Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Nyota ya Asubuhi ya Matengenezo

  Katika kame ya kumi na nne, huko Uingereza kulitokea mtu fulani aliyeitwa John Wycliffe, aliyestahili, kuitwa “nyota ya asubuhi ya Matengenezo.” Yeye ndiye aliyekuwa mtangulizi wa matengenezo ya kanisa, si kwa Uingereza peke yake, bali katika nchi zote za Kikristo. Alikuwa kama mzazi wa watu ambao baadaye waliitwa “Puritans.” Wakati wake ulikuwa kama maji jangwani, kama taa siku zile za giza.VK 30.2

  Bwana Mungu aliona ya kwamba kazi hii ya matengenezo ilifaa kuwekwa mkononi mwa mtu mwenye akili na uwezo, ambaye angeonyesha tabia njema na uaminifu katika kazi yake aliyopewa. Hali hii iliwanyamazisha wale wenye kuidharau dini, na iliwazuia adui za ukweli wasiidhihaki kazi ya Mungu kwa kuuchekelea ujinga wa wakili wake. Wycliffe alipohitimu katika mafundisho ya skuli, alianza kujifunza mambo yaliyomo ndani ya Biblia. Katika Biblia alipata mafundisho ambayo alikuwa ameyatafuta muda mrefu asiyapate. Humo katika Biblia aliona ya kwamba azimio la wokovu lilifunuliwa, na Kristo alionyeshwa kuwa mpatanishi wa pckee wa wanadamu. Aliona kwamba Kanisa la Kirumi lilikuwa limeacha njia za Biblia na kuyafuata mapokeo ya kibinadamu.VK 30.3

  Kazi kubwa zaidi aliyoifanya katika maisha yake ilikuwa kuifasiri Biblia katika lugha ya Kiingercza. Tafsiri lake la Biblia ndilo lililokuwa la kwanza la Kiingereza lililokamilika tangu awali. Kwa jinsi ambavyo kazi ya kupiga chapa ilikuwa haijajulikana, ilichukua muda mrefu na kazi ngumu kuandika vitabu vingi; walakini, kazi hii ikafanywa, na watu wa Uingereza waliipata Biblia katika lugha yao wenyewe. Hivyo ndivyo nuru ya Neno la Mungu ilivyoanza kuangaza giza nene. Mkono wa Mungu ulikuwa ukitayarisha njia kwa Matengenezo Makubwa.VK 31.1

  Kuwavuta watu kutumia akili zao juu ya mambo ya dini kuliwaamsha wasikubali bila kufikiri wenyewe masharti yaliyotolewa na askofu mkuu wa Kirumi. Biblia ilipokewa kwa furaha na watu wenye chco, ambao tu ndio waliokuwa wenye elimu katika zamani zile. Wycliffe alianza kufundisha mafundisho halisi ya Uprotestanti—yaani wokovu upatikanao kwa kumwamini Kristo tu, na ya kwamba Maandiko Matakatifu ndiyo maandiko peke yake yasiyoweza kukosa. Makasisi wengi waliungana naye katika kuzieneza Biblia, na kuihubiri injili; na mafundisho haya, pamoja na maandiko ya Wycliffe yalikuwa na nguvu sana, hata karibu nusu ya watu wa Uingereza waliikubali imani mpya hii. Ufalme wa giza ulitetemeka. Jitihadi zote zilizofanywa na adui za Wycliffe ili kuikomesha kazi yake na kuharibu maisha yake, yote hazikufaulu, na alipokuwa na umri wa miaka sitini na moja, akafariki kwa amani katika kazi ya Mungu.VK 31.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents