Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Pambano Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura ya 24—Ndani ya Patakatifu pa Patakatifu

    Somo la patakatifu lilikuwa ufunguo uliofungua siri ya kukatishwa tamaa kwa mwaka 1844. Ulifungua mfumo kamili wa ukweli, ulioshikamana na kuafikiana, ukionesha kuwa mkono wa Mungu uliongoza vuguvugu kuu la marejeo na ulifunua wajibu wa sasa kwa kuonesha nafasi na kazi ya watu Wake. Kama vile wanafunzi wa Yesu baada ya usiku wa huzuni na kukatishwa tamaa “walivyofurahi walipomwona Bwana,” ndivyo walivyofurahi sasa wale waliokuwa wametazamia kwa imani ujio Wake wa pili. Walimtarajia aonekane katika utukufu atoe ujira kwa watumishi Wake. Matumaini yao yalipokatishwa tamaa, walishindwa kumwona Yesu, kama Mariamu kwenye kaburi walilia: “Wamemwondoa Bwana wangu, na sijui wamemweka wapi.” Sasa ndani ya patakatifu pa patakatifu walimwona tena, Kuhani wao Mkuu mwenye huruma, ambaye hivi karibuni atatokea kama mfalme na mkombozi wao. Nuru kutoka katika hekalu iliangazia wakati uliopita, wakati uliopo, na wakati ujao. Walielewa kuwa Mungu alikuwa amewaongoza kwa njia ya hekima yake isiyokosea. Ingawa, kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa kwanza, na wao wenyewe walishindwa kuelewa ujumbe waliouhubiri, ingawa ulikuwa sahihi katika kila kipengele. Katika kuuhubiri walitimiza kusudi la Mungu, na kazi yao haikuwa ya bure katika Bwana. Wakiwa wamezaliwa “tena katika tumaini hai,” walifurahi “kwa furaha isiyoneneka na iliyojaa utukufu mwingi.”PKSw 324.1

    Unabii wa Danieli 8:14, “Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa,” na ujumbe wa malaika wa kwanza, “Mcheni Mungu na kumtukuza; kwa maana saa ya hukumu Yake imekuja,” ulielekeza kwa huduma ya Kristo ndani ya patakatifu pa patakatifu, na kwa ujio wa Kristo kwa ajili ya ukombozi wa watu Wake na uangamizaji wa waovu. Kosa halikuwa katika ukokotoaji wa vipindi vya kiunabii, lakini kosa lilikuwa katika tukio ambalo lingetokea mwishoni mwa siku 2300. Kwa njia ya kosa hili, waaminio walipata uzoefu wa kukatisha tamaa, lakini yote yaliyotabiriwa katika unabii huu, na yote waliyoyatarajia yaliyokuwa na ushahidi wa Maandiko, yalikuwa yametimia. Wakati ambao walikuwa wakiomboleza wakiwa wamepoteza matumaini yao, tukio lilikuwa limetokea ambalo lilitabiriwa na ujumbe huo, na ambalo lazima litimizwe kabla Bwana hajarudi kutoa ujira kwa watumishi Wake.PKSw 324.2

    Kristo alikuwa amekuja, sio duniani, kama walivyotarajia, lakini, kama ilivyokuwa imetabiriwa katika mifano, ndani ya patakatifu pa patakatifu katika hekalu la Mungu mbinguni. Amewakilishwa na nabii Danieli kama Yeye anayekuja wakati huu kwa Mzee wa Siku:“Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja”—siyo kuja duniani, bali kuja kwa—“huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye” (Danieli 7:13).PKSw 324.3

    Ujio huu umetabiriwa pia na nabii Malaki: “Naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:1). Kuingia kwa Bwana katika hekalu lake kulikuwa kwa ghafla, bila kutarajia, kwa watu Wake. Hawakumtarajia kwenda pale. Walimtarajia kuja duniani, “katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu” (2 Wathesalonike 1:8).PKSw 325.1

    Lakini watu hawakuwa tayari bado kumpokea Bwana wao. Kulikuwa bado kuna kazi ya maandalizi kwa ajili yao. Ilipasa nuru itolewe, ikielekeza akili zao ndani ya hekalu la Mungu la mbinguni; na wakati wakimfuata kwa imani Kuhani wao Mkuu katika huduma Yake pale, majukumu mapya yangefunuliwa. Ujumbe mwingine wa onyo na maelekezo ulipaswa kutolewa tena kwa kanisa.PKSw 325.2

    Nabii anasema: “Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki” (Malaki 3:2, 3). Watakaokuwa wakiishi duniani wakati maombezi ya Kristo yakiwa yamekoma katika hekalu la mbinguni watasimama mbele ya macho ya Mungu bila mpatanishi. Majoho yao yanapaswa yasiwe na doa, tabia zinapaswa ziwe zimesafishwa dhambi kwa kunyunyiziwa damu ya Kristo. Kwa njia ya neema ya Mungu na kwa njia ya juhudi binafsi inawapasa wawe washindi katika vita dhidi ya uovu. Wakati hukumu ya upepelezi ikiendelea mbinguni, wakati dhambi za waaminio wanaotubu zikiondolewa hekaluni, kuna kazi maalumu ya utakaso ambayo inapaswa ifanywe, ya kuachana na dhambi, miongoni mwa watu wa Mungu duniani. Kazi hii imewasilishwa kwa uwazi zaidi katika ujumbe wenye sehemu tatu wa Ufunuo 14.PKSw 325.3

    Wakati kazi hii itakapokuwa imekamilika, wafuasi wa Kristo watakuwa tayari kwa ajili ya ujio Wake. “Ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za Bwana, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani” (Malaki 3:4). Ndipo kanisa ambalo Bwana wetu wakati wa ujio Wake atalipokea litakuwa “Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa” (Waefeso 5:27). Ndipo litaonekana “kama alfajiri, Mzuri kama mwezi, safi kama jua, Wa kutisha kama wenye bendera” (Wimbo Ulio Bora 6:10).PKSw 325.4

    Pamoja na ujio wa Bwana ndani ya hekalu Lake, Malaki pia hutabiri ujio Wake wa pili, ujio Wake kwa ajili ya kutekeleza hukumu, katika maneno haya: “Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi” (Malaki 3:5). Yuda anarejea mandhari hiyo hiyo anaposema, “Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu, ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu” (Yuda 14, 15). Ujio huu, na kuja kwa Bwana ndani ya hekalu Lake, ni matukio mawili yaliyo tofauti kabisa.PKSw 326.1

    Kuja kwa Kristo kama kuhani wetu mkuu ndani ya patakatifu pa patakatifu, kwa ajili ya utakaso wa hekalu, kunakotajwa katika Danieli 8:14; kuja kwa Mwana wa Adamu kwa Mzee wa Siku, kama kulivyoelezwa katika Danieli 7:13; na kuingia kwa Bwana ndani ya Hekalu Lake, kulikotabiriwa na Malaki, ni maelezo ya tukio lile lile moja; na limewakilishwa pia na ujio wa bwana arusi kwenye harusi, ulioelezwa na Kristo katika mfano wa wanawali kumi, wa Mathayo 25.PKSw 326.2

    Wakati wa kiangazi na wa vuli mwaka 1844 tangazo, “Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki,” lilitolewa. Makundi mawili yanayowakilishwa na wanawali wenye busara na wapumbavu yalijitokeza—kundi moja lililotazamia ujio wa Bwana, na ambao walikuwa wakijiandaa kwa bidii kukutana Naye; na kundi jingine ambalo, wakiwa wamebanwa na hofu na wakitenda kwa msisimko, waliridhishwa na nadharia ya ukweli, lakini hawakuwa na neema ya Mungu. Katika mfano, bwana arusi alipokuja, “nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini.” Kuja kwa bwana arusi kunakooneshwa hapa, kunatokea kabla ya arusi. Arusi huwakilisha upokeaji wa Kristo wa ufalme Wake. Mji Mtakatifu, Yerusalemu Mpya, ambao ni mji mkuu nao huwakilisha ufalme, na unaitwa “bibi arusi, mke wa Mwanakondoo.” Malaika alimwambia Yohana: “Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.” “Akanichukua katika Roho,” anasema nabii, “akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu” (Ufunio 21:9, 10). Kwa hakika, hiyo basi, bibi arusi huwakilisha Mji Mtakatifu, na wanawali wanaokwenda kumlaki bwana arusi ni mfano wa kanisa. Katika Ufunuo watu wa Mungu wanasemekana kuwa ni wageni katika karamu ya arusi (Ufunuo 19:9). Ikiwa ni wageni, hawawezi tena kuwakilisha bibi arusi. Kristo, kama ilivyoelezwa na nabii Danieli, atapokea kutoka kwa Mzee wa Siku mbinguni, “mamlaka, na utukufu, na ufalme;” Ataupokea Yerusalemu Mpya, mji mkuu wa ufalme Wake ambao, “umewekwa tayari, kama bibiarusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe” (Danieli 7:14; Ufunuo 21:2). Akiwa amepokea ufalme, atakuja katika utukufu Wake, kama Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana, kwa ajili ya ukombozi wa watu Wake, ambao “wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo,” kando ya meza Yake katika ufalme Wake (Mathayo 8:11; Luka 22:30), kushiriki katika karamu ya arusi ya Mwana Kondoo.PKSw 326.3

    Tangazo, “Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki,” katika kiangazi cha 1844, liliwasababisha maelfu ya watu kutarajia ujio wa haraka wa Bwana. Kwa wakati uliopangwa Bwana arusi alikuja, siyo duniani, kama watu walivyotarajia, bali kwa Mzee wa Siku mbinguni, arusini, karamu ya ufalme Wake. “Nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa” Wasingeweza kuwepo arusini kimwili; kwa sababu arusi inafanyikia mbinguni, wakati wao wakiwa duniani. Wafuasi wa Kristo wanapaswa kuwa “watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini” (Luka 12:36). Lakini inawapasa kuelewa kazi Yake, na wamfuate kwa imani anapoingia ndani mbele ya Mungu. Ni katika maana hii ambapo wanaelezwa kuwa wanakwenda arusini.PKSw 327.1

    Katika mfano wa wanawali kumi ni wale waliokuwa na mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao ambao walienda arusini. Wale ambao, pamoja na kuujua ukweli kutoka katika Maandiko, walikuwa pia na Roho na neema ya Mungu, na ambao, katika giza la majaribu makali, walingoja kwa uvumilivu, wakichunguza Biblia ili kupata nuru kubwa zaidi—hawa waliuona ukweli kuhusu hekalu la mbinguni na badiliko la huduma ya Mwokozi, na kwa imani walimfuata katika kazi Yake katika hekalu mbinguni. Na wale wote ambao kwa njia ya ushuhuda wa Maandiko wanaukubali ukweli huo huo, wakimfuata Kristo kwa imani anapoingia mbele ya Mungu kufanya kazi ya mwisho ya upatanisho, na mwisho wa kazi hiyo apokeee ufalme Wake—yote haya yamewakilishwa na kwenda arusini.PKSw 327.2

    Katika mfano wa Mathayo 22 kielelezo hicho hicho cha arusi kimetumiwa, na hukumu ya upelelezi imeoneshwa wazi wazi ikitokea kabla ya arusi. Kabla ya arusi mfalme anakuja kuona wageni wake, kuona kama wote wamevaa vazi la arusi, joho lisilokuwa na doa la tabia lililofuliwa na kufanywa jeupe katika damu ya Mwana Kondoo (Mathayo 22:11; Ufunuo 7:14). Anayekutwa akiwa na mapungufu anatupwa nje, lakini wote ambao baada ya kuchunguzwa wanaonekana wakiwa wamevaa vazi la arusi wanakubaliwa na Mungu na wanahesabiwa kuwa wanastahili kuwa na sehemu katika ufalme Wake na kuketi juu ya kiti Chake cha enzi. Kazi hii ya kuchunguza tabia, ya kubaini wanaojiandaa kwa ajili ya ufalme wa Mungu, ni ile ya hukumu ya upelelezi, kazi ya mwisho katika hekalu la mbinguni.PKSw 327.3

    Kazi ya upelelezi ikiisha, wakati kesi za wale ambao katika zama zote walikiri kuwa wafuasi wa Kristo zitakapokuwa zimechunguzwa na kufanyiwa uamuzi, ndipo, na ni hadi hapo, ndipo kazi ya upelelezi itafikia kikomo, na mlango wa rehema utafungwa. Hivyo katika sentensi moja fupi, “Nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa,” tunachukuliwa na kupitishwa katika huduma ya mwisho ya Mwokozi, hadi wakati ambapo kazi kubwa ya wokovu wa mwanadamu itakapokamilika.PKSw 328.1

    Katika huduma ya hekalu la duniani, ambayo, kama tulivyokwisha kuona, ni kielelezo cha huduma ya mbinguni, wakati kuhani mkuu siku ya Upatanisho alipoingia ndani ya patakatifu pa patakatifu, huduma katika chumba cha kwanza ilisitishwa. Mungu aliamuru: “Wala hapatakuwa na mtu katika hema ya kukutania, wakati aingiapo ili kufanya upatanisho katika patakatifu, hata atakapotoka nje” (Walawi 16:17). Hivyo Kristo alipoingia patakatifu pa patakatifu kufanya kazi ya mwisho ya upatanisho, alisitisha huduma Yake katika chumba cha kwanza. Lakini huduma katika chumba cha kwanza ilipoisha, huduma katika chumba cha pili ilianza. Katika huduma ya mfano kuhani mkuu alipoondoka patakatifu katika Siku ya Upatanisho, alienda mbele za Mungu kupeleka damu ya mnyama wa sadaka ya dhambi kwa niaba ya Waisraeli wote ambao walitubu kwa dhati dhambi zao. Kwa hiyo Kristo alimaliza sehemu moja tu ya kazi Yake kama mwombezi, ili aingie katika sehemu nyingine ya kazi, na bado aliendelea kutumia damu Yake kumwomba Baba kwa niaba ya wenye dhambi.PKSw 328.2

    Somo hili halikueleweka kwa Waadventista mwaka 1844. Baada ya kupita kwa wakati ambao Mwokozi alikuwa akitarajiwa, bado waliamini ujio Wake ulikuwa karibu, walishikilia kuwa walikuwa wamefika kipeo kikuu muhimu na kuwa kazi ya Kristo kama Mwombezi wa mwanadamu ilikuwa imekoma. Ilionekana kwao kana kwamba wamefundishwa katika Biblia kuwa mlango wa rehema wa mwanadamu ungefungwa muda mfupi kabla ya ujio halisi wa Bwana katika mawingu ya mbinguni. Hili lilionekana kuwa dhahiri kutokana na yale maandiko yanayoelekeza kwa wakati ambao watu watatafuta, watagonga, na watalia kwenye mlango wa rehema, na hautafunguka. Na ilikuwa swali kwao ikiwa tarehe waliyotarajia ujio wa Kristo ingeweza kuwa mwanzo wa kipindi hiki ambacho kingetangulia muda mfupi kabla ya ujio Wake. Wakiwa wamemaliza kutoa onyo la hukumu iliyo karibu, walihisi kuwa kazi yao kwa ajili ya ulimwengu ilikuwa imekwisha, na walipoteza mzigo kwa ajili ya wokovu wa roho za wenye dhambi. Wakati huo huo dhihaka za kijasiri na kufuru za watu wasiomcha Mungu zilionekana kwao kama ushahidi mwingine kuwa Roho wa Mungu alikuwa ameondolewa kutoka kwa waliokataa rehema Yake. Yote haya yalithibitisha kwao kuwa muda wa rehema ulikuwa umekwisha kwa ajili yao, au, kama walivyolieleza hili, “mlango wa rehema ulikuwa umefungwa.”PKSw 328.3

    Lakini nuru kubwa zaidi ilipatikana kwa kuchunguza suala la patakatifu. Sasa waliona kuwa walikuwa sahihi kuamini kuwa mwisho wa siku 2300 mwaka 1844 ulikuwa alama ya kipeo kikuu muhimu. Lakini wakati ambapo ilikuwa kweli kuwa ule mlango wa tumaini na rehema ambao kwao, kwa miaka elfu moja mia nane, watu walikuwa na njia ya kumfikia Mungu, ulikuwa umefungwa, mlango mwingine ulikuwa umefunguliwa, na msamaha wa dhambi ulitolewa kwa wanadamu kwa njia ya maombezi ya Kristo ndani ya patakatifu pa patakatifu. Sehemu moja ya huduma Yake ilikuwa imefungwa, ili kutoa nafasi kwa ajili ya nyingine. Bado kulikuwa na “mlango uliofunguliwa” wa hekalu la mbinguni, ambapo Kristo alikuwa akihudumu kwa ajili ya mwenye dhambi.PKSw 329.1

    Sasa yalionekana matumizi ya yale maneno ya Kristo katika kitabu cha Ufunuo, yanayolihusu kanisa wakati huu: “Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye. Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga” (Ufunuo 3:7, 8).PKSw 329.2

    Ni wale ambao kwa imani wanamfuata Yesu katika kazi kubwa ya upatanisho wanapokea manufaa ya upatanisho Wake kwa ajili yao, wakati ambapo wale wanaokataa nuru inayoonesha huduma hii hawanufaishwi nayo. Wayahudi waliokataa nuru iliyotolewa wakati wa ujio wa kwanza wa Kristo, na kukataa kumwamini kama Mwokozi wa ulimwengu, hawakupokea msamaha unaopatikana kwa njia Yake. Wakati Yesu alipopaa kwenda mbinguni aliingia kwa njia ya damu Yake ndani ya patakatifu pa mbinguni kumwaga mibaraka ya maombezi Yake, Wayahudi waliachwa katika giza totoro wakiendelea na kafara na sadaka zisizo na manufaa yo yote. Huduma ya mifano na vivuli ilikuwa imekoma. Ule mlango ambao hapo awali watu waliweza kupitia na kumfikia Mungu haukuwa wazi tena. Wayahudi walikuwa wamekataa kumtafuta kwa njia ambayo kwayo peke yake angeweza kupatikana, kwa njia ya huduma ya hekalu la mbinguni. Hivyo hawakuwa na mawasiliano na Mungu. Kwao mlango ulikuwa umefungwa. Hawakumtambua Kristo kama kafara halisi na mpatanishi pekee mbele ya Mungu; kwa hiyo hawakupata manufaa ya upatanisho Wake.PKSw 329.3

    Hali ya Wayahudi wasioamini ni mfano wa hali ya watu wasiojali na wasioamini miongoni mwa wanaodai kuwa Wakristo, ambao kwa kuchagua kwao wenyewe hawaijui kazi ya Kuhani wetu Mkuu mwenye rehema. Katika huduma ya mfano, kuhani mkuu alipoingia patakatifu pa patakatifu, Waisraeli wote walitakiwa kukutana pamoja karibu na hema na kunyenyekesha nafsi zao kwa kicho kikuu mbele za Mungu, ili wapate msamaha wa dhambi zao na wasikatiliwe mbali kutoka katika mkutano. Ni kwa kiasi gani ni muhimu katika Siku hii ya Upatanisho halisi inatupasa kuelewa kazi ya Kuhani wetu Mkuu na kujua majukumu tunayotakiwa kuyafanya.PKSw 329.4

    Wanadamu hawawezi kupuuza onyo ambalo Mungu, kwa rehema Yake, analituma bila wapuuziaji kuadhibiwa. Ujumbe ulitumwa kutoka mbinguni kwenda kwa ulimwengu wa siku za Nuhu, na wokovu wao ulitegemea jinsi ambavyo wangeutendea kazi huo ujumbe. Kwa kuwa walilikataa onyo, Roho wa Mungu aliondolewa kutoka kizazi kile cha dhambi, na waliangamia kwa maji ya Gharika. Wakati wa Ibrahimu, rehema iliacha kusihi kwa ajili ya wakazi wa Sodoma wenye hatia, na wote waliteketezwa kwa moto uliotoka mbinguni isipokuwa Lutu na mke wake na mabinti zake wawili. Hivyo, katika siku za Kristo, Mwana wa Mumgu aliwaambia Wayahudi wasioamini: “Nyumba yenu mmeachiwa ukiwa” (Mathayo 23:38). Akiangalia katika zama zote hadi siku za mwisho, Mungu mwenye nguvu isiyo na kikomo, anasema, kuhusu watu ambao “hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa”: “Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu” (2 Wathesalonike 2:10-12). Wanapokataa mafundisho ya neno Lake, Mungu anaondoa Roho Wake na kuwaacha katika udanganyifu wanaoupenda.PKSw 330.1

    Lakini Kristo bado anafanya maombi kwa ajili ya wanadamu, na nuru inatolewa kwa wale wanaoitafuta. Ingawa jambo hili halikueleweka kwa Waadventista wa awali, baadaye liliwekwa wazi wakati Maandiko yanayofasili nafasi yao halisi yalipoanza kufunguka mbele yao.PKSw 330.2

    Kupita kwa wakati mwaka 1844 kulifuatwa na kipindi cha jaribu kubwa kwa wale waliobaki wakishikilia imani ya marejeo. Nafuu yao pekee, kwa kadiri uhakikisho wa nafasi yao sahihi ulivyohusika, ulikuwa nuru iliyoongoza akili zao kuelekea patakatifu pa mbinguni. Baadhi waliikana imani yao kuhusu ukokotoaji wao wa awali wa vipindi vya kiunabii na nguvu ya Roho Mtakatifu iliyoambatana na vuguvugu la marejeo waliihusisha na mawakala wa kibinadamu au wa kishetani. Kundi jingine walishikilia kwa nguvu kuwa Bwana aliwaongoza katika uzoefu wao uliopita; na walivyongoja na kukesha na kuomba kujua mapenzi ya Mungu waliona kuwa Kuhani wao Mkuu alianza kazi nyingine ya huduma, na, wakimfuata kwa imani, walioongozwa kuona pia kazi ya mwisho ya kanisa. Walikuwa na ufahamu wa wazi wa ujumbe wa malaika wa kwanza na wa pili, na walikuwa tayari kupokea na kutoa ulimwenguni onyo kali la malaika wa tatu wa Ufunuo 14.PKSw 330.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents