Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Luther Mbele ya Baraza

    Hatimaye Luther alisimama mbele ya baraza. Mfalme aliketi juu ya kiti cha enzi. Alizungukwa na watu mashuhuri sana katika ufalme wake. Hakuna mtu ye yote aiiyekuwa amesimama mbele ya baraza kuu ya kushangaza kama ile ambayo Luther alisimama mbele yake ili kuitetea imani yake.VK 43.2

    Kuonekana kwake hivi mbele ya baraza kulikuwa dalili ya ushindi wa ukweli wa Mungu. Mtu ambaye alikuwa amehukumiwa tayari na Papa, tena kuanza kuhukumiwa na baraza nyingine, jambo hilo lilionekana kana kwamba utawala wa juu wa Papa unaanza kupunguka. Mtengenezaji Luther, baada ya kulaaniwa, na kuharamishwa kanisani na Papa, aliahidiwa ya kwamba atalindwa, na kusikizwa mbele ya baraza ya wakuu wa taifa. Amri ilikuwa imetoka Rumi kumkataza asinene tena, lakini sasa alikuwa amepewa nafasi ya kuhutubu mbele ya maelfu ya watu waliotoka katika nchi zote za Kikristo. Kwa utulivu na upole, lakini kwa ushujaa na usharifu, alisimama kama shahidi wa Mungu mbele ya wakuu wa dunia. Luther aliyajibu maswali yao kwa sauti ya upole na unyenyekevu, pasipo hasira wala haraka. Hali yake ilikuwa ya heshima, na hakuegemea nguvu zake mwenyewe; walakini alionyesha matumaini na furaha iliyowashangaza watu waliohudhuria katika baraza ile.VK 43.3

    Wale waliokataa kuipokea nuru kwa ajili ya ukaidi tu, na kukaza nia zao wasiikubali kweli, walikasirishwa na nguvu ya maneno ya Luther. Alipomaliza maneno yake, mwenye kiti katika baraza akamjibu kwa hasira akisema, “Hukujibu swali maalum uliloulizwa. . . Inatakiwa utoe jibu lililo fupi na lenye maana. . . Je, utakubali, au hutakubali kuikanusha imani yako?”VK 44.1

    Mtengenezaji akajibu akisema: “Kwa jinsi wewe mfalme mtukufu na ninyi wakuu wa milki mnavyotaka kwangu jibu lililo safi, fupi, na lenye maana, nitawapeni jibu moja, nalo ni hili: Siwezi kuacha imani yangu kwa ajili ya Papa wala baraza, kwa kuwa imeonekana dhahiri ya kwamba mara nyingi wamekosa, na mafundisho, yao hayapatani. Kwa hivyo basi, nisiposadikishwa na Maandiko Matakatifu ama na majadiliano yaliyo dhahiri kabisa, nisiposhurutishwa na mafungu ambayo nimeyatoa, na yasiponionyesha moyoni ya kwamba nimefarakana na Neno la Mungu. sitaikana imani yangu kamwe, wala siwezi kufanya hivyo. kwa kuwa Mkristo anajihatarisha kama akiyakiri mambo yafarakanayo na dhamiri yake. Hapa nimesimama, siwezi kugeuka; Mungu na anisaidie. Amina.”VK 44.2

    Hivyo ndivyo alivyosimama huyu mtu wa haki, akisimania imara kabisa juu ya msingi imara wa Neno la Mungu. Nuru ya mbinguni iliangaza usoni pake. Ukuu wake na tabia iliyo safi, amani na furaha aliyokuwa nayo moyoni mwake, zilionekana mbele ya wote alipokanuslia mamlaka ya uongo na kushuhudia ukuu wa imani ilc ishindayo ulimwengu.VK 44.3

    Alisimama imara kama mwamba, wakati mawimbi makali ya uwezo wa dunia yalipompiga huko na huko yasimdhuru. Nguvu iliyokuwa katika maneno yake, jinsi alivyosimama bila hofu, macho yake yaliyong’aa na kuonyesha amani yake, na uthabiti wake usiogeuka ulioonekana katika kila neno na tendo lake, ziliwashangaza sana wakuu wa baraza. Ilionekana dhahiri ya kwamba hakuweza kushawishwa kwa ahadi wala vitisho, ili ainame mbele ya mamlaka ya Rumi.VK 45.1

    Kristo ndiye aliyenena katika ushuhuda wa Luther kwa nguvu na ufasaha, hata maneno yake yakawachoma moyo na kuwashangaza rafiki zake pamoja na adui zake pia. Roho wa Mungu alikuwako katika baraza ile, akigusa mioyo ya wakuu wa dola. Wengine kati ya wale wakuu walikiri dhahiri ya kwamba jambo la Luther lilikuwa jambo la haki kabisa. Wengi walisadikishwa na ukweli wa maneno yake, lakini kwa wengine maono yao hayakudumu sana Kulikuwako na watu wengine pia ambao wakati ule hawakuonyesha ya kwamba waliyasadiki mambo yale; lakini baada ya kujisomea wenyewe Maandiko Matakatifu, katika siku za baadaye kwa ushujaa walitetea Matengenezo ya dini.VK 45.2

    Yule elector Frederick wa Saxony alitazamia mambo ya baraza ile kwa wasiwasi naye alisikiliza hotuba yake Luther kwa kushtuka sana moyoni. Alifurahia ushujaa, uthabiti na ukavu wa macho wa yule mtauwa maarufu, naye alifurahia kuwa mtetezi na mlinzi wake. Elector Frederick alipolinganisha wale waliotetana, aliona ya kwamba utetezi wa Luther ulikuwa na nguvu zaidi, na aliona ya kwamba akili ya Papa, ya wafalme na ya maaskofu ilishindwa kabisa na ukweli alioshuhudia Luther. Ilikuwa ya kwamba utawala wa Kanisa la Kirumi umeshindwa kwa namna ambavyo matokeo yake yangeenea kwa mataifa yote na kwa vizazi wote vya baadaye.VK 45.3

    Kama Luther angalishindwa katika jambo moja tu, Shetani na malaika zake wangalipata ushindi. Lakini uthabiti wake na jinsi alivyosimama imara bila kusitasita, ulikuwa njia ya kuleta uhuru kanisani, na huo ndio mwanzo wa wakati mpya wa amani. Mvuto wa mtu huyu mmoja, ambaye alithubutu kusimama peke yake kwa maoni yake juu ya mambo yanayohusu dini, ulikuwa na nguvu ya kugeuza hali ya kanisa na dunia pia, wala si katika siku za maisha yake tu, bali katika vizazi vya baadaye pia. Uthabiti wake na uaminifu wake ungewatia watu nguvu mpaka mwisho wa dunia, yaani wote watakaopata mateso kama yale. Uwezo na utukufu wa Mungu ulidhihirika ya kwamba unashinda mashauri ya wanadamu, hata na uwezo mkuu wa Shetani pia.VK 46.1

    Naliona ya kwamba Luther alikuwa shujaa, mwenye juhudi, mwenye macho makavu, mtu asiye na woga kwa kuikaripia dhambi na kuitetea haki. Hakuwaogopa waovu wala mashetani: alijua ya kwamba pamoja naye alikuwa Mmoja aliye na nguvu zaidi ya wote. Luther alikuwa na juhudi, ushu.jaa, na uthabiti, na mara zingine alikuwa katika hatari ya kufanya ujasiri kupita kiasi. Lakini Mungu alimwinulia Melancthon, ambaye alikuwa na tabia iliyo mbali na ile ya Luther, apate kumsaidia katika kuiendesha kazi ya Matengenezo ya kanisa. Melancthon alikuwa mwoga, mwenye kuwa na hadhari, mwangalifu na mvumilivu. Alikuwa mpendwa sana wa Mungu. Alikuwa na ujuzi sana kwa Maandiko Matakatifu, tena alikuwa mwenye busara sana kwa kukata mashauri. Upendo wake kwa kazi ya Mungu ulikuwa sawa na ule wa Luther. Bwana Mungu aliiunganisha pamoja mioyo ya watu hawa; walikuwa rafiki wasiotengana. Luther alimsaidia sana Melancthon alipokuwa katika hatari ya kuonyesha woga na upole zaidi na kwa upande wake Melancthon alimsaidia sana Luther alipokuwa katika hatari ya kuharakisha mambo kupita kiasi.VK 46.2

    Busara na uangalifu wa Melancthon uliwawezesha kuepuka matata ambayo yangalitokea juu ya kazi ya Mungu kama kazi ingalikuwa mkononi mwa Luther peke yake; na mara nyingi kazi isingaliendelezwa vizuri kama ingaliachwa kwa Melancthon peke yake. Nalionyeshwa hekima ya Mungu katika kuwachagua watu hawa wawili kuiendesha kazi hii ya Matengenezo.VK 47.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents