Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Yerusalemu Mpya

    Yerusalemu Mpya ni hapo, “wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri.” Ufunuo 21:11. Bwana asema, “Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu.” Isaya 65:19. “Maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza vamekwisha kupita.” Ufunuo 21:3,4.VK 141.2

    Katika mji wa Mungu “hamna usiku.” Hakuna atakayctaka kupumzika. Hakuna ye yote atakayechoka kwa kuyatenda mapenzi ya Mungu na kulisifu jina lake. Tutadumu katika hali njeina, wenye afya. “Wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua: kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru.’‘ Ufunuo 22:5. Badala ya mwanga wa jua utakuwako mwanga utakaong’aa bila kuyatia macho kiwi, ingawa utaangaza kwa nguvu zaidi ya mwanga wa adhuhuri yetu ya sasa. Utukufu wa Mungu na wa Mwana Kondoo utaufunika mji mtakatifu na mwanga usiofifia. Waliookolewa watatembea katika nuru mchana wa daima usio na haja ya mwangaza wa jua.VK 142.1

    “Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake.” Ufunuo 21:22. Watu wa Mungu watakuwa na haki ya kuzungumza na Baba bila kizuizi. “Wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo.” 1 Kor. 13:12. Tunauona mfano wa Mungu, kama kitu kionckanacho kwa kioo, tukimwona katika kazi zake za uumbaji, na kwa mambo anayowatendea wanadamu; lakini baadaye tutamwona uso kwa uso, bila kizuizi cho chote. Tutasimama mbele zake na kuutazama utukufu wa uso wake.VK 142.2

    Katika nchi ile watu walio na hali ya kutokufa watajifunza kwa furaha isiyo na mwisho, wakiyachunguza maajabu ya uwezo wa uumbaji. na siri ya upendo ule uliowakomboa. Yule adui mkali hatakuwako, hakuna atakayewadanganya watu wamsahau Mungu. Uwezo wa akili za kila namna utaongezeka. Uwezo wa kufahamu utazidishwa. Fikara za watu hazitachoka kwa kujifunza mambo mapya, wala uchovu wo wote hautakuwako. Katika nchi ile, kazi zilizo bora kabisa zitaendeshwa, na mambo makuu yatafanywa, haja kuu zitatimizwa, na siku zote kutakuwako na mambo makuu zaidi ambayo itawapasa watu kujifunza, maajabu mapya ya kustaajabia, mafundisho mapya ya kufahamiwa, mambo mapya yatakayohitaji kufanywa kwa uwezo wa mikono, kwa fikara na moyo.VK 143.1

    Na miaka ikizidi kupita, watu wataendelea kuyavumbua mambo makuu zaidi juu ya Mungu na juu ya Kristo. Kwa jinsi ujuzi utakavyoongezeka, ndivyo kutakavyokuwa na upendo, heshima na furaha pia. Kwa kadiri watu watakavyozidi kujifunza juu ya Mungu, ndivyo watakavyozidi kupendezwa na tabia yake. Yesu atakapowafunulia mambo makuu ya wokovu, na ushindi wa ajabu katika mashindano yake na Shetani, mioyo ya watakatifu itajaa furaha na heshima, na watazinyakua nvuzi za vinanda vya dhahabu kwa nguvu zaidi; na sauti elfu kumi na mara elfu kumi, na sauti maelfu maelfu zitaungana kwa kuuimba wimbo wa kumsifu Mungu.VK 143.2

    “Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi na juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.” Ufunuo 5:13.VK 143.3

    Dhambi na watenda dhambi hawataonekana tena, ulimwengu wote wa Mungu utakuwa safi, na shindano kuu litakuwa limekoma kabisa.VK 143.4

    *****

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents