Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    18—Kuyaponya Maji Machungu

    Nyakati zile wazee hao walizoishi bonde la mto wa Yordani lilikuwa lenye “maji mengi. . . kama bustani ya Bwana.” Katika bonde hili zuri ndipo Lutu alichagua kuishi, ambavyo akajongeza hema yake mpaka Sodom.” Mwanzo 13:10, 12. Wakati miji iliyokuwa uwandani ilipoharibiwa, sehemu yote iliyozunguka hapo iligeuka kuwa kame kabisa, na tangu hapo ndipo ilikuwa asili ya jangwa ya Yuda.MwI 191.1

    Sehemu yenye rutuba ya bonde ilibaki ikiwa yenye chemchemi nzuri za maji safi yenye kuwaburudisha wanadamu. Katika bonde hili lenye mashamba mazuri ya nafaka na misitu ya mitende, na miti mingine yenye matunda mazuri, ndipo Wana wa Israeli walipiga kambi baada ya kuuvuka mto wa Vordani. Hapo ndipo walianza kula matunda ya nchi waliyoahidiwa. Mbele yao kuta imara za Yeriko zilisimama. Yeriko ilikuwa ngome ya umizimu na ibada ya sanamu. Hapo ndipo ukafiri wote wa Kanaani wa kuabudu Ashtorethi ulikuwa ukifanyika. Baada ya muda si mrefu kuta hizo ziliangushwa na wenyeji wake waliangamizwa, na wakati huo wa kuanguka, tangazo la kiapo lilitangazwa hadharani likisema: “Na alaaniwe mbele za Bwana mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake wa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo.” Yoshua 6:26.MwI 191.2

    Karne tano zilipita. Kiwanja hicho kikiwa katika hali ya uharibifu, kwa ajili ya kulaaniwa na Mungu. Hata chemchemi za maji zilizokuwa zikiparutubisha mahali hapo, ziliharibika kwa ajili ya laana. Lakini katika siku za uasi wa Ahabu, wakati ibada ya Ashtorethi iliporudishwa nchini na Yezebeli. Yeriko. ambao ulikuwa kiini cha ibada hii hapo zamani, ulijengwa; ingawa ni kwa kujihatarisha kwa wajengaji. Hieli Mbetheli akajenga Yeriko, “akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.” 1 Wafalme 16:34.MwI 192.1

    Shule mojawapo ya shule za manabii ilikuwa katikati ya miti ya matunda, karibu na Yeriko. Baada ya kupaa kwa Eliya, Elisha alienda huko. Wakati wa matembezi yake huko watu wa mjini walimwendea nabii na kusema: “Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza.” Chemchemi ambayo hapo zamani ilikuwa nzuri, ikiwapatia wakaaji wa mjini na ujirani maji safi ya kunywa, sasa haifai kwa lo lote.MwI 192.2

    Katika kujibu ombi la wana mji Elisha alisema: “Nileteeni chombo kipya. mtie chumvi ndani yake.” Alipokwisha kupata chombo hicho na chumvi, “akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, Bwana asema hivi, Nimeyaponya maji haya hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza.” 2 Wafalme 2:19-21.MwI 192.3

    Kuyaponya maji ya Yeriko hakukufanyika kwa hekima ya kibinadamu, bali kwa mwujiza wa Mungu. Watu walioujenga mji wa Yeriko, walifanya kinyume cha mapenzi ya mbinguni; walakini, yule ambaye “huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki,” aliona kuwa inafaa kwa hali hii kudhihirisha dalili ya fadhili zake katika kuponya maradhi ya kiroho ya Waisraeli. Mathayo 5:45.MwI 192.4

    Uponyaji huo wa maji ulikuwa wa kudumu. “Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.” 2 Wafalme 2:22. Kwa vizazi na vizazi maji hayo yamekuwa yakibubujika daima, na kuifanya sehemu hiyo ya nchi kuwa na chemchemi nzuri.MwI 192.5

    Yako mafundisho mengi ya kiroho kutokana na kuponywa huko kwa maji. Chombo kipya, chumvi, na chemchemi vyote ni mifano bora.MwI 193.1

    Elisha alipoitupa chumvi ndani ya chemchemi za maji machungu, alitoa fundisho lile lile lililotolewa na Mwokozi baadaye kwa wanafunzi wake, wakati alipotamka na kusema, “Ninyi ni chumvi ya dunia.” Mathayo 5:13. Chumvi ilipochanganyika na maji ya chemchemi iliyoharibika, iliyasafisha maji hayo, yakawa mazuri yenye kuleta uzima na burudiko, ambavyo hapo kwanza yalikuwa yenye maradhi na kifo. Mungu anapowalinganisha watoto wake na chumvi, huwafundisha kwamba, makusudi yake ya kuwahesabu kuwa raia za neema yake, ni kuwafanya vyombo vyake vya kuokolea wengine. Shabaha ya Mungu ya kuwateua watu kabla ulimwengu haujakuwapo, si kuwafanya wana wake na binti zake tu, bali kwa njia yao ulimwengu upate neema ya wokovu. Bwana alipomwita Ibrahimu, si kwamba amfanye rafiki yake maalum, ila alitaka awe njia ya kupitisha mibaraka ya Mungu ili iwafikie walimwengu.MwI 193.2

    Ulimwengu unahitaji ushuhuda wa ukristo halisi. Sumu ya dhambi imewaingilia wanadamu. Mijini na vijijini kumejaa uovu na uharibifu. Ulimwengu umejaa na ugonjwa, masumbuko, na uovu. Hapa na kule kuna watu masikini, wenye taabu, wanaolemewa na mizigo ya dhambi ambao wanakufa kwa kukosa njia ya kuwaokoa. Injili ya kweli inanenwa kwao, hata hivyo wanapotea, kwa sababu mivuto ya wale ambao wangewavutia kwenye uzima, huwavutia mautini. Wanakunywa maji machungu kwa sababu chemchemi zimetiwa sumu, badala ya kutoa maji ya uzima, hutoa maji machungu.MwI 193.3

    Chumvi lazima ichanganyike na kile inamotiwa, lazima ipenye na kukoleza, ili ipata kuhifadhi. Hali kadhalika mivuto ya uzima itokanayo na injili, hutokeza uzima kwa wale wanaoshiriki nayo. Watu hawaokolewi kwa makundi, bali kwa mmoja mmoja. Mvuto wa mtu una uwezo. Lazima uwe wa Kikristo ili uinue watu kama Kristo alivyowainua, upate kuwapa kanuni iliyo kamili, na kuwazuilia wasikumbwe na mafuriko ya uovu wa dunia. Lazima kueneza neema ya Kristo, ambayo hutoka kwake tu. Kuinua, na kukolewa maisha na tabia za wengine kwa uwezo wa mvuto bora na kielelezo halisi kinachochanganyika pamoja na imani na upendo.MwI 193.4

    Kuhusu chemchemi za pale Yeriko, Bwana alisema: “Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa, wala kuzaa mapooza.” Kuharibika kwa chemchemi ni mfano wa mtu aliyejitenga na Bwana. Dhambi haimtengi mtu na Mungu tu, bali huharibu ile nia ya mtu ya kumjua Mungu. Mtu huishi vivi hivi tu bila kujua nyuma wala mbele. Dhambi huharibu kabisa hali yote ya mtu, mawazo hupotoshwa, na uwezo wa nia huchafuliwa; hali ya utu huwa hafifu. Mtu hubaki bila ya dini safi, na utakatifu wa moyo. Uwezo wa Mungu wa kubadili hali ya maisha na tabia unakosekana. Kwa hiyo mtu huwa mnyonge, maana uwezo unaomwezesha kushinda umeharibika.MwI 194.1

    Mtu ambaye moyo wake umesafishwa, kila kitu kimebadilika. Mabadiliko ya tabia na hali ya mtu ndio ushahidi kwa walimwengu kwamba, Kristo anaishi ndani yake. Roho wa Mungu huzaa maisha mapya moyoni, akitokeza mawazo na makusudi yanayomtii Kristo na kufuata mapenzi yake; kwa hiyo utu wa ndani wa mtu huumbika katika sura ya Mungu. Watu wanyonge na wenye makosa, huuonyesha ulimwengu kwamba, uwezo wa neema ya Mungu iokoayo unaweza kutengeneza tabia mbaya ya mtu ikawa bora, yenye matunda mazuriMwI 194.2

    Moyo unaolipokea neno la Mungu haufanani na dimbwi la maji, ambalo maji yake hunywewa na jua na kukauka, wala haufanani na birika lenye kuvuja, lisiloweka kitu; bali ni kama kijito kibubujikacho kutoka mlimani ambako chemchemi zake hazikauki, maji yake hububujika katika miamba, nayo humburudisha mchovu, mwenye kiu, na mwenye kulemewa na mzigo. Ni kama mto unaobubujika daima, unaoendelea na kuzidi kupanuka na kuwa na kina mpaka kueneza maji yake katika nchi nzima. Ni kama kijito kinachovuma kikienda huku nyuma kikiacha karama ya rutuba na ustawi wa mimea. kandokando yake majani hustawi, na miti hustawi na kuzaa matunda. Nchi inapokauka wakati wa kiangazi kwa ajili ya jua kali, kandokando ya kijito cha maji huwa na mimea mibichi iliyojipanga msitarini kufuatana na kijito hicho.MwI 194.3

    Hivyo ndivyo ilivyo na mtoto wa Mungu. Dini ya Kristo hujitambulisha yenyewe kuwa yenye uhai na kanuni za wima zenye kufanya kazi bora maishani. Moyo unapokubali kupokea ukweli wa mbinguni na kanuni zake za upendo, kanuni hizi hufanana na kijito cha maji kifurikacho katika nchi kame, nazo hufurika nje kwa walimwengu mahali ambapo leo ni ukiwa.MwI 195.1

    Wale waliotakaswa na kweli ya Biblia wanaposhughulika katika kazi ya kuwaokoa wengine, huwa na mvuto au ladha iletayo uzima kwa wanadamu. Na kwa kadiri wanavyokunywa katika kisima cha neema na maarifa, ambacho hakikauki, kila siku wataona kuwa roho zao zinajazwa na Roho wa Mungu na kufurika, na kwa njia yao watu wengi watafaidika, kimwili, kimawazo, na kiroho. Wachovu wataburudika, wagonjwa watapona, na wenye mizigo ya dhambi watapata pumziko. Sifa za watu zitasikika kutoka mbali zikisifu shani ya Mungu, sifa za watu ambao hapo kwanza walimtumikia Ibilisi, na sasa “ni watumishi wa Mungu.MwI 195.2

    “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa,” kwa maana neno la Mungu ndilo “chemchemi ya bustani, kisima cha maji yaliyo hai, vijito vya Lebanoni.” Luka 6:38; Wimbo Ulio Bora 4:15.MwI 195.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents