Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Vita Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya Kwanza - Uasi Mkuu

    *****

    YESU alipowafunulia wanafunzi wake ajali itakayoujia Yerusalemu, na mambo yatakayoonekana katika marejeo yake, aliwaambia pia juu ya hali ya Maisha ya watu wake tangu wakati atakapochukuliwa kwao, mpaka kurudi kwake pamoja na uwezo na utukufu apate kuwaokoa. Pale katika mlima wa Mizeituni, Mwokozi aliiona mbele dhoruba ya mateso ambayo yalitaka kuja kulipata kanisa la mitume; na alipotazama sana mambo yajayo, macho yake yalitambua taabu na zama za giza na mateso makali yatakayokuja kuwataabisha wafuasi wake. Kwa maneno machache, yenye maana sana, ya kutisha, alitabiri juu ya mambo ambayo watawala wa dunia hii wangeyafanya juu ya kanisa katika njia ya udhilifu, mashutumu na mateso ambayo Bwana wao aliyapitia. Uadui ambao watu wa dunia walikuwa nao juu ya Mwokozi wa dunia, ungeonyeshwa vivyo hivyo kwa watu wanaoliamini jina lake.VK 9.1

    Habari za kanisa la zamani zilionyesha utimizo wa maneno ya Mwokozi. Mamlaka za dunia na za ahera zilishindana na Kristo kwa njia ya kuwatesa wafuasi wake. Mamlaka za kishenzi kwenye kuabudu miungu ya uongo waliona mbele ya kwamba Injili ikipata kusitawi, hekalu na madhabahu yao yatatokomelea mbali: kwa hivyo mamlaka yale yakatumia uwezo wake wote kwa kuiharibu dini ya Kikristo. Mateso makali sana yakaanzishwa. Wakristo walinyang’anywa mali zao na kufukuzwa katika nyumba zao. “Wengine walijaribiwa kwa dhihaka na mapigo, naam, kwa mafungo, na kwa kutiwa gerezani.” Ebr. 11:36. Watu wengi sana walitimiza ushuhuda wao kwa damu yao. Watu mashuhuri na watumwa, matajiri na maskini, walioelimika na wasio na elimu, waliuawa wote bila rehema.VK 9.2

    Lakini Shetani alishindwa kuliharibu kanisa la Kristo kwa jeuri, ingawa alijaribu sana. Shindano lile kuu ambalo kwalo wanafunzi wa Yesu walitoa maisha yao halikukoma wakati wale mitume waaminifu walipouawa. Ushindi ulikuwa wao. Watenda kazi wa Mungu waliuawa, lakini kazi yake iliendelea kusitawi. Injili iliendelea kuenea, na idadi ya wafuasi wa Injili iliongezeka. Injili ilipenya katika sehemu za nchi zisizoingiliwa hata mahali pa mamlaka ya Rumi. Mkristo fulani alisema maneno haya alipokuwa akiwagombeza watawala washenzi waliokuwa wakichochea sana yale mateso: “Mnaweza kutuua, kututesa, kutuhukumu. . . . Dhulumu lenu ndilo linaloshuhudia ya kwamba hatuna hatia. . . . Wala jeuri yenu haiwafaidieni kitu.” Lakini mateso haya yalikuwa kama mwito wa kuwavuta wengine washirikiane nao katika imani yao. Wakristo walisema hivi “Kwa kadiri mnavyotufyeka kama majani, ndivyo tunavyozidi kusitawi: damu ya Wakristo ni kama mbegu.”VK 10.1

    Watu maelfu walifungwa gerezani na kuuawa: lakini wengine walitokea na kujaza mahali pao. Na wale waliouawa kwa ajili ya imani yao, waliyakinishwa kuwa wa Kristo, wakahesabiwa naye kuwa washindi. Walikuwa w»mepiga vita vilivyo vizuri, na walitazamia kuipata taji ya haki siku Kristo atakaporudi. Maumivu ambayo Wakristo waliyavumilia yaliwaleta karibu na wenzao zaidi, na pia karibu na Mwokozi wao. Mfano wao wakati walipokuwa wazima, na ushuhuda wa kufa kwao, ulishuhudia daima juu ya ukweli wa Mungu; na mahali pasipotazamiwa kamwe, raia za Shetani walikuwa wakiacha kumtumikia na wakajitia chini ya bendera ya Kristo.VK 10.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents