Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya Ishirini - Mlaka Elfu

  *****

  NALIONYESHWA dunia tena. Waovu walikuwa wameharibiwa, na maiti zao zilikuwa zikitapakaa usoni pa dunia. Ghadhabu ya Mungu ilikuwa imemiminwa juu ya watu wakaao duniani kwa mapigo sabz ya mwisho, nao wakalazimishwa kuzitafuna ndimi zao kwa ajili ya maumivu, na walikuwa wakimtukana Mungu. Wachungaji wa uongo ndio ambao ghadhabu ya Mungu ilikuwa kali zaidi juu yao. Macho yao yalikuwa yamedhoofika katika vitundu vyao, vivyo hivyo na ndimi zao midomoni mwao wakati walipokuwa wanasimama kwa miguu yao. Watakatifu walipokwisha kuokolewa kwa sauti ya Mungu, ndipo umati wa waovu wakaanza kufanyiana ukali wao kwa wao. Dunia ilionekana kwamba imegharikishwa na damu, na maiti ilionekana kutoka upande mmoja wa dunia mpaka upande mwingine.VK 123.1

  Dunia ilionekana kuwa jangwa la ukiwa kabisa. Miji na vijiji, kwa vile vilivyobomolewa na tetemeko la nchi, vikawa mafungu mafungu. Milima ilikuwa imehamishwa kutoka mahali pake, ikiacha mapango makubwa mahali ilipotoka. Miamba iliyopasuka, iliyotupwa kutoka baharini, au iliyobomoka yenyewe kutoka usoni pa dunia, ilitapakaa huko na huko usoni pa nchi. Miti mikubwa ilikuwa imeng’olewa na kutawanywa juu ya nchi. Hapa ndipo patakapokuwa makao ya Shetani na malaika zake kwa miaka elfu. Hapa ndipo atakapokuwa kama mfungwa, akitembea huku na huko juu ya uso wa dunia iliyobomoka apate kuyaona matokeo ya uasi wake kwa Mungu na sheria yake. Kwa miaka elfu atayaona mazao ya laana ambayo aliileta duniani.VK 123.2

  Kwa jinsi atakavyokuwa akifungwa duniani yeye peke yake, hatakuwa na ruhusa ya kwenda katika sayari nyingine apate kuwajaribu na kuwasumbua wale ambao hawakuanguka dhambini. Wakati huu Shetani atataabika vibaya sana. Tangu kuanguka kwake, tabia zake za uovu zimezoezwa juu ya wanadamu. Lakini wakati ule atanyang’anywa uwezo wake naye ataachwa peke yake apate kuyawaza mambo ambayo alikuwa ameyatenda tangu kuanguka kwake, na apate kutazainia kwa hofu na kutetemeka mambo ya kuogofya yatakayompata mbeleni, atakapoadhibiwa kwa ajili ya maovu yote aliyokwisha kuyatenda, na kwa ajili ya dhambi ambazo aliwashawishi wengine wakazitenda.VK 124.1

  Nalisikia sauti za shangwe za malaika na za watakatifu waliookolewa, sauti zilizofanana na vilio vya vinanda elfu kumi, kwa kuwa haitawezekana kwao kujaribiwa wala kuudhiwa tena na Shetani, na kwa kuwa wenyeji wa sayari nyingine walilindwa asiwaendee na kuwajaribu.VK 124.2

  Ndipo nikaona viti vya enzi, na Yesu na watakatifu waliookolewa waliketi juu ya viti vile; na watakatifu walimiliki kama wafalme na makuhani kwa Mungu. Kristo, pamoja na watu wake, aliwahukumu waovu waliokuwa wamekufa, akiyalinganisha matendo yao na Kitabu cha Sheria, yaani Neno la Mungu, na akikata kila hukumu kwa jinsi matendo ya kimwili yalivyo. Halafu wakawapimia waovu hukumu iliyowapasa kupata kwa namna ya matendo yao, na hukumu zote ziliandikwa juu ya majina yao katika kitabu cha mauti. Shetani pia, pamoja na malaika zake walihukumiwa na Yesu na watakatifu. Shetani alipaswa kupata adhabu kali zaidi ya watu ambao aliwadanganya. Adhabu yake haina budi kuwa kali zaidi hata isiweze kulinganishwa na adhabu ya wengine. Baada ya kufa kwa wale aliokwisha kuwadanganya, Shetani aliachwa apate kuishi akiendelea kuyasikia maumivu kwa muda mrefu zaidi.VK 124.3

  Hukumu ya waovu ilipokwisha, mnamo mwisho wa miaka elfu, Yesu alitoka katika mji, na watakatifu pamoja na mwandamano wa malaika walimfuata. Yesu alishuka kwenye mlima mkubwa, na mara ile miguu yake ilipougusa mlima ule, mlima ulipasuka vipande viwili ukawa uwanja mkuu. Ndipo tukaangalia juu tukauona mji mzuri ule ulio mkuu, uliojengwa juu ya misingi kumi na miwili, na milango kumi na miwili, milango mitatu kila upande. na malaika mmoja katika kila mlango. Tulipaaza sauti zetu tukisema, “Mji ule! mji mkuu! Unashuka chini kutoka kwa Mungu mbinguni!” Mji ule ukashuka chini kwa fahari yake ya utukufu unaoshangaza, ukatua juu ya uwanja ule mkubwa uliokuwa umetayarishwa na Yesu.VK 125.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents