu yake, wala hakuacha nayo; hali maovu hayo ndiyo yaliyosababisha shambulio la Shishaki juu ya taifa la Yuda. Baada ya miaka michache ya wasiwasi, ambayo Mfalme “alitenda maovu, kwa kuwa hakuukaza moyo wake amtafute Bwana, Reheboamu akalala na babaze, akazikwa katika mji wa Daudi, na Abiya mwanawe alitawala mahali pake.” Mafungu 14, 16.MwI 69.2

    Ufalme uliporaruliwa mwanzo wa kutawala kwa Rehoboamu, utukufu wa Israeli ulianza kuondoka, na wala hautarudi, kama ulivyokuwa kwanza. Wakati fulani katika karni zilizofuata, kiti cha enzi cha Daudi kilikaliwa na watu wanyofu, waliokuwa wakifuata hukumu ya haki, chini ya utawala wa watu hawa, baraka nyingi ziliwakalia watu wa Yuda, hata zikawafikia mataifa yaliyowazunguka. Pengine jina la Mungu lilitukuzwa juu ya miungu yote, na sheria yake iliheshimiwa. Mara kwa mara manabii waliondokea waliowatia nguvu wafalme pamoja na raia ili waendelee kuwa waaminifu. Lakini mbegu za uovu, ambazo zilikuwa zimeota wakati wa kutawazwa kwa Rehoboamu, zilidumu kuendelea, wala hazikung'olewa zote kabisa; na pengine watu waliochaguliwa na Mungu, walizama maovuni kabisa, wakawa mithali kwa mataifa ya kishenzi.MwI 69.3

    Waiakini, ingawa watu walikuwa wakaidi sana wenye kupendelea ibada ya sanamu, Mungu, kwa rehema zake, alifanya awezavyo ili kuuokoa ufalme huo uliogawanyika usiangamie kabisa. Kadiri miaka ilivyopita, ndivyo na makusudi yake yalivyodharauliwa na watu wake Israeli, maana walikuwa wakiongozwa na nguvu ya Kishetani; walakini hata hivyo, alitimiza mapenzi yake kwao kwa njia ya kuchukuliwa mateka na kurudishwa tena, maana ni taifa lake teule.MwI 69.4

    Kuraruliwa kwa ufalme kulikuwa mwanzo tu wa historia ya ajabu, ambayo huonyesha uvumilivu na rehema za Mungu. Kwa njia ya kupitia katika tanuru ya mateso ambayo ilisababishwa na hali yao ovu waliyorithi kwa vizazi vilivyopita, wale watakaotakaswa na Mungu ili wawe watu wake kweli wenye juhudi katika matendo mema, mwishowe watakiri na kusema: “Hapana hata mmoja aliye kama wewe, Ee Bwana; wewe ndiwe uliye mkuu, na jina lako ni kuu katika uweza. Ni nani asiyekucha wewe, Ee mfalme wa mataifa? . . . Miongoni mwa wenye hekima wote wa mataifa, na katika hali yao ya enzi yote pia, hapana hata mmoja kama wewe.” “Bwana ndiye Mungu wa kweli, ndiye Mungu aliye hai Mfalme wa milele.” Yeremia 10:6, 7, 10.MwI 70.1

    Mwishowe, wenye kuabudu sanamu walielewa kuwa, rniungu ya uongo haina uwezo wo wote wa kusaidia na kuokoa. “Miungu hiyo isiyofanya mbingu na nchi, hiyo itaangamia katika nchi nayo itatoweka chini ya mbingu.” Fungu la 11. Ni katika Mungu aliye hai, Mwumbaji wa vitu vyote, na Mtawala wa vitu vyote, kwake tu, ndipo mwanadamu anaweza kupata pumziko na amani.MwI 70.2

    Mwishowe, Waisraeli na Yuda, ambao wamerudiwa na kutubu walifanya upya agano lao na Mungu, Yehova wa majeshi, Mungu wa baba zao, kwake huyo walitoa sifa wakisema:MwI 70.3

    Ameiumba dunia kwa uweza wake,
    Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake,
    Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.
    Atoapo sauti yake, pana msindo wa maji mbinguni,
    Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi;
    Huifanyia mvua umeme,
    Huutoa upepo katika hazina zake.
    Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa; Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu
    yake ya kuchonga,
    Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo,
    Wala haina pumzi ndani yake.
    Ni ubatili tu, ni kazi ya udanganyifu;
    Wakati wa kujiIiwa kwao watapotea.
    Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa;
    Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote;
    Na Israeli ni kabila ya urithi wake;
    Bwana wa majeshi ndilo jina lake.”
    MwI 70.4

    Mafungu 12-16.MwI 71.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents