Sura Ya Kumi Na Saba - Wakati Wa Taabu Ya Yakobo
*****
NALIYVAONA watakatifu wakitoka katika miji na vijiji, wakiungana pamoja kwa makundi, wakienda kukaa katika hali ya upweke. Malaika waliwapa chakula na maji, lakini waovu waliumwa na njaa na kiu. Ndipo nikawaona wakuu wa dunia wakishauriana pamoja, na Shetani na malaika zake wakishughulika karibu nao. Naliiona barua fulani, ambayo nakili zake zilitawanywa katika nchi mbali mbali, ikitoa amri ya kwamba watakatifu wasipoacha imani yao iliyo maalum, kuacha kuishika Sabato na kuitunza siku ya kwanza ya juma, baada ya muda fulani watu watakuwa na ruhusa ya kuwaua. Lakini katika wakati huu wa taabu watakatifu walitulia na kuwa na amani rohoni, wakimwamini Mungu na kiitegemea ahadi yake ya kwamba watapata njia ya kuokoka.VK 114.1
Katika nchi nyingine, waovu waliwarukia watakatifu ili kuwaua kabla ya siku ile iliyoagizwa; lakini malaika waliochukua mfano wa wanadamu waliwapigania watakatifu. Shetani alikuwa na hamu ya kuwa na uwezo wa kuwaharibu watakatifu wake Alive Juu, lakini Yesu aliwaambia malaika zake wawalinde. Mungu angeheshimiwa mbele za washenzi waliowazunguka, kwa kulifanya agano na wale waliozishika amri zake; na Yesu angeheshimiwa kwa kuwahamisha wale waaminifu waliokuwa wakimngoja kwa muda mrefu, wasione mauti.VK 114.2
Baada ya muda kitambo niliwaona watakatifu wakiona maumivu makuu mioyoni mwao. Walionekana wakizungukwa na waovu wa dunia. Kwa kadiri ilivyoonekana, walikuwa katika hali mbaya sana. Wengine walianza kuogopa ya kwamba labda Mungu amewaacha wapate kutaabishwa na waovu. Lakini kama macho yao yangalifunguliwa, wangaliona ya kwamba walizungukwa na malaika za Mungu. Ndipo kundi la waovu wakaja wamekasirika, na nyuma yao kundi la malaika watakatifu, wenye nguvu. Jambo hili halikuwezckana. Malaika za Mungu waliwafanya waovu warudi nyuma, hata na malaika wa-ovu waliokuwa wakisongana karibu nao waliwafanya warudi nyuma.VK 115.1