Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    5—Toba Ya Sulemani

    Bwana alimtokea Sulemani mara mbili wakati wa utawala wake, akimhakikishia ukubali wake, na kumshauri adumu kuwa mnyenyekevu na mtiifu. Mara ya kwanza ni huko Gibeoni katika njozi ya usiku, wakati alipoahidiwa kupewa hekima, utajiri na heshima; mara ya pili ni pale wakati wa kuzinduliwa kwa hekalu, ambapo tena Bwana alimwonya asisahau kuwa mwaminifu. Sulemani alipewa maonyo dhahiri na kupewa ahadi za ajabu; walakini, yeye ambaye alionekana kufaa kabisa kuyatii maonyo na kufikiliza kusudi la mbinguni, kwake huyo imeandikwa: “Lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana.”MwI 53.1

    “Moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine.” 1 Wafalme 11:9, 10. Basi akaasi kabisa, moyo wake ukazama katika uasi, hata ikaonekana wazi kuwa kwake hakuna tumaini lo lote tena.MwI 53.2

    Sulemani akageuka kabisa kutoka katika furaha ya kushirikiana na Mungu, akawa radhi kutumikia anasa za mwili. Katika mambo hayo, alisema:MwI 53.3

    “Nikajifanyizia kazi zilizo kubwa; nikajijengea nyumba; nikajipandia mashamba ya mizabibu, nikajifanyizia bustani na viunga. . . . Nikanunua watumwa na wajakazi. . . .MwI 54.1

    Nikajikusanyia fedha na dhahabu, na tunu za kifalme na za kutoka katika majimbo. Nikajipatia waimbaji, waume kwa wake, nao wale ambao wanadamu wanawatunuka, masuria wengi sana. Basi nikawa mkuu, nikaongezeka kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu. . . .MwI 54.2

    Wala sikuyanyima macho yangu cho chote yalichokitamani, wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote, maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote. . . . Kisha nikaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu, na taabu yote niliyotaabika katika kuzitenda; na tazama, yote ni ubatili na kujilisha upepo, wala faida hakuna chini ya jua.MwI 54.3

    “Nikageuka ili kuipambanua hekima, na wazimu, na upumbavu. Kwa maana mtu amfuataye mfalme nini? Lilo hilo tu lililokwisha kufanywa. . . Basi, nikachukia uhai. . . . Nami nikaichukia kazi yangu yote niIiyojishughuIisha nayo chini ya jua.” Mhubiri 2:4-18.MwI 54.4

    Sulemani alijifunza kutokana na maisha yake machungu kwamba, maisha ni ubatili mtupu, hasa ikiwa mtu hutafuta anasa na mema ya duniani tu. Alijengea miungu mahekalu, lakini hakuona faraja yo yote, wala utulivu wa moyo. Yote yalikuwa kazi bure. Wasiwasi na mahangaiko ya moyo vilim- sumbua mchana na usiku. Kwake furaha ya maisha ilitoweka kabisa, wala hakuwa na utulivu moyoni; alipofikiri mambo ya usoni yalimtia giza na mashaka ya kukatisha tamaa.MwI 54.5

    Hata hivyo Bwana hakumtupa. Kwa njia ya ujumbe wa maonyo makali pamoja na adhabu kali, Bwana alitaka kum- wamsha mfalme aone uovu wa njia zake. Alimwondolea ulinzi wake, akawaruhusu maadui wamshambulie na kumdhoofishia ufalme wake. “Ndipo Bwana akamwondokeshea Sulemani adui, Hadadi Mwedomi; . . . Tena Bwana akamwondokeshea adui mwingine, Rezoni, . . . akawa mkuu wa jeshi, . . . na kumiliki huko Dameski. . . Akawa adui wa Israeli. . . . Na Yeroboamu, . . mtumwa wake Sulemani . . . mtu hodari . . . akainua mkono wake juu ya mfalme.” 1 Wafalme 11:14-28.MwI 54.6

    Mwisho Bwana akampelekea Sulemani ujumbe wa kutisha kwa kinywa cha nabii, akisema, “Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako. Walakini katika siku zako sitafanya haya, kwa ajili ya Daudi baba yako; nitaurarua utoke katika mkono wa mwana wako.” Mafungu 11, 12.MwI 56.1

    Akiamshwa kama mtu aliyestushwa katika ndoto, Sulemani alianza kuona wazi kwa upya njia zake za kipumbavu. Akiwa amerudiwa katika roho, mwenye nia iliyotulia na mwili uliodhoofika, alijuta, akageuka kutoka katika kunywa takataka za udongo, akaanza tena kunywa katika chemchemi ya uzima, akiwa mwenye kiu ya haki kweli kweli. Kwake mateso yamemwadibisha. Alikuwa amehangaika na kuwa na wasiwasi muda mrefu, maana alishindwa kuondoka katika upumbavu wake; lakini sasa katika ujumbe aliopewa ameona kuwa kuna tumaini ndani yake. Mungu hakumtupa kabisa, lakini alikuwa tayari kumwokoa kutoka katika utumwa mbaya zaidi ya kaburi. Utumwa ambao hakuweza kujiongoa ndani yake yeye mwenyewe.MwI 56.2

    Sulemani alishukuru mno na kukubali kuongozwa na uwezo na wema wake aliye “juu kuliko walio juu” (Mhubiri 5:8), na kwa moyo wenye majuto na toba, akaanza kupiga hatua kuelekea mahali pa utakatifu na usafi, ambako alianguka mbali nao. Asingaliweza kuwa na utulivu wa dhamiri asiyakumbuke mambo aliyoyatenda; lakini angejitahidi kuwashawishi wengine wasifuate njia hiyo ya kipumbavu. Angejidhili na kuungama makosa yake, halafu atoe maonyo kwa watu wengine wasije wakaingia katika hali ya upotevu mkuu kwa sababu ya mvuto mbaya aliouweka.MwI 56.3

    Toba ya kweli haimsahaulishi mtu makosa yake ya zamani. Baada ya kusamehewa dhambi zake na kuwa na utulivu wa moyo, hawezi kusahau habari ya dhambi zake alizofanya zamani. Huwafikiria watu aliowakosesha, na hujaribu kwa njia zo zote kuwashawishi, ili warudi katika njia ya kweli. Kadiri anavyopata nuru ya wazi juu ya hali yake, ndivyo atakavyojitahidi kuwasimamisha wengine katika njia ya kweli. Hawezi kufunikafunika makosa yake na kuyafanya kuwa ni kitu kidogo, lakini atayadhihirisha wazi yawe onyo la hatari kwa watu wengine, wasije wakatumbukia ndani yake.MwI 56.4

    Sulemani alikiri kwamba, “Mioyo ya wanadamu imejaa maovu, na wazimu umo mioyoni mwao.” Mhubiri 9:3.MwI 57.1

    Kisha tena alisema, “Kwa sababu hukumu juu ya tendo baya haitekelezwi upesi, mioyo ya wanadamu huthibitishwa ndani yao ili kutenda mabaya. Ajapokuwa mwenye dhambi amefanya maovu mara mia, akazidisha siku zake; lakini hata hivyo najua hakika ya kwamba itakuwa heri kwao wamchao Mungu, wenye kicho mbele zake; walakini haitakuwa heri kwa mwovu, wala hatazidisha siku zake, zilizo kama kivuli; kwa sababu hana kicho mbele za Mungu.” Mhubiri 8:11-13.MwI 57.2

    Kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, mfalme ahandika habari za miaka yake iliyopotezwa katika ufisadi, akitoa maonyo na mafundisho kwa ajili ya vizazi vijavyo. Hivyo, basi, ijapokuwa mbegu ya uovu aliyowapandia watu ilikuwa inatoa matunda yake, lakini yeye mwenyewe na kazi yake yote haikupotea kabisa. Katika miaka yake ya mwisho, Sulemani aliwafundisha watu kwa unyenyekevu wa moyo. Imeandikwa, “Aliendelea kuwafundisha watu maarifa; naam akatafakari, akatafuta- tafuta, akatunga mithali nyingi.” “Akatafuta-tafuta apate kuona maneno yapendezayo, na yale yaliyoandikwa kwa unyofu, yaani, maneno ya kweli.” “Maneno yao wenye hekima huwa mfano wa michokoo; na kama misumari iliyogongomewa sawa; ndivyo yalivyo maneno yao walio wakuu wa makusanyiko, ambayo yatoka kwa mchungaji mmoja. Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo.” Muhubiri 12:9-12.MwI 57.3

    Akaendelea kusema, “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.” Mafungu 13, 14.MwI 57.4

    Maandiko ya Sulemani ya miaka ya baadaye yanadhihirisha kwamba alikuwa ameelewa ubovu wa njia yake zaidi na zaidi, akajitahidi kuwaonya vijana wajihadhari wasije kutumbukia katika makosa yale yale yaliyomkumba yeye hata akatumia karama za mbinguni katika ubatili na ufidhuli. Kwa masikitiko na aibu nyingi, Sulemani aliungama na kukiri kwamba, katika utu uzima wake amepoteza miaka yake bure katika kuabudu sanamu, badala ya kumfanya Mungu kuwa faraja yake, kinga yake na mwenzi wake. Na sasa, baada ya kujifunza katika hali ngumu ya uchungu mwingi, maisha ya kipumbavu aliyoishi, nia yake kuu ilikuwa kuwahadharisha wengine na kuwaokoa wasitumbukie katika ubaradhuli huo, kama yeye alivyoanguka humo.MwI 57.5

    Kwa huruma nyingi akaandika kuhusu bahati na wajibu wa vijana katika kazi ya Mungu: “Kweli nuru ni tamu, tena ni jambo la kupendeza macho kutazama jua. Naam, mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote; lakini na azikumbuke siku zijazo za giza, kwa maana zitakuwa nyingi. Mambo yote yajayo ni ubatili. Wewe, kijana, uufarahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako; lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni. Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini mwako; kwa maana ujana ni ubatili, na utu uzima pia.” Mhubiri 11:7-10.MwI 58.1

    “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako,
    Kabla hazijaja siku zilizo mbaya,
    Wala haijakaribia miaka utakaposema,
    Mimi sina furaha katika hiyo.
    Kabla jua, na nuru, na mwezi,
    Na nyota, havijatiwa giza;
    Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;
    Siku ile walinzi wa nyumba watakapotetema,
    Hapo wenye nguvu watakapojiinamisha;
    Na wasagao kukoma kwa kuwa ni haba;
    Na hao wachunguliao madirishani kutiwa giza;
    Na milango kufungwa katika njia kuu;
    Sauti ya kinu itakapokuwa ni ndogo;
    Na mtu kusituka kwa sauti ya ndege;
    Nao binti za kuimba watapunguzwa;
    Naam, wataogopa kilichoinuka;
    Na vitisho vitakuwapo njiani;
    Na mlozi utachanua maua;
    Na panzi atakuwa ni mzigo mzito; Na pilipili hoho itapasuka;
    Maana mtu aiendea nyumba yake ya milele,
    Nao waombelezao wazunguka njia.
    Kabla haijakatika kamba ya fedha;
    Au kuvunjwa bakuli la dhahabu;
    Au mtungi kuvunjika kisimani;
    Au gurudumu kuvunjika birikani;
    Nayo mavumbi huirudia nchi kama yalivyokuwa,
    Nayo roho humrudia Mungu aliyeitoa.”
    MwI 58.2

    Mhubiri 12:1-7.

    Maisha ya Sulemani yamejaa maonyo tele kwa watu wote, vijana kwa watu wazima, na kwa wazee pia ambao wanashuka mlima wao wa. . . . kuelekea magharibi, huko jua la maisha yao linakochwea. Tunaona na kusikia hali ya msimamo usio thabiti kwa vijana. Vijana hutangatanga kati ya haki na upotovu, hatutazamii kuona hali hiyo ya kuwayawaya. Tunatazamia kuona tabia bora zilizoimarishwa katika haki kwa wingi wa miaka yao. Lakini mara nyingi haiwi hivyo. Badala ya Sulemani kuwa na tabia thabiti, hodari kama mti mgumu, alianguka chini kabisa katika majaribu. Badala ya kuwa hodari, mwenye nguvu, alionekana dhaifu kabisa.MwI 59.1

    Kwa mambo hayo tunaonywa wazi kuwa, usalama wetu, vjjana kwa wazee, ni kukesha katika sala tu. Usalama hautokani na cheo kikubwa na mafanikio makubwa. Mtu anaweza kutunza ukristo wake kwa muda wa miaka mingi, biIa wasiwasi, lakini hata hivyo yumo katikati ya mashambulio ya shetani. Katika vita ya kupigana na dhambi za moyoni na majaribu ya nje, hata Sulemani mwenye hekima nyingi na nguvu nyingi alishindwa. Anguko la Sulemani linatufundisha kwamba, hata kama mtu akiwa hodari na mwenye akili kiasi gani, au hata kama amemtumikia Mungu kwa uaminifu kiasi gani miaka iliyopita, hawezi kutegemea hekima yake na uaminifu wake kwa kuwa salama.MwI 59.2

    Msingi wa kujenga tabia na kielelezo halisi, ni kile kile kwa kila kizazi na kwa kila nchi. Agizo la Mungu, lisemalo, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote. . . ., na jirani yako kama nafsi yako,” ambalo ndilo kanuni kuu iliyodhihirishwa katika maisha ya Mwokozi wetu, ndilo msingi halisi na mwongozo wa kweli. Luka 10:27. “Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa.” Isaya 33:6. Hekima na maarifa hupatikana kwa neno la Mungu tu.MwI 59.3

    Maneno yaliyonenwa kwa Waisraeli kuhusu utii wa sheria za Mungu ni yale yale hata leo: “Maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa.” Kumbukumbu la Torati 4:6. Huu ndio mwongozo wa hakika kwa mtu binafsi, kwa usafi wa unyumba, au kwa ustawi wa taifa. Katikati ya wasiwasi na mahangaiko ya maisha, na hatari zitokanazo nayo, njia moja tu iliyo ya usalama, ambayo ni ya hakika, ni kufanya kama vile Mungu asemavyo. “Maagizo ya Bwana ni ya adili,” tena, “Mtu atendaye mambo hayo hataondoshwa milele.” Zaburi 19:8; 15:5.MwI 60.1

    Watu wanaojali maonyo yatokanayo na uasi wa Sulemani wataepukana na dhambi zile zilizomwangusha Sulemani. Kule kuyatii maagizo ya mbinguni, ndiko tu kutamkinga mtu asianguke dhambini. Mungu amemfunulia mwanadamu nuru kubwa na majaliwa mengi; lakini nuru hii na mibaraka hii isipokubaliwa, haiwezi kumzuia mtu mwasi asianguke. Watu ambao Mungu amewatunukia hadhi ya heshima, kama wakimwacha na kugeukia hekima ya kibinadamu, ile nuru waliyopewa hugeuka kuwa giza, na majaliwa yao hugeuka kuwa mtego unasao.MwI 60.2

    Kutakuwako na watu wanaojitenga na Mungu siku zote mpaka mwisho wa vita kuu kati ya haki na uovu. Shetani atafanya hali ya mambo iwe ya hila mno, hata iwe vigumu kuepukana na kunaswa nayo, kama hatukulindwa na nguvu za Mungu. Tunahitajika kuhoji kwa kila hatua kwamba, “Je, hii ni njia ya Bwana Mungu?” Kadiri maisha yetu yanavyoendelea, ndivyo tunahitaji kuangalia na kukesha, ili kutawala mapenzi yetu na tamaa zetu. Hatuwezi kuwa salama hata kwa dakika moja, tusipomwegemea Mungu hasa hasa, na maisha yetu yafichike ndani ya Kristo. Kukesha katika sala ndiyo salama yetu ya kukaa katika hali ya usafi.MwI 60.3

    Wote watakaoingia mji wa Mungu, wataingia kwa kupitia mlango mwembamba-kwa njia ya shida na juhudi kubwa kwa maana, “Ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge.” Ufunuo 21:27. Lakini watu walioanguka dhambini wasife moyo. Wazee ambao wamekuwa wapendwa wa Mungu kwa miaka, wanaweza kuanguka maovuni na kuchafua roho zao na ukristo wao, kwa kuitupa imani yao na kuandamana na tamaa zao; lakini kama watatubu na kujitenga na maovu, na kumgeukia Mungu kwa kweli, liko tumaini kwao la kupokelewa. Yeye aliyesema, “Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima,” alisema pia, “Mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake; na amrudie Bwana, naye atamrehemu; na arejee kwa Mungu wetu, naye atamsamehe kabisa.” Ufunuo 2:10; Isaya 55:7. Mungu huchukia dhambi, lakini humpenda mwenye dhambi. Asema, “Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo.” Hosea 14:4.MwI 60.4

    Toba ya Sulemani ilikuwa ya kweli; lakini mabaya yaliyoletwa kwa ajili ya mvuto wake, hayawezi kuachwa vivi hivi tu. Wakati yeye alipokuwa ameasi palikuwapo watu katika ufalme wake waliosimama katika kweli. Lakini wengi walipotoka. Maovu mengi yaliyoingia kwa ajili ya kuruhusu ibada ya sanamu na kufuata matendo ya kimataifa, hayakuzuiliwa kwa urahisi na mfalme huyu aliyetubu. Mvuto wake wa kutenda mema ulikuwa umedhoofishwa vikubwa. Wengi walikuwa na mashaka kwa uongozi wake. Ingawa mfalme aliungama dhambi zake, na kuandika maonyo mengi kwa ajili ya vizazi vijavyo kuhusu upumbavu wake, hakuwa na tumaini la kufuta kabisa hali mbaya iliyoletwa na vitendo vyake viovu. Wengi walishupazwa kwa uasi wake kutenda maovu zaidi na zaidi. Na mvuto wake mbaya wa kutumia majaliwa ya Mungu, huenda, ulisababisha maasi ya wafalme wengi waliotawala baada yake.MwI 61.1

    Kwa uchungu wa moyo kwa ajili ya maovu aliyoya- sababisha, Sulemani alitamka na kusema, “Hekima ndiyo bora kupita silaha za vita; lakini mkosaji mmoja huharibu mema mengi.” “Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye; ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana.” “Mainzi mafu huvundisha marhamu ya mwuza marashi; kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima.” Muhubiri 9:18; 10:5, 6, 1.MwI 61.2

    Miongoni mwa mafundisho mengi yaliyofundishwa kwa njia ya maisha ya Sulemani, hakuna IiIilotiliwa mkazo zaidi kuliko lile lihusulo mvuto wa kutenda mema au mabaya. Ingawa hali yetu ni ndogo kiasi gani, walakini inao mvuto kwa wema au kwa uangamivu. Hali hiyo huwafanya watu wawe wema au waovu, ingawa sisi hatukusudii hivyo, huwaletea watu baraka au laana. Hali hiyo inaweza kuwa ya ubaridi, manung'uniko na choyo, au inaweza kuwa ni sumu ya dhambi fulani tunayoshikilia maishani; au inaweza kuwa ni hali iliyojaa imani tele, ujasiri mwingi na matumaini, na upendo safi usio na unafiki. Lakini nguvu yake itavutia kutenda mema au kutenda maovu.MwI 62.1

    Tukifikiri kuwa mvuto wetu unaweza kusababisha uangamivu kwa wengine, tunatishika sana, lakini inawezekana kuwa hivyo. Nani awezaye kukisia hasara ya kumkosesha mtu mmoja uzima wa milele! Waiakini tendo letu moja la harara, neno letu moja lililotamkwa kipumbavu, bila kulifikiri, linaweza kumleteleza mwingine kuangamia. Dosari moja katika tabia zetu inaweza kuwafukuza watu wengi kutoka kwa Kristo.MwI 62.2

    Jinsi mbegu iliyopandwa huzaa, na halafu hupandwa na kuzaa zaidi, hali kadhalika tunapoishi na wenzetu mambo kama hayo hutendeka. Kila tendo tutendalo, na kila neno tusemalo ni mbegu iliyopandwa, ambayo itazaa matunda. Kila tendo jema tutendalo, ambalo ni la utii na kujinyima, litazaa matunda katika maisha ya watu wengine; wao nao watawaambukiza wengine. Hivyo kila tendo la kijicho tutendalo, kila tendo la ukorofi tutendalo, au la fitina, ni mbegu ipandwayo ambayo itaota katika “shina la uchungu”, na kuwaharibu wengi. Waebrania 12:15. Na watu watakaotiwa “uchungu”, ni wengi kadiri gani! Hivyo basi upandaji wa mbegu njema na mbegu ovu unaendelea wakati huu hata katika umilele pia.MwI 62.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents