Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya Ishirini Na Nne - Ulimwengu Mpya

    *****

    KISHA nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita.” Ufunuo 21:1. Moto utakaoteketeza waovu ndio utakaoitakasa dunia. Dalili zote za laana zitafutiliwa mbali. Hakuna jehanum yo yote ambapo moto utawaka milele na kudumu kuwakumbusha waliookolewa matokeo na adhabu ya dhambi. Kutabaki ukumbusho mmoja tu: yaani, Mwokozi wetu atadumu kuwa na alama zile za kusulibishwa kwake. Kichwani mwake, mikononi na miguuni mwake, hapo tu ndipo zitakapoonekana alama za matendo ya ukali ambayo yaliletwa na dhambi.VK 140.1

    “Na wewe, Ee mnara wa kundi, kilima cha binti Sayuni, utajiliwa; naam, mamlaka ya kwanza yatakuja.” Mika 4:8. Ufalme ule uliokuwa umepotezwa kwa ajili ya dhambi, ulikombolewa na Kristo, na waliookolewa wataurithi pamoja naye. “Wenye haki watairithi nchi, nao watakaa humo milele.” Zaburi 37:29. Kwa ajili ya kuogopa ili wasifanye makao ya watakatifu ya mbinguni kuwa kitu cha hakika hasa, wengi wameongozwa wayabatilishe mafundisho ya kweli yanayotuonyesha ya kwamba dunia mpya itakuwa makao yetu, nao wanasema ya kwamba maneno hayo hayaelezi juu ya makao halisi. Yesu aliwaahidia wanafunzi wake ya kwamba alikwenda kuwaandalia makao. Wale ambao wanayakubali mafundisho ya Neno la Mungu hawatakosa kujua habari ya makao ya mbinguni. Lakini mtume Paulo asema hivi, “Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (wala hayakuingia katika moyo wa wanadamu), mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.” 1 Kor. 2:9. Lugha za kibinadamu haziwezi kuusimulia ujira wa watakatifu. Ujira ule utafahamiwa na wale tu watakaoupokea. Hakuna fikara ya kibinadamu inayoweza kuufahamu utukufu wa pale anapokaa Mungu.VK 140.2

    Katika Biblia, urithi wa watakatifu umeitwa nchi. (Ebr. 11:14-16). Hapo Mchungaji mkuu atawaongoza watu wake kwenye maji ya uzima. Mti wa uzima utatoa matunda yake kila mwezi, na majani ya mti ule ni ya kuwaponya mataifa. Kutakuwako na vijito vinavyotiririka daima, vyenye maji yaliyo safi kama kioo, na kando ya mito hiyo imepandwa miti ambayo itatupa vivuli vyake juu ya barabara itakayotembelewa na waliokombolewa na Bwana. Katika nchi ile, mabonde yatainuka na kuwa vilima vya kupendeza, na milima ya Mungu itainua vilele vyake. Katika nyanda zile za amani, kando ya mito hiyo ya maji ya uzima, watu wa Mungu, ambao tangu miaka mingi wamekuwa wageni na wasafiri, watayapata makao ya milele.VK 141.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents