Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    17—Mwito Wa Elisha

    Mungu alikuwa amemwagiza Eliya amtie mafuta nabii mwingine badala yake. “Na Elisha mwana wa Shafati . . . mtie mafuta awe nabii mahali pako.” (1 Wafalme 19:16), hayo ni maneno Mungu aliyomwagiza Eliya, kwa hiyo, kwa kuyatii maneno hayo, Eliya alimtafuta Elisha. Eliya alipokuwa akisafiri kuelekea upande wa kaskazini, lo, nchi ilikuwa imekauka kiasi gani! Nchi ya neema imegeuka kuwa kama jangwa kwa ajili ya ukame wa kutokunyesha kwa mvua muda wa miaka mitatu na nusu. Sasa mimea ilikuwa ikiota ili kufidia ukame na njaa vilivyopita.MwI 179.1

    Baba yake Elisha alikuwa mkulima mwenye mapato, ambaye wakati wa uasi mkuu, yeye na nyumba yake hawakumpigia magoti Baali. Katika mji wake, ndimo jina la Mungu lilikuwa linaheshimiwa, na imani ya wazee wa Kiisraeli ilikuwamo. Katika mazingara ya namna hiyo ndimo Elisha alilelewa. Alikulia katika hali tulivu ya shambani, mahali alipopokea mafundisho ya maana, katika hali ya adabu kwa wazazi wake, na kazi ya kilimo, ambavyo vilimfanya astahili kupata madaraka makuu ya baadaye.MwI 179.2

    Mwito uliomjia Elisha ili awe nabii, ulimkuta akilima pamoja na watumishi wa baba yake. Alikuwa akifanya kazi iliyoonekana kuwa karibu naye. Alikuwa na kipawa cha kuwaongoza wengine pamoja na kuwa na hali ya adabu na unyenyekevu, tayari kutumika kwa kila hali. Pamoja na hali hiyo, alikuwa na bidii na juhudi. Alikuwa mwaminifu, mwenye kumcha Mungu. Kwa vile alivyokuwa akifanya kazi yake kila siku kwa uaminifu na bidii, alizidi kupata maarifa na neema ya Mungu. Kwa vile alivyojifunza kushirikiana na baba yake katika shughuli za kila siku, ndivyo aliweza kushirikiana na Mungu pia. Kule kuwa mwaminifu katika vitu vidogo, kulimfanya Elisha afae kukabidhiwa mambo makubwa. Alivyojizoeza kufanya mambo yake kila siku kwa uaminifu, ndivyo alivyostahili kufanya kazi kuu pia. Alijizoeza kufanya kazi zo zote, na kwa hiyo alipata ujuzi wa kuongoza wengine na kuwafundisha. Mambo hayo ya Elisha, yanatufundisha sisi sote. Hakuna mtu ajuaye kuwa mambo Mungu anayomtendea yana makusudi gani; lakini wote lazima wafahamu kuwa uaminifu katika mambo madogo, huongoza kwenye mambo makuu. Kila tendo mtu atendalo hudhihirisha tabia yake ilivyo. Na mtu ambaye huonyesha uaminifu katika mambo madogo, akijitahidi kujionyesha kuwa “mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari,” (2 Tim. 2:15), Mungu atamtukuza kwa kumpa madaraka makuu.MwI 180.1

    Mtu asiyejali shughuli ndogo ndogo hafai kupewa shughuli kubwa. Huenda akajidhania mwenyewe kuwa anafaa; lakini Mungu anayeangalia mpaka ndani huona kuwa hafai. Baada ya kumjaribu-jaribu na kumpima-pima, huandikiwa sentensi hii: “Umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.” Kutofaa kwake humdhuru mwenyewe. Hushindwa kupokea neema, uwezo, na ubora wa tabia ambavyo hupatikana kwa njia ya kujitoa wakfu kabisa-kabisa.MwI 180.2

    Watu wengi hujiona kuwa hawafai eti kwa sababu hawana kazi maalum kanisani, kwamba hawana kazi inayoonekana wazi ya kuendesha injili. Kama wangepata jambo fulani kuu wangelipokea kwa furaha jinsi gani! Lakini sasa kwa kuwa wanafanya kazi ndogo ndogo, huzidharau, na kuona kuwa hawana la kufanya. Hayo ni makosa, mtu anaweza kuhesabiwa na Mungu kuwa mtenda kazi wake mwenye juhudi, naye kumbe hufanya mambo madogo madogo ya kila siku tu; kama vile kufanya. Hayo ni makosa. Mtu anaweza kuhesabiwa na Mungu kuwa mtenda kazi wake mwenye juhudi, naye kumbe hufanya mambo madogo madogo ya kila siku tu; kama vile kufyeka miti, kusafisha kiwanja, au kulima. Mama anayewalea watoto wake na kuwafundisha ukweli, Mungu humhesabu kuwa mhubiri mkuu kama vile mchungaji anavyohubiri mimbarani.MwI 180.3

    Watu wengi hutamani madaraka makuu ili watende mambo makuu, wakati ule ule hawazijali shughuli ndogo ndogo zilizo karibu yao, ambazo wakizitenda zitayafanya maisha kuwa matamu. Watu kama hao, hebu kwanza watimize wajibu wa kutenda shughuli ndogo zilizo mbele ya macho yao. Kufaulu siko kupata madaraka makubwa, bali hutokana na juhudi na moyo wa hiari. Sivo kazi va madaraka makuu inavotuwezesha kuwa watenda kazi wa kweli, ambao kazi zao hukubalika mbele za Mungu, bali ni utendaji wa kazi yo yote kwa moyo, roho inayotosheka na kile mtu anachotenda, roho ya kutojipenda, ila kuwafikiria wengine. Katika shughuli ndogo ndogo kuna ubora wa kweli. Kazi ndogo za kila siku zikitendwa kwa uaminifu na kwa moyo wa upendo hupendeza mno mbele za Mungu.MwI 182.1

    Eliya kama alivyoamuriwa na Mungu kumtafuta atakayekuwa badala yake, alipitia katika shamba Elisha alilokuwa akilima. Alimtupia vazi lake. Wakati wa ukame na njaa watu wa jamaa ya Shafati walifahamu kazi ya Eliya. Sasa kitendo cha nabii Eliya kiligusa moyo wa Elisha, na Roho wa Mungu alimwamsha. Alifahamu wazi kuwa Mungu anamwita awe badala ya Eliya.MwI 182.2

    “Akawaacha ng'ombe, akamfuata Eliya mbio, akasema, Nipe ruhusa, nakuomba, nimbusu baba yangu na mama yangu, kisha mimi nitakufuata.” Eliya akamjibu, “Enenda urudi; ni nini niliyokutendea?” Huo haukuwa msukumo tu, bali ni jaribio la imani. Lazima Elisha ahesabu gharama, kwamba ataukubali mwito huo au la. Kama nia yake inafungamana na mji wao na mafanikio yake, basi atakaa kwao tu. Lakini Elisha alifahamu maana ya mwito. Alijua kuwa huu ni mwito wa Mungu, kwa hiyo hakusita kuutii. Hakuacha faida yo yote ya ulimwengu, wakati akiitii sauti ya Mungu na kushirikiana na mtumishi wake. Akatwa lile jozi la ng'ombe, akawachinja, akatokosa nyama zao kwa ile miti ya ng'ombe, akawapa watu wakala. Kisha akainuka akamfuata Eliya, akamhudumia.” 1 Wafalme 19:20, 21. Bila kusitasita aliondoka, akatoka kwao, akafuatana na nabii Eliya asiyekuwa na makao makuu.MwI 182.3

    Kama Elisha angalimwuliza Eliya mambo yahusuyo kazi yake na matokeo yake, Eliya angalimjibu hivi: “Mungu ajua, atakujulisha. Kama ukimtegemea na kumngoja, yeye atajibu maswali yako yote. Ukiamini kwamba Mungu amekuita, njoo tufuatane tu. Elewa kwamba Mungu ananena kupitia kwangu. Ukiacha vyote ukivihesabu kuwa hasara, ili umpate Mungu, basi njoo.”MwI 183.1

    Mwito uliomjia Elisha ulifanana na jawabu Kristo alilompa yule Kijana aliyemjia na swali, kwamba: “Nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele?” Kristo alimjibu, akasema, “Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.” Mathayo 19:16, 21.MwI 183.2

    Elisha aliukubali mwito bila kufikiria maisha ya anasa aliyo- kuwa nayo. Lakini yule kijana alipoyasikia maneno ya Mwokozi, “Akaenda zake kwa huzuni, kwa sababu alikuwa na mali nyingi.” Fungu 22. Hakupenda kujitolea. Alipenda mali zake zaidi kuliko alivyompenda Mungu. Alipokataa kuacha vyote kwa ajili ya Kristo, alijionyesha jinsi asivyofaa kuwa katika kazi ya Bwana.MwI 183.3

    Mwito wa kuacha vyote na kuvitoa juu ya madhabahu unamjia kila mtu. Hatuitwi sisi sote kuuza vitu tulivyo navyo; lakini Mungu hututaka tutangulize kazi yake mbele. Siku isipite bila kutenda jambo fulani la kuutangaza ufalme wake. Mungu hatazamii watu wote wafanye kazi ya namna moja. Mmoja anaweza kutumwa katika nchi za mbali; mwingine anaweza kuulizwa atoe mali zake zifanye kazi ya Mungu. Mungu anatazamia kila mtu afanye kitu fulani. Tunapojitoa sisi na mali zetu wakfu, huwa tumetimiza yote. Watu wenye kujitoa namna hii watautii mwito wa mbinguni.MwI 183.4

    Kila mtu aliyeshiriki neema yake, Bwana amempangia kazi ya kufanya, yaani kuwashughulikia wengine. Kila mmoja wetu lazima tusimame msitarini, na kusema, “Mimi hapa, nitume mimi.” Kila mtu anao wajibu katika kazi ya Mungu, kwamba yeye ni mchungaji, au kwamba ni tabibu, au mfanya biashara, au mkulima; mtu mtaalam aliyeajiriwa kazi, au fundi afanyaye kazi zake mwenyewe. Kila mmoja anao wajibu katika kazi yake atawadhihirishia wengine injili ihusuyo wokovu wao. Kazi yo yote mtu afanyayo lazima iwe ndiyo njia ya kukamilisha kusudi hili.MwI 183.5

    Elisha alipoitwa mara ya kwanza hakupewa kazi kubwa ya ajabu. Kazi ndogo za kawaida ndizo zilimwinua. Kwake inasemwa kwamba alikuwa akimnawisha Eliya mikono. Yeye alikuwa tayari, kwa hiari ya moyo kutenda kazi yo yote aliyopewa na Bwana. Katika kila hatua alionyesha unyenyekevu na utumishi. Alipokuwa akimhudumia nabii alijionyesha kuwa mwaminifu katika vitu vidogo; ambavyo vilimfanya kuinuka na kufanya kazi kubwa aliyopewa na Mungu.MwI 184.1

    Maisha ya Elisha alipokuwa na Eliya yalijaa majaribu, lakini katika kila jambo alimtegemea Mungu. Alijaribiwa kufikiri juu ya mji wa kwao alikotoka, lakini hakushindwa. Alipokwisha kutia mkono wake kwenye jembe, hakuangalia nyuma tena.MwI 184.2

    Kazi ya huduma takatifu si kuhubiri neno tu. Maana yake ni kuwafundisha vijana, kama vile Eliya alivyomfundisha Elisha, kuwazoeza katika kazi ya Mungu, baada ya kuwatoa katika shughuli zao za kawaida. Kwanza kuwapa madaraka madogo, na kuwapa madaraka makubwa kadiri wanavyoendelea. Katika kazi hii ya injili wako watu wenye imani na wenye maombi, watu wawezao kusema; “Lile lililokuwako tangu mwanzo, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya neno la uzima. . . hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi.” 1 Yohana 1:1-3. Vijana, ambao wanaingia kazini, lazima wazoezwe namna ya kufanya kazi na wazee ambao ni watumishi wa Mungu. Na kwa njia hiyo watafahamu namna ya kubeba mizigo.MwI 184.3

    Wale wanaofanya kazi hii ya kuwafundisha Vijana, wanafanya kazi bora sana. Bwana mwenyewe hushirikiana nao katika kazi hiyo. Vijana ambao wamebahatisha kuongozwa na wazee hawa wenye imani, ambao ni watumishi wa Mungu, lazima wajitahidi kuchuma kwao maarifa kadiri iwezekanavyo. Mungu amewaheshimu kwa kuwaingiza katika kazi yake, na kwa kuwaunganisha na wazee hao, ambao wanaweza kuwasaidia mpaka wafae kabisa kuwa wenye unyenyekevu, uaminifu, utii na hiari ya kuhudumia wengine. Kama wakikubali kujitia chini ya malezi ya Mungu, wakifuata maagizo yake, na kuambatana na watumishi wa Mungu ambao ni wazee kuwa washauri wao, watakuza hali ya haki na kanuni bora na uthabiti katika maisha yao, hata Mungu atawakabidhi madaraka makuu.MwI 184.4

    Kadiri injili itakavyohubiriwa katika utakatifu wake ulimwenguni, ndivyo watu watakavyoitwa kuacha kazi zao za kawaida, za kilimo, na biashara na shughuli zo zote, nao wataelimishwa na wazee wenye ujuzi juu ya kazi ya Mungu, ili wapate kutenda kazi ya injili. Kadiri watakavyojizoeza kutenda kazi vema, ndivyo watakavyokuwa wahubiri wa injili walio hodari. Kwa njia ya uwezo wa Mungu watatenda makuu ujumbe unaohitajiwa mno na wakaaji wa duniani utatangazwa na kufahamika. Watu wataelewa ukweli jinsi ulivyo. Kazi hii itaendelea zaidi na zaidi mpaka dunia yote itaonywa, kisha, ndipo ule mwisho utakuja.MwI 185.1

    Baada ya kuitwa kwa Elisha, waliendelea kufanya kazi na Eliya kwa miaka kadhaa, Kijana Elisha akijifunza na kujitayarisha kwa kazi yake ya usoni. Eliya amekuwa chombo cha Mungu cha kupinga uovu mkuu mno. Ibada ya sanamu iliyoendeshwa na Yezebeli mshenzi, na kuungwa mkono na Ahabu, ambayo ilipotosha taifa zima, ilikuwa imepata pigo la kutosha. Manabii wa Baali walikuwa wamechinjwa. Taifa zima la Israeli lilitiwa msukosuko, na watu wengi walimrudia Mungu. Hivyo basi Elisha ataendeleza kazi hiyo ya kuwadumisha watu katika njia ya Mungu, kama mtangulizi wake Eliya alivyofanya. Kule kushirikiana na Eliya, ambaye ni nabii mkuu tangu siku za Musa, Elisha alitayarishwa kwa kazi kuu atakayofanya mwenyewe.MwI 185.2

    Wakati wa miaka hiyo ya kazi ya shirika, kila mara Eliya aliitwa huko na huko ili akakemee maovu fulani yaliyotokea. Wakati Ahabu mwovu alipolitwaa konde la Nabothi, Eliya ndiye alitabiri juu ya ajali yake na ya nyumba yake yote. Na wakati Ahazia, baada ya kufa kwa baba yake, alipomwacha Mungu na kugeukia Baalzebub, mungu wa Ekroni sauti ya Eliya ndiyo iliyosikika ikimkemea.MwI 185.3

    Shule za manabii zilizojengwa na Samweli, zilikuwa zimeharibika kabisa wakati wa uasi mkuu wa wana wa Israeli. Eliya ndiye aliyezisimamisha tena, ili Vijana wapate kufundishwa elimu halisi inayotukuza sheria ya Mungu. Zimetajwa shule tatu: moja ikiwa Gilgali, nyingine Betheli na nyingine Yeriko. Kabla Eliya hajachukuliwa kwenda mbinguni, yeye pamoja na Elisha walizitembelea shule hizi. Mafundisho yaliyotolewa humo hapo zamani, sasa yanarudiwa. Hasa mkazo ulitiwa kuhusu kuambatana kwao na Mungu wa mbinguni. Mkazo pia ulitiliwa juu ya umuhimu wa kuwa na elimu ya kuongoza maisha katika hali ya kawaida yenye kuridhika. Kwa njia hiyo tu ndipo itafanya mibaraka ya mbinguni iwakalie na kuifanikisha kazi yao.MwI 187.1

    Eliya alifarijika sana alipoona matokeo ya shule hizo. Matengenezo kamili ya dini yalikuwa bado kukamilika, lakini po pote nchini palionekana utimizo wa neno la Mungu, kwamba: “Nimejisazia katika Israeli watu elfu saba, kila goti lisilomwinamia Baali.” 1 Wafalme 19:18.MwI 187.2

    Kadiri Elisha alivyofuatana na Eliya katika kazi, toka shule hii hata shule ile, ndivyo imani yake na nia yake ilijaribiwa tena. Huko Gilgali, Betheli na Yeriko Elisha aliambiwa arudi iwapo anaona kuwa hawezi kuvumilia. Eliya alimwambia, “Tafadhali, kaa hapa, maana Bwana amenituma niende mpaka Betheli.” Elisha alikuwa amejifunza kutokukata tamaa, wakati alipokuwa akilima, na kushughulika na kazi za kawaida. Na sasa ametia mkono wake katika kazi ya Mungu, hawezi kugeuzwa aliache kusudi lake. Hakubali kuachana na Bwana wake Eliya iwapo muda wa kujifunza maarifa kwake ungalipo. Mpango wa kuchukuliwa kwa Eliya kwenda mbinguni, bila kujulikana kwake mwenyewe, ulifunuliwa kwa wana wa manabii waliokuwa katika shule hizo, na kwa Elisha. Kwa hiyo mtumishi wa Mungu mwenye wasiwasi aliandamana na Bwana wake Eliya. Kila mara alipoambiwa kubaki pale, jawabu lake lilikuwa lile lile: “Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha.”MwI 187.3

    “Wakaendelea mbele wote wawili . . .na hao wawili wakasimama karibu na Yordani. Eliya akalitwaa vazi lake la juu, akalikunja, akayapiga maji, yakagawanyika huku na huku, na hao wawili wakavuka pakavu. Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, “Omba kwangu lo lote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa kwako.”MwI 187.4

    Elisha hakuomba heshima ya dunia hii, au ukuu na cheo kati ya watu. Kitu alichotamani ni roho ile Mungu aliyompa mtumishi wake anayetaka kuchukuliwa. Elisha alijua kuwa, pasipokuwa na roho kama ile iliyokuwa ndani ya Eliya, hawezi kutenda kitu cho chote, kwa Waisraeli ambako Mungu amemweka awashughulikie. Kwa hiyo aliomba: “Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu.”MwI 188.1

    Eliya alimjibu kwa ombi hilo kwa kusema: “Umeomba neno gumu; lakini, ukiniona nitakapoondolewa kwako, utalipata; la, hukuniona, hulipati. Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli.” 2 Wafalme 2:1-11.MwI 188.2

    Eliya alikuwa aina ya watakatifu watakaokuwa wakiishi duniani, wakati wa kurudi kwake Bwana Yesu, ambao “Watabadilika kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho,” bila kuonja mauti. 1 Wakorintho 15:51, 52. Karibu na huduma ya Yesu duniani kukoma, Eliya na Musa walikutana na Mwokozi katika mlima, Eliya akiwawakilisha wale watakaohamishwa bila kuonja mauti. Katika mfano huo, wale wanafunzi waliona kwa sehemu namna ufalme wa watakaokombolewa utakavyokuwa. Walimwangalia Yesu akiwa na utukufu wa mbinguni; walisikia “sauti ikitokea katika wingu ikisema, huyu ni mwanangu” (Luka 9:35); walimwona Musa, anayewawakilisha wale watakaofufuliwa wakati wa kurudi kwake Kristo; waliona Eliya akisimama, mjumbe wa watakaochukuliwa bila kufa.MwI 188.3

    Kule jangwani, Eliya alipokuwa peke yake katika hali ya kukata tamaa, aliomba apate kujifia. Lakini Bwana Mungu, kwa fadhili zake hakutenda kama Eliya alivyomba. Eliya alikuwa angali na kazi kubwa ya kufanya; na kazi hiyo ikikamilika, hangekufa na kuoza duniani. Bali atapandishwa katika utukufu, akaishi huko mbinguni.MwI 188.4

    “Naye Elisha akaona, akalia, Baba yangu, baba yangu, gari la Israeli na wapanda farasi wake! Asimwone tena kabisa; akashika mavazi yake mwenyewe, akayararua vipande viwili. Kisha akaliokota lile vazi la Eliya lililomwangukia, akarudi, akasimama katika ukingo wa Yordani. Akalitwaa lile vazi la Eliya lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, yuko wapi Bwana, Mungu wa Eliya? Naye alipoyapiga maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka. Na hao wana wa manabii, waliokuwako Yeriko wakimkabili walipomwona, walisema, roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha. Wakaja kuonana naye, wakainama kifudifudi mbele yake.” 2 Wafalme 2:12-15.MwI 188.5

    Bwana, kwa hekima yake, akiona vema kuwapumzisha watenda kazi wake katika kazi, huwapa hekima wale wanaowafuata na kuchukua madaraka badala yao, ikiwa watamtafuta na kutegemea uongozi wake. Wanaweza kuwa wenye busara hata kuliko waliowatangulia, maana watakuwa wamejifunza kutokana na makosa yaliyofanyika nyuma. Hivyo Elisha alikuwa badala ya Eliya. Aliyekuwa mwaminifu kwa madogo, amekabidhiwa makubwa.MwI 189.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents