Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    12—Kutoka Yezreeli Hata Horebu

    Kule kuwaua manabii wa Baali kulifungua milango ya kufanya matengenezo ya kiroho yaliyo makuu, kati ya makabila kumi ya ufalme wa kaskazini Eliya aliwaeleza watu wazi kuhusu uasi wao alikuwa ametoa mwito kwao ili wamrudie Mungu na kujinyenyekeza kwake Adhabu ya mbinguni imetimia; watu wameungama na kukiri maovu yao, na wamemkiri Mungu wa baba zao kuwa Mungu wao; na laana iliyoikalia nchi kwa muda huo wote ilikuwa karibu kuondolewa, ili hali ya kawaida ya kila siku irudishwe. Ilipasa mvua iinyeshee nchi sasa. Kwa hiyo Eliya alimwambia Ahabu, “Haya! inuka, ule, unywe; kwani pana sauti ya mvua tele.’ Kisha nabii alipanda juu ya kilele cha mlima kwenda kuomba.MwI 121.1

    Hapakuwako na alama yo yote ya kuonyesha kuwa mvua itanyesha, ambayo ilimfanya Eliya amhakikishie Ahabu. Nabii Eliya hakuona hata wingu moja mbinguni; wala hakusikia ngurumo. Yeye alinena maneno yale Roho wa Mungu aliyomsukuma kunena, kwa njia ya imani yake. Mchana kutwa alikuwa akifanya mapenzi ya Mungu, na ameonyesha jinsi anavyoamini unabii wa neno la Mungu; na sasa baada ya kufanya yote aliyoweza, alijua kuwa mbingu itamwaga mibaraka yake, kama ilivyotabiriwa Mungu yule yule aliyeleta ukame nchini, ndiye aliyeahidi kuineemesha nchi, kama watu watatubu na kumgeukia yeye. Sasa Eliya akangoja ahadi ya kunyesha mvua. Akiwa katika hali ya unyenyekevu sana, “akasujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini,” akamsihi Mungu kwa ajili ya Waisraeli waliotubu.MwI 121.2

    Alimtuma mtumishi wake kila mara akachungulie upande wa bahari ya Mediterranea akaone kama kuna dalili ya mawingu ili kujibu sala yake Kila mara mtumishi aliporudi alisema, “Hakuna kitu.” Nabii hakukata tamaa au imani yake kufifia, lakini aliendelea na maombi yake. Mara sita mtumishi wake alirudi na kusema kuwa, hakuna hata dalili ya wingu katika mbingu kavu kama shaba. Bila kuwa na wasiwasi, Eliya alimtuma mara moja zaidi Safari hii mtumishi alirudi na neno hili: “Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu.”MwI 122.1

    Hii ilitosha. Eliya hakungoja mpaka mbingu ziwe nyeusi. Katika wingu dogo hilo, kwa imani aliona kuwa mvua ni tele. Akatenda kadiri ya imani, akamtuma mtumishi wake aende kwa Ahabu upesi, ampelekee ujumbe huu: Tandika ushuke, mvuaisikuzuie.”MwI 122.2

    Ni kwa ajili ya imani kuu aliyokuwa nayo Eliya ndiyo ilifanya Mungu akamtumia wakati huu wa kutatanika kwa Waisraeli. Alipokuwa akiomba, imani yake ilizishikilia ahadi za Mungu, naye alidumu katika maombi mpaka akapata majibu. Hakungoja mpaka aone mambo makubwa, yawe ushahidi kuwa amejibiwa na Mungu, lakini alithubutu kutenda kwa imani ijapokuwa kitu alichoona ni kidogo sana. Hata hivyo yale aliyotenda kwa uongozi wa Mungu, watu wote pia wanaweza kuyatenda katika kazi ya Mungu; maana kuhusu Eliya wa milima ya Gileadi, ambaye ni nabii imeandikwa: “Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe; na mvua haikunya juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.” Yakobo 5:17MwI 122.3

    Imani ya namna hii inahitajika ulimwenguni siku hizi imani ambayo itazishikilia ahadi za neno la Mungu, na kuzing'ang'ania mpaka mbingu zijibu. Imani ya namna hii hutuunganisha na mbingu, na kutupa nguvu za kushindania na uwezo wa giza. Kwa njia ya imani wana wa Mugu walishinda milki za wafalme, walitenda haki, walipata ahadi, walifunga vinywa vya simba, walizima nguvu za moto, waliokoka na makali ya upanga. Walitiwa nguvu baada ya kuwa dhaifu, walikuwa hodari katika vita, walikimbiza majeshi ya wageni.” Waebrania 11:33, 34. Na kwa imani sisi leo tunaweza kuyafikia makusudi ya Mungu kwetu. “Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye.” Marko 9:29.MwI 122.4

    Imani ni muhimu sana kwa maombi yenye kushinda. “Maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawahu wale wamtafutao.” “Tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.” Waebrania 11:16; 1 Yoh. 5:14, 15. Kwa imani kama ile ya Yakobo yenye kuvumilia, na ya Eliya isiyoyumbayumba, sisi twaweza kupeleka haja zetu kwa Baba yetu, tukidai ahadi zile alizotuahidi. Heshima ya kiti chake cha enzi inadumu kwa ajili ya kutimiza ahadi alizoahidi.MwI 123.1

    Ahabu alipojitayarisha kutelemka toka mlima wa Karmeli, vivuli vya jioni vilikuwa vinafunika nchi. “Ikawa muda si muda, mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo, ikanya mvua nyingi. Ahabu akapanda garini, akaenda zake Yezreeli.” Ahabu alipokuwa akienda mjini kwake, hakuweza kuona njia kwa ajili ya giza la mvua. Eliya, ambaye amemwaibisha Ahabu mbele ya watu wake, na kuwaua manabii wake waabuduo sanamu, hata hivyo bado angali akimheshimu kama mfalme wa Israeli. Na sasa kama kitendo cha heshima kwa mfalme, Eliya nabii alipiga mbio mbele ya gari la mfalme ili kumwongoza njia, akiwezesh- wa na uwezo wa Mungu.MwI 123.2

    Kitendo bora hiki nabii wa Mungu alichomtendea mfalme huyu mwovu, kimekuwa fundisho kubwa kwa wote wale wanaojidai kuwa ni watumishi wa Mungu, hali wakikosa unyenyekevu, ila tu wanajitukuza wenyewe. Wako watu ambao huhesabu kazi fulani kuwa hizo haziwafai, ni za chini sana, zinafaa watumishi tu. Husitasita kufanya shughuli fulani, ijapokuwa ni za lazima kabisa, ili wasionekane kuwa wanafanya kazi za kitumishi. Watu kama hao inawapasa wajifunze kwa mfano wa Eliya. Kwa neno lake, hazina za mbinguni zilifungwa kwa miaka mitatu na nusu; ameheshimiwa wazi pale mlimani Karmeli kwa kushusha moto kutoka mbinguni na kuteketeza kafara; mkono wake umetekeleza hukumu ya Mungu kwa kuwaulia mbali manabii wa Baali; maombi yake ya kuombea mvua yamejibiwa wazi. Hata hivyo pamoja na heshima zote hizo alizo nazo, alihiari kukimbia mbele ya gari la mfalme, ambayo ni kazi ya kitumishi.MwI 123.3

    Eliya na Ahabu waliachania penye lango la kuingia Yezreeli. Nabii hakutaka kuingia mjini, lakini alilala nje ya mji, chini ardhini, ambapo alitandika matandiko yake.MwI 124.1

    Mfalme alipoingia kwake, alimweleza Yezebeli mkewe, habari za ajabu zilizotendeka mlimani, jinsi Mungu wa kweli alivyojidhihirisha kwa Israeli wazi wazi, na kwamba Eliya ni mtumishi wake kwa kweli. Ahabu aliposimulia kisa cha kuchinjwa manabii wa Baali, Yezebeli akafurika kwa ghadhabu. Alikataa kabisa kukubali mambo yaliyotokea mlimani Karmeli, kwamba, eti Mungu ndiye atawalaye, kwa hiyo akatangaza kwamba Eliya hana budi kufa.MwI 124.2

    Usiku ule ule, mjumbe kutoka kwa Yezebeli alimwamsha nabii aliyechoka kwa shughuli za jana yake, na ujumbe huu Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao.”MwI 124.3

    Ingeonekana kwamba, Eliya baada ya kusimama imara kabisa, bila hofu, na baada ya kufaulu na kuwanyamazisha wenye kuabudu sanamu wote pamoja na mfalme wao, asingeweza kamwe kuwa mwoga, mwenye kukata tamaa upesi hivyo. Lakini sasa, kumbe, mtu ambaye ameona ushahidi wa dhahiri jinsi Mungu anavyohifadhi watu wake, alikuwa katika hali ile ile ya udhaifu na unyonge wa kibinadamu. Na katika saa hiyo yenye giza na mashaka, imani yake ilitoweka. Akagutuka katika usingizi wake, hali akiwa amefadhaika sana. Mvua ilikuwa ikinyesha sana, na giza nene lilifunika nchi. Akisahau jinsi Mungu alivyomficha kwa muda wa miaka mitatu, kutokana na hasira ya Yezebeli na Ahabu, alitoroka, akakimbia ili ajiponye. Alipofika Beer-sheba, “akamwacha mtumishi wake huko. Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja.”MwI 124.4

    Haikumpasa Eliya akimbie na kuacha kazi yake. Ilimpasa ayakabili matisho ya Yezebeli kwa njia ya kuomba ulinzi kutoka kwake aliyemwagiza na kumpa kazi hiyo ya kuwarudisha Israeli katika njia ya kweli. Alipaswa kumwambia mjumbe wa Yezebeli kwamba, Mungu wa mbinguni, ambaye yeye ni mtumishi wake, atamlinda salamini kutokana na matisho ya malkia.MwI 125.1

    Saa chache tu zimepita, tangu alipoona uhakikisho wa kuwako kwa Mungu, na jinsi alivyojidhihirisha kwake wazi. Mambo hayo yangempa matumaini juu ya ulinzi wa Mungu kwamba, hata katika matisho haya Bwana hatamwacha. Kama angekumbuka mahali alipokuwa na kama angalimtegemea Mungu kabisa, na kusimama imara kuitetea kweli, angali- hifadhiwa asidhuriwe. Bwana angalimpa ushindi mwingine kwa kumwadhibu Yezebeli. Kwa njia hiyo mambo yaliyofanyika mlimani yangalidumu mioyoni mwa watu na mfalme na kuwaleta katika matengenezo halisi.MwI 125.2

    Eliya alitumaini kuwa mambo yaliyofanyika mlimani Karmell yalitosha kabisa. Hakudhani kuwa baada ya maajabu hayo Yezebeli ataendelea kushindana na kweli, kiasi cha kumshawishi Ahabu ayapuuze: alidhani kuwa watu watageuka mara moja na kuacha njia mbaya. Mchana kutwa alikuwa akishughulika juu ya mlima wa Karmeli, bila kula cho chote. Hata hivyo alikuwa na nguvu wakati alipoliongoza gari la mfalme Ahabu kwenda Yezreeli, hakuzimia kwa njaa, wala uchovu wa shughuli nyingi.MwI 125.3

    Lakini Eliya alipatwa na hali inayotokea kila mara baada ya tendo la ujasiri wa imani. Alihofu kwamba matengenezo yaliyoanza juu ya mlima Karmeli, hayatadumu kwa hiyo akashikwa na wasiwasi. Alipokuwa juu ya kilele cha Pisga, alitukuzwa, na sasa yumo bondeni. Kule mlimani alikuwa jasiri kabisa kwa kutiwa nguvu na Mwenyezi akakabili jaribio kali kabisa la imani: lakini wakati huu, matisho ya Yezebeli yanapogonga masikioni mwake, na Shetani akimwongoza mwanamke huyu mwovu, Eliya alipoteza imani yake kwa Mungu. Alikuwa jasiri mkuu: na sasa akashikwa na hofu kuu. Akimsahau Mungu, Eliya aliendelea kukimbia, mpaka akajikuta amefika jangwani, hali yu peke yake. Aliketi chini ya mti wa mretemu kupumzika akiwa hoi kabisa. Akiwa pale, aliomba ajifie. “Yatosha, sasa Ee Bwana, uiondoe roho yangu, kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu.” Mkimbizi, ambaye yuko mbali na makao ya wanadamu, roho yake ilijaa uchungu mwingi na kukata tamaa, wala hakutamani kukutana na watu. Mwishowe, akaanguka na kulala usingizi, huku amechoka mno.MwI 125.4

    Katika maisha ya watu, huja wakati wa kukata tamaa na kuona uchungu mwingi wakati ambapo huzuni na masikitiko huwa sehemu ya maisha. Wakati kama huo huwa vigumu kuamini kuwa Mungu huwafadhili wanadamu hapa chini. Siku ambazo taabu huwasonga watu, na mauti huonekana kana kwamba ndiyo ifaayo mahali pa uhai. Wakati kama huo, ndipo wengi huiacha imani yao kwa Mungu: nao huogelea mashakani, huwa watumwa wa kutokuamini. Wakati kama huo, kama tungepambanua hifadhi tunayopewa na Mungu wetu, tungeona katika macho ya kiroho jinsi malaika wanavyotushughulikia, kwa makini, ndipo maisha mapya na imani mpya vingechipuka ndani yetu.MwI 126.1

    Ayubu, ambaye ni mwaminifu, alipopita katika shida kuu
    na giza kuu maishani mwake, alinena hivi:
    Na ipotelee mbali ile siku niliyozaliwa mimi.
    Laiti uchungu wangu ungepimwa,
    Na msiba wangu kutiwa katika mizani pamoja
    Laiti ningepewa haja yangu,
    Naye Mungu angenipa neno hilo ninalolitamani sana
    Kwamba Mungu angekuwa radhi kuniseta:
    Kwamba angeulegeza mkono wake na tilia mbali
    Hapo ndipo ningefarijika hata sasa.
    Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu,
    Nitanena kwa mateso ya roho yangu.
    Nitalia kwa uchungu wa nafsi yangu.
    Hata nafsi yangu huchagua . . .
    kifo kuliko maisha yangu.
    Ninadhoofika: sitaishi siku zote,
    Usinisumbue, kwani siku zangu ni uvuvio.”
    MwI 126.2

    Ayubu 3:3; 6:2, 8-10; 7:11, 15, 16.

    Lakini hata kama Ayubu alichoka na maisha ya taabu, hakuruhusiwa kufa. Kwake, uwezekano wa baadaye ulidhihirishwa, naye alipewa ujumbe wenye matumaini:MwI 128.1

    Naam, utathibitika, wala hutakuwa na hofu:
    Kwa kuwa utasahau mashaka yako,
    Utayakumbuka kama maji yaliyokwisha pita:
    Na maisha yako yatakuwa meupe kuliko adhuhuri:
    Lijapokuwa ni giza, litakuwa kama alfajiri.
    Nawe utakuwa salama:
    Kwa sababu kuna matumaini. . . .
    Utalala, wala hapana atakayekutia hofu:
    Naam, wengi watakutafuta uso wako.
    Lakini macho ya waovu yataingia kiwi,
    Nao hawatakuwa na njia ya kukimbia
    Na matumaini vao yatakuwa ni kutoa roho.”
    MwI 128.2

    Ayubu 11:15-20.

    Ayubu aliinuka kutoka katika kukata tamaa na kufa moyo akafikia kilele cha matumaini ya rehema za Mungu na uwezo wake wa kuokoa. Alishangilia kwa kusemaMwI 128.3

    Tazama, ataniua. . . . Ila hata hivyo nitaithibitisha njia.
    yangu mbele yake
    Hili nalo litakuwa ni wokovu wangu
    Lakini mimi najua ya kuwa Mtetezi wangu yu hai,
    Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.
    Na baada ya ngozi yangu kuharibika hivi,
    Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu:
    Nami nitamwona mimi nafsi yangu,
    Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine.”
    MwI 128.4

    Ayubu 13:15, 16; 19:25-27.

    Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli,” (Ayubu 38:1) akajidhihirisha kwa mtumishi wake kwa uwezo wake mkuu. Ayubu alipofunuliwa na kumwona Mwumba wake, alijichukia, akatubu kwa mavumbi na majivu. Ndipo Bwana alimbariki mno, akafanya miaka yake ya mwisho kuwa bora katika maisha yake.MwI 128.5

    Matumaini na ujasiri ni vitu muhimu sana katika kazi ya Mungu. Hivyo ni tunda la imani. Kukata tamaa ni dhambi. Na hakuna maana. Mungu aweza, na anataka zaidi sana (Waebrania 6:17) kuwapa watumishi wake uwezo wanaohitaji wakati wa majaribu. Mipango mipotofu ya adui wa kazi ya Bwana, inawezekana kuonekana kana kwamba imepangwa vema sana, tena ni imara, lakini Mungu anaweza kuibatilisha yote. Naye hufanya hivyo kama apendavyo. Anapoona kuwa imani ya watumishi wake imejaribiwa vya kutosha, huingia kati mara moja.MwI 128.6

    Kwa mtu mwenye kukata tamaa, dawa yake ni kuwa na imani, maombi na kufanya kazi. Imani na juhudi ya utendaji wa kazi, vitaleta hakikisho halisi pamoja na kuridhika, ambavyo huongezeka siku kwa siku. Je, unajaribiwa kubashiri mambo yenye kukukatisha tamaa? Wakati wa giza kali la maisha, wakati mambo yote yanapoonekana kuwa hayavumiliki, usiogope lo lote. Mtegemee Mungu tu. Anajua mahitajj yako. Yeye ni mweza vote. Upendo wake na huruma zake havichakai kamwe. Asihofu kwamba, atashindwa kufikiliza ahadi zake. Yeye ni wa kweli milele. Kamwe hatabadili agano lake, na wale wam- pendao. Atawamwagia watumishi wake uwezo tele wanaouhitaji Mtume Paulo ameshuhudu akisema: “Naye akaniambia, Neema vangu yakutosha, maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. . . Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, n ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu, ndipo nilipo na nguvu.” 2 Wakorintho 12:9, 10MwI 129.1

    Je, Mungu alimwacha Eliya katika saa ya majaribu? La, hata kidogo! Alimpenda mtumishi wake wakati alipojisikia kana kwamba ameachwa na Mungu na wanadamu, sawasawa na wakati alipoomba moto ushuke kutoka mbinguni na kuung'aza mlima. Sasa wakati Eliya alipolala, aliguswa taratibu akaamka. Alishtuka kwa hofu, akataka kukimbia, maana alidhani kuwa adui yake amemgundua.MwI 129.2

    Lakini aliyemwinamia, mwenye uso wa huruma, hakuwa adui, ila rafiki. Mungu amemtuma malaika amletee mtumishi wake chakula. Malaika akasema, “Inuka, ule. Akatazama, kumbe! pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake.”MwI 129.3

    Eliya alipokwisha kula, akalala tena. Mara ya pili malaika akaja, akamgusa mtu mchovu huyu, akasema kwa upole, “Inuka, ule, maana safari hii ni kubwa mno kwako. Akainuka akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu” Akajificha pangoni.MwI 130.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents