Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mnyama na Sanamu (Mfano) Yake

  Mnyama huyu wa kwanza anasimama badala ya Kanisa la Kirumi, ambalo ni shirika la kanisa lililofunikwa na nguvu ya serikali, kanisa lenye mamlaka ya kuwahukumu watu wakataao kulitii. Sanamu ya mnyama inasimama badala ya dini nyingine inayojivika na uwezo wa namna ile. Kutengeneza sanamu hii ni kazi ya mnyama yule ambaye kuondoka kwake kwa amani, na mafundisho ya upole yanamfanya kuwa mfano wa ajabu wa nchi ya Amerika (U. S. A.)., Katika Amerika ndipo tunapoweza kuipata sanamu au mfano wa mamlaka ya Papa. Makanisa ya nchi hiyo, yatakapoungana pamoja katika mafundisho ya dini yanapofuatwa nao kwa kawaida, na pia kuivuta Serikali ya nchi ya Amerika ipate kuzitilia nguvu amri zao. na kuzihifadhi kawaida zao, ndipo Waprotestanti wa Amerika watakapokuwa wameifanya sanamu ya mamlaka ya Kanisa la Kirumi. Ndipo kanisa la kweli litashambuliwa na kuteswa, kama watu wa Mungu wa zamani walivyotendwa.VK 84.1

  Mnyama mwenye pembe kama za mwana kondoo awaamuru “wote wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao: tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.” Ufunuo 13:16,17. Alama au chapa hii ndiyo ambayo malaika wa tatu alitoa onyo juu yake. Ni alama ya yule mnyama wa kwanza, au mamlaka ya Papa, na kwa hiyo alaina hii inaweza kupatikana katika tabia kuu za mamlaka ya Papa. Nabii Danieli alisema ya kwamba Kanisa la Kirumi, lililofananishwa na pembe ndogo, ndilo litakatakalotumaini kubadili majira na sheria (Dan. 7:25), na Paulo amelitaja kanisa lile kuwa ni mtu wa dhambi (2 The. 2:3, 4), ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu. Mamlaka ya Papa haikuweza kujiinua juu ya Mungu isipokuwa kwa njia ya kubadili sheria ya Mungu; na mtu ye yote ambaye kwa makusudi aishika sheria jinsi ilivyogeuzwa na kujua hivyo, anamheshimu kamili yule aliyegeuza sheria hivi.VK 84.2

  Amri ya nne, ambayo Kanisa la Kirumi limejitahidi sana kuibadili, ndiyo amri ya pekee kati ya amri zote kumi inayomtaja Mungu kuwa Muumba wa mbingu na dunia, na hivi humdhirisha Mungu wa kweli kati ya miungu ya uongo. Sabato iliwekwa kuwa ukumbusho wa kazi ya uumbaji, na hivi kuelekeza fikara za wanadamu kwa Mungu wa kweli aliye hai. Ukweli wa uwezo wake wa kuumba umeonyeshwa pote katika Maandiko kwa kuthibitishwa ya kwamba Mungu wa Israeli ndiye aliye mkuu zaidi ya miungu ya ushenzi. Kama Sabato ingalitunzwa daima, ndipo fikara za wanadamu na upendo wake zingaliongozwa kwa Muumba wao kama mmoja tu anayestahili kuheshimiwa na kuabudiwa; na asingalikuwako mwabudu sanamu, wala asiyeamini ya kwamba Mungu yuko, wala mtu asiye na dini yo yote.VK 85.1

  Amri ile inayomtaja Mungu kama Muumbaji ndiyo dalili ya haki aliyo nayo ya kuwa na mamlaka juu ya viumbe vyakc. vyote. Tena kugeuzwa kwa Sabato ni dalili au alama ya mamlaka ya Kanisa la Kirumi. Wale ambao, ingawa wanafahamu matakwa va amri ya nne, huchagua kuitunza Sabato iliyofanyizwa badala ya ile ya asili, kwa hiyo humheshimu yule aliyetoa agizo hilo.VK 85.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents