Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya Tisa - Kilio Cha Usiku Wa Manane

    *****

    HATA bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. Lakini usiku wa manane» pakawa na kelele, “Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao.” Mathayo 25:5-7.VK 69.1

    Kati kati ya mwaka wa 1844 wale waliokuwa wakitazamia kurudi kwa Kristo wakatambua kosa lao kwa namna walivyohesabu nyakati za unabii mwanzoni, wakauthibitisha wakati ulivyo halisi. Siku 2,300 zilizoandikwa katika Danieli 8:14, ambazo wote waliamini ya kwamba zitafikia kuja kwa Kristo mara ya pili, zilifikiriwa ya kwamba zitaishia mwaka wa 1844 mnamo mwezi wa Machi au Aprili; lakini ilionekana ya kwamba zinaendelea mpaka wakati wa vuli kama mwezi wa Oktoba katika mwaka ule ule, tena watu wale walitazamia siku zile kama wakati wa kuonekana kwa Bwana. Tangazo la ujumbe huu juu ya wakati lilikuwa hatua nyingine kwa utimilizo wa mfano ule wa arusi” ambao matumizi yake kwa kueleza mambo yaliyotokea yameonekana tayari katika mambo yaliyowapata wale waliokuwa wakimtazamia Yesu.VK 69.2

    Kama ilivyoandikwa katika mfano wa wanawali, kilio kile kilitokea mnamo usiku wa manane, kikitangaza kukaribia kwa bwana arusi, vivyo hivyo katika utimizo wake, katikati ya mwaka wa 1844, baada ya siku zile ilipofikiriwa mara ya kwanza ya kwamba siku 2,300 zitakoma, na kabla ya mwezi wa Oktoba, 1844, ambao baadaye ilionekana ya kwamba siku zile zitakoma, ndipo kilio cha namna ile kilipotokea, kwa maneno yale yale yaliyoandikwa katika Biblia: “Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.”VK 69.3

    Habari ile ilienea pote kama maji yanavyogharikisha nchi. Ilienea katika kila nchi, kutoka mji mpaka mji mwingine, tokea kijiji mpaka kijiji kingine, hata na katika mashamba palipokuwa mbali sana na mji, mpaka watu wa Mungu. wakaamshwa kabisa. Ushupavu wa dini ulitoweka kabla ya tangazo hili, kama umande utowekavyo jua lichapo. Waaminio walipata kusimama imara tena, na mioyo yao ikaanza -kujaa tumaini na uthabiti.VK 70.1

    Kazi ilikuwa haikuzuiliwa na mambo ya ushupavu wa dini ambayo kwa kawaida huonekana kila mara panapokuwa hamaniko la kibinadainu pasipo kutawaliwa na kuongozwa na Neno la Mungu na Roho Mtakatifu. Siku zile zilifanana na siku za udhilifu na kumrudia Bwana zilizoonekana katika siku za Waisraeli wa zamani, baada ya kupata ujumbe wa lawama kutoka kwa watumishi wa Bwana. Kazi ile ilionekana kuwa mamoja na kazi za Mungu katika vizazi vyote. Si kwamba ilikuwako hali ya furaha nyingi mno, bali ilikuwako hali ya kumwaza Mungu na kutafutia mioyo, kuziungama dhambi na kuacha mambo ya dunia na anasa zake. Kujitayarisha kumlaki Bwana kulikuwa jambo lililolemea roho za watu. Kulikuwa na maombi ya juhudi na kujitoa kabisa kwa Mungu.VK 70.2

    Ujumbe wa kilio cha usiku wa manane haukuendeshwa kwa njia ya majadiliano, ingawa maneno yaliyoandikwa katika Biblia yalikuwa dhahiri na ya kuthibitisha jambo lile kwa hakika. Kilio kilikuwa na uwezo wa kuigusa mioyo ya watu. Hayakuwako mashaka wala tashwishi. Siku ile Kristo alipoingia Yerusalemu kwa shangwe, watu waliokusanyika kutoka pande zote kwa kufanya siku kuu ya Pasaka, walikusanyika katika Mlima wa Mizeituni, na walipoungana na makutano ya watu waliofuatana na Yesu, walivutwa na jambo lile lililofanywa kwa maongozi ya Roho, wakapaaza sauti pamoja wakisema, “Ndiye mbarikiwa, Yeye ajaye kwa jina la Bwana.” Mathayo 21:9. Hivyo ndivyo ilivyokuwa na watu wasioamini walikusanyika katika mikutano ya wale waliokuwa wakimtazamia Yesu—wengine walikuja kwa ajili ya upekuzi tu na wengine kwa minajili ya kuwachekelea—hao nao walivutwa na kusadikishwa na uwezo ule ulioutia nguvu ujumbe ukisema hivi, “Haya, Bwana arusi anakuja!”VK 70.3

    Wakati ule kulikuwa na imani iliyoyafanya maombi kujibiwa—imani iliyotazamia hayo malipo ya mwisho. (Ebr. 11:26). Roho wa neema aliwashukia wale waombaji kama manyunyu ya mvua yaangukayo juu ya ardhi iliyokauka. Wale wliokuwa wakitazamia kumwona Mwokozi uso kwa uso karibuni walikuwa na furaha isiyokadirika. Uwezo mkuu wa Roho Mtakatifu, unaolainisha na kuutiisha moyo, uliingia katika mioyo ya watu, kwa jinsi utukufu wa Mungu ulivyoongezeka juu ya wale waaminifu wenye imani.VK 71.1

    Kwa kicho na utulivu wale walioupokea ujumbe waliufikia wakati ambao walikuwa wakitumaini kumwona Bwana wao. Kila asubuhi waliona ya kwamba ilikuwa wajibu wao wa kwanza kuhakikisha ya kwamba wamekubaliwa na Mungu. Walikuwa na umoja na upendano wa moyo, na waliombeana sana wao kwa wao. Walizoea kukusanyika mahali pa faragha wapate kuzungumza na Mungu, na sauti zao za maombezi zilipanda hata mbinguni kutoka mashambani na vichakani walipokusanyika. Walikuwa na hamu ya kuhakikisha ya kwamba walikubaliwa na Mwokozi, zaidi ya jinsi walivyotaka chakula chao cha kila siku, na mioyo yao ilipoingiliwa na shaka fulani, hawakuweza kutulia mpaka shaka ile iondolewe. Waliposikia moyoni ushuhuda wa kusamehewa dhambi kwa neema ya Mungu, walitumaini zaidi kumwona Yeye ambaye walikuwa wanampenda.VK 71.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents