Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Vita Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya Ishirini Na Mbili - Kumtawaza Kristo

  *****

  KRISTO alionekana tena mbele ya adui zake. Juu sana, kuelekea ule mji, juu ya msingi wa dhahabu inayong’aa sana, kulikuwa na kiti cha enzi, kilichoinuliwa juu sana. Mwana wa Mungu aliketi juu ya kiti kile, akizungukwa na raia za ufalme wake. Hakuna lugha inayoweza kuusimulia uwezo na utukufu wa Kristo, wala hakuna kalamu inayoweza kuuchora kadiri ya utukufu ule. Utukufu wa Baba wa Milele humfunika Mwana wake. Mwanga wa kuwapo kwake unajaza mji wa Mungu, hata ikaipita milango, ukiifunika dunia yote na kung’aa kwake.VK 129.1

  Karibu na kiti cha enzi wanakaa wale ambao zamani walikuwa watenda kazi hodari wa Shetani, lakini walikuwa kama kinga kilichopokonywa motoni, wakamfuata Mwokozi wao kwa moyo wa upendo na bidii. Nyuma yao kuna watu wale waliotakasa tabia zao za Kikristo kati ya unafiki. wale walioiheshimu sheria ya Mungu, wakati ambao Wakristo wengine wengi walisema ya kwamba sheria ya Mungu imetanguka, na pamoja nao watu mamilioni katika vizazi vyote, waliouawa kwa ajili ya imani yao. Baada ya hayo nikaona “mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kiti kile cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.” Ufunuo 7:9. Vita vyao vimekoma, ushindi wameupata. Shindano lao limekwisha, nao wamelipokea tuzo. Matawi ya mitende mikononi mwao ni dalili ya shangwe yao kuu, na mavazi meupe ni dalili ya utakatifu wa Kristo usio na mawaa, ambao umekuwa wao.VK 129.2

  Waliookolewa huimba wimbo wa sifa ambao unasikika kama rnwangwi unaosikika katika pande zote za mbinguni, wakisema, “Wokovu una Mungu wetu aketive katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.” Malaika na maserafi huungana kwa sauti wakimsujudu Mungu. Waliookolewa walipokwisha kuuona uwezo na uovu wa Shetani, wakafahamu kuliko walivyojua mara ya kwanza, ya kwamba hakuna uwezo wo wote, isipokuwa ule wa Kristo mwenyewe, ulioweza kuwafanya wawe washindi. Katika kundi lile kubwa lenye kumetameta, hakuna hata mmoja mwenye kujidai ya kwamba uwezo wake ndio uliomwezesha kuupata wokovu, kana kwamba walishinda kwa ajili ya uwezo na wema wao wenyewe. Hakuna neno lo lote lisemwalo juu ya jambo lo lote walilotenda, wala maumivu yo yote waliyoyavumilia, lakini habari yote ya wimbo wao ndiyo hii: “Wokovu una Mungu wetu . . . na Mwana-Kondoo.” Ufunuo 7:10.VK 130.1

  Mwana wa Mungu atatawazwa mbele ya makutano ya wakaao mbinguni na duniani. Naye akipewa enzi kuu na mamlaka, Mfalme wa wafalme atawahukumu wale waliomwasi, tena atawahukumu kwa haki wale walioharibu amri zake na kuwatesa watu wake. Nabii wa Mungu asema hivi: “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake, ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.” Ufunuo 20:11,12.VK 130.2

  Vitabu vya majina vitakapofunguliwa, na macho ya Yesu yatakapowatazama waovu, watayafahamu maovu yote ambayo walikuwa wameyatenda. Wataona dhahiri mahali ambapo miguu yao iliteleza ikiacha njia ya usafi na utakatifu, jinsi kiburi na uasi ulivyowaongoza hata wakaziharibu amri za Mungu. Madanganyifu na majaribu ambayo waliyakuza kwa ajili ya kuishikilia dhambi, mibaraka waliyoitumia vibaya, habari za rehema zilizowajia ambazo walizikataa kwa ajili ya mioyo migumu isiyoweza kugeuka—haya yote yataonekana kana kwamba yaliandikwa kwa nukta za moto.VK 131.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents